Tundu Lissu: Baada ya uchaguzi nilitakiwa kushughulikiwa, amri ilisema wasikosee shabaha

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,227
5,950
Kama mikutano ya hadhara ni fursa ya kufitinisha na kuchafua watu tunahaja ya kuangalia. Ila pia ni vizuri kuwapa fursa watu kutema sumu

======

Tundu Lissu amesema alirejea Tanzania mwaka 2020 kwa ajili ya uchaguzi na alilazimika kuondoka tena mwaka huo kwa sababu mtesi wake alitoa amri ashughulikiwe tena bila kukosea shabaha. Tundu Lissu ambaye sasa ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa alishambuliwa kwa risasi 16 siku ya Septemba 7, mwaka 2017 na kuondoka nchini kwa sababu ya matibabu.

Lissu amesema baada ya kupewa taarifa kuwa anatafutwa ili auawe mara baada ya uchaguzi, Oktoba 31, 2020 alijificha. Baadae alipata taarifa kuwa maficho yake yamejulikana na akashauriwa akimbie ndipo alipowasiliana na balozi wa Ujerumani ili kunusuru nafsi yake.

Alipofika katika Ubalozi wa Ujerumani, kabla ya kuruhusiwa kuingia magari matatu yalifika katika ubalozi na kutaka kumchukua kumpeleka kituo cha polisi. Lissu alibisha kwa kutaka kujua kosa lake na sababu ya kupelekwa kituoni.

Wakati wametaka kumuingiza kwenye gari, Naibu Balozi wa Ujerumani alitoka na kuwahoji waliokuwa wanataka kumchukua Lissu. Naibu balozi aliomba kama wanaweza kwenda na Lisu kwenye mahojiano ambapo waliotaka kumchukua walikubali, hivyo Naibu Balozi na Polisi na Lissu walienda wote kituoni na Naibu balozi aliuliza kuhusu muda watakao muhoji na kusubiri ili wakimaliza waondoke nae.

Baada ya majibizano, Naibu balozi alimuambia Lissu kuwa nchi hii sio salama hivyo wakampa makazi katika makazi ya ubalozi wa ujerumani. Alikaa hapo kwa siku nane akisaidiwa kupata vitu vyote vya safari ikiwemo Passport na VISA. Siku husika ya safari Naibu Balozi alimsindikiza Lissu hadi kwenye ndege ili kwenda Ujerumani kujificha






 
Kama mikutano ya hadhara ni fursa ya kufitinisha na kuchafua watu tunahaja ya kuangalia. Ila pia ni vizuri kuwapa fursa watu kutema sumu

View attachment 2508265
Kama siyo kweli. Waambie waunde Tume kuchunguza Jaribio la kumuua Lissu. Kuna vitu mnaponda kisiasa kupotosha ukweli. Hivi ulishawahi kujiuliza ni kwa nini hii kesi ya Lissu hakuna anayezungumza wala kuchunguza!?

Muacheni Lissu azungumze. Asipofanya hivyo kesi yake itasahaulika. Jinai haifi.
 
Yule diktetor bora alikufa
Iyo haitoshi afe tu tena huko kuzimu alipo asije kuwa reincarnated arudi duniani kama fisi na kuleta zahama na uhalifu aliofanya akiwa hai kama ubakaji, ushirikina, uonevu, uzinzi, uchawi, ufisadi, uporaji, ujambazi, ugaidi, uuaji, kuiba wake za watu name them all.

mkorinto Magonjwa Mtambuka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom