Tribute to Halima Mchuka: Alikuwa Mtu wa Watu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tribute to Halima Mchuka: Alikuwa Mtu wa Watu!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pascal Mayalla, Dec 29, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,618
  Trophy Points: 280
  Wanabodi leo saa 11:30 alfajiri nimepokea simu ya Da Mwajuma Mchuka kunijulisha kuhusu huu msiba!.

  Hii ni thread ya Tribute kuhusu nilivyonfahamu marehemu.


  My Tribute To Halima Mchuka!

  Halima Mchuka alipoajiriwa RTD, batch yangu ndiyo iliwatangulia!. Ilitokea tuu huyu dada tulielewana sana na alitokea kuwa ni mtu wangu wa karibu!.

  Wakati huo akiishi na dada yake anayefanya kazi ATC, Mwajuma Mchuka sisi tukimwita kwa kifupi Da Mwajuma. Da Mwajuma alikuwa anamiliki flat ya familia mbili hapo Ilala Shariff Shamba nyumba ya pili kutoka lile ghorofa refu pale kituo cha Bungoni.

  Wakati huo mimi nikiishi kwa wazazi Mikocheni, kufuatia umbali kati ya RTD na Mikocheni enzi hizo lazima upande mabasi matatu, Utoke Mikocheni upandishe njia ya TPDC mpaka kituo cha Maji Machafu (siku hizi Sayansi), upande gari ya Mwenge Kariakoo ushuke Magomeni. Upande gari ya Ilala Drive-In ushuke Ilala Boma, upande gari ya Buguruni Kariakoo, ushuke Buguruni utembee kwa miguu mpaka Tazara ndipo uingie ofisini!.

  RTD walikuwa na basi moja la wafanyakazi route yangu halipiti, hivyo mimi nilikuwa ni mtu wa kuchelewa kufika kazini kila siku ambazo sikuwa zamu. Siku ukiwa zamu, unafuatwa nyumbani.

  Kufuatia kuchelewa huko, Halima Mchuka akanishauri kwanini nisihame nyumbani na kuhamia eneo la karibu na kazini?. Akasema kama vipi azungumze na Da Mwajuma, aniruhusu nitumie chumba kimoja kwenye flat yao ina vyumba 4 na wao wako watatu, yeye, dada yake Da Mwajuma na mdogo wake Rehema!.

  Da Mwajuma alikubali ombi la mdogo wake Halima hivyo mimi nikakaribishwa rasmi Ilala na huo ndio ukawa mwanzo wangu wa maisha ya kujitegemea!.

  Asante sana Halima Mchuka kunifungulia milango ya maisha ya kujitegemea!.

  Nikiishi hapo yeye na Da Mwajuma walinichukulia kama mwanafamilia, sikuwahi kupika!. Asante Halima Mchuka kwa yote!.

  Baada ya kipindi kifupi, Da Mwajuma alihamia kwenye nyumba yake Masaki hivyo kutuachia flat zima la two appartments za two bedroms each, ndipo Halima akachukua upande wake na mimi upande wangu ambapo nami nikamkaribisha mtangazaji mwenzangu Aboubakar Liongo.

  Tuliishi vizuri tuu akaanza Halima kuolewa na kuishi na mmewe kule upandewake, nikafutia mimi nikao hapo hapo familia ilipoanza kuwa kubwa nikahama na kumuchia Abou ambaye nae aliolea hapo hapo!

  Halima ameacha mume, watoto watatu Amina, Yekini na Prince Naseem.

  Thanks a Millions Halima Mchuku, Mungu Aiweke Roho yako mahala pema peponi.

  RIP Halima Mchuka!.
  Update 1.

  Msiba wa Halima Mchuka, upo nyumbani kwa dada yake mkubwa Mwajuma Mchuka, Mbezi Beach nyuma ya maghorofa ya BOT.

  Mazishi ni kesho saa 5 asubuhi katika makaburi ya Msasani. Mwili utaswaliwa katika msikiti wa Msasani kabla ya swala ya Ijumaa.

  Chanzo cha kifo ni shinikizo la damu. Jana mchana alitangaza kipindi cha salaam za mchana TBC-Taifa na inasemekana alitangaza vizuri ajabu!. Kitu cha ajabu jana aliwatumia sms wanae wawili waliopo nchini, na kuwaambia wamsikilize akitangaza akawaambia na muda. Masikini kumbe ndio kama kuwaaga kiaina kwa kuwaambia waisikilize sauti yake kwa mara ya mwisho!. Mara baada ya kipindi ndipo pressure ikampanda, akakimbizwa pale Dar Group na baadae Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mauti yalipomkuta!.​
  Update Two.
  Mwili utaswaliwa msikiti wa Muhimbili saa 3:30 asubuhi na maziko yatafanyika makaburi ya Msasani.
  Update 3.
  Leo asubuhi, Mwili wa Halima Mchuka, umeswaliwa katika msikiti wa Muhimbili na kuagwa na umati mkubwa wa waombolezaji ukiongozwa na rais Jakaya Kikwete, mkuu wa mkoa wa DSM, mawaziri, wabunge, likiwemo kundi kubwa la wanahabari.

  Msafara kuelekea mazikoni makaburi ya Msasani ukafuatia na hatimaye kuzikwa na umati mkubwa wa watu.

  Halima Mchuka pata pumziko la milele...
  Amen.
  Final Update.  [​IMG]
  HALIMA M. MCHUKA (18 Mar.1967- 29 Dec. 2011)​

  Familia ya Mchuka wa Dar es Salaam, pamoja na ndugu wote walioko Miono na Kibindu-Bagamoyo, wanatoa shukrani za dhati kwa wote mlioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kipindi kigumu cha msiba wa mpendwa wao, Halima Mohamed Mchuka uliotokea tarehe 29/12/2011 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuzikwa tarehe 30/12/2011 katika makaburi ya Msasani Dar es Salaam.

  Shukrani za pekee ziwaendee, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo,Mhe. Dkt.Emanuel Nchimbi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto, Mhe. Sofia Simba, Naibu Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo,Mhe. Dkt. Fenella Mukangara, Waheshimiwa wabunge wa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam, IGP, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mstahiki Meya wa Ilala.

  Shukrani nyingine ziwaendee viongozi na wafanyakazi wa TBC wakiongozwa na M/Kiti wa Bodi ya TBC, Wilfred Nyachia na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana, wafanyakazi wastaafu wa RTD, wafanyakazi wa kampuni ya Ndege Tanzania, Madaktari na wauguzi wa hospitali za Dar Group na Muhimbili, viongozi wa vyama vya michezo, waandishi wa habari na watangazaji wa vyombo mbalimbali vya habari, Uongozi wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, BAMITA, majirani wa Karakata, Msasani, Mabibo na Mbezi, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote wa familia ya MCHUKA wa ndani na nje ya nchi. Tunawaomba mpokee shukrani zetu za dhati kwa kutufariji kufuatia kifo cha HALIMA MCHUKA.

  Arobaini ya Marehemu itafanyika Miono Bagamoyo siku ya Ijumaa Tarehe 3/02/2012 kuanzia saa 11:00 jioni na Hitma itasomwa Jumamosi ya Tarehe 04/02/2012 saa 3 :00 asubuhi.Nyote mnakaribishwa.

  Kwa taarifa zaidi wasiliana na wanafamilia moja kwa moja au kupitia simu namba 0713477790 au 0784737253.Karibuni.

  INNA LILLAH WAINNA ILAYHI RAAJIUN

   
 2. s

  sawabho JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Ingawa sijawahi kufanya naye kazi kwa karibu, lakini nilikuwa navutiwa sana na sauti yake wakati akitangaza mpira wa miguu.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  rip halima!
   
 4. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Siamini kama ni makosa kukupa pole Pascal kwa msiba huu. Fikisha pole zangu kwa Da Mwajuma, Rehema, Mume na Watoto wa Marehemu pamoja na wanafamilia wote! Ni msiba mkubwa kwa kweli!
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Pasco,

  Pole kwa msiba wa Halima Mchuka, naamini kwa namna ulivyoishi naye umekuwa sehemu ya familia yao.

  Mimi namkumbuka nikimsikia akirindima redioni RTD kwenye vipindi vya michezo na hatimaye akitangaza mpira wa miguu.

  Ni mwanamke wa kwanza kupata kumsikia akiandaa vipindi vya michezo na kubwa kuliko yote alikuwa ni mwanamke pekee niliyepata kumsikia akitangaza mpira wa miguu "live" kutoka viwanjani. Mara ya mwisho kumsikia akitangaza mpira ilikuwa michuano ya kombe la tusker, wakati huo ikishirikisha vilabu vya Tanzania pekee.
   
 6. M

  Masuke JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mimi nimesikia taarifa hizi alfajiri kwenye kipindi cha Kombora usingizi ukaishia hapo hapo, pole Pasco, Da Mwajuma na watangazaji wote wa TBC, hakika tutaimiss sana saut ya mwanadada huyu, nakumbuka jinsi walivyokuwa wanatangaza mpira na ndugu Ezekiel Malongo kwa kweli ilikuwa raha kuwasikiliza hata kama timu yako imefungwa bado ungetamani tu kuendelea kuwasikiliza.
   
 7. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  pole wafiwa
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Pasco.

  Pole kwa msiba mzito.Baada ya kusoma bandiko lako mara moja nikapata picha Halima Mchuka alikuwa mtu wa namna gani.

  Sina uhakika sana ila nahisi Halima Mchuka na wewe hamtoki mkoa mmoja wala si waumini wa dini moja kama ndivyo basi shukrani za mwanzo ziende kwa Baba wa Taifa letu changa Mwl J K Nyerere ambaye alijitahidi katika uongozi wake wote kutufanya waTanzania wamoja.Alipiga vita ukabila,alipiga vita udini vitu hivi viwili alifanikiwa sana na pengine ndiyo maana Da Mwajuma alikuwa mwepesi sana kukukaribisha Ilala Flat bila kujali kabila lako au dini yako aliutazama uTanzania wako.

  Mkuu Pasco nimeanza mbali kidogo si bahati mbaya ila nimeona niwakumbushe viongozi wetu hasa wanasiasa wanaotafuta madaraka kwa msingi wa ukabila ama udini waache mara moja watanzania tumeishi na tunaishi kwa upendo yamkini mfano wako unawakilisha mifano mingi jinsi wananchi tusivyo na huu upuuzi wa ubaguzi.


  Mkuu Pasco pole sana hakika umeondokewa na mtu muhimu sana katika maisha yako.
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ahsante marehemu halima kwa yote pia msiba wako kutudhihilishia kuwa Pasco ndio Pascal Mayalla!!
   
 10. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ungeipeleka kule kwenye thread ya habari za kifo chake..
   
 11. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  R.I.P Halima Mchuka
   
 12. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hujaelewa thread. hii sio Rip. by the way, niliwahi kumuona mara moja ila nilikuwa naipenda sana sauti yake akiwa anatangaza alikuwa na sauti nzuri, iliyojaa ucheshi na uchangamfu. Pumzika kwa amani maana sote mavumbini tutarudi.
   
 13. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #13
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Paschal una historia ya maana mno najifunza sana kwako
   
 14. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #14
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Halima Mchuka,ni miongoni mwa Watangazaji walionivutia sana.RIP
  Kumbe ndio maana nilikuwa nakuona Kanisani Msimbazi,Siku hizo nikiwa nasoma shule ya msingi Na sekondari.Nilikuwa nafurahi kukuona.Ulikuwa unakaa karibu Na Priva Mtema?
   
 15. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  sijui hamsomi au hamuelewi. yaani umeambiwa no rip ww unaandika tu. wa wapi wewe.
   
 16. b

  baba koku JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 340
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Nilimfahamu katikati ya miaka ya tisini wakati wa kurekodi vipindi vya idhaa ya biashara ambapo alikuwa anatangaza viopindi vya m ashirika na taasisi mbalimbali. Alifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa kwani kuna wakati wa kurekodi vipindi hivyo,ilitokea wawakilishi wa taasisi na mashirika wakawa wanamtegemea yeye kuwapangia ratiba ya kutumia studio moja kila mwakilishi kwa wakati wake bila kusababisha misuguano miongoni mwao. Alikuwa na PR nzuri kwao.
   
 17. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  R.I.P sister !
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,618
  Trophy Points: 280
  Kombo, sio makosa, thanks pole nitazifikisha na update nitawapa!.
  thanks
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,618
  Trophy Points: 280
  Mhe. Regia Mtema asante. Nilisoma TSJ na Bonga Bar ndio palikuwa outing yetu pale next to Priva!.

  Mimi najihesabu ni mtoto wa Ilala tangu nasoma TSJ miaka yangu 10 ya ujana imekatikia Ilala.

  Huyu Halima Mchuka na dada yake Mwajuma kwangu ni zaidi ya ndugu!

  Huyu ni mwanamke wa shoka kama ulivyo wewe Mhe. Regia!.
   
 20. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #20
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Asante kwa habari nzuri. Mungu amlaze pema peponi.

  Kwa kweli sielewi kwanini unalazimisha iwe tribute tuu acha wa RIP waweke sababu sio wote tunamjua mie simfahamu

  Mie sioni y kucontrol thread wakati ni mod ndie mkuu. Ni msiba hakuna haja ya kutoa onyo, just let it flow

  Poleni wafiwa

  May she RIP
   
Loading...