Uchaguzi 2020 Tundu Lissu anaanza kutumia lugha chafu

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,750
4,958
Ukisikiliza Hotuba zake za Kagera, utaona TL anaanza kutumia lugha chafu na za kichochezi.

Lissu amekuwa na mvuto, sijui kwanini ameanza kujiletea utata kwa matusi na tuhuma asizo na ushahidi nazo, Amemwiita Rais Magufuli Mwizi pamoja na MaRais wote waliopita isipokuwa Nyerere.

Yeye ni mwana Sheria na anajua mafunzo yake ya sheria yanasema " INNOCENT UNTIL PROVEN GUILTY", sasa sijui ni sheria gani anayoitumia kuwaita waheshimiwa hawa wezi, na kama anao ushahidi kama ni wezi, kwa nini asiwafungulie kesi na iwapo mahakama itawahukumu, basi hata sie tutakuwa na haki ya kuwaita wezi.

Lissu anazungumzia HAKI, na anailaumu awamu hii kuwa haitendi haki. Jee yeye hapa anatenda haki?? TL Practice what you preach
 
Dawa imewaingia eeeh? Ndo mana tunataka tubadirishe mfumo wa utawala wa nchi hii maana nchi hii sasa kwa mfumo huu viongozi pekee ndo watakaokuwa na ukwasi wa kutisha huku wananchi wengi wakiwa masikini wa kutupwa.

Ndo mana CCM mnalishwa matango pori kukataa mfumo mpya wa utawala wa nchi hii maana viongozi wetu wa sasa wanatumia mfumo huu huu kutubabua vibaya sana!

Mwambieni Magufuli arudishe ardhi ya watu aliyopora na kujianzishia ranch.
Dawa yenu ni October 28 tu!
 
Hata Mimi nimeshangaa kuna mahala anatumia lugha ambayo haipaswi kutolewa na mtu anayegombea nafasi muhimu kama hii.Wale viongozi wawili wa dini ina maana hawamshauri? Hata kumuita mgombea mwenzake "jiwe" I don't think it is fair. Pia sioni kama anawanadi vizuri wagombea udiwani.
 
Kuna vitu vengine ata km shule ukwenda unaona kabisa live.

Kuna ile michango ya tetemeko la ardh kagera nchi za ulaya zilichanga zaid ya bilion 900 kuchangia ile adha lkn mshikaji alichokifanya dah na kuna zile billion 200 alizoleta bill gates km msaada za zenyewe hazielewek zilienda wap hii ndo raha ya kuongoza nch yenye katiba mbovu kuna mmoja anakuwa na nguvu mno ata mawaziri.mahakama.bunge hawamuwez maana uko kote yy ana familia majaji na mawazir anateua yy na kwann mawazir wawe wabunge apo sasa uko bungen ni ubabe na dharau inafika wakati aya bunge watu tunalidharau kwa kupitisha sheria mbovu kumbe tatizo sio km wabunge akili hawana NOO tatizo ni mfumo kuna jamaa mmoja upo sehemu anawalazimisha wafanye anavyotaka

Ebu chek kule afrika ya kusin yule jamaa alipoona kule katiba kali sn bunge lipo huru mahakama ipo huru na mfumo haumbebi akamua kuingia chaka akacheza dili bank zimsaidia kuiba bado akadakwa na kizimban kapandisha sasa apo kwetu mjomba kwa katiba hii lazima anateua mpaka CAG na GAVANA WA BOT dili zinapigwa pale pale benk kuu wale hamba kucheza dili na CRDB wala TPB pale pale benk kuu watu wanamalizana

Nch km hz ukombolewa kwa maandamano kuipinga katiba na utawala mbovu jambo ambalo hupelekea serikali kupiga raia na kutokea ghasia kisha UMOJA WA MATAIFA na NCH ZENYE NGUVU pamoja ns nchi jiran kuingilia na kuifokea serikal na serikal ikaufyata ktk ikabadilishwa na mchakato wote ukasimamiwa na UN

Kwisha habar yao

Kutumia uchaguz kuipindua serikali hii ni kupoteza mda hawawez kukubal maana uko kwenye familia zao ni full raha asubuh supu ya kuku na mchana ni main ucku n chiken wings leo hii waipe upinzan nchi ili waanze kula maandaz ya mabahresa hawawez kukubal narudia tena hawawez kukubali
 
Ukisikiliza Hotuba zake za Kagera, utaona TL anaanza kutumia lugha chafu na za kichochezi.

Lissu amekuwa na mvuto, sijui kwanini ameanza kujiletea utata kwa matusi na tuhuma asizo na ushahidi nazo, Amemwiita Raisi Magufuli Mwizi pamoja na MaRaisi wote waliopita isipokuwa Nyerere. Yeye ni mwana Sheria na anajua mafunzo yake ya sheria yanasema " INNOCENT UNTIL PROVEN GUILTY", sasa sijui ni sheria gani anayoitumia kuwaita waheshimiwa hawa wezi, na kama anao ushahidi kama ni wezi, kwa nini asiwafungulie kesi na iwapo mahakama itawahukumu, basi hata sie tutakuwa na haki ya kuwaita wezi.

Lissu anazungumzia HAKI, na anailaumu awamu hii kuwa haitendi haki. Jee yeye hapa anatenda haki?? TL Practice what you preach
Ungeanza kueleza hoja ya Lisu kabla hajahitimisha kwa kauli hiyo.
 
Ukisikiliza Hotuba zake za Kagera, utaona TL anaanza kutumia lugha chafu na za kichochezi.

Lissu amekuwa na mvuto, sijui kwanini ameanza kujiletea utata kwa matusi na tuhuma asizo na ushahidi nazo, Amemwiita Raisi Magufuli Mwizi pamoja na MaRaisi wote waliopita isipokuwa Nyerere. Yeye ni mwana Sheria na anajua mafunzo yake ya sheria yanasema " INNOCENT UNTIL PROVEN GUILTY", sasa sijui ni sheria gani anayoitumia kuwaita waheshimiwa hawa wezi, na kama anao ushahidi kama ni wezi, kwa nini asiwafungulie kesi na iwapo mahakama itawahukumu, basi hata sie tutakuwa na haki ya kuwaita wezi.

Lissu anazungumzia HAKI, na anailaumu awamu hii kuwa haitendi haki. Jee yeye hapa anatenda haki?? TL Practice what you preach
Niambie TRION 1.7 ZIKO WAPI?? KWANINI CAG ANAZUILIWA KUKAGUA NDEGE MANUNUZI??🤣🤣🤣 AMA KWELI UJINGA NI MZIGO
 
Kuna masheikh wako jela miaka 7 sasa, mbona serikali imeshindwa kupeleka ushahidi mahakamani?

Wafanyabiashara wanabambikiziwa kodi ili kuwatemesha mpunga

Wamachinga wamewekewa vitambulisho feki ili wacheue elfu ishirini-ishirini

Ndege zimenunuliwa bila kufuata sheria za manunuzi ya umma na hakuna ruhusa CAG kukagua.

Huo kama siyo upigaji ni nini?

Pia, kama wamejimilikisha mahekari ya ardhi za wananchi wazirudishe tutatue migogoro ya wakulima na wafugaji!. Wananchi wanahitaji ardhi.

Lissu katueleza wazi:

1. AHM ana maelfu ya ardhi huko Morogoro
2. FTS ana maelfu ya heka za ardhi huko Morogoro
3. BWM ana maelfu ya heka za ardhi huko morogoro
4. Jiwe kajimilikisha ranchi ya huko Karagwe na maelfu ya heka za ardhi

Hawa wanajiita wajamaa kumbe makabaila wakubwa.

Wazirudishe tu ardhi za wananchi maana hamna namna!
 
Hata Mimi nimeshangaa kuna mahala anatumia lugha ambayo haipaswi kutolewa na mtu anayegombea nafasi muhimu kama hii.Wale viongozi wawili wa dini ina maana hawamshauri? Hata kumuita mgombea mwenzake "jiwe" I don't think it is fair.Pia sioni kama anawanadi vizuri wagombea udiwani.
Wakati Magufuli anajibatiza jina la Jiwe wewe ulikuwa kuzimu?
 
Tundu Lissu shikilia hapo hapo baba - MATAGA washaanza kulia huku.

sisi wapiga kura tunakuelewa sana.

mtu ambaye anachagua maeneo ya CAG kukagua na kutokaguliwa tumwiteje kwa mfano?

halafu mara paap - intaneshono eapoti imejengwa kijijini ilhali haikuwepo hata kwenye mipango yetu wananchi.

piga spana Lissu, pigaaa!
 
Back
Top Bottom