Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Katika ziara zao huko ulaya na kwineko mfano Kagame walipokutana na Trump pembezoni mwabmkutano flan mwaka jana uliona akimuhoji lolote kuhusu yanayoendelea Rwanda?


Sent using Jamii Forums mobile app

Trump ni mwandishi wa habari au mtangazaji mpaka amuhoji Kagame? Jana Tundu Lissu alikuwa anahojiwa na Theresa May? Unajua unachoongea au umevurugwa?
 
Hapa kwetu hatukimudu kiingereza, na mtawala wetu hamudu mahojiano, je tunawazidi nini hao wengine?
Mkuu nchi inazidi kubadilika kuelekea kwenye maendeleo. Hao wanaojua kingereza hawatupunguzii wala kutuongezea kitu.

Mahojiano sio kila kitu, sio ukamilifu wa sifa ya mtu kuweza kuwa kiongozi mzuri. Unaweza ukawa unakijua kingereza kuliko huyo mzungu aliyemhoji TL halafu ukawa mzembe na mvivu kikazi.

Nchi z kiafrika zinahitaji viongozi wafuatiliaji wa maagizo wanayowapa walio chini yao, zinahitaji watu wasioogopa kufanya maamuzi magumu.

Huyo mzungu alikuwa anamshangaa TL anatoa tuhuma wakati wao wanazo taarifa zote za ukusanyaji wa kodi na uwepo wa nidhamu ya ufanyaji kazi.

Kingereza ni lugha tu, ukiwa na utumwa wa mawazo unaweza kuibiwa na mzungu mjinga tu huku ukibakia kumnyenyekea ukimuona kama vile katoka mwezini.
 
Watu wanalalamika kwanini ameongea hayo hawajiulizi angekufa angeongelea wapi nyambafu
Kwanza CCM ndiyo wa kubeba lawama zote kwani kama sio unyama na udikteta wao leo hii Tundu Lisu asingekuwa huko ulaya
 
Sihitaji kuhoji ila naona ni 1) safari ya kusaka marafiki jambo ambalo si kosa, kwani anausaka urais, hivyo ni vyema kuanza kuwa na mahusiano mazuri na jumuiya za kimataifa, iwapo atapata ridhaa ya kuongoza ataweza kuwashawishi kuwekeza hapa nchini. 2) Anaeleza dunia nini kilimkuta siku ya shambulio lake na udhaifu wa serikali kwenye hilo. 3) Manufaa kwa taifa ni kuimarisha demokrasia na kulinda uhuru wa kujieleza kwa wenye mtazamo tofauti na watawala.
Hahahahahah akili za usiku hizi.Yaani lisu anasaka marafiki Ulaya. Mkiambiwa anatumiwa na mbuz dume mnakuja na mapovu. Hao unaowaambia kuwa huku hamna democracy kwamba ndio watakuja kufanya nini?Waje wamtoe magufuli wakuweke wewe au?Hahahahahah kweli Africa is a SHITHOLE CONTINENT. Yaani bado tuna wasomi ambao wanaamini bila mzungu hawawez fanya lolote na mzungu ndiye wakuja kusolve mattz yake.Yaani kwa jicho la tatu tu hoja itakayokuja kumpoteza lisu kwenye siasa ni UKIBARAKA. Now huwez ona lkn wananchi ukishawajaza Hii elimu basi kisiasa umeisha na hii ziara na zile kelele anazidi kujipambanaua ye ni nani.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
Cha muhimu tuendelee kuwapa uhuru wa kupiga kazi wale ambao ilani yao imekubalika na wengi.

Ni nani umeona ameenda kung'oa mataruma ya reli ya SGR? Mpinzani gani umemuona akiharibu miundo mbinu ya maji, barabara, shule nk? Kinachofanyika ni malumbano ya kisiasa ili kupata ubora. Sasa kupiga wengine risasi kwa kujifanya wazalendo inatokea wapi?
 
Mbona mwalimu Nyerere alisema ikulu isigeuzwe pango la wanyang'anyi na ikulu ni mahali patakatifu yanayofanyika ikulu si ndio hayohayo aliyoyakemea.
 
Utashitakiwa huko MIGA umezuia maslahi gani ya mzungu? Hao Acacia na Barrick mpaka leo wapo na hawajalipa hata shilingi na bado wanaendelea na shughuli zao. Wakushitaki kwa lipi? Hakuna kiongozi yoyote ambaye hajawahi kuifaa nchi, bali ni kiwango gani anaifaa nchi hilo ndio jambo la msingi. Hata Hitler aliifaa nchi yake japo aliwaingiza matatizoni.
Sasa ndio uone pia kwamba Lisu anajisumbua, hivi mzungu aje amtoe Magu kwa maslahi gani ya mzungu yaliyoguswa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kawekwa kwenye kona maskini alidhani wazungu wajinga. Nafikiri ataacha sasa kujipeleka peleka.
Kahaibika sana kujaribu kulazimisha ila mzungu yuko smart, inflamatory allegation!
Hahahaaaaa

Wewe ndiyo hujui kingereza hata hujaelewa kitu inaelelekea wewe ni mbumbumbu hata hujui kuwa Tundu Lisu hakujipeleka huko bali wenyewe ndiyo walimwalika baada ya wewe kumpiga Risasi akaenda kutibiwa huko, chanzo ni wewe kama wewe ungeacha njama za kumuua leo hii asingekuwa huko angekuwa nyumbani Tanzania anaendelea na kazi zake.
 
Hivi kushabikia kingereza kama hoja nako kuna shiko kweli??? Karine ya 21??

bugs
Lugha Hiyo hiyo Ndio Inayotumika Kufundishia, Inatumika Bungeni, Inatumika Mahakamani, Ukienda Kuomba Kazi Hata Serikalini Lazima Uijue Alafu Wewe Unasema Kuijua Ni shiko kweli? Alafu Kama Huoni Aibu Mafanikio Unayoyapata Na hiyo Lugha Kwanini Uone Aibu Kujivunia? Have a strap
 
Hahahahahah akili za usiku hizi.Yaani lisu anasaka marafiki Ulaya. Mkiambiwa anatumiwa na mbuz dume mnakuja na mapovu. Hao unaowaambia kuwa huku hamna democracy kwamba ndio watakuja kufanya nini?Waje wamtoe magufuli wakuweke wewe au?Hahahahahah kweli Africa is a SHITHOLE CONTINENT. Yaani bado tuna wasomi ambao wanaamini bila mzungu hawawez fanya lolote na mzungu ndiye wakuja kusolve mattz yake.Yaani kwa jicho la tatu tu hoja itakayokuja kumpoteza lisu kwenye siasa ni UKIBARAKA. Now huwez ona lkn wananchi ukishawajaza Hii elimu basi kisiasa umeisha na hii ziara na zile kelele anazidi kujipambanaua ye ni nani.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
Mzungu ni mtu makini sana. Ujumbe wa TL umekutana na akili ambazo zimeutilia shaka.
 
Uzuri wa JIWE hajui Kingereza, hivyo hata hajui kilichoendelea.

Le mutuz kaitwa ikulu kwenda kumtafasiria na huko kubwa jinga le mutuz lazima litandanganya kwani na lenyewe halijua kingereza vizuri, hata Kiswahili chenyewe halijua kuandika vizuri.
 
*LISSU ATAABIKA SANA, AISHIA KUAIBIKA LONDON, ABANWA VIKALI NA KUTOA MAPOVU*

_NA Mwamba wa Kaskazini_

Leo ndio msemo kuwa Kiingereza sio maarifa umethibitika.

Tundu Lissu ana uwezo wa kutosha tu kuongea Kiingereza lakini asubuhi ya kuamkia leo kukosa maarifa kujawa na umbea, uongo na uzushi na uzandiki dhidi ya nchi yake kumemtokea puani akifanya mahojiano na Kipindi cha Hard Talk cha BBC.

Sikiliza haya.

*1.Aonesha Chuki Binafsi Kwa Magufuli*

Kosa la kwanza ni kutojadili hoja bali mtu.Kila alipoulizwa aliishia kutaja jina la Magufuli hata asipohusika.

Mtangazaji mzungu akabaki anashangaa na kumbana kwa maswali zaidi akaishia kutoa macho maskini.

*2.Lissu Hakutegema*

Hakika hata mimi sikutegema kama yule mzungu angefanya utafiti kiasi kile na kuyajua mengi ya Tanzania kiasi cha Lissu mwanzoni tu kubabaika na kuanza kuzusha uongo.

*3. Jaribio la kumdanganya Mzungu lakwama*

Baada ya kuzoea kuandika viwaraka vyake na kuwapa akina Martin Malera wa Tanzania Daima au Ibrahim Yamola wa Mwananchi leo Tundu Lissu kakutana na mwanahabari wa level nyingine.

Akajikuta anakosa ushahidi...anaambiwa unalalamika kila siku Serikali imekushambulia, unaushahidi gani anasema niliona gari inanifuatafuata, mzungu akambana kwani gari ziko ngapi na mtu yeyote si anaweza kukufuatilia kwani umeshafanya kazi ngapi za kukuweka katika risk ikiwemo kuwa wakili, Lissu akajikuta anakiri kuwa ni kweli hana ushahidi wa moja kwa moja bali ushahidi wa mazingira.

Asante sana mzungu, huyu Bwana leo baada ya mbwembwe nyingi sasa kakiri hana ushahidi zaidi ya mazingira tu ambayo pia yanaweza kuonesha chama chake kinahusika au hata dereva wake.

*4.Akosa maarifa kwenye madini*

Maskini hapa ndio jamaa alitoa mimacho tu baada ya mzungu kumbana kuwa yeye alipigania sana masuala ya nchi kufaidika na madini haoni kuwa JPM anachukua hatua nzuri?

Kwa hakika na mimi hapa nilipoteza Kiingereza changu[emoji3][emoji3]Sikumbuki hata Lissu alikuwa anajibu nini, aliishia maskini kutaabika na kuruka ruka huku na kule.Mzungu akaona isiwe shida, akahamisha mada!

Kwa kifupi hapa Lissu alijikuta anatamani kumpinga Magufuli, lakini pia akawaza anampinga kwa lipi?Kurekebisha mikataba ili nchi ifaidike? Akabaki anataja taja tu majina mara uwanja wa ndege Chato wakati nchi nzima vjwanja zaidi ya 15 vinajengwa[emoji3][emoji3]

*5.Mtangazaji aamua kutaja mwenyewe mazuri ya Tanzania.*

Baada ya kuona Lissu hana analolikubali katika nchi yake mzungu wa watu akaamua kutaja mwenyewe mageuzi makubwa yanayoendelea Tanzania.

Akataja mapambano dhidi ya rushwa, akataja kuongezeka kwa mapato akataja kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya kijamii na miundombinu.

Usiniulize wakati wote huu mzungu anashusha nondo Lissu alikuwa kwenye hali gani[emoji3][emoji3]Kumbuka mwenyewe kisa cha chura aliyebanwa na mlango[emoji3]


*6. Atoa mfano wa kitoto, wamuumbua*

Akieleza kwa nini wapinzani wenzake wamekuwa wakirejea CCM kuunga mkono juhudi za JPM Lissu aliishia kirusha matuhuma ambayo hadi mtangazaji akamuonya aache kuropoka bil ushahidi.


Lakini yotrme hii ni kwamba alishachanganyikiwa. Sasa sikia hii: akapewa mfano wa Masha aliyetoka CCM na kwenda upinzani (ingawa badae alirudi CCM) kama naye alihongwa huko upinzani? Usiniulize Lissu alikuwa katika hali gani hapa tena[emoji3]

*7.Akata fahamu, aunga mkono ushoga*

Akiwa hoi bin taaban na kisaikolojia akionekana mtu anayetamani mahojiano yaishe tu, Lissu akaulizwa ukiwa kiongozi wa upinzani na siku ukiingia Ikulu utafuta sheria zinazoelezwa kuwa kandamizi zinazoufanya ushoga kuwa kosa la jinai?

Maskini, mwisho wa zama ukatimia, baba la watu likajikanyagaaaa mwishowe likaingia kingi eti litafuta sheria zote zinazozuia ushoga nchini.Maweeeee[emoji17]

Rasmi Lissu kaunga mkono ushoga. Hakika ametaabika sana.

Kwa nini utaabike lakini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee mbona povu, kama kaaibika si ndio vizuri? Maana umeandika makala ndefu as if upo obssessed na huyo Lissu.
 
Hapa ninahasira sana
Lissu na wapambe wako nakuuliza ni faida gani umeipata kuichafua Tanzania hii na kumchafua Rais Magufuli?
Kweli umeshindwa kuelezea hata jema moja alilofanya huyu Rais?kweli tunamponda magufuli lakini sio huko mnakoenda huo sii utamaduni wetu watanzania.
Haahaaa tulia tuli Dawa iingie mlikosea na mnazidi kukosea zaidi
 
BBC Steven Sanker's command of political trending and goings on in Tanzania has belittled Tundu Lissu arguments just like a piriton tablet. So pity to Lissu. So sad that Lissu has dillydallied to answer a question regarding his party's position on homo sexuality.
 
Back
Top Bottom