Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeo (Chadema), Tundu Antiphas Lissu, leo Jumatatu, Agosti 10, 2020 amefanya Misa ya Shukrani kwenye kanisa la Mtakatifu Rita wa Kashia lililopo Ikungi, jimboni kwake Singida Mashariki.
Kwenye Misa hiyo iliyoongozwa na Paroko Laurent Bahale, Mheshimiwa Lissu amewashukuru Watanzania kwa kumuombea alipokuwa mgonjwa mpaka sasa alipopona kabisa.
“Nichukue fursa hii kuwashukuru Watanzania wote kwa dini zao kwa kuniombea wakati nilipokuwa mahututi, nilipopata nafuu mpaka nilipopona kabisa"
“Mungu wetu ni wa ajabu. Amesikia sala zenu na leo nipo nanyi mzima wa afya tayari kutekeleza kazi iliyosalia. Niliumizwa sana ndugu zangu. Wiki mbili za mwanzo baada ya kushambuliwa nilipata maumivu makali ambayo sikuwahi kuhadithiwa. Mwili ulikuwa unawaka moto. Naahidi sitampitisha mtu yeyote kwenye maumivu yale niliyoyapata hata kama atakuwa amenikosea kwa kiwango gani” alisema Mheshimiwa Lissu
Kwenye Misa hiyo, mheshimiwa Lissu aliongozana na mgombea mwenza, Mheshimiwa Salum Mwalim ambao juzi Jumamosi, Agosti 8 walichukua fomu ya kugombea Urais kupitia Chadema.
Imetolewa leo Jumatatu, Agosti 10, 2020