Tunaweza kuwa waislam au wakristo bila ya kubeba tamaduni za waliotuletea dini hizo?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,330
33,961
Nimejikuta nawaza kama mkristo anaweza kuvaa kanzu na Barghashia na kwenda ibadani kanisani na wakristo wenzake wakawa na amani naye.

Lakini nikawaza pia kama Muislam anaweza kumuadhinia mtoto wake Jina la Edward na waislam wenzake wakaona ni sawa.

Hivi tunaweza kuwa waislam ama wakristo huku tukitupilia mbali tamaduni za waliotuletea dini hizo?
 
Ndio hapa utajua wavaa kamzu akili hawana, hawajui kwamba wale waarabu walivaa kanzu, kufuga ndevu na kuongea kiarabu kabla hata mudi hajazaliwa
Rudi kusoma kwanza ,maelezo yote yapo kweny uislamu ,jaribu kusoma kwanza usiwe unakurupuka waislamu wanatao kila kitu kilchopo kimefundishwa 😅😅.

Hamna mavazi kama kanzu sio lazima ,unavaa chochote kile na watu wote wapo sawa ... Fashion ya mvazi hata suti tunatumia za wazungu sio utamaduni wa Africa.

Nenda angalau senegal ,Nigeria ukaone wanavyovaa kiasilia si waislamu wala wakristo.

Mavazi ni kwa vile imported watu wanavaa styl watakazo, kuna black American style kama jeans na mavqzi ya mashariki ya kati
 
Nimejikuta nawaza kama mkristo anaweza kuvaa kanzu na Barghashia na kwenda ibadani kanisani na wakristo wenzake wakawa na amani naye.

Lakini nikawaza pia kama Muislam anaweza kumuadhinia mtoto wake Jina la Edward na waislam wenzake wakaona ni sawa.

Hivi tunaweza kuwa waislam ama wakristo huku tukitupilia mbali tamaduni za waliotuletea dini hizo?
Ukristo wa ukatoliki uliweza kufanya hivyo ila lengo kuu ilikua ni kuvuta watu wa jamii hio kuwa upande wao.
Kwa mfano kule Kilimanjaro wakati wanaingia wamisionari hawakuenda kinyume na utamaduni wao, kwamba utabatizwa jina la kidini lakini lazima uwe na jina la nyumbani ambalo litakuwa la kikabila au utamaduni huo ambalo lita wekwa pamoja kwenye kitambulisho cha ubatizo.
Pombe aina ya mbege hakikuzuiliwa hata sehemu ya matoleo kanisani mbege ilipelekwa, jani fulani la ki mila lilitumika kuombea msamaha nalo lilikuwa sehemi ya ibada, na mengi mengi lakini yote hayo yalifanyika bila kuathiri utamaduni wa kirumi mpaka leo.
 
Wakristo wanaovaa kanzu na bargashea wapo ,hii ilikuwa ni tamaduni ya waafriva kabla ya kuja kwa mzungu ,sina hakika kama walileta waarabu ila ukiangalia hata machifu huko uchagani walikuwa wanavaa muundo wa kofi na panjabi.

Waafrica walivaa nguo ndefu katika mfumo wa mashuka ,pajabi au kanzu ...Pia utaratibu wa kufunika kichwa ,ndio maana watu walikuwa wanafikria Mrema ni muislamu 😅😅😅.

Suti zililetwa na wazungu na kulazimisha kweny Uongozi wao kuwalisha watu.

Vijijini vingi kaskazini wanavaa wazee .

Screenshot_20240401-123035.png

tanzania_mangi-meli-and-his-njama-1890s-at-moshi-boma.jpg
 
Nimejikuta nawaza kama mkristo anaweza kuvaa kanzu na Barghashia na kwenda ibadani kanisani na wakristo wenzake wakawa na amani naye.

Lakini nikawaza pia kama Muislam anaweza kumuadhinia mtoto wake Jina la Edward na waislam wenzake wakaona ni sawa.

Hivi tunaweza kuwa waislam ama wakristo huku tukitupilia mbali tamaduni za waliotuletea dini hizo?
Sahau kwani aujui dini ni kama ugonjwa wa akili yani ukijiingiza tu tiyali Mizembe moja iyo.
 
Zanzibar mbona wapo waislamu wanaitwa Makame, jecha, pandu, Mosi, Shaame n.k
hayo yote si majina ya kiarabu bali ni ya kiasili ya mswahili

edward ni majina ya kimagharibi, naamini huko kwenye nchi za kimagharibi wapo waislamu wenye majina hayo.

Je kuna muislamu mwenye asili ya kiarabu anayeitwa EDWARD?
sidhani, kwa sababu si majina ya asili yao.
==================
Mikoa wapo wana majini ila dini tofauti ,nimesoma na jamaa wawili ni maostadh tena wakubwa wana majina ya kikristo full .

Historia ya hii nafikiria tusiweke hapa panaweza kuibuka mjadala ,ila ukweli waliweka majina hayo ili wasome palikuwa na ubaguzi wa kielemu kidogo.

Ukienda Mbeya wapo wana majina ya kiislamu ila ni wakristo maana wamekulia kule ...Kuna jamaa mmoja alikuwa anaitwa Hashimu said ni mkristo pure .

Ukienda Tanga ,lindi , Mtwara watu wana majina mawili mawili la kikristo ndio wanatumia shule ..Ndio manaa mikoa hiyo kukuta familia ina wakristo na waislamu kawaida na wanaishi fresh .
 
Ngumu sana hasa kwa jirani wa mwarabu. Ukiangalia sinema ya Yesu mavazi wanayovaa wana wa mnyazi wameyaiga pale hadi kufuga ndevu tele na bado wanakomalia ni utamaduni wao na wao ndio wameigwa duh aiseee
 
Ukristo wa ukatoliki uliweza kufanya hivyo ila lengo kuu ilikua ni kuvuta watu wa jamii hio kuwa upande wao.
Kwa mfano kule Kilimanjaro wakati wanaingia wamisionari hawakuenda kinyume na utamaduni wao, kwamba utabatizwa jina la kidini lakini lazima uwe na jina la nyumbani ambalo litakuwa la kikabila au utamaduni huo ambalo lita wekwa pamoja kwenye kitambulisho cha ubatizo.
Pombe aina ya mbege hakikuzuiliwa hata sehemu ya matoleo kanisani mbege ilipelekwa, jani fulani la ki mila lilitumika kuombea msamaha nalo lilikuwa sehemi ya ibada, na mengi mengi lakini yote hayo yalifanyika bila kuathiri utamaduni wa kirumi mpaka leo.
Ukatoliki unaendana na mambo mengi ya asili
 
Kuhusu jina waislam hatuna shida wala hatuja katazwa kutumia jina la kingereza cha msingi tu liwe na maana nzuri
Lakini nikawaza pia kama Muislam anaweza kumuadhinia mtoto wake Jina la Edward na waislam wenzake wakaona ni sawa.
Ni utamaduni tu wa waswahili kwa waislam majina ya kiarabu na wakristo ya kizungu
 
Nilipanda usafiri wa umma naona mdada mmoja kavaa shungi yuko na kisimu chake ana play nyimbo sijui za kihindi,kiarabu mithili ya nyimbo za dini yao ,, nikamuangalia nikacheka tu,, niliwaza vitu vingo sana namna tunadanganywa
 
Rudi kusoma kwanza ,maelezo yote yapo kweny uislamu ,jaribu kusoma kwanza usiwe unakurupuka waislamu wanatao kila kitu kilchopo kimefundishwa 😅😅.

Hamna mavazi kama kanzu sio lazima ,unavaa chochote kile na watu wote wapo sawa ... Fashion ya mvazi hata suti tunatumia za wazungu sio utamaduni wa Africa.

Nenda angalau senegal ,Nigeria ukaone wanavyovaa kiasilia si waislamu wala wakristo.

Mavazi ni kwa vile imported watu wanavaa styl watakazo, kuna black American style kama jeans na mavqzi ya mashariki ya kati
Umeielewa hoja? Hoja inahoji juu ya imani kubebeshwa utamaduni.
Unakuta jitu liko Mtwara ndani ndani huko, linaotwa Omar Omar Ramadhan, au Erick Patrick Steven, sasa unajiuliza, jina lake la ukoo la mababu zake liko wapi?! Mtu hawezi akaitww Omar maneno na akawa muislam?
 
Back
Top Bottom