Tundu Lissu: Walimu wasisimamie uchaguzi

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
14,304
29,837
Amesema walimu wote niwaoga wanatishwa na kuperekeshwa na wakurugenzi kuiba kura za wananchi .

======

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema kabla ya Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ujao, kuna haja kufanya kila linalowezekana kubadili katiba ili kuwaondoa walimu kuusimamia.

Amesema mabadiliko wanayoyataka katika mfumo huo wa uchaguzi ni pamoja na kuhakikisha walimu na watumishi wengine wa serikali hawasimamii uchaguzi.

Lissu alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Shirati, mkoani Mara ikiwa ni mwendelezo wa mikutano ya chama hicho iliyopewa jina la Oparesheni +255#KatibaMpya inayofanywa na viongozi wakuu wa chama hicho nchi nzima.

“Pendekezo langu ni kwamba kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka ujao na kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, tufanye lolote linalowezekana tubadilishe Katiba na mfumo wa uchaguzi.

“Kama tusipofanya linalowezekana kuhakikisha kwamba walimu na watumishi wengine wa serikali hawasimamii uchaguzi tena kama ilivyo kwa nchi nyingine, na kama ambavyo imependekezwa na wasimamizi wa uchaguzi wa kimataifa ambao wanaangalia uchaguzi wetu, mjue kwamba uchaguzi huo utakuwa kama wa 2020.

“Tusipofanya linalowezekana kubadilisha Katiba na kuwa na Tume huru ya Uchaguzi badala ya hii iliyopo sasa, tujue yatatokea ya 2020. Tusipotengeneza sheria na Katiba inayokataza watu kupita bila kupingwa, mjue enguaengua haitoisha,” alisema.

Lissu alisema kudai Katiba Mpya pamoja na kubadilishwa mfumo wa uchaguzi ni jukumu la kila mtu na si la CHADEMA pekee.

“Lazima tulazimishe kufanyike mabadiliko katika eneo hili, na kama tusipolazimisha tumekwisha. Na hilo ni jukumu letu sote. Tutengeneze vuguvugu la kitaifa nchi nzima kuhakikisha hatuendi katika uchaguzi ujao bila Katiba Mpya.
 
Amesema walimu wote niwaoga wanatishwa na kuperekeshwa na wakurugenzi kuiba kura za wananchi View attachment 2743902
Ni kweli kabisa walimu ni waoga Sana Mimi nakumbuka wakati wa semina ya Sensa idadi kubwa ya wanasensa walikuwa walimu, tulikuwa tunaangushwa Sana kwenye madai mtu mwezi mzima hatujalipwa mkitaka kutoa malalamiko mnakuwa wachache Sana walimu ndiyo kabisa walikua wanatuhimiza tuvumilie tukama kulipwa tutalipwa ni watu wa ajabu Sana wamejengeka kisaikolojia kuvumilia Sana Kama mtumwa hawalalamiki waoga wa mwisho ktk watumishi nahisi ni kutokana na neno mwalimu anatakiwa awe mfano na mwenye tabia njema kwenye jamii
 
Amesema walimu wote niwaoga wanatishwa na kuperekeshwa na wakurugenzi kuiba kura za wananchi View attachment 2743902
Sio waoga, mkurugenzi ni mwajiri wao, wanaweza Je kukataa muongozo wao, hii ni Sawa na wakurugenzi kusimamia uchaguzi, wakati Raisi ndio boss Lao.. Wacha tuone kama hukumu Ya kesi ya Bob wang we iliyotolewa na mahakama ys Africa iliyokataa na juu Shauri serikali khbadili sheria ya uchaguzi na kuwa toa wakurugenzi itatejekezwa.
 
Kiukweli hii kada inashda sababu ni nying...
1. Weng wa walimu n kutoka familia maskin sana...kifikra na kiuchumi
2. Naunga mkono kwasababu ya protocol zao sjui n waoga sana kuchukua hatua mwalim anaweza kutembelewa na mkaguz wa kanda shulen sku hiyo hata mchana hatakula anatetemeka ...
3. Serikali kuna kipindi walikuwa wanachagua failure's ndoo wakasomee ualimu wale cream walikuwa wanaenda kupiga fani zenye mashko.

NB: nilialikwa kama mgen KAHAMA kumuaga mkuu wa shule flan hafla ilifanyikia sehem inaitwa NITESH aseeee jamaaa walimu wanagombana kisa soda na bia...nliondoka kabla hata nusu ya sherehe haijafka..
 
Apambane kwanza kuhakikisha Tume Huru ya Uchaguzi inapatikana kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, na ule mkuu wa 2025! Asisahau hii Tume ya sasa, watumishi wake wote wanateuliwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa!!

Hivyo tatizo la uchakachuaji wa matokeo kwenye uchaguzi, halisababishwi na walimu! Walimu hawatangazi matokeo ya uchaguzi! Walimu wanafanya kazi za Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa miaka mingi, na kwa uaminifu mkubwa!! Mbona hatusikii kelele za kutoka kwa wadau wa elimu?

Tatizo la kuchakachua matokeo kwenye uchaguzi linafanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuwaachia makada wa CCM (Wakurugenzi wa Halmashauri/Miji/Manispaa, nk pamoja na Wakuu wa Wilaya, Mikoa, nk kusimamia/kuingilia hilo zoezi!
 
Kiukweli hii kada inashda sababu ni nying...
1. Weng wa walimu n kutoka familia maskin sana...kifikra na kiuchumi
2. Naunga mkono kwasababu ya protocol zao sjui n waoga sana kuchukua hatua mwalim anaweza kutembelewa na mkaguz wa kanda shulen sku hiyo hata mchana hatakula anatetemeka ...
3. Serikali kuna kipindi walikuwa wanachagua failure's ndoo wakasomee ualimu wale cream walikuwa wanaenda kupiga fani zenye mashko.

NB: nilialikwa kama mgen KAHAMA kumuaga mkuu wa shule flan hafla ilifanyikia sehem inaitwa NITESH aseeee jamaaa walimu wanagombana kisa soda na bia...nliondoka kabla hata nusu ya sherehe haijafka..
Wew ni mpu.mbavu nani kakufundisha huo ujanja kama siyo walimu,Nani alikuwa anahimiza kupiga dawa vyoo vyenu vya shuleni ulipokojoa kwenye sakafu
 
Wew ni mpu.mbavu nani kakufundisha huo ujanja kama siyo walimu,Nani alikuwa anahimiza kupiga dawa vyoo vyenu vya shuleni ulipokojoa kwenye sakafu
Ww n falaaa sn jibu hoja unaleta hadith...za kichoko hapaa unagongwa ..kwann lisu hatak walim
..kwann walim wanazaraulika sn
..swala la kufundshwa sio hawa walim wa kileo mafala kama ww
 
Back
Top Bottom