Tundu Lissu acha utoto, jaribu kuvaa viatu vya Mandela na Martin Luther King

Binafsi nimeelewa concern yako japo waliocomment baada yako wanajaribu kukulazimisha uwe CCM kama wao, ni kweli hata Mimi sikisikia msamaha wa moja kwa moja toka kwa Lissu kitu ambacho kilikuwa muhimu sana kukiweka katika lugha nyepesi.
Lakini Lissu Jana kaongea mambo mawili makubwa;

1.Anaipenda nchi yake sana, alitamani kuibusu ardhi ya nchi yake akiwa amepiga magoti lakini goti lake moja halikunjiki kabisa

2.Alitambua Taifa liko kwenye msiba mkubwa wa kumpoteza Mwenyekiti mstaafu wa Chama tawala, Rais mstaafu na Amiri jeshi kwa miaka kumi.

3.Alimtambua mkuu wa nchi wa sasa na kumpa heshima yake na pole kwa msiba wa mtagulizi wake.

4.Amewahimiza watanzania kutumia msiba wa Rais wao kuwa wamoja na kuwataka kesho (Leo) wajitokeze uwanja wa Taifa kutoa heshima za mwisho kwa mtiwa mafuta wa nchi.

5.Ameeleza chanzo cha tatizo lake kitu ambacho hata Mandela alikieleza na ndo maana amewataja wahanga wenzie kina Azory Gwanda, Mawazo, Akwilina na Ben kwa uchache.

6.Ameeleza uminywaji wa haki ya kujieleza kama chanzo cha madhila yake. Kwa hili hujatenda haki kufananisha scinerio ya Jana kwa Lissu kuwekewa mike nyingi na uminywaji wa haki ya habari. Hapa umejifanya kipofu lakini hata wewe unajua Uhuru wa habari umetikiswa.

7.Kwa mtu smart Jana haikuwa siku ya kuongelea tatizo la korosho na mishahara ya watumishi, usichanganye mambo muda wake bado.
 
Mtu kafika siku ya kwanza tu unataka azungumzie korosho??? Unataka azungumzie uchumi??? Wakati ndo amefika kwa mara ya kwanza nchini kwake alipoondoka karibu miaka 3 iliyopita akiwa nusu mfu!!!

Jana hotuba ya Lissu ilikuwa ni kuwashukuru Watanzania na kuwaeleza ni kwa jinsi gani CCM mlivyomfanyia next phase ni kuanza kuelezea watanzania Kwa nini anataka kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania hapo October 2020 ambapo ataelezea sera zake na mikakati yake pamoja na Chama chake.

CCM tulieni tu dawa ziwaingie. Ndo kwanza kumekucha
 
Binafsi nimeelewa concern yako japo waliocomment baada yako wanajaribu kukulazimisha uwe CCM kama wao, ni kweli hata Mimi sikisikia msamaha wa moja kwa moja toka kwa Lissu kitu ambacho kilikuwa muhimu sana kukiweka katika lugha nyepesi.
Lakini Lissu Jana kaongea mambo mawili makubwa;
1.Anaipenda nchi yake sana, alitamani kuibusu ardhi ya nchi yake akiwa amepiga magoti lakini goti lake moja halikunjiki kabisa
2.Alitambua Taifa liko kwenye msiba mkubwa wa kumpoteza Mwenyekiti mstaafu wa Chama tawala, Rais mstaafu na Amiri jeshi kwa miaka kumi.
3.Alimtambua mkuu wa nchi wa sasa na kumpa heshima yake na pole kwa msiba wa mtagulizi wake.
4.Amewahimiza watanzania kutumia msiba wa Rais wao kuwa wamoja na kuwataka kesho (Leo) wajitokeze uwanja wa Taifa kutoa heshima za mwisho kwa mtiwa mafuta wa nchi.
5.Ameeleza chanzo cha tatizo lake kitu ambacho hata Mandela alikieleza na ndo maana amewataja wahanga wenzie kina Azory Gwanda, Mawazo, Akwilina na Ben kwa uchache.
6.Ameeleza uminywaji wa haki ya kujieleza kama chanzo cha madhila yake. Kwa hili hujatenda haki kufananisha scinerio ya Jana kwa Lissu kuwekewa mike nyingi na uminywaji wa haki ya habari. Hapa umejifanya kipofu lakini hata wewe unajua Uhuru wa habari umetikiswa.
7.Kwa mtu smart Jana haikuwa siku ya kuongelea tatizo la korosho na mishahara ya watumishi, usichanganye mambo muda wake bado.
Safi sana, kwa kifupi jana hao kuwa siku ya kuelezea sera. Ilikuwa siku ya mapokezi na Lisse kwa jana tu ameongea kila kitu kilichotakiwa kusikiwa Jana na watanzania
 
Alipoanza kuhutubia alisema. Nanukuu "hiki ni kipindi cha maneno mengi, lakini mimi nitaongea machache".


Ukiitazama hii kauli unaona kabisa lisdu kapangilia mfumo wa speech zake. Leo kawashuhudia watanzania yaliyomkuta na kumshukuru Mungu kwa muujiza wake ndio maana amesisitiza sana "Mungu ni mwema".

Wewe leo hii unamdharau na kumtaka ajikite kwenye hotuba za maendeleo.

Huo sio muda wake, ataongea sana mbeleni. Punguzeni jaziba jamani. Hamna hata chembe za upendo mpaka mmekalia kumsema jamaa.

Najua mmeumia sana kuona mategemeo yenu yameenda kinyume. Mmliwaaminusha wengi kwamba CHADEMA imekufa. Leo mmeona. Just imagine polisi wasingetoa tamko la kuzuia watakaompokea lissu

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app

Ubaya mnakosea Sana kuweka ushabiki kindaki kwenye siasa. Lazima apange vizuri speech zake. Hayo Mateso anayosimulia yasiwe head of story. Anaweza akadokeza tu kwenye kuimalisha umoja na mshikamano wa taifa. Kuna kero kibao Kama kiongozi hatakiwi kusemea kero zake na chama chake tu Bali kero za watanzania wote
 
Japo mimi huwa natofautiana na ww mara nyingi, lakini hapa nakuunga kwa ushauri wako huu kwa Lissu. Ni kweli Lissu ana mtaji mkubwa wa watu, ni vyema cdm, na sisi wafuasi wake tumshauri namna nzuri ya kuutumia mtaji huu wa watu.

Wakati huu ni wakati sahihi kabisa wa yeye kujikita katika siasa za maendeleo ya watu, kuliko mateso yake binafsi kwani yameshatokea. Anapaswa kuwa mkombozi wa kweli wa watu katika mustakabali wa maisha yao, hivyo anapaswa kila akiongea aondoe taswira ya kuwa hana simile na yoyote, bali aongee kama mkombozi wa watu kwenye shida zao kimaisha.

Nawashauri sana wapinzani tumshauti Lisu atumie shambulio lake kwa njia chanya kuliko njia hasi, maana asipoangalia kwa huu ushawishi wake, anaweza kuliingiza taifa hili katika machafuko. Bado cdm tunaweza kuwashinda kabisa ccm kwa hoja positive, kuliko hoja za uhasama. Hili ni jukumu letu wapinzani bila kuona aibu.
Muda bado, ukifika hata nyie mtafurah, mtu hata hajaoga bado mnataka kusikia aseme mnachotaka ninyi?

Ushaur wng ni kwamba chama kihakikishe Nyumba anayo lala lisu Na popote atakapo kuwa kuwe na ulinzi wa kutosha. Ili wakizingua safari hii tugawane mbao
 
Beba msalaba wa Lisu kama utauweza
Binafsi sikutegemea nisikie kingine chochote ni ‘one trick pony’ baada ya hadithi wa mkasa wake ambao tushasikia mara 1000 akaja na mambo ya ukandamizaji wa vyombo vya habari wakati mbele yake kajaziwa mic za vyombo mbalimbali mpaka kimataifa he has no ‘tricks left up his sleeves’.

Poor Lissu
 
Wahusika waliomfunga na kumtesa Mandela walishugulikiwa!??. Njia ya kuiponya nchi na nafsi NI msamaha na visasi havina nafasi kabisa. Atawasha Moto usiozimika

Namna ya kuiponya nchi ni wale waliomtendea unyama Lissu, wafikishwe kwenye mkono wa sheria za nchi na sheria ichukue mkondo wake.

Alichofanyiwa Lissu ni crime, na crime haiondoki kwa aliyetendewa crime kusamehe.

Mandela alifungwa Jela kupitia kortini, hakuna mahali popote Mandela alipigwa risasi ili auwawe.

Kama kusamehe Mandela angemsamehe nani, Korti iliyomfunga miaka 27 au?

Mimi nasema hivi, Lissu aendelee kuelezea mkasa wake hadi wananchi huko vijijini waelewe unyama wa tawala za kikatili.

Human rights na right to live ni mambo ya kikatiba na ni lazima yaelezwe kwa wananchi ili wayaelewe na wayashike kwelikweli.

Mbona CCM wanawatendea wananchi mambo ya kihuni lakini huwa hawaachi kuimba habari za amani utulivu na mshikamano, umewahi wewe kuchoka hizo meseji za amani utulivu na mshikamano, zinazoimbwa na kurudiwa kila wakati?
 
Kila mtu ameumbwa kivyake, si lazima afuate hao unaowasema. Wewe kubali upigwe risasi moja tu ndo ufanye hayo ya ukubwa, ya Mandela, ya Martine Luther.
Unazungumzia lisasi kwa huyo mboga mboga achomwe na msumari tu uone atakavyojidekeza hospital hadi uji atashindwa kunywa kwa madai ya kuhisi maumivu makali mwilini.
 
Kama wewe unajikata na wembe tu unampigia yule kimada wako, unatangazia rafiki zako mwezi mzima!! Ijekuwa TL aliyenusuruka kifo kwakupigwa risasi 16??. Hebu muache aseme analoweza kusema maana uwepo wake nikuushudia ukuu wa Mungu juu yake, usimpangie Cha kusema Mambo yanayohusu sera na mienendo ya kiuchaguzi muda wake upo.
 
Asipohubiri thamani ya haki ya kuishi, akahubiri tu unayoona ni ya maana kwako ni bure!
Uchumi usiwe kigezo cha kuchinja watu hovyo!
Uchumi wenyewe upo wap ni danganya toto hapo mabeberu yana set gap tu tujione tupo sehemu flani na kutuweka kwenye 18 zao tukiingia king tu tunakuwa kama Zimbabwe

We huoni kuwa uchumi wa kati wa chini kulivyoshangiliwa na watawala ndivyo mabepari walitaka iwe hivyo, lkn amini nakuambia wana ajenda yao sio bure time will tell
 
Unataka aseme hayo kwani Lissu kashapitishwa na chama chake kua mgombea rasmi wa kiti cha urais.na je kampeni zimeanza ili anadi sera zake?.Naamini yote hayo bado sasa kwanini unakimbilia mambo.Sasa hivi ni muda wake wakuongea madhila yaliyomkuta ayo mengine yana muda na wakati wake endapo atapata wasaa.
 
Tatizo ni kwamba tumeishikia sana hiyo story.
Weka story yako ya maana kuliko hiyo watu wakuelewe na kukufuata !!. Siyo kudharau ambacho huwezi kukifanya. Huwezi ,

Ndiyo kwanza kaingia na jana hiyo wananchi kabla walipigwa mkwara wasiende kumpokea . Hiyo yote hukuona kama kasoro ya kuzungumzwa hapo !!
 
Unasema Unataka Lissu ahubiri Amani na Upendo kwa Watesi wake....Labda tuanzie hapo, Watesi wake ni akina nani hata wewe uwaonee huruma na kuwaombea Msamaha?
 
Ndio amefika tu na amechoka kwa safari ndefu bado hajaongea lolote kubwa tumwache ajipange kuna mengi yanakuja.
 
Back
Top Bottom