Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Kweli huyu ni msomi nimeamini kupitia majibu yake, Lissu come back home waendelee kupoteana hawa
 
Kabla na baada ya kipindi kuruka nimeona wanachama, wapenzi na viongozi wa ccm wakiwemo wa kiserikali wamepaniki sana, nikajiuliza kulikoni? Ndipo nikaamua kufuatili coverage ya bbc duniani.

Kulingana na ripoti zilizopo za mwaka 2017 bbc imefikisha rasmi watazamaji watu wazima wanaokadiriwa kufikia 376 milioni hapa hujazungumza wasio rasmi kama kina siye. Kwa mantiki hii ujumbe wa Lissu umefia zaidi ya watu 376 milioni. Na mwandishi alivyo mbobezi kwa dk 22 kagusia mambo mengi yaliyolenga kuupaka tope utawala wa JPM

BBC - BBC’S Global audience rises to 376m - Media Centre
 
Kabla na baada ya kipindi kuruka nimeona wanachama, wapenzi na viongozi wa ccm wakiwemo wa kiserikali wamepaniki sana, nikajiuliza kulikoni? Ndipo nikaamua kufuatili coverage ya bbc duniani.

Kulingana na ripoti zilizopo za mwaka 2017 bbc imefikisha rasmi watazamaji watu wazima wanaokadiriwa kufikia 376 milioni hapa hujazungumza wasio rasmi kama kina siye. Kwa mantiki hii ujumbe wa Lissu umefia zaidi ya watu 376 milioni. Na mwandishi alivyo mbobezi kwa dk 22 kagusia mambo mengi yaliyolenga kuupaka tope utawala wa JPM

BBC - BBC’S Global audience rises to 376m - Media Centre
kaka BBC ile version ya Hardtalk sio.mchezo halafi walidhani Lissu anatania vile.
 
Mimi nashauri hawa niliowataja mmoja wao kwa dhamana walizopewa waende kuhojiwa katika kipindi hicho kuhusu shambulio la Lissu na hatua walizochukua na kama hawajachukua hatua waeleze sababu ni nini na mtangazaji awahoji kadri watakavyojibu alafu tuone nini kitatokea.

Na ikiwezekana hata mkulu nae ahojiwe jinsi alivyosimamia swala hili.
 
MAHOJIANO YA TUNDU LISSU BBC DHIDI YA DHANA KUHUSU UKWELI


Januari 21 mwaka huu ,Mbunge wa Singida mashariki alihojiwa katika kipindi maarufu kinachorushwa na Shirika la habari la Uingereza BBC idhaa ya Kiingerezwa cha Hard Talk.

Katika mahojiano hayo mbunge huyo aliyepigwa risasi September 7,2017aliulizwa jumla ya maswali 25 na mtangazaji wa kipindi hiko Stephen Sackur huku swali la 22 lililohusu uhuru wa mapenzi ya jinsia moja likirudiwa mara 5 baada ya kuonekana analikwepa ama jibu halikuridhisha.

Kuanzia swali la kwanza mpaka la 6 yalihusu moja kwa moja shambulio la risasi alilofanyiwa Dodoma na maswali 18 yalijikita kwenye kukubali au kukataa kuhusu umadhubuti wa serikali ya Dr Magufuli kasoro la 22 ambalo lilikua mahususi kuhusu mapenzi ya jinsia moja hasa ushoga.

Makala haya yanasadifu dhana ya ukweli na uwongo kupima mantiki na hoja ya Tundu lissu ili kuhitimisha alichosema kinaangukia kundi gani katika dhana hizo mbili.

UKWELI NI NINI?

Ukweli ni lengo la akili katika kujua mambo yote kwa dhati iwezekanayo.Huanza kujulikana kuanzia hisi,kwa kufikiria,kushika

Watu wengi hutumbikia kwenye mkondo wa kusema uwongo kwa sababu ya pupa authority kujitakia makuu ya kuwashinda wengine kwa uchoyo.

Mwanzoni mwa historia ya wanadamu, kila kitu kilitegemea ukweli. Mambo ya hakika hayakupotoshwa, ama kupindwa pindwa.

Mwanafalsafa maarufu wa Kigiriki Aristotle anasema Ukweli ni muafaka baina ya habari ya kilichotokea na usahihi wa mambo.Anaongeza pia hakuna ukweli nusu nusu.Ukweli hauchanganywi na uongo.Akimaanisha ukidondosha tone la ukweli katika uwongo huo ni uongo kamili.

LISSU AMEONGEA UKWELI ?

Kama umetengeneza picha ya nchi inayoitwa Tanzania kupitia mahojiano aliyofanya Lissu kwenye kipindi hiko basi ni wazi Tanzania inayozungumzwa na Lissu sio Tanzania hii tunayoishi.

Tanzania imezungumzwa kama nchi ambayo hakuna chochote kilichofanyika wakati wa Magufuli .Watu wanauwawa hovyo,serikali haina pesa,hakuna uhuru na mengineyo.

Ukweli sio chochote kile,uongo unaweza kuonekana kuwa ukweli lakini bado ni uongo sio ukweli.

Ukweli sio kinachokufanya ujisikie vizuri au vibaya ,hata ukweli uongo una uwezo wa kukufanya ujisikie hivyo haufafanuliwi na kile kilichopangwa,Ukweli sio jinsi tunavyojua .

Kweli sio inayohusika na inayoendelea inawezekana ikawa iliyopita.Ukweli sio pana peke yake hata nyembamba pia,Ukweli sio tu kinachoamuliwa hata hufanyiwa maamuzi.

Ukweli ni kusema tu kama ilivyo ndio ambavyo hali ilivyo na maoni mengine yoyote ni makosa.Tundu Lissu ametoa maoni ambayo yameondoa sifa ya alichongumza kuitwa kweli iliyokamilika.

Kwenye aina tatu za propaganda tunashauriwa tutumie propaganda ya kijivu ambayo ni mchanganyiko kati ya ukweli na uongo ili angalau kabla ukweli ukiwa haujavaa chupi uongo uwe umekwisha sambaa ,kuliko kutumia propaganda nyeusi ambayo ni uongo peke yake kwakua uhai wake ni mfupi mithili ya mshale wa sekunde.

Lissu ametumia propaganda nyeusi iliyofuta kabisa nukta chache za ukweli ndani ya bongo za wanaojua kufikiri.Ukweli kidogo alioumiliki umefifishwa na uongo mwingi uliozungumzwa.

HOJA YA SHAMBULIO LA RISASI.

Katika hoja ya kupigwa risasi ni kweli Lissu amepigwa risasi na amabaye anafurahia tukio hilo ni punguani.Lakini ni upunguani zaid kutumia maoni ama uongo nusu kuthibitisha ni nani aliyempiga risasi mbunge huyo.

Tunaambiwa na Lissu wakati akijibu swali la 1-3 yaliyomtaka kuthibitisha ushiriki wa serikali katika shambulio la risasi alilofanyiwa kuwa ukimya wa rais Magufuli na serikali yake kuhusu tukio lile na kutomjulia afya ni ushahidi unaotosha kabisa.

Inaonekana hapa Lissu hakuwa makini kwenye kumbukumbu au ameghafilika na pupa.Wakati fulani amenukuliwa akisema suala la kusafirishwa kwake kwenye matibabu ya Nairobi yaliamuliwa katika kikao.

Katika kikao hiko kilochofanyika Dodoma siku aliyopigwa risasi kilimhususisha Spika Ndugai,naibu wake Dr Tulia Aksoni,aliyekua katibu wa bunge Thomas Kashilila,Freeman Mbowe,waziri wa afya Ummy Mwalimu na aliyekua waziri wa mambo ya ndani wakati huo Dr Mwigulu Nchemba.

Matokeo ya kikao hiko ni pamoja na kuruhusu ndege kuruka saa sita usiku kwa kibali maalumu kilichotolewa na serikali.Sasa ukimya upi wa serikali unasemwa na Lissu katika kipindi?

Kimtazamo baada ya makelele mengi ambayo yalipazwa na upinzani kuihusisha serikali na tukio hilo ndivyo na yenyewe ilipoamua kujiweka mbali.

Kukosekana kwa uwiano wa alichozungumza siku za nyuma na alichokisema kwenye mahojiano ndani ya kipindi hiko katika mizania ya ukweli ni sawasawa na ukweli nusu ambao kwa mujibu wa Aristotle ni ukweli kamili.

KOSA LA MSINGI KATIKA MAHOJIANO YALE.

Jambo lingine ambalo limeweka utata katika kutambua anachosema Lissu kwenye kipindi hiko ni ukweli ama uwongo ni kutokubali kutoa muono chanya hata katika eneo moja ndani ya serikali ya Magufuli.

Alipaswa kuchagua maeneo machache ya kusifia ambayo ni kweli yanaonekana kwa macho baadae angeweza kutengeneza kuaminika wakati wa kukosoa.

Serikali yoyote ile hata ingeongozwa na shetani haikosi kufanya kitu .Ndio maana pamoja na ubaya wao wakoloni walijenga reli,shule na mengineyo.

Mfano swali la 10 mtangazaji alimuuliza kuhusu uongezeko la ukusanyaji wa mapato Tanzania,akapinga,Swali la 9 aliulizwa kuhusu kuminywa kwa mirija ya rushwa na kuondolewa kwa watumishi hewa akabeza.

Aidha swali la 14 aliulizwa kuhusu wabunge 10 wa upinzani waliohamia CCM kwa jibu la Lissu kuwa wamenunuliwa mtangazaji akamchukua Laurent Masha aliyetoka CCM kwenda Chadema na kurudi tena CCM kukutaa jibu la Lissu.

Hivyo kukataa hakuna zuri lililofanyika wakati wanafunzi wa sekondari wanasoma bure,kuna ujenzi wa mradi wa umeme wa Strigles Gorge,reli ya kisasa katika falsafa ya ng'amuzi juu ya ukweli ni vigumu kuamini mengine yaliyobaki.

Mtiririko huo wa majibu ya Tundu Lissu katika kipindi hiko kilichowahi pia kuwahoji watu maarufu duniani kama aliyekua rais Marekani Geoge W Bush,Tony Blair,Rais wa Afrika kusini Thabo Mbeki,unaleta ukakasi wa kimantiki juu ya nia yake katika kipindi hiko.

KOSA LINGINE

Majibu ya Lissu yalizingatia zaidi nasaba,uchama kuliko matabaka.Mara kwa mara ameeleza watu kwa wasifu wa mtu kwa misingi ya chama tawala au chama cha upinzani.

Lissu alizungumza kama vile watanzania wote ni upinzani au Ccm.Hakukumbuka zaidi ya nusu ya watanzania hawana vyama vya siasa.Hakukumbuka zaidi ya 65% ya watanzania ni wakulima.Hakujenga hoja ya matabaka amejenga hoja nyingi za kiitikadi na nasaba za kisiasa.

Katika mtazamo wake huo chama tawala ndio watesi na vyama vya upinzani ni wateswaji.Lakini yupo mbunge wa Chama cha upinzani anayetoka kwenye moja ya majimbo yaliyopo jijini Dar essential Salaam anadaiwa kumpiga mbunge wa chama cha mapinduzi ambaye sasa ni waziri.

Lakini dhana ya ubaya au uzuri aliyojenga kinasaba kupitia upinzani au chama tawala unaweza kukoselewa kupitia ndoa ya Jesca Kishoya mbunge wa upinzani(Chadema)mumewe ni mwanachama wa chama cha mapinduzi na kwa sasa ni mkuu wa wilaya.

Kwa kuzingatia dhana ya unasaba badala ya matabaka Lissu amejikuta akizungumza zaidi siasa za upinzani na chama tawala kuliko wakulima,wafanyakazi,wwanafunzi na maskini wengine ambao ni tabaka linalonufaika na utawala wa Magufuli.


HITIMISHO

Ukweli haumuliwi kwa wingi wa kura.Ukweli unaamuliwa na "facts"(ukweli dhahiri).Daktari akisema unaumwa Malaria ni fact.Msukuma mkokoteni akisema unaumwa Malaria ni maono tu (Opinion) sio ukweli halisi.

Sehemu kubwa ya majibu ya Lissu katika mahojiano yale yalikua ni maoni yake .Hayakua na facts ndio maana kwenye swali la 16 mtangazaji alihoji anawazaje kuzungumza mambo yote yale yeye kama mwanasheria bobezi hakiwa hana ushahidi usioacha shaka?

Kila uwongo ni jambo lisilo la kweli,lakini si kila kila jambo lisilo la kweli ni uwongo,kwa sababu uwongo ni habari ambayo mtu anayeitoa anajua au kuamini kwamba si ya kweli na anaitoa kwa kusudi la kudanganya.Hivyo kusema jambo lisilo la kweli bila kukusudia si sawa na kusema uwongo.Kwenye mahojiano yale Lissu alidhamiria kutosema kweli hasa alipokosa facts za kujazia alichokisema.


Noel Nguzo.
21/1/2019.
 
Hebu jaribu kutamka ujasiriamali kwa kingereza ndio utajua matokeo ya hardtalk yatakuwaje
 
Jamani tuacheni masihara, Lissu ni kichwa cha kimataifa. Lugha, upeo, kujiamini na uwezo wa kupangua maswali aliouonyesha Lissu ulikuwa wa juu mnoo. Fantastic.

Baada ya kile kipindi kuruka hewani, huko Kenya wameanza kudai kuwa Lissu ni mkenya.
 
Back
Top Bottom