Tundu Lissu atapewa" kesi ya kujibu

Tundu Lissu atapewa" kesi ya kujibu

Sioni kesi hapo.
Nadhani mkakati ni kwamba imeachiwa Mahakama ndiyo iamue.Wameona aibu kuondoa kesi kwa Nolle ili isionekane walimuonea.
 
Tafsiri ya maneno haya ya uasi ni nyumbufu mno kiasi cha kutoweza kumtia hatiani achilia mbali uwezekano wa kukubalika kama msingi wa kosa.
UASI- hauwezi kuwa UHAINi...

Ni vitu viwili tofauti... Tanzania tuna kamusi Maalum inatumika hata Mahakamani...

Shida inakuja Wapelelezi wetu wakati wanaanzisha kesi walikariri neno WAASI wa Congo.... Sasa wakajua ..huyu mtu tukimpeleka Mahakamani ushindi huu hapa.... Sasa hivi wameshakula shule ya kutosha na tafsiri ya Uasi wanaijuia vizuri kesi ikiwa Mahakamani
 
Baada ya kukubaliana namna ya kuondoa kesi na ili isionekane kuwa serikali alimbambikia kesi "atapewa" kesi ya kujibu kisha muda mfupi baada ya kuanza utetezi ndipo DPP ataleta ile "taarifa". (Rejea kesi ya FEM) Hii itawapa faraja kubwa wahafidhina kuwa pamoja na serikali kutoendelea na kesi mhaini alikutwa na kesi ya kujibu.
It doesn't work that way...

Scenario ya kesi hii Iko hivi:

Juma.Pumba .Maharage(JPM) amemshitaki mahakamani Makoye Membe Ng'wigulu kwa kosa la kumuibia baiskeli yake..

Mlalamikaji au mshitaki ata lay down kesi yake mbele ya mahakama na mwisho wa siku ataitoa hiyo baiskeli iliyoibiwa na kukamatwa kama ushahidi kuthibitisha maelezo yake..

Katika kuu - scrutinize huo ushahidi baadaye inagundulika receipt ya kielelezo hicho (baiskeli)kilicholetwa mahakamani kama ushahidi ina jina la Gigwa Pondamali Maige..

Kwa sbb hiyo tu, mtuhumiwa anapinga kupokelewa kwa kielelezo hicho kama ushahidi wa upande wa mashitaka. Mahakama inakubaliana na upande wa utetezi na kielelezo hicho kinakataliwa kuingizwa.

SWALI: Unafikiri Mahakama mwisho wa siku itaamua nini?

Obvious uamuzi utakuwa ni huu:

Upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kosa la mtuhumiwa kwa ushahidi ulio wazi. Kwa hiyo mahakama haijamwona mshitakiwa na kosa lolote. Mshitakiwa huna kosa, wewe ni mtu huru..!

Ndivyo ilivyo katika Shauri hili la uhaini kati ya Jamhuri vs Tundu Lissu kwa sbb:

1. Ushahidi mkuu (video clip ya JamboTV iwe upo kwenye flash disk au CD) ambayo ndiyo yenye maneno hayo yanaoitwa "uhaini" haipo mahakamani kwa kuwa ilikosa vigezo vya kisheria kuingia kama kielelezo cha ushahidi dhidi ya mtuhumiwa..!

Mtuhumiwa ajitetee kutokea wapi? Utetezi uwe ktk sababu hiyo ili akubali au akanushe???

2. Mashahidi wote 16 ukimwacha PW17 walidai kuhamasika kufanya uasi tokana na maneno ya mtuhumiwa. Lakini swali linabaki kuwa, hayo maneno yako wapi ili mahakama nayo iyasikie na iyapime kisheria ili Ione km yana elements za uhaini?

Jibu ni kuwa hayapo. Na kama hayapo mahakama itatumia ushahidi gani wa vielelezo vilivyobeba kosa (la kutamka maneno ya uhaini) ili kuiwezesha mahakama kujua iwapo mtuhumiwa hayo yanayodaiwa ni kosa la uhaini kweli ni kosa kwa kipimo cha sheria ya uhaini Ili ajitetee au ni blahblah tu za wahuni na hayawani wa CCM?

3. Upande wa mashitaka unamtegemea PW17 pekee aliyesema yeye alikuwepo siku mtuhumiwa akisema maneno na aliyarekodi. Lakini naye hajakitenda mahakamani kielelezo hicho, wanacho wao mpaka leo walipofunga ushahidi wao.

Sasa mahakama izingatie ushahidi upi ili imwone mtuhumiwa kuwa ana kesi ya kujibu?

Na hata ikisema mtuhumiwa ajitetee kwa kuwa ana kesi ya kujibu. Swali utetezi wake usimame ktk msingi upi ulio mbele ya mahakama?

Tundu Lissu aliuliza swali simple tu, kuwa, nijitetee kwa kipi hasa??

Sikiliza ndugu: HATA SAA MBOVU KUNA WAKATI HUONESHA MUDA SAHIHI KAMA SAA ILIYONZIMA!

Majaji hawa hawawezi ku - ruin reputation yao kwa kufanya maamuzi ya kijinga huku wakijuwa kwa uwazi kabisa kuwa wanadanganya..!
 
Muasi ili atimize lengo lake lazima atumie silaha za maangamizi vivyo hivyo kwa haini pia.
Soma tena, tope uliloandika kisha linganisha na silaha yoyote aliyonayo Lissu ili kuthibitisha uhaini wake.

Kabla ya kuandika weka kadi ya CCM kando, halafu tumia ubongo na vidole kuandika. Hapa umetumia vidole tu, ubongo umeuacha wapi, utajua mwenyewe.
 
Baada ya kukubaliana namna ya kuondoa kesi na ili isionekane kuwa serikali alimbambikia kesi "atapewa" kesi ya kujibu kisha muda mfupi baada ya kuanza utetezi ndipo DPP ataleta ile "taarifa". (Rejea kesi ya FEM) Hii itawapa faraja kubwa wahafidhina kuwa pamoja na serikali kutoendelea na kesi mhaini alikutwa na kesi ya kujibu.
Jamaa wanaendesha kesi kwa mipango thabiti..hawakurupuki, wakiamua iende hivi inaenda na wakiamua iwe hivi inakuwa. TL anapambana na watu wamipango, wao ndo wameamua wamshahidi waishie idadi hiyo na sikiliza hiyo tarehe 21, TL atakutwa na kesi ya kujibu..kila kitu kipo mikononi mwao,dunia haina HAKI!! TUOMBE IWE JUU YA MIPANGO YAO!
 
Jamaa wanaendesha kesi kwa mipango thabiti..hawakurupuki, wakiamua iende hivi inaenda na wakiamua iwe hivi inakuwa. TL anapambana na watu wamipango, wao ndo wameamua wamshahidi waishie idadi hiyo na sikiliza hiyo tarehe 21, TL atakutwa na kesi ya kujibu..kila kitu kipo mikononi mwao,dunia haina HAKI!! TUOMBE IWE JUU YA MIPANGO YAO!
Inajulikana ni kesi ya kupangwa, na sio jinai, uhaini, ugaidi wala uasi au uvunjifu wowote wa sheria.

Swali ni: Je, mipango yao ikikwama,, nini kinatokea, watumie nguvu ya mipango, (dictatorship) au nguvu ya sheria (judiciary decisions) ?
 
Lissu anaingie kwenye Magwiji watatu wa Sheria kwenye Hii nchi..

LISSU NI BINGWA WA MASUALA YA KISHERIA YUPO MBALI MNO.
USIMLINGANISHE NA MBOWE MLEVI YULE.
 
Inajulikana ni kesi ya kupangwa, na sio jinai, uhaini, ugaidi wala uasi au uvunjifu wowote wa sheria.

Swali ni: Je, mipango yao ikikwama,, nini kinatokea, watumie nguvu ya mipango, (dictatorship) au nguvu ya sheria (judiciary decisions) ?
Mkuu, mimi nafatilia kesi ila si mtu wa sheria kwkweli..mengi nayasikia na tafsiri za kisheria baada ya kesi ila mwisho kwa maoni yangu ataachiwa ila nadhani itakuwa nje ya calenda ya yote. Kama ataachiwa basi kuna vitu watakuwa wamevipanga kuhakikisha jamaa hatambi jukwaa lolote. TL huwa anatamba nje tu ya mahakama akishinda kesi...huu mwiba hawautaki Kijani maana utabadiri mengi. Ikiisha hii watamrudisha ndani kwa kesi nyingine, tume ya bimkubwq bado ipo!!
 
Pale anaenda kujibu nini? Bila mabadiliko hamna uchaguzi? Kushinikiza mabadiliko ya sheria ndiyo kuitisha Serikali? Au anaenda kujibu kitu gani hasa?
Ataenda kujibu jinsi yeye,mtu mmoja,alivyotaka kufanya uhaini peke yake.
 
Kwa sababu jumuia ya kimataifa imepiga kelele sana huenda ikawa dismissed case!
 
Uchochezi wa kufanya uhaini, Uchochezi ni sentensi ambayo haijitoshelezi lazima iambatane na vishazi saidizi,
So kwa kufupisha, lissu alichochea uhaini.
Nimecheka kwa nguvu, vilaza wa ccm bana, mna mashahidi zaidi ya 30 wanaongea utoto mtupu. Ni vile mahakama ni za ccm, vinginevyo saa hii mngekuwa kwenye mchakato wa kumlipa fidia.
 
Back
Top Bottom