GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,694
- 109,128
Jina la Marehemu nalihifadhi...
Kazaliwa tarehe 7 Mwezi July, 2023
Kafariki tarehe 6 Mwezi July, 2023
Kaburi la huyu Marehemu Mpendwa liko Makaburi ya Mzimuni Kawe mita chache tu upande wa Mashariki ulipo Mbuyu mkubwa wenye Vitimbi vingi na Matukio mengi.
Kadhia hii hii (ambayo ipo sana katika Makaburi ya Ndugu zetu Waislamu japo hata kwa Wakristo pia hutokea japo kwa Nadra sana) nimeshawahi kuiona pia katika Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam na yale ya Kola Morogoro.
Ulale mahala pema Peponi Rafiki yangu wa Ujanani na Ukubwani hivi Hamad Abdallah Abedi (Mtoto wa Imam wa Msikiti mkubwa wa Kawe Ukwamani) uliyefariki dunia Jana Kijijini Kwenu Kilwa.
Hukuwa na Cheo chochote, Utajiri wowote wala Umaarufu wowote, ila Umati mkubwa sana Uliokuzika leo Saa 5 Asubuhi kuelekea Saa 6 Mchana ni Kiashirio tosha kuwa ni kweli ulikuwa ni Mtu wa Watu katika Jamii na ndiyo maana Umeliliwa na kila Mtu na GENTAMYCINE nitakukumbuka mno, kwa mengi na hasa Urafiki wako mkubwa nami huku ukiwa pia ni Msaada Kwangu Kiushauri na hasa ukiwa ni Mtani wangu mkubwa wa Mpira Wewe ukiwa ni Yanga SC lia lia nami nikiwa ni Simba SC Kindakindaki.
Mwenyezi Mungu ampe Subira Shemeji (Mkeo) na Mtoto wako, awapiganie, awape Nguvu na anibariki Uchumi mzuri nami GENTAMYCINE ili basi Siku moja niweze kuwa Msaada kwa Mjane (Mkeo) na Mwanao Mpendwa.
Pumzika mahala pema Peponi Hamadi Abdallah Abed.
Nitakukumbuka na sijui sasa Yanga SC yako ikishinda au ikifungwa nitataniwa na nani au nitamtania nani.