Uchaguzi 2020 Tundu A.M. Lissu: Mgombea Urais wa upinzani machachari zaidi kuwahi kutokea katika chaguzi zote chini ya mfumo wa vyama vingi kurudi 1992

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Tangu kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na uchaguzi mkuu wa kwanza wa mwaka 1995, Tanzania haijawahi kushuhudia na kupata mgombea wa upinzani machachari na mwenye ufahamu wa hali ya juu wa mambo mbalinbali kitaifa na kimataifa katika nyanja za elimu, siasa, historia, sheria, uchumi nk kama Tundu Lissu (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020.

Kina Mrema (1995), Lipumba (2000), Freeman Mbowe na Lipumba (2005), Dr Slaa (2010) na Lowassa (2015) walikuwa wagombea Urais wenye sifa zao za kipekee, lakini Tundu Lissu anawazidi wote kwa kuwa na sifa za ziada na kufanya upekee wake uwe maalumu kama nitakavyojaribu kueleza hapa chini.

Naandika thread hii baada ya kuisikiliza sehemu ya hotuba ya mgombea Urais huyu kwa tiketi ya CHADEMA ya jana tarehe 28/9/2020 akiwa Mugumu - Serengeti mkoa wa Mara.

Ni hotuba ambayo imajaa elimu ya uraia na sheria huku ikifunua UJINGA na UPUMBAVU wa viongozi wengi wa serikali ya CCM ya Magufuli wasiojua sheria, kanuni na taratibu za kusimamia dhamana zao za uongozi kwa ajili ya ustawi wa jamii na amani yetu.

RCO ya Mara, DC na DED wa Serengeti ni mfano mzuri wa viongozi wajinga na wapumbavu. Wapewa dhamana ya uongozi wa mamilioni ya watu, lakini kwa kutojua ama kwa makusudi wao ndiyo wanakuwa wavunjaji wakubwa wa sheria na taratibu.

Ukiacha hili, upekee wa Tundu Lissu ukilinganisha na wagombea wote wa upinzani waliowahi kugombea Urais tangu mwaka 1995 unajitokeza katika maeneo haya;

1. UFAHAMU MKUBWA WA MAMBO:

Huyu bwana amejaliwa kuwa na ufahamu wa hali ya juu wa mambo mengi kuanzia ktk nyanja ya historia, uchumi, jamii, siasa, sheria na utamaduni.

Hii humwongezea ujasiri wa kusimama na kutetea chochote kinachokuja mbele yake na mara zote anakuwa mshindi tu. Hii inatuleta kwenye sifa ya pili.

2. UJASIRI:

Kwa kuwa kajaliwa kuwa na ufahamu mpana wa mambo mbali ya kitaifa na kimataifa karibu katika nyanja zote za maisha, hii imempa hiki kitu kingine yaani - UJASIRI.

Naye sasa anatumia kila njia ku - influence tabia hii ya ujasiri, kutokuwa na hofu ama woga kwa watu wote anaokutana nao. Hapa ndipo hasa ulipo mgogoro wake na watawala. Hili huwatia hofu na woga mkubwa watawala hawa waovu.

Wanajua kuwa watu wakielimishwa, wakatambua WAJIBU na HAKI zao, wataiondoa serikali hii madarakani kufumba tu na kufumbua. Hili linaiogopesha sana CCM na serikali wanayoingoza.

3. NI MSOMAJI SANA WA VITABU HUYU JAMAA:

Ili kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali, sharti utafute maarifa. Sharti usome vitabu na vyanzo vingine mbalimbali vya maarifa.

Huyu ndugu anasoma sana. Simjui na wala sijawahi kukutana naye uso kwa uso karibu. Lakini ninapomtazama kwenye TV akiongea, mtu mdadisi atatumbua hili moja kwa moja.

Ukisikiliza na kutazama hotuba yake ya jana Serengeti utaelewa nikisemacho hapa. Utaelewa kuwa huyu mtu amejaza maarifa kichwani mwake na si matope kama alivyo Polepole ama Cyprian Musiba wa CCM.

4. NI MGOMBEA PEKEE KATI YA WOTE ALIYETOA UHAI WAKE KWA AJILI YA HAKI ZA WENGI:

Hii ni sifa very exceptional. Huyu bwana amepitia njia ngumu mno hadi kufikia hatua hii aliyonayo hapo kwa ajili ya kutetea haki za wananchi wa taifa hili zuri la Tanzania.

Huyu ndugu kwa siku saba achilia mbali miaka miwili na ushee akiuguza majeraha ya risasi kitandani, alikuwa kuzimu. Alionja KIFO na MAUTI lakini kwa sababu anazojua Mungu mwenyewe, alimfufua tena Tundu Lissu. Yuko hai na ndiye huyu ambaye watu wanamuona kama Messiah wao na basically ndivyo ilivyo, ndivyo itakavyokuwa.

5. NI SPEECH GIVER & INFLUENCER MZURI KUPINDUKIA. HUCHOKI KUMSIKILIZA

Wanasiasa wenye kipaji cha namna hii ni wachache mno Tanzania. Huko nje namfahamu mtu mmoja, Martin Luther King Jr, mpigania haki za weusi wa Marekani miaka ile

Hotuba za Tundu Lissu ni za kushawishi, kuhamasisha, kutia morali na kuwaondolea watu hofu, mashaka na woga.

Watu kama hawa siku zote ni HATARI katika serikali zote za kidikteta zinazogandamiza UHURU na HAKI za kiraia.

Huwindwa kama wanyama pori ili kuwaua kama njia pekee ya kuwaondoa maana HOJA ZAO mara zote hazijibiki na Mara zote ni chungu na zinachoma mithili ya mkuki moyoni.

Mara zote watu wa aina hii hugeuziwa kibao na kuitwa wachochezi, wahamasisha vurugu na wahatarisha amani. Hutungiwa hata sheria kwa ajili yao tu.

Hii yote, kosa lao ni moja tu. Kufumbua macho, akili na ufahamu wa watu wa kutambua WAJIBU na HAKI zao dhidi ya serikali na viongozi wao.

6. ANA "SPEAKING SKILLS" YA HALI YA JUU. ANAJUA KUIFUNDISHA NA KUELEKEZA KWA LUGHA NYEPESI NA YENYE KUELEWEKA KWA URAHISI KWA HADHIRA YA RIKA ZOTE:

Licha ya kwamba ana uwezo mzuri ktk kuhutubia, pia ukimlinganisha na wagombea wenzake kama Magufuli ama Prof. Lipumba ama Bernard Membe, Tundu Lissu anajua kuelekeza na kufundisha watu....

Anatumia lugha rahisi na yenye kueleweka kwa rika zote. Anaweza ku - engage vizuri hadhira inayomsikiliza na hapo ndipo ambapo mtu anavutiwa tu kuendelea kumsikliza

Hizi ni "attributes" zinazompa advantage za kuwa kiongozi bora....

7. KILA ANALOSEMA KAMA AHADI, HUMAANISHA KUWA ATALITENDA NA KULITEKELEZA:

Moja ya sifa za wanasiasa ni UONGO. Kusema na kutoa ahadi za uongo kwa wanasiasa ni kama utamaduni na mazoeà yao....

Nimemfutilia Tundu Lissu kwenye mikutano yake ya kampeni, ahadi zake chache kubwa alizokwisha zitoa zinapimika na zinaweza kutekelezeka...

Mfano ahadi ya Katiba mpya, kulipa mishahara nyongeza za mishahara ya wafanyakazi ambazo kwa miaka mitano zimeminywa na serikali ya CCM mpya ya Magufuli zinapimika na kutekelezeka....

Aidha tukumbuke pia alipikuwa uhamishoni Ubelgiji kwa matibabu alianza kuwaahidi watanzania kuwa atarudi Tanzania na atagombea Urais, akatenda sawasawa na maneno yake. Vivyo hivyo katika maeneo mengine. Sikumbuki kutamka jambo halafu asilitende bila sababu za msingi....!

Kwangu mimi huyu ndiye mgombe aliyeni - inspire na kunivutia katika uchaguzi huu. Sina mashaka wala wasiwasi naye. Nafsi yangu ni nyeupe kabisa...

Huyu ndugu kwa hakika ni TUNU YA TAIFA hili. Ni machachari and very unique. Nitampa kura yangu mimi na familia na jamaa na rafiki zangu wote....
 
Ongezea na hii: ....mgombea urais aliyekuja na nuksi ya kuambulia wabunge 4 tu kwa chama chake na kupata kura kiduchu kuwahi kutokea single digit 7% ya kura za urais!
 
Ongezea na hii: ....mgombea urais aliyekuja na nuksi ya kuambulia wabunge 4 tu kwa chama chake na kupata kura kiduchu kuwahi kutokea single digit 7% ya kura za urais!

Wewe kweli ni "ndebile" mtoto uliyezaliwa prematurely hata ufahamu na akili yako ni purely prematurely hata sasa...!!
 
Acha wivu wa kike mtoto,hata wewe utaolewa tu
Unadhani kura za lissu zitahesabiwa? Wanakadilia tu za kumtosha yeye na mbowe basi..., 7% bado naona nyingi sana.tatizo kuu ni kwamba lissu si mtu mzuri kwa usalama wa taifa,hafai.ilikuwa makosa tu akapona zile risasi,kimahesabu hakutakiwa kuwa hai.hivi unadhani waliompiga risasi hawana akili?
 
Tangu kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na uchaguzi mkuu wa kwanza wa mwaka 1995, Tanzania haijawahi kushuhudia na kupata mgombea wa upinzani machachari na mwenye ufahamu wa hali ya juu wa mambo mbalinbali kitaifa na kimataifa katika nyanja za elimu, siasa, historia, sheria, uchumi nk kama Tundu Lissu (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020...!

Kina Mrema (1995), Lipumba (2000), Freeman Mbowe na Lipumba (2005), Dr Slaa (2010) na Lowassa (2015) walikuwa wagombea Urais wenye sifa zao za kipekee, lakini Tundu Lissu anawazidi wote kwa kuwa na sifa za ziada na kufanya upekee wake uwe maalumu kama nitakavyojaribu kueleza hapa chini...

Naandika thread hii baada ya kuisikiliza sehemu ya hotuba ya mgombea Urais huyu kwa tiketi ya CHADEMA ya jana tarehe 28/9/2020 akiwa Mugumu - Serengeti mkoa wa Mara....

Ni hotuba ambayo imajaa elimu ya uraia na sheria huku ikifunua UJINGA na UPUMBAVU wa viongozi wengi wa serikali ya CCM ya Magufuli wasiojua sheria, kanuni na taratibu za kusimamia dhamana zao za uongozi kwa ajili ya ustawi wa jamii na amani yetu....

RCO ya Mara, DC na DED wa Serengeti ni mfano mzuri wa viongozi wajinga na wapumbavu. Wapewa dhamana ya uongozi wa mamilioni ya watu, lakini kwa kutojua ama kwa makusudi wao ndiyo wanakuwa wavunjaji wakubwa wa sheria na taratibu....

Ukiacha hili, upekee wa Tundu Lissu ukilinganisha na wagombea wote wa upinzani waliowahi kugombea Urais tangu mwaka 1995 unajitokeza katika maeneo haya;

1. UFAHAMU MKUBWA WA MAMBO:

Huyu bwana amejaliwa kuwa na ufahamu wa hali ya juu wa mambo mengi kuanzia ktk nyanja ya historia, uchumi, jamii, siasa, sheria na utamaduni...

Hii humwongezea ujasiri wa kusimama na kutetea chochote kinachokuja mbele yake na mara zote anakuwa mshindi tu. Hii inatuleta kwenye sifa ya pili...

2. UJASIRI:

Kwa kuwa kajaliwa kuwa na ufahamu mpana wa mambo mbali ya kitaifa na kimataifa karibu katika nyanja zote za maisha, hii imempa hiki kitu kingine yaani - UJASIRI...

Naye sasa anatumia kila njia ku - influence tabia hii ya ujasiri, kutokuwa na hofu ama woga kwa watu wote anaokutana nao. Hapa ndipo hasa ulipo mgogoro wake na watawala. Hili huwatia hofu na woga mkubwa watawala hawa waovu....

Wanajua kuwa watu wakielimishwa, wakatambua WAJIBU na HAKI zao, wataiondoa serikali hii madarakani kufumba tu na kufumbua. Hili linaiogopesha sana CCM na serikali wanayoingoza....

3. NI MSOMAJI SANA WA VITABU HUYU JAMAA:

Ili kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali, sharti utafute maarifa. Sharti usome vitabu na vyanzo vingine mbalimbali vya maarifa...

Huyu ndugu anasoma sana. Simjui na wala sijawahi kukutana naye uso kwa uso karibu. Lakini ninapomtazama kwenye TV akiongea, mtu mdadisi atatumbua hili moja kwa moja...

Ukisikiliza na kutazama hotuba yake ya jana Serengeti utaelewa nikisemacho hapa. Utaelewa kuwa huyu mtu amejaza maarifa kichwani mwake na si matope kama alivyo Polepole ama Cyprian Musiba wa CCM.....

4. NI MGOMBEA PEKEE KATI YA WOTE ALIYETOA UHAI WAKE KWA AJILI YA HAKI ZA WENGI:

Hii ni sifa very exceptional. Huyu bwana amepitia njia ngumu mno hadi kufikia hatua hii aliyonayo hapo kwa ajili ya kutetea haki za wananchi wa taifa hili zuri la Tanzania...

Huyu ndugu kwa siku saba achilia mbali miaka miwili na ushee akiuguza majeraha ya risasi kitandani, alikuwa kuzimu. Alionja KIFO na MAUTI lakini kwa sababu anazojua Mungu mwenyewe, alimfufua tena Tundu Lissu. Yuko hai na ndiye huyu ambaye watu wanamuona kama Messiah wao na basically ndivyo ilivyo, ndivyo itakavyokuwa....

5. NI SPEECH GIVER & INFLUENCER MZURI KUPINDUKIA. HUCHOKI KUMSIKILIZA..!!

Wanasiasa wenye kipaji cha namna hii ni wachache mno Tanzania. Huko nje namfahamu mtu mmoja, Martin Luther King Jr, mpigania haki za weusi wa Marekani miaka ile...

Hotuba za Tundu Lissu ni za kushawishi, kuhamasisha, kutia morali na kuwaondolea watu hofu, mashaka na woga....

Watu kama hawa siku zote ni HATARI katika serikali zote za kidikteta zinazogandamiza UHURU na HAKI za kiraia...

Huwindwa kama wanyama pori ili kuwaua kama njia pekee ya kuwaondoa maana HOJA ZAO mara zote hazijibiki na Mara zote ni chungu na zinachoma mithili ya mkuki moyoni...

Mara zote watu wa aina hii hugeuziwa kibao na kuitwa wachochezi, wahamasisha vurugu na wahatarisha amani. Hutungiwa hata sheria kwa ajili yao tu...

Hii yote, kosa lao ni moja tu. Kufumbua macho, akili na ufahamu wa watu wa kutambua WAJIBU na HAKI zao dhidi ya serikali na viongozi wao....!!

Huyu ndugu kwa hakika ni TUNU YA TAIFA hili. Ni machachari and very unique. Nitampa kura yangu mimi na familia na jamaa na rafiki zangu wote....

Mwanasiasa mmoja hata awe mzuri kiasi gani, hawezi kuleta mabadiliko katika li nchi kubwa kama Tanzania.

Wanatakiwa wawepo kina Lissu wengi na karibu kila sehemu ili anayotamka kubadilika yatokee.

Tuendako atapotea kwa kuwa atapoteza jukwaa baada ya uchaguzi na platforms za kuzungumzia zitakua chache sana.

Kwa generation ya elected leaders wa CCM watakao kuja bungeni patawaka moto.

Angekuwa na impact kubwa sana kama angechagua topics mbili au tatu na akasimamia hizo hizo kama alivyokuwa Dr. Slaa kuhusu Ufisadi. Vinginevyo akiwa generality politician atashindwa kusimamia anachokitaka kupandikiza kwa Watanzania.
 
Rudia kumsikiliza
Amechagua topic ya kubadili mfumo wa utawala wa nchi kupeleka nguvu za utawala katika majimbo.
Mwanasiasa mmoja hata awe mzuri kiasi gani, hawezi kuleta mabadiliko katika li nchi kubwa kama Tanzania.

Wanatakiwa wawepo kina Lissu wengi na karibu kila sehemu ili anayotamka kubadilika yatokee.

Tuendako atapotea kwa kuwa atapoteza jukwaa baada ya uchaguzi na platforms za kuzungumzia zitakua chache sana.

Kwa generation ya elected leaders wa CCM watakao kuja bungeni patawaka moto.

Angekuwa na impact kubwa sana kama angechagua topics mbili au tatu na akasimamia hizo hizo kama alivyokuwa Dr. Slaa kuhusu Ufisadi. Vinginevyo akiwa generality politician atashindwa kusimamia anachokitaka kupandikiza kwa Watanzania.
 
Lisu mdio mgombea pekee atakae sababisha ruzuku ya chadema kupungua kutokana na kupata kura kidogo sana
 
Ogopa sana spana za huyu mtu anayeitwa Tundu Lissu zimewaingia CCM hadi imefikia hatua mgombea wa CCM na polepole na meza kuu wanawapigia wananchi magoti na kuwaomba kura 🤣
 
Ongezea na hii: ....mgombea urais aliyekuja na nuksi ya kuambulia wabunge 4 tu kwa chama chake na kupata kura kiduchu kuwahi kutokea single digit 7% ya kura za urais!
Haya mawazo ya kipumbavu inafaa uwapelekee wapumbavu wenzako huko Lumumba
 
Rudia kumsikiliza
Amechagua topic ya kubadili mfumo wa utawala wa nchi kupeleka nguvu za utawala katika majimbo.

Mkuu nitafurahi kama tutakuwa na uchambuzi bila ushabiki ili kila mmoja wetu atajirike na mwenzake, na sio vinginevyo. Sisi watu wa mjini tumekwisha piga kura myoyoni kwetu itakapo fika tarehe 28th, October tutatumbukiza kura tuu, kwa hiyo michango ituelimishe.

Mimi ninajitahidi sana ninapokuwa na muda kufuatilia kwa undani kinacho endelea na philosophy ya Mwanasiasa. Lissu anaweza kuelezea jambo kwa upana bila philosophy yake, kitu ambacho kwa kufananisha, Dr. Slaa alikuwa mzuri sana.
Mfano: Suala la majimbo kuna maeneo ambayo jamii haina intergration kubwa hilo swala watalikubali kirahisi, lakini sehemu yeyote ambayo jamii imekuwa na intergration ya juu na mikoa na jamii nyingine, suala la majimbo linakuwa mtihani.

Mfano, suala la majimbo mkoa wa kilimanjaro itabidi ufanye kazi ya ziada wananchi walikubali, japo utekelezaji uko tofauti na wanavyo dhani, na sababu ni jamii ya Kilimanjaro imetawanyika sana karibu nchi nzima na wakirudi Kilimanjaro hawatotosha.

Nitakupa mfano mwingine wa mawasiliano ambao watu wengi ambao hawajui umuhimu wa kuconnect message yako kwa walengwa wana shangaa sana Magafuli anavyo fanya kampeni zake.

Kwa muono wa kawaida Magufuli ni mshamba: Lakini sisi binadamu tuna taabu sana.
Mfano kwetu Upareni, ukichonga kiswahili na kikanyooka wazee watakwambia huyu ni Mnyika na mswahili. Maana yake halisi ni mtoka mbali kwa hiyo wanatakiwa kujihadhari na wewe. kiswahili kikikupa taabu kidogo, yaani hakikunyooka, wao ni rahisi kukuamini. Mwenye kunyoosha kiswahili anaitwa Mswahili- maana kamili ni mtu wa kuchukulia tahadhari nae.

Tusishangae Magufuli ambae sisi tuna muona mshamba, kwa watu wa mikoani inawezekana wanamuani zaidi kwa kuwa wanamuona ni mshamba mwenzao kwa kusindwa kunyoosha kiswahili, kwa hiyo wanaona hawadanganyi.

kila Mwanasiasa lazima achomeke uongo japo kidogo anapotaka kunogesha ujumbe anao uwakilisha.
 
Back
Top Bottom