Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 264
Nimekuwa mpiga debe mkubwa wa Diaspora kuingia kwenye uongozi wa hii nchi. Nina uhakika kwamba, wapo baadhi ya vijana wenye uwezo mkubwa sana, kwenye medani tofauti za Kijamii, Sheria, Siasa na Uchumi. Bila kutaja majina, wapo vijana wengi ila wawili (standouts) ndio wanaofahamika zaidi kwa vipaji vyao; Moja ni mchambuzi mkubwa humu JF na mwingine ni mfanya kazi huko Wall-street. Kuna baadhi pia wapo Uingereza na kwingineko
Kinachonishangaza ni kwamba, hakuna hata mmoja wa hawa vijana aliyejitokeza kugombea nafasi yoyote ya uongozi. Tukiwaweka kando Dr. Hildebrand Shayo na Dr.Kaborou, Tunaowaona kwenye medani za siasa ndio kama wale (waropokaji) waliosafirishwa na CCM kutoka DMV kuhudhuria Mkutano mkuu wa CCM wakiongoza na Kituko LeTotoz.
Je hawa Diaspora wanadharau siasa au wanaogopa kuingia kwenye uongozi. Je kuna vipingamizi vingine vinavyowazuia vijana wetu kurudi kulijenga taifa?..........CDM , CUF, CCM, TLP na mengineyo ina mikakati gani?