Chilli
JF-Expert Member
- Jul 17, 2011
- 1,655
- 746
Wataalamu wa lugha yetu adhimu watuambie maana ya neno "Toka nje"
Mimi nijuavyo "kutoka nje" ni kinyume cha "ingia ndani". Hivyo sikumshangaa Tundu Lissu kumshangaa J. Ndugai alipotamka "...Tundu Lissu toka nje..." Sasa atoke nje aende wapi wakati alikuwa tayari yumo ndani ya ukumbi?Wale askari walivyo ambiwa "Askari mtoeni Tundu Lissu nje" nao bila kuelewa vizuri wakaenda kumshinikiza Lissu aende nje. Wao walitakiwa waulize kama Mh. Lissu anatakiwa atolewe ndani ya ukumbi au la!
Hivyo sioni kosa la Tundu Lissu wala wabunge wa CHADEMA kwenda kuwazuia wale askari wasimtoe ndani na kumpeleka nje, kwani walikuwa wanatekeleza amri ya kiti; Mtoeni nje muingize ndani! Askari walitekeleza kinyume chake! Lol!
Swali: Je kama hatufahamu kiswahili kwa kiasi hiki, kiingereza tutakiweza? Hapa naungana na wale wanaosema kiswahili kiwe ni lugha ya kufundishia mpaka mwisho wa darasa!
Ngoja nikupe darsa la lugha kidogo.
Katika lugha ya kiswahili kuna Uhusiano mbali mbali wa sentensi katika kiwango cha maana. Uhusiano huu waweza kuwa wa Usawe, Utata, Ukinzani, Upotoo nk.
Katika hii sentensi ilyotoka 'toka nje' inahusiana zaidi na utata.
Utata ni ile hali ya Sentensi kuwa na maana zaidi ya moja. Ambao nao umegawanyika katika sehemu mbili kuu. Utata wa Kileksika na Utata wa Kimuundo.
Sentensi tajwa imo katika Utata wa Kimuundo ambao mara nyingi huhusika na mpangilio wa Sentensi.
'Toka nje' sentensi hii ina utata ambao kimuundo waweza pata maana
1. Toka nje uongie ndani
2. Toka ndani uende nje
Ili kupata maana ya tungo hii mtu inatakiwa azingatie muktadha wa kimazungumzo.
*Muktadha maana yake ni mazingira ambayo mazungumzo hufanyika.
Kimuktadha, Tundu alikua ndani na aliambiwa atoke nje. Katika hali halisi ni mtu mkorofi tu ama juha ambaye anaweza kufikiri kwamba ameambiwa atoke nje aingie ndani ilihali muktadha wa kimazungumzo ni ndani.
Hivyo basi, kwa mtu muelewa kama Lissu, hiyo sentensi ilikua haina shida na ilieleweka kabisaaa, labda kama kulikua na sababu nyinginezo.