Tunaomba Kujua Mchango Wa Diaspora Kisiasa Na Kiuchumi; Kwa Nini Tuwakumbatie?

Mimi nahisi hata general elections 2015 zitakuwa na mauzauza mengi kama vile GHOST VOTERS n.k

Hichi kitu DMV automatically ni mtaji wa mastermind wa huo mpango. Yaani ni wazi kura zao zililenga wagombea fulani
 
Hakuna "cha ajabu" wala "cha kutisha", bro. In fact, hakuna mtu perfect achilia mbali mfumo perfect wa siasa au wa jamii.

To each, their own, kama ilivyoandikwa kwenye msahafu. Kama kuna lolote wewe ungetakiwa kujifunza baada ya miaka 20 na pengine zaidi Ughaibuni ni kwamba uheshimu maoni na mitazamo ambayo ni tofauti na yako, hata kama hayaendani na moral and ethical standards ulizojiwekea binafsi.

Halafu muanzisha maada naye asitake kupotosha watu na references zake bogus za majina ya Watu anaodai wanawakilisha watu wa diaspora.

Bro nimekuelewa kabisa.

Suala ni kwamba moral and ethical standards zinawekwa na wale watu wenye muono na wenye kuelewa kwamba dhamana waliyopewa kuongoza ni kubwa.

Kwahio hapo zinawekwa moral na ethical standards kuonyesha kabisa wapi mtu anakuwa wrong na wapi anakuwa right kwenye uwajibikaji katika mfumo uliopo.

Sasa ukiweka masuala kama la wizi wa kule kwenye akaunti ya EPA na sasa kuhusu mabilioni kufichwa Uswiss tutasema mfumo huohuo uachwe tu kwasababu hakuna moral na ethical standards?

Au kama vipo ni nani anaweka na zinafuatiliwa? si ni wale wenye dhamana?

Ethics inawezesha kuwepo na morality hasa kwenye mahusiano ya jamii mbalimbali, na ni Ethics hiyohiyo itakayo-analyze asili na mfumo wa ndani wa morality.

Hatuwezi tukawa na watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi na wakapewa platforms za kutaka uongozi wa juu wa nchi, hiyo ni degradation kubwa ya ethics na moral standards.
 
If there's any country that's immensely dependant on those in the diaspora for remittance I would say Uganda!

Almost in every family in Uganda there's a member living overseas. I for one think most people fled that country during Amin regime

But the most interesting thing about Uganda is that MOST THINGS are imported from Japan, cars, SILVERWARE in the kitchen, electronics etc

I don't recall seeing WESTERN UNIOUN in Tanzania but there are western union branches all over Uganda

Mkuu,

The words in red, are you serious?
 
Si kweli kwamba kuna mtu anajua Watanzania wa Diaspora wanaingiza pesa ngapi Tanzania kwasababu hii kubwa Mwaka jana kwenye mkutano wa Dicota uliofanyika Virginia Gavana wa bank kuu alisema data zao zinatokana na West Union, Banks na Money Gram na hawana data za pesa zinazotumwa kwa kupeana. Sasa gazeti la Citizen limetoa wapi data ambazo wanajua lakini Gavana wa Bank hana na ni njia gani wametumia?. Nilikuwa Tanzania mwezi wa Tano nimeenda na pesa hakuna mtu airport alinuuliza nakiasi gani sasa je walijua vipi mimi nimeingia na pesa gani? Je record hizo ziko wapi na ukiangalia vizuri Watanzania wangapi wanatoka nje kwa ndugu zao kila siku na pesa ngapi wanazo hakuna utaratibu wowote uliowekwa wa kujua. Hivyo mimi siamini hilo gazeti hata kidogo. Kuna mwaka mmoja Tanzanite Account ya CRDB wakati bado ikiwa active ilikuwa na $10M na pesa hizo zote ni za diaspora na Kimei ndiyo alisema hivyo je kuna pesa ngapi ambazo hatujui
 
Bro nimekuelewa kabisa.

Suala ni kwamba moral and ethical standards zinawekwa na wale watu wenye muono na wenye kuelewa kwamba dhamana waliyopewa kuongoza ni kubwa.

Kwahio hapo zinawekwa moral na ethical standards kuonyesha kabisa wapi mtu anakuwa wrong na wapi anakuwa right kwenye uwajibikaji katika mfumo uliopo.

Sasa ukiweka masuala kama la wizi wa kule kwenye akaunti ya EPA na sasa kuhusu mabilioni kufichwa Uswiss tutasema mfumo huohuo uachwe tu kwasababu hakuna moral na ethical standards?

Au kama vipo ni nani anaweka na zinafuatiliwa? si ni wale wenye dhamana?

Ethics inawezesha kuwepo na morality hasa kwenye mahusiano ya jamii mbalimbali, na ni Ethics hiyohiyo itakayo-analyze asili na mfumo wa ndani wa morality.

Hatuwezi tukawa na watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi na wakapewa platforms za kutaka uongozi wa juu wa nchi, hiyo ni degradation kubwa ya ethics na moral standards.

Mkuu, hii issue ni pana na ipo nje ya point yangu.

La msingi ni kwamba siyo wote ambao wana vouch for CCM wanapenda ufisadi na nia yao pekee ni kujilimbikizia utajiri binafsi kwa namna zozote.

Nadhani kama ingekuwa the case kwamba kila anayeshabikia CCM ni totally corrupt and irresponsible both morally and ethically, basi bila shaka nchi nzima inge-collapse kabisa long time...politically, socially, economically, you name it, kama Zaire enzi za Mobutu, na kusingekuwa na any semblance of civility or rule of law in the country.
 
Hivi vyote unavyovitaja ndo vinaonekana sasa hivi. Yaani kila mtu anakula pale alipo. Umeambiwa makuruta wa polisi wamenusa CCP siku ya kwanza ya pili wanaambiwa chuo hakiwatambui

Mahospitalini naskia madokta huwa wanawaambia wagonjwa ungekuja kwenye clinic yangu ungekuwa umeshapona

Usalama barabarani tabu tupu
 
Hivi kwani kuosha wazungu (wazee) siyo kazi jamani?

Mbona watu wanakuwa wana dhihaka hivyo? Sasa kama mtu anadharau kazi ambazo zinawapatia watu riziki zao hata kama hizo kazi ni nje ya nchi je wale ambao wapo Tanzania na ni wapiga debe, waendesha boda boda, waendesha bajaji, and such si wanaonwa kuwa ni takataka tu?

Inasikitisha sana.

Mkuu Ngabu;

Chukua tano. Kuosha wazungu ni kazi halali na anayefanya hivyo anaisaidia jamii kwa mambo mengi kwani kuna vitu vingi haramu angeweza kufanya kujipatia kipato. Angeweza kuwa mwizi, fisadi au jambazi.

Vilevile kuna-myths kuwa watu waliopo nje ni watoto wa wakubwa. Ndio wapo watoto wa wakubwa. Lakini vilevile tukumbuke hata hao wakubwa wametoka kwenye familia masikini au wana ndugu wa karibu ambao ni masikini.
 
Nimekuwa mpiga debe mkubwa wa Diaspora kuingia kwenye uongozi wa hii nchi. Nina uhakika kwamba, wapo baadhi ya vijana wenye uwezo mkubwa sana, kwenye medani tofauti za Kijamii, Sheria, Siasa na Uchumi. Bila kutaja majina, wapo vijana wengi ila wawili (standouts) ndio wanaofahamika zaidi kwa vipaji vyao; Moja ni mchambuzi mkubwa humu JF na mwingine ni mfanya kazi huko Wall-street. Kuna baadhi pia wapo Uingereza na kwingineko

Kinachonishangaza ni kwamba, hakuna hata mmoja wa hawa vijana aliyejitokeza kugombea nafasi yoyote ya uongozi. Tukiwaweka kando Dr. Hildebrand Shayo na Dr.Kaborou, Tunaowaona kwenye medani za siasa ndio kama wale (waropokaji) waliosafirishwa na CCM kutoka DMV kuhudhuria Mkutano mkuu wa CCM wakiongoza na Kituko LeTotoz.

Je hawa Diaspora wanadharau siasa au wanaogopa kuingia kwenye uongozi. Je kuna vipingamizi vingine vinavyowazuia vijana wetu kurudi kulijenga taifa?..........CDM , CUF, CCM, TLP na mengineyo ina mikakati gani?

Mke ya Muzungu;

Niliudhuria kikao cha Ndugu Mbowe hapa DMV. Na yeye alituomba tuchangie chama chake na akatoa mfano wa watanzania wa Texas kumpa mchango ambao unaweza kununua pikipiki 100 ambazo zitatumika kwenye kampeni na shughuli zingine za chama. Kama maneno yake yalikuwa ya kweli, je mchango gani zaidi wa kisiasa unataka?

Pili ni lazima ukumbuke watanzania tumechelewa sana kuja katika nchi za magharibi. Nchi kama Uganda, Kenya, Ethiopia, Rwanda na zinginezo za Afrika mashariki zina vizazi ya vitatu vya nguvu katika nchi hizi. Mtu anayetoka Ethiopia akija Marekani anakuja kwa mjomba na anakuta vitu vimeandaliwa.

Wengi wa watanzania tumekuja miaka ya 90s na ya hivi karibu. Tumeanza maisha wenyewe na tunajaribu kufungua milango kwa ndugu na jamaa zetu kwa uwezo tulio nao. Kuna wachache wenzetu wamefanikiwa lakini matokeo yake isiwe ni kipimo cha wote. Give us another 10 years and we will surprise you.
 
Nimekuwa mpiga debe mkubwa wa Diaspora kuingia kwenye uongozi wa hii nchi.
Diaspora ni watu walio uhamishoni, sasa utaingiaje kwenye uongozi ukiwa uhamishoni?

Zama za kale kabisa diaspora ilikuwa ni vizazi vya watu waliochukuliwa misukule kwa bakora na bunduki kwenda kulima uhamishoni.

Siku hizi diaspora anajipeleka mwenyewe uhamishoni, anachagua kuwa mhamiaji mbali na kwao, sasa utamwambiaje mtu huyo eti aje awe kiongozi, hayupo na hasaidii lolote zaidi ya kutumia pound mia hapa mia mbili pale kumsaidia mama yake anapokwenda kwenye soko la dagaa au duka la dawa baridi, hawajengi nchi. Kiongozi?
 
Zakumi,

You have nailed it.Actually,huki mbeleni 7-10 years mchango wa Diaspora utakua mkubwa sana.

Kinachotakiwa sasa ni serikali na hata vyama vya siasa kuandaa mazingira ya kisera kuhakikisha Taifa linanufaika na Diaspora

-Nimekua nikifurahi mbinu ambazo vyama vya siasa nchini Nigeria wanatumia kupata sapoti ya Diaspora.Raila Odinga n chama chake cha ODM waliiga mbinu hiyo

Diaspora ni kundi muhimu kisiasa na kiuchumi kama watapewa umuhimu wanaostahili
 
Kwani nchi inajengwa vipi? Si inajengwa kwa paundi mia hapa paundi mia mbile pale?
 
Kwani nchi inajengwa vipi? Si inajengwa kwa paundi mia hapa paundi mia mbile pale?
Sidhani. Marekani kwa mfano, kwenye transportation infrastructure, tunasoma kwenye historia kwamba yale ma highway na mabarabara ilikuwa ni mpango maalum wakati wa Rais Eisenhower kujipanga, kutenga fedha kujenga ma highway, tena juzi tu hapa in the 50's. Na hata hapa kwetu miradi ya mabarabara, mitambo ya gridi ya umeme, viwanda n.k, haijengwi kwa kuchanga paundi mia hapa mia mbili pale.

Nikupe hadithi fupi, na kama Rais Kikwete au his handlers wanaingia humu watakumbuka. Siku moja wakati ndio ameingia ingia madarakani JK alikuwa na mkutano na Watanzania New York, dada mmoja akamuuliza, "nifanye nini kusaidia tatizo la umeme [akataja kwao], tuleta hela?" Kikwete akatoa maelezo halafu akasema hiyo hela mtumie mamaako ale, haijengi mradi wa umeme!

Ni jibu lililokaa kama kidhihaka dhihaka lakini lina ukweli. We uko Ulaya unatuma Tanzania paundi mia hapa mia mbili pale, hiyo haijengi nchi zaidi ya kumsaidia mjomba wako akienda kwenye duka la dawa baridi! Marekani ilijengwa na wahamiaji walioenda Marekani, sio wahamiaji waliokimbia Marekani, mtu hajengi alipopakimbia.
 
Nikikubali kuwa ni jibu la dhihaka nitakupa sifa uzizostahili. Hili ni jibu la mtu asiyeelimika. Serikali kuu ya Marekani, serikali za majimbo na serikali za mitaa zinajenga mabarabara au miundombinu kwa kutumia BONDS. Bonds zinatokana na michango ya watu au mashirika kuchangia mifuko ya uwekezaji.

Michango ya watu inatokana na paundi au dola mia au mia mbili ambazo watu wanawekeza. Uwekezaji huo unaweza kuwa wa mafao ya kustaafu au uwekezaji mwingine.

Serikali haiwezi kujenga mabarabara mara moja kwa kutumia pesa za walipa kodi. Inakopa katika BONDS. Inajenga barabara haraka na baadaye inalipa Bonds polepole.

Kwa wewe usiye na elimu ya finance utasema kuwa serikali ya Rais Eisenhower ilijipanga, ilitenga fedha kujenga ma highway. Lakini kilichofanyika serikali ili-issue BONDS ambazo watu kwa kutumia dola mia au mia mbili walizinunua na kuifanya serikali kuokoteza pesa nyingi kwa kipindi kifupi kujenga barabara.

Tukirudi kwenye mifano yako. Rais Kikwete ana elimu ya finance kama yako. Tanzania ina miradi mingi ambayo ingeweza kuendelezwa kwa kutumia government issued bonds. Watanzania waliopo nje na ndani ya nchi wangeweza kununua bonds hizo kwa kutumia shilingi mia, shilingi elfu, dollar 100, au paund 50. Hizi ni pesa ambazo hazina riba kubwa zingeifanya serikali kufanya miradi mingi bila kujichosha na madeni ya riba kubwa.

Lakini kutokana na upeo mdogo wa viongozi wa Tanzania wanaona ni afadhari wakope mikopo kutoka benki zenye riba kubwa kuliko kuanzisha mifuko ya pesa.

Hivyo jibu la rais Kikwete kumwambia mtanzania aliyepo New York kutumia pesa zake kwa matumizi ya wazazi tu alinishangazi. Ndivyo Alivyo.
 
Zakumi,

You have nailed it.Actually,huki mbeleni 7-10 years mchango wa Diaspora utakua mkubwa sana.

Kinachotakiwa sasa ni serikali na hata vyama vya siasa kuandaa mazingira ya kisera kuhakikisha Taifa linanufaika na Diaspora

-Nimekua nikifurahi mbinu ambazo vyama vya siasa nchini Nigeria wanatumia kupata sapoti ya Diaspora.Raila Odinga n chama chake cha ODM waliiga mbinu hiyo

Diaspora ni kundi muhimu kisiasa na kiuchumi kama watapewa umuhimu wanaostahili

Tatizo la watanzania tuzoea siasa za mapinduzi. Unapanga leo na kesho unataka uone matokeo. Diaspora imeanzwa kujengwa miaka ya 90 na leo tunataka kuona matokeo yake.

Awamu ya watu wa Diaspora kwenda shule, kujenga familia, kununua nyumba inaanza kupita. Na nina uhakika mchango mkubwa utafuatia.
 
Hivyo jibu la rais Kikwete kumwambia mtanzania aliyepo New York kutumia pesa zake kwa matumizi ya wazazi tu alinishangazi. Ndivyo Alivyo.

Hizo pesa za remittance zinaingia kwenye mzunguko wa pesa. Zinaongeza buying power ya mwananchi. Matokeo yake zinachangia uchumi kukua
 
Kiukweli kuna watanzania wengi wenye taaluma na exposure nzuri sana wanatumikia minchi ya watu tuu, ambao wangetumiwa vizuri hii nchi yetu ingefika mbali sana.Tatizo kubwa hakujawahi kutokea serikali ya ccm ikawa na sera za kuzitumia hizi resource watu.Kuna madokta, maainjinia na wahadhiri wengi tuu walioko nje wanashindwa kutumika hali ya kuwa wana skills na exposure kuwa kwenye haya manchi yenye maendeleo makubwa dunia ya viwanda na uchumi bora. We have to have good policy to utilize these resources.Bila hivyo tutaendelea kutumia mawazo ya hawa yaliyoganda ya hawa wanaccm na wizi wao.Wachina wamewasambaza raia wao duniani kusoma na kupata skill then wanarudi nyumbani kujenga nchi! Hivi TZ tumelogwaaaa na mchawi yupi ambaye hatutatibika???
 
Back
Top Bottom