Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Ndugu zangu,

Maandalizi yoyote yanakuwa na mantiki pale unapopata matokeo mazuri. Hapa ndipo utakapogundua maana ya kocha wa yanga mkongomani Mwinyi Zahera alipoona mambo yatakuwa magumu kwenye kombe la mapinduzi akaja na propaganda ya kuwa ''atapeleka kikosi B'' kwa sisi watu wazima tuliupata ujumbe.

Turudi kwenye hoja, huenda maandalizi ya kuongea na media za kimataifa yalikuwa mazito na yamegharimu mamilioni ya dola. Inapotokea matokeo yanakuwa madogo sana kulinganisha na uwekezaji tusipeleke ''timu A''.

Ndugu zangu, kule CNN akienda Lissu atakutana na Richard Austin Quest , huku mambo yatakuwa mabaya zaidi kuliko yalivyokuwa kwa Stephen Sackur. Kwani Richard atapata wasaa wakuangalia mahojiano baina ya Steve na Tundu na hapo kazi itakuwa imekwisha, hata akiuliza maswali yale yale hali itakuwa mbaya zaidi.

Hapa ndipo mantiki ya kuitimia timu B, ambapo hapa ndipo Mange Kimambi 'anafit'. kwanini Mange? angalau ana cha kuzungumzia kuhusu maandamano yake yaliyoshindwa ya 26 Aprili, 2018.

Pili, kama kweli Lissu bado anaumwa si busara, Chadema watumie sababu hii kukwepa kiti moto pale CNN kwani kushindwa kwake ni kuanguka kwa chama na aibu zaidi kwa kukosa misingi ya kujenga hoja kimataifa.

Nimalizie tu kwa kusema, 'mzima nguo ikidondoka chutama', sisi wenyewe ni mashaidi wafuasi wengi wa Bavicha hawasherehekei clips za BBC sasa mkiongeza mziki wa CNN ya Richard Quest hali itakuwa mbaya zaidi.

Mahojiano ya CNN aende Mange na sio Lissu kuepuka aibu zaidi.
Acha ungese kingereza chenyewe hujuii utaelewa nini? CCM wote hakuna anayejua kingereza zaidi ya mzee mkapa na pengine kikwete kidogo, Tundu Lisu kaongea vizuri ingawa mtangazaji alikuwa na maswali ya mtego ndiyo maana watetezi wa CCM hamjapata usingizi mmekalia kupanga mada za kifala fala, kama ingekuwa haiwaumi msingehangaika kutengeneza story zenu za kijinga jinga.
 
Acha ungese kingereza chenyewe hujuii utaelewa nini? CCM wote hakuna anayejua kingereza zaidi ya mzee mkapa na pengine kikwete kidogo, Tundu Lisu kaongea vizuri ingawa mtangazaji alikuwa na maswali ya mtego ndiyo maana watetezi wa CCM hamjapata usingizi mmekalia kupanga mada za kifala fala, kama ingekuwa haiwaumi msingehangaika kutengeneza story zenu za kijinga jinga.
Jenga hoja bila matusi, wewe ulihama na Lowassa kutoka CCM umeshajua Kiingereza?
 
nimeshasema kwenye nyuzi zangu, 2020 chadema itapangaranyika na kuvurugika si kwa sababu wametaka bali wanachama watagawana fito za nyumba ambayo wameijenga na hapo ndipo tutapata CCM ushindi mkubwa sana. Mpaka sasa chadema hawajui ni lowassa, lissu au nyarandu kuelekea 2020
Kabla hamjamwaga mapovu yeni ni vyema mngemtafuta mtaalamu Steven Wassira mkamuuliza kuwa ni lini chadema itakufa. Kwani yeye ndiye muasisi wa huu msemo kuwa chadema itakufa
 
Ushahidi kwamba hakupigwa risasi?
Ushahidi wa Kimazingira unaonyesha kuwa hao anaowatuhumu ndiyo walimpiga risasi!
Hili linaitaji mtu mwenye akili ya juu kidogo above average kuweza kuconnect dots za matukio mazima kuanzia

1.alipotoa tahadhari kuwa anafuatiliwa, mpaka yule mzee aliyesema anajua namna ya kudeal na "wasaliti",

2. vitisho alivyokuwa akipewa na makada wa chama cha Mafisadi,

3. kuondolewa kwa walinzi siku ile anachapwa risasi kwenye makazi ya wabunge,

4.mpaka leo hii kunyimwa pesa za matibabu,

5.Mpaka leo hii kutokuwepo kwa uchunguzi rasmi wa kuhusu shambulio alilofanyiwa, hakuna jalada, wala mtu waliyemshuku, yaani wamepotezea mazima.

Sasa kama viashiria vyote hivyo huvioni bali unataka uletewe CCTV footage, Unataka uletewe sauti au Vimemo vya Wauaji wakipanga hizo njama, Unataka Lissu akupe bunduki na Fingerprints za aliyeifyatua basi utasubiri sana. HIVYO VITU ULIPASWA UILIZE JAMHURI maana ndo ina mandate ya kuvikusanya .

Kwa viashiria namba moja 1 hadi 5 kule juu Hao ambao Lissu anawatuhumu wanafit Exactly katika Suspects nambari moja kutokana na matendo yao
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Leo ni Lissu day au ?
kila mahali yeye hapa naogopa hata kufungua friji naweza nikamkuta lissu
 
lissu haogopi kupanda ndege anazunguka tu huko duniani

Sent using Jamii Forums mobile app

Tundu Lisu amealikwa sehemu zote na vyombo mbalimbali na taasisi mbalimbali atakwenda haogopi CCM watasema nini yeye atasimama kwenye Ukweli kwani msema kweli ni mpenzi wa mungu ingawa sasa magufuli si msema kweli tena kawa mnyanyasaji muonevu mkandamiza demokrasia nchini , kawa msema uongo ni mpenzi wa shetani.
 
Nionavyo Lissu anazidi kuibana mbavu serikali dhalimu ya Rais JPM!
Mkuu;
Kuona ni haki yako lakini haina maana kuwa unachokiona ni kweli!

Binadamu tumeumbwa na macho yenye nguvu tofauti katika kuona pamoja na kwamba hayo yote ni macho yanayoona!
 
Back
Top Bottom