Tundu Lissu aendelea kushikiliwa na polisi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Polisi kanda maalum ya Dar es salaam walikwenda nyumbani kwa Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kufanya upekuzi baada ya Tundu kushikiliwa toka jana.

Baada ya kurudishwa kituo kikuu cha Polisi kati Dar es salaam kilichokua kinasubiriwa ni kama Tundu Lissu ataachiwa kwa dhamana ambapo mpaka jioni hii siku ikielekea kuisha CHADEMA imeeleza walipofikia.

Taarifa iliyotolewa na CHADEMA leo imesema >>> “Jitihada za kuhakikisha Lissu anapata haki yake ya kisheria ya dhamana leo zimeshindikana hivyo bado yuko chini ya Polisi kituo kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam”

“Tunasubiri utaratibu mwingine kesho wa ama kupata dhamana akiwa mikononi mwa polisi au kufikishwa Mahakamani” imeeleza taarifa ya CHADEMA

Chanzo:
Millard Ayo
 
Kama haongei wanamshikilia wa nini sasa kama si misifa tu. Basi tu kujionyesha wako kazini. Kama ni kujipanga naamini Lissu alishajipanga. So awe ndani ama nje, mahakamani anajuwa cha kufanya. Kisheria hawaruhusiwi kumshikilia zaidi ya masaa 48 bila kumfungulia mashtaka. Polisi huwa wanavunja hii sheria kibabe tu. Ninaamini wanatakiwa waeleze mahakamani kwanini wamemshikilia mtuhumiwa kwa muda mrefu kinyume cha sheria bila kumfikisha mahakamani.
 
Tumeishi kwenye chuki na visasi toka awamu ya tatu hadi Leo vinaendelezwa.

Watawala wenye viburi,kujiona ,wezi,mafisadi na wabadhirifu.

Watawala wasio na hata lepe la huruma kwa raia wake.

Watawala wasio na hata hekima na Busara.Wako kwa ajili moja tu kujilimbikizia mali.
 
Ha ha ha, sasa mbona Lisu (mzalendo) aliwaramba miguu hao wazungu na kuwasihi wakate misaada?

Ulimuona akiramba hiyo miguu??Miaka 55 chini ya CCM Taifa ni masikini kupindukia.Mijitu isiyo na akili inadhani Lissu ndiyo sababu.

Watawala majizi ndiyo yanayopigiwa makofi.

wanakubali kutumiwa na mitawala mijizi,mibovu,kupita kiasi kwa ajili ya kushibisha tumbo.

Siku mijitu kama hii ikipata akili ndipo tutapata maendeleo.

Na alaaniwe yeyote aliyechagua hiki Kituko kututawala
 
Nchi imekua ya hovyo sana, inaendeshwa hovyo hovyo. Huyu Yohana anavuruga nchi, anafarakanisha taifa, anajenga chuki kwenye jamii. Wananchi wana manung'uniko, hawana furaha.

Watanzania
tuna bahati mbaya sana.
Umevurugwa wewe ulikuwa umezoea madili sisi wenzio tunapiga kazi na tunapata pesa ya kutosha kuendesha maisha. Wewe si ulizoea maisha ya mkato basi endelea kusoma namba!
 
muona akiramba hiyo miguu??Miaka 55 chini ya CCM Taifa ni masikini kupindukia.Mijitu isiyo na akili unadhani Lissu ndiyo sababu.

Watawala majizi ndiyo yanayopigiwa makofi.

Wapumbavu wanakubali kutumia na mitawala mijizi,mibovu,kupita kiasi kwa ajili ya kushibisha tumbo.

Siku mijitu kama hii ikipata akili ndipo tutapata maendeleo.

Na alaaniwe yeyote aliyechagua hiki Kituko kututawala
Masikini ni wewe unayesubiri serikali ikuletee maendeleo. Badili piga kazi mkuu acha udaku haulipi
 
Kama haongei wanamshikilia wa nini sasa kama si misifa tu. Basi tu kujionyesha wako kazini. Kama ni kujipanga naamini Lissu alishajipanga. So awe ndani ama nje, mahakamani anajuwa cha kufanya. Kisheria hawaruhusiwi kumshikilia zaidi ya masaa 48 bila kumfungulia mashtaka. Polisi huwa wanavunja hii sheria kibabe tu. Ninaamini wanatakiwa waeleze mahakamani kwanini wamemshikilia mtuhumiwa kwa muda mrefu kinyume cha sheria bila kumfikisha mahakamani.
Kuna makosa hata mwaka unakaa ndani wewe!
 
Tundu ni 'unbitabo' wakimweka selo huwa anasikiliza maabusu na kujua namna haki inavyopindishwa ya kufikishwa mahakaman kwa mtuhumiwa baada ya mufa fulan kupita tangu akamatwe. naimani wanampa nafasi ya kueneza uharakati mahabusu na magereza. mtaja sikia kitakachotokea ktk magereza yetu baada ya miaka kadhaa kupita. kunawatu wana miaka ndani na hakuna kinachoendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom