Tundu Lissu acha utoto, jaribu kuvaa viatu vya Mandela na Martin Luther King

Acha utoto wewe jamaa Yule ni Mandela uyu ni. Tundu lisu,unataka vipikuwalinganisha??lisu kapigwa lisasi ili afe tena lisasi nyingi si moja wala mbili,Yule kapigwa vibakola Na kifungo, unawezaje kuwalinganisha hawa wawili??Acha utoto wewe jamaa
 
Umeumia sana uliposikia maumivu aliyapata? Umesononeka sana uliposikia akizungumzia “ramani ya mwili wake” baada ya kupona risasi 16 mwilini? Mkuu wewe ni mpuuzi kweli kweli! Guilty conscious , zisikufanye uone kwamba alichosema ni chuki! Wewe sema unaogopa watu wakijuwa mwili wake ulivyoharibika kwenye jaribio la kuondoa uhai wake!

Mmepanic, period! Wengine tulisema siasa zitabadilika akitua, wewe kiazi leo ndo mshauri wa kitu gani aongee?

Namshauri Lissu asiache kuongelea hiyo sehemu kwenye hotuba zake zote. Hiyo namna ya ku connect na wananchi. Mfano wa Mandele hapa ni wa kijinga! Kwanza makaburu wali negotiate naye miaka kabla ya kumuachia!

Mbona haya Yesu mateso yake yanazungumzwa tuu? Acha ulevi wewe! Halafu ndo thread hii? Jinga wewe!
 
Tundu Lissu acha utoto, jaribu kuvaa viatu vya Mandela na Martin Luther King
William Mshumbusi, kwa ufahamisho, kwa kuweka kumbukumbu sahihi na kwa mkazo wa kihistoria, shujaa Tundu Antiphas Lissu ataingia kwenye historia kama binadamu wa kipekee aliyekutana uso kwa uso na mauti lakini akakataa kuitikia wito wa kifo.

Kumbuka kwamba risasi moja tu inatosha kabisa kumtoa mtu uhai kama ilivyotokea kwa Martin Luther King na pia kama ilivyotokea kwa Rais Kennedy wote wa USA lakini risasi 16 pamoja na kupenya mwilini hazikuweza kumtoa roho shujaa Tundu Antiphas Lissu.

Kwamba shujaa Tundu Antiphas Lissu yuko hai, kwamba pamoja na makovu ya risasi na vyuma vilivyotapakaa mwilini bado anaweza kutembea na kuongea na kucheka ni moja ya maajabu ambayo mwenye majibu yake ni Mungu tu ambaye kwake kila kitu kinawezekana.

Kumkebehi kunusurika kwa Shujaa Tundu Antiphas Lissu ni kukebehi Uwezo na Ufalme wa Mungu Baba ambaye alimpa ujasiri wa kutoogopa nguvu na uwezo wa shetani kupitia mikononi mwa waovu walioamini walikuwa na uwezo na rukhsa ya kumtoa roho.

William Mshumbusi, wewe unamkejeli shujaa Tundu Antiphas Lissu bila kujiuliza kwa nini Mungu alipowapiga stop wauaji alikuwa na mpango gani naye wala hukumu gani inawasubiri waliodhani wana uwezo wa kuagiza mtu yeyote anayepinga matendo yao maovu afe.
 
Umeonyesha wazi kwamba uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana, haya yeye ameanza kwa kusimulia adha na maumivu makali aliyopitia,ambayo hata MANDELA HAKUWAHI KUYAPITIA, hivi unataka kufananisha viboko na mvua ya risasi zaidi ya 30 na bado unataka asisemee Jambo hilo kwa kisingizio cha kujenga chuki?

Kama hilo linajenga chuki kwanini watu walitekeleza UNYAMA ULE, mimi binafsi sikuwahi kufikiria kumpigia kura Tundu kwa ngazi ya urais,Ila NITAMPIGIA KWANI NAAMINI SASA MUNGU ALIKUWA NA KUSUDI JUU YAKE, ni muujiza usio wa kawaida!

Halafu ulivyo Mjinga unasema kwanini hazungumzii korosho sijui na nini nini huko,kwani ni lazima awe Lissu tu wa kuyasema hayo? Wewe umeyasemea kwa kiwango gani? Wenye korosho zao wamejisemea kwa kiwango gani? Watumishi wenyewe wanajisemea kwa kiwango gani?(si ndiyo hao hao wa kwanza kumshangilia mzee)

Umezungumzia Upendo,Upendo upi unaouzungumzia hapa,ratiba yake pamoja na mambo mengine atakwenda kuaga mwili wa aliyewahi kumtesa sana pia,lakini kwa Upendo anakwenda kumuaga akiwa kwa "coffin" kuna Upendo zaidi ya huu?

Kwa uzi wako na maneno yako umeonyesha namna ulivyo MPUMBAVU SANA!SOMA TENA KISHA JISAHIHISHE URUDISHE HESHMA YAKO ANGALAU KIDOGO!
 
Katikati ya ubaguzi, Mateso na shida kwa jamii ya weusi martini alihubiri upendo, umoja na msamaha. Kudai haki bila kuhubiri chuki zidi ya watesi wake ndio njia pekee ya Mungu kumuinua mja wake. Ukifeli hapo Mungu ashindwi kukuacha upotee kabisa.
Wewe ndio msemaji wa Mungu?
Mnataka kamshambulia Tena Tundu Lissu halafu mumsingizie Mungu?
Naendelea kuyasoma hayo maneno yako niliyo ya bold, hakika yamejaa Nia ovu.
Hivi mkiua ndio kwamba nyie mtaishi milele?
 
Bro naona unajinyea tu, Lissu kahamasisha watu kwenda kuaga mwili wa rais mstaafu Benjamin Mkapa uwanja wa Uhuru. Hilo hulioni kuwa Ni hatua ya kwanza kuleta umoja. Watakaa meza moja na JPM na mawaziri na watu wengi mashuhuri. Hata asipopewa mapokezi atakaa na watanzania wenzake.
Sijui unaelewa ulichoandika bro. Jaribu kuvuta subiri, this man is next level usipime.
 
Wahusika waliomfunga na kumtesa Mandela walishugulikiwa!??. Njia ya kuiponya nchi na nafsi NI msamaha na visasi havina nafasi kabisa. Atawasha Moto usiozimika
Tunajua kuwa waliomtesa na kumfunga Mandela ni serikali ya makaburu, ndio maana hakukuwa haswa mtu wa kumchukulia hatua. Hivyo kwa mfano wako, wataka kutuambia kuwa waliohusika kumpiga TL risasi ni serikali ya Tanzania?
 
Kila mtu ameumbwa kivyake, si lazima afuate hao unaowasema. Wewe kubali upigwe risasi moja tu ndo ufanye hayo ya ukubwa, ya Mandela, ya Martine Luther.
 
Tatizo ni kwamba tumeishikia sana hiyo story.

Tatizo ni pale unapotaka ahutubie kama wewe unavyotaka. Leo watu walitaka kumdikia kwa kibywa chake akisimulia yaliyomkuta. Pua hakuna sehemu kaongea kwa chuki. Amesisitiza sana kwamba Mungu ni mwema. Na kahamasisha sana watu kwenda kumuaga mkapa
 
Asipohubiri thamani ya haki ya kuishi, akahubiri tu unayoona ni ya maana kwako ni bure!
Uchumi usiwe kigezo cha kuchinja watu hovyo!
 
Alipoanza kuhutubia alisema. Nanukuu "hiki ni kipindi cha maneno mengi, lakini mimi nitaongea machache".


Ukiitazama hii kauli unaona kabisa lisdu kapangilia mfumo wa speech zake. Leo kawashuhudia watanzania yaliyomkuta na kumshukuru Mungu kwa muujiza wake ndio maana amesisitiza sana "Mungu ni mwema".

Wewe leo hii unamdharau na kumtaka ajikite kwenye hotuba za maendeleo.

Huo sio muda wake, ataongea sana mbeleni. Punguzeni jaziba jamani. Hamna hata chembe za upendo mpaka mmekalia kumsema jamaa.

Najua mmeumia sana kuona mategemeo yenu yameenda kinyume. Mmliwaaminusha wengi kwamba CHADEMA imekufa. Leo mmeona. Just imagine polisi wasingetoa tamko la kuzuia watakaompokea Lissu
 
Back
Top Bottom