Tunaweza kuwa waislam au wakristo bila ya kubeba tamaduni za waliotuletea dini hizo?

Dini ni utamaduni. Dini ni mwenendo. Utakuaje na dini kisha usifuate utamaduni,mwenendo na maadili yake?
Labda iwe dini mpya ila sio hizo
Unaweza kumuabudu YAHWE na ALLAH bila kufuata Tamaduni za Kigeni.

Hii inaitwa Africanization.
 
Ukristu inawezekana ila Kwa wale wanaomwabudu mwarabu haiwezekani ,kuanzia Mavazi, lugha, vyakula, Kila kitu wamemwiga mwarabu
 
Umeielewa hoja? Hoja inahoji juu ya imani kubebeshwa utamaduni.
Unakuta jitu liko Mtwara ndani ndani huko, linaotwa Omar Omar Ramadhan, au Erick Patrick Steven, sasa unajiuliza, jina lake la ukoo la mababu zake liko wapi?! Mtu hawezi akaitww Omar maneno na akawa muislam?
Majina hayana tofauti ,kwa sababu yana maana yake ...

Jina halina maana kama utazingatia maana yake ,naweza kumuita mwanangu jina ila nina maana fulani au linawakilisha kitu fulani...Kikubwa ni kujua maana tu.

Mfano wangoni wanaita watoto wao majina ya wanyama kama komba ,tembo ,nyani hata nguruwe ila wanajua maana yao kweny tamaduni zao
 
Nimejikuta nawaza kama mkristo anaweza kuvaa kanzu na Barghashia na kwenda ibadani kanisani na wakristo wenzake wakawa na amani naye.

Lakini nikawaza pia kama Muislam anaweza kumuadhinia mtoto wake Jina la Edward na waislam wenzake wakaona ni sawa.

Hivi tunaweza kuwa waislam ama wakristo huku tukitupilia mbali tamaduni za waliotuletea dini hizo?
Wafadhili wakituona hivyo watakubali kweli kuendelea kutuletea tende na vile viatu/nguo za mitumba wanazotuleteaga?
 
Ndio hapa utajua wavaa kamzu akili hawana, hawajui kwamba wale waarabu walivaa kanzu, kufuga ndevu na kuongea kiarabu kabla hata mudi hajazaliwa
Yeah, na ndo hapo utajua wavaa misalaba akili WANAZO tele maana utaona mapaja na vyupi kwenye mabenchi ndani ya kanisa kama wazungu huku nao wakifurahia ruhusa ya papa ya wanaume kuolewa........wanajihisi wazungu kamili, tena wale original wa uingereza.
 
Kinacho nisikitisha tumeyatelekeza hata Majina yetu ya Mila zetu.

Tumebaki kuitwa akina Ramadhani na Joseph.
Na kupoteza hata lugha zetu za Asili na kumpenda Kiarabu.
 
Inawezekanaje mkuu na wapi imewahi kutokea?!!!
Mbeya wanasali mpaka kwa kinyakyusa na BIBLIA ya Kinyakyusa huwezi kuwaambia eti lugha fulani ndio ya kusalia watakuona mwehu,vyakula vya kwao huwezi kuwaambia eti vya kizungu au kiarabu ndio vizuri kama huko Pwani.Kanzu ishafanywa ni utamaduni wa mashariki ya kati huwezi kumshawishi mtu mwenye utimamu wa akili ukaihusisha na imani.Andendekisye,Tumpale,Aswile,Bupe....ni majina pendwa na ya kujivunia.Nachukia kukutana na mtu ananisalimia salam aleko ni utumwa maana kiswahili kipo cha maana ya hiyo salaam.
 
Nimejikuta nawaza kama mkristo anaweza kuvaa kanzu na Barghashia na kwenda ibadani kanisani na wakristo wenzake wakawa na amani naye.

Lakini nikawaza pia kama Muislam anaweza kumuadhinia mtoto wake Jina la Edward na waislam wenzake wakaona ni sawa.

Hivi tunaweza kuwa waislam ama wakristo huku tukitupilia mbali tamaduni za waliotuletea dini hizo?
SIjui kama uislamu unawezekana bila uarabu wa aina fulani.
 
Mbeya wanasali mpaka kwa kinyakyusa na BIBLIA ya Kinyakyusa huwezi kuwaambia eti lugha fulani ndio ya kusalia watakuona mwehu,vyakula vya kwao huwezi kuwaambia eti vya kizungu au kiarabu ndio vizuri kama huko Pwani.Kanzu ishafanywa ni utamaduni wa mashariki ya kati huwezi kumshawishi mtu mwenye utimamu wa akili ukaihusisha na imani.Andendekisye,Tumpale,Aswile,Bupe....ni majina pendwa na ya kujivunia.Nachukia kukutana na mtu ananisalimia salam aleko ni utumwa maana kiswahili kipo cha maana ya hiyo salaam.
Okaaay!
 
Utanadunisho.Yawezekana ukawa na/dini fulani na kuendelea na mambo yahusuyo utamaduni wako.Lakini,usichanganye na yanayokatazwa na hiyo dini.Kwa mfano,ulozi na kuabudu miungu hasahasa ukristu.
 
Yeah, na ndo hapo utajua wavaa misalaba akili WANAZO tele maana utaona mapaja na vyupi kwenye mabenchi ndani ya kanisa kama wazungu huku nao wakifurahia ruhusa ya papa ya wanaume kuolewa........wanajihisi wazungu kamili, tena wale original wa uingereza.
Kushabikia dini bila elimu ni ujinga na utumwa.
 
Hata kama watu tunajadili kishabiki Lakini tuzame kwenye mantiki ya swali.

Siku hizi ni kawaida kukutana na kina Irene Joseph Paul bila kujua kama huyu ni mtoto wa Mzee Joseph kimemeneke wa Lindi.

Ukifika Zanzibar unakutana na kina Omar Jafar Mohamed kumbe ni mfarinyaki wa kutoka Songea.

Tukisema inawezekana kuwa Muislam bila ya kuonesha kuegemea kwenye tamaduni za Kiarabu, tutakuwa tunadanganya.

Na tukisema inawezekana kuwa Mkristo bila ya kuonesha kuegemea kwenye tamaduni za kizungu, tutakuwa tunadanganya pia.

Hivi tende na father krismass ni sehemu ya Imani!!??
 
Dini ni utamaduni. Dini ni mwenendo. Utakuaje na dini kisha usifuate utamaduni,mwenendo na maadili yake?
Labda iwe dini mpya ila sio hizo
Tamaduni zilikiwepo kqbla ya dini,
Mfano kuvaa bulqa,lile vazi kama wavaavyo wanawake wa Afghanistan, lilikuwepo kqbla ya uislam,
Kule ni, jangwa, hakuna vichaka, sasa, mwanamke akitaka kujihifadhi, ilikuwa,shida,wanawake walihitaji, kujihifadhi, lile vazi linawawezesha kuchutama na kujihifadhi, sasa akaja Mudi na uislam wake, akalifanya vazi la dini,
Mikate ni cha kula cha watu wa Arabia, Sisi tutasema utupe ugari wetu wa kila siku, sio mikate, dini ni uhusiano na Mungu,dini sio kabila, tamaduni zote ni za Mungu, lazima yupo comfortable kufatwa kupitia utamaduni wowote,
Yani niitwe Rahman, au Hashim, harafu mkristo, Jesus aseme sikutambuhi,! Kisa sijaitwa Joseph, Mike au Luke, au Jordan! yaani, Mungu anabagua majina na tamaduni,! Pathetic
 
Back
Top Bottom