Tundu Lissu acha utoto, jaribu kuvaa viatu vya Mandela na Martin Luther King

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,079
2,000
Baada ya kutua nchini umeongea vitu vingi Sana. Lakini vya habari vimekosa chochote Cha kusimulia kwenye alichoutubia zaidi ya kuripoti umekuja tu.

Mandela baada ya Mateso yote jela, baridi, fimbo na minyororo alipotoka tu aliendelea kuhubiri Amani, umoja na kuaminiana Kati ya watesi wake Wazungu. Umoja na msamaha utakujenga Sana bro acha utoto kabisa. Nazani angeanza kutaja majina ya waliouliwa na makaburu asingemaliza vya kuongea. Kama angesimulia Mateso ya jela sijui angesema vitu gani.

Katikati ya ubaguzi, Mateso na shida kwa jamii ya weusi martini alihubiri upendo, umoja na msamaha. Kudai haki bila kuhubiri chuki zidi ya watesi wake ndio njia pekee ya Mungu kumuinua mja wake. Ukifeli hapo Mungu ashindwi kukuacha upotee kabisa.

Sijapenda kabisa ulichokisema leo. NI chuki,Ujinga na Nini sijui.

Tundu Kama ukizunguka kuhubiri tu siasa za chuki, uchonganishi na uzandiki na kusaahau kuangalia msoto walinao wakulima na wafanyakazi na kufanya tafiti na kuja na Majibu ya kero zao.

Tundu Kama utahubiri muda wote vidonda na makovu yasitibika tu habari za saa nane na gwanda tu na ukaacha habari za korosho, mpunga, pamba ,buni Basi unacho Cha kujibu juu ya Mungu. Utakuwa mbinafsi na unataka uraisi kwaajili ya kulipiza kisasi. Huna la kutufanyia kwenye uchumi wetu, huna la kuwafanyia wakulima wetu. Huna la kuwafanyia wafanyakazi wetu. NI visasi tu. Hutajenga utavuruga nchi na kutuacha kwenye chuki Kati ya CCM na upinzani.

Utakuwa unatofautiana Nini na watesi wako. Mandela alisema ukitaka kuwa kiongozi Cha kwanza Zuia chuki na hasira. Chuki na hasira huzuia uwezo wa kufikiria.


Najua uliteseka, najua unamaumivu Ila hutakiwi kutugawa Tena. Acha kauli za masisiemu. Ubiri upendo, msamaha na uoneshe ukomavu.

Watanzania wanamengi ya kusemewa. Usiwe mbinafsi kabisa. Utapata kura za kutosha ukisimama na hoja za kutujenga na so kutugawa.

Hivi jeshi litakuamini vipi kwa mitazamo hii. Usalama watakuamini vipi. Weka njia ya msamaha na malidhiano acha utoto kabisa. Ndio maono haya uliyokuja nayo.

Mazao ya Pamba,. Alizeti, tumbaku na kahawa za korosho, Yana hoja nyingi sana. Fanya utafiti mje na suluhu. Watumishi Wana yao mengi.
Jenga Sera.
Usikubali kuharibu. Ongelea shida za majolity. Usiue malengo yako na taifa kwa hasira na chuki Kama Patrice Lumuba.

Patrice Lumumba baada ya CONGO DRC kupewa Uhuru alipewa nafasi ya kutoa hotuba. Hotuba yake ilikuwa yakijinga Sana Kama yako ya Jana. Aliwatusi watesi wake,Hakuhubiri msamaha ata kidogo. Alishindwa kutambua hata kidogo mbeligiji alichokiacha Kongo. Akataka kufanya visasi na chuki.kilichotokea baada ya hotuba yake NI machafuko na vurugu. Hotuba yake Kama ilivyo ya lissu ya Jana ilishangiliwa na wananchi wengi kwasababu ya umbumbu wao. Kwa hotuba ya Jana inahitaji kushinda kwa asilimia zaidi ya 80 labda ndio upewe nchi. Nani amkabidhi Rungu adui. Hotuba ya Patrice Lumumba ilikuwa ndio kifo chake, hotuba ya Patrice Lumumba iliicha Kongo kwenye Vita na machafuko Hadi leo. Hotuba ya Lumumba ndio sababu ya wazungu kutuona hatuwezi kujitawala.

Zuia chuki na visasi. Hubiri upendo na umoja. Nazani Mungu na akubarik I.
 

Shehullohi

JF-Expert Member
Jul 21, 2020
1,670
2,000
Angalau leo kujua Neno la Mungu wetu ni mwema.

Katolea mfano wa Mandela. Kifo na usingizi. Mandela hakuwahi kufikiria kuwa wakilisha makaburu ili kuwasaidia kushinda kesi za ubaguzi dhidi ya weusi wa SA.

Yeye kasahau kuwa alikuwa akiwaomba Barrick/Accasia awe wakili wao. Kabagua Wapemba katika speech yake. Ana chezeshachezesha sana kichwa akiongea. Ashauriwe atubu hakuna namna. Dhambi ile ya kuwalaghai wananchi waandamane bila utaratibu na utii wa sheria bila shuruti, wapambane na vyombo vya Dola na wakapata madhila mbalimbali haita waacha salama. Wana watumia wananchi ili kutimiza malengo yao ya kubadili gia angani hawako salama labda watubu na wajutie Maovu yao kwa kumaanisha.
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,752
2,000
Binafsi sikutegemea nisikie kingine chochote ni ‘one trick pony’ baada ya hadithi wa mkasa wake ambao tushasikia mara 1000 akaja na mambo ya ukandamizaji wa vyombo vya habari wakati mbele yake kajaziwa mic za vyombo mbalimbali mpaka kimataifa he has no ‘tricks left up his sleeves’.

Poor Lissu
 

Boeing 757

JF-Expert Member
May 18, 2020
291
1,000
Binafsi sikutegemea nisikie kingine chochote ni ‘one trick pony’ baada ya hadithi wa mkasa wake ambao tushasikia mara 1000 akaja na mambo ya ukandamizaji wa vyombo vya habari wakati mbele yake kajaziwa mic za vyombo mbalimbali mpaka kimataifa he has no ‘tricks left under his sleeves’.

Poor Lissu
Nakusikitikia Sana sijui kwanini nikiona replies zako... Maisha haya mafupi broh usijenge chuki sana
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,752
2,000
Nakusikitikia Sana sijui kwanini nikiona replies zako... Maisha haya mafupi broh usijenge chuki sana


Siwezi kumchukia mtu ata siku moja especially ambae sina interactions nae na yeyote mwenye tabia hizo elewa ni psychological issues uwezi mchukia mtu usiemjua.

Na mungu ni mwema kwa Lissu baada ya mkasa uliompata kumuweka hai wakati wengi wetu sidhani kama tungechomoka.

Hila hiyo story tumeshaisikia jamani inatosha ebu sikiliza kipi kigeni hapo kwenye hiyo hotuba kila siku story ya kupigwa risasi tu life has to go on; haya mic zote hizo mbele yake bado anadai hakuna kupashana habari kuna mtu kakamatwa na polisi baada ya kutoka hapo.
 

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
13,033
2,000
Acha upuuzi, mtu ndio katua nchini baada ya majanga yaliyomkuta,nafasi ndogo aliyopata kuongea unataka azungumzie korosho? Subiri akipitishwa na chama chake ndio utasikia akinadi sera ikiwamo hayo uliyotaja! Kwasasa acha aseme kilichoko rohoni kwake atoe dukuduku!
 

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
13,033
2,000


Siwezi kumchukia mtu ata siku moja baada ya mkasa uliompata mungu ni mwema kumuweka hai wengi wetu sidhani kama tungechomoka.

Hila hiyo story tumeshaisikia inatosha kaka ebu sikiliza kipi kigeni hapo kwenye hiyo hotuba inatosha story ya kupigwa risasi tumesikia life has to go on.
Amekuja kuzungumzia nyumbani bado mnateseka!
 

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,079
2,000
Wakati huu anatueleza akiwa hapa hapa nyumbani! Aendelee kueleza ili haki itendeke na wahusika wapatikane!
Wahusika waliomfunga na kumtesa Mandela walishugulikiwa!??. Njia ya kuiponya nchi na nafsi NI msamaha na visasi havina nafasi kabisa. Atawasha Moto usiozimika
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,752
2,000
Wakati huu anatueleza akiwa hapa hapa nyumbani! Aendelee kueleza ili haki itendeke na wahusika wapatikane!
Good for him, mungu pia kamuacha hai aje ashuhudie kwa macho yake kazi aliyompa Magufuli kuwafanyia watanzania anavyoifanya kwa ufasaha.

Aone nini alikuwa anataka kuvuruga kwa kutumishwa na mabeberu mpaka apatwe na aibu.

Hila yeye story yake tushaisikia atuambie na yeye Mungu kamtuma kuwafanyia nini watanzania zaidi ya kutaka kutukumbushia kilichomkuta.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
40,872
2,000
Japo mimi huwa natofautiana na ww mara nyingi, lakini hapa nakuunga kwa ushauri wako huu kwa Lissu. Ni kweli Lissu ana mtaji mkubwa wa watu, ni vyema cdm, na sisi wafuasi wake tumshauri namna nzuri ya kuutumia mtaji huu wa watu.

Wakati huu ni wakati sahihi kabisa wa yeye kujikita katika siasa za maendeleo ya watu, kuliko mateso yake binafsi kwani yameshatokea. Anapaswa kuwa mkombozi wa kweli wa watu katika mustakabali wa maisha yao, hivyo anapaswa kila akiongea aondoe taswira ya kuwa hana simile na yoyote, bali aongee kama mkombozi wa watu kwenye shida zao kimaisha.

Nawashauri sana wapinzani tumshauti Lisu atumie shambulio lake kwa njia chanya kuliko njia hasi, maana asipoangalia kwa huu ushawishi wake, anaweza kuliingiza taifa hili katika machafuko. Bado cdm tunaweza kuwashinda kabisa ccm kwa hoja positive, kuliko hoja za uhasama. Hili ni jukumu letu wapinzani bila kuona aibu.
 

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
7,555
2,000
Eti umeongea nini sijui, hujui ameongea ukweli mtupu naona kijani kibichi mmeumia kweli leo mtalala kweli?
 

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,938
2,000
bila kuyataja hayo uliyosema mashabiki wa chadema hawawezi kumwelewa, pia yeye hana uwezo wa kujenga hoja za wenye shida ila anachojua ni demokrasia na kupigwa risasi basi na zaidi ya hapo atafyatuka kutuhumu watu moja kwa moja kisha akipelekwa mahakamani ataje anaowatuhumu atashindwa na kurukaruka huku akisubiri wafuasi wake wamtetee.

Sioni cha maana alichoongea leo,
Ni bora angefika atulie hata siku mbiri kisha afanye tafiti kisha arudi kwenye jukwaa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom