Tunaomba Kujua Mchango Wa Diaspora Kisiasa Na Kiuchumi; Kwa Nini Tuwakumbatie?

Kama hii ni kweli, basi CCM imeshakufa

Mwenyekiti, Katibu pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM, waliwalipa Watanzania waishio Marekani kiasi cha $9,500 kila mmoja pamoja na tiketi za ndege kuja kwenye mkutano mkuu ili kumpigia kura Mwenyekiti pamoja na wajumbe wengine, kama Membe. Hii ni kashfa ambayo CCM lazima iijibu, kwani haya yametoka vinywani mwa wana DMV wenyewe waliokuja hapa Dodoma kwenye mkutano mkuu
 
hakuna mfumo mzuri wa kuwajali vijana wetu, walioko nje ya nchi, kwanza viongozi wetu ndo hawawapendi kabisa, na hata mmojammoja wanaoamua kurudi nyumbani akibahatika kupata ajira serikalini , basi watafanya kila jitihada kumkatisha tamaa ili akate tamaa na wao, kupata la kusema.tulijua atashindwa tuu, alidhani hapa ni....... kingine vijana wengi tayari wamepata uraia ughaibuni sasa hawataki majungu ya kibongobongo tazama, waziri nyarandu alivyopata msukosuko akidaiwa ana uraia wa marekani, tuache fitna na hata kusema watoto wa mafisadi ndo wako majuu ni kufirisika kifikra na fitna na woga wakati kuna watu wengi wako kule miaka na miaka wameenda kwa njia mbalimbali za haki na ujanja ujanja lkn sasa wako njemas na vizazi vyao , dawa ni kuruhusu uraia wa nchi 2.
 
hakuna mfumo mzuri wa kuwajali vijana wetu, walioko nje ya nchi, kwanza viongozi wetu ndo hawawapendi kabisa, na hata mmojammoja wanaoamua kurudi nyumbani akibahatika kupata ajira serikalini , basi watafanya kila jitihada kumkatisha tamaa ili akate tamaa na wao, kupata la kusema.tulijua atashindwa tuu, alidhani hapa ni....... kingine vijana wengi tayari wamepata uraia ughaibuni sasa hawataki majungu ya kibongobongo tazama, waziri nyarandu alivyopata msukosuko akidaiwa ana uraia wa marekani, tuache fitna na hata kusema watoto wa mafisadi ndo wako majuu ni kufirisika kifikra na fitna na woga wakati kuna watu wengi wako kule miaka na miaka wameenda kwa njia mbalimbali za haki na ujanja ujanja lkn sasa wako njemas na vizazi vyao , dawa ni kuruhusu uraia wa nchi 2.

Hata wakiruhusu uraia wa nchi 2 hakuna kitakachobadilika, zaidi ya kuzidi kuwanufaisha Wahindi, waarabu, Wazungu, Wachina na sio Watanzania asilia, na sababu kubwa ni malezi, hatuna malezi ya kutufanya tuwe wavumilivu na watu wa kuangalia mbali, na ndio maana kila siku hatuishi visingizio, waliokuwa nyumbani Tz watakwambia wanashindwa kutoka kwa maana mambo yamebana na hakuna mianya, waliobahatika kwenda huko nje kuliko enendelea wanalalamika wanashindwa kutoka kwa maana hawana uraia wa nchi mbili, basi tu ili mradi visingizio na kila siku kutafuta mtu au kitu cha kulaumu, tunalaumu kila kitu na kila mtu isipokuwa sisi wenyewe!
 
Serikali imeshindwa kuwakomboa wananchi wake kiuchumi. Leo hii mtu wa diaspora anabeba mzigo wa serikali anaishia kubezwa!!!
 
Hata wakiruhusu uraia wa nchi 2 hakuna kitakachobadilika, zaidi ya kuzidi kuwanufaisha Wahindi, waarabu, Wazungu, Wachina na sio Watanzania asilia, na sababu kubwa ni malezi, hatuna malezi ya kutufanya tuwe wavumilivu na watu wa kuangalia mbali, na ndio maana kila siku hatuishi visingizio, waliokuwa nyumbani Tz watakwambia wanashindwa kutoka kwa maana mambo yamebana na hakuna mianya, waliobahatika kwenda huko nje kuliko enendelea wanalalamika wanashindwa kutoka kwa maana hawana uraia wa nchi mbili, basi tu ili mradi visingizio na kila siku kutafuta mtu au kitu cha kulaumu, tunalaumu kila kitu na kila mtu isipokuwa sisi wenyewe!

kama watawala wataishia kubadilisha uraia tu, na kuacha kila kitu kiendelee kama kilivyo ni kweli litakuwa tatizo ,halijatatuliwa .hivi sasa hatujapitisha hiyo sheria lkn wahindi , bado wanafaidika nayo'nakubali taifa letu limekuwa la lawama ,kila mtu lawama, kiongozi anallalamika, mtawaliwa analalamika nani? atupe ufumbuzi. THOMAS sankara, alisema nyuma ya mwanasiasa mbovu kuna captain wa jeshi[ mapinduzi] inaweza kuwa suluhisho?
 
Nimekuwa mpiga debe mkubwa wa Diaspora kuingia kwenye uongozi wa hii nchi. Nina uhakika kwamba, wapo baadhi ya vijana wenye uwezo mkubwa sana, kwenye medani tofauti za Kijamii, Sheria, Siasa na Uchumi. Bila kutaja majina, wapo vijana wengi ila wawili (standouts) ndio wanaofahamika zaidi kwa vipaji vyao; Moja ni mchambuzi mkubwa humu JF na mwingine ni mfanya kazi huko Wall-street. Kuna baadhi pia wapo Uingereza na kwingineko

Kinachonishangaza ni kwamba, hakuna hata mmoja wa hawa vijana aliyejitokeza kugombea nafasi yoyote ya uongozi. Tukiwaweka kando Dr. Hildebrand Shayo na Dr.Kaborou, Tunaowaona kwenye medani za siasa ndio kama wale (waropokaji) waliosafirishwa na CCM kutoka DMV kuhudhuria Mkutano mkuu wa CCM wakiongoza na Kituko LeTotoz.

Je hawa Diaspora wanadharau siasa au wanaogopa kuingia kwenye uongozi. Je kuna vipingamizi vingine vinavyowazuia vijana wetu kurudi kulijenga taifa?..........CDM , CUF, CCM, TLP na mengineyo ina mikakati gani?
Tehe tehe tehe yako mengine ya kuudhi mkuu kutoka huko huko!! Mzee Ruksa kwa nia njema kabisa alipita huko nje akiwahamasisha watz warudi "kujenga nchi yao" unajua aliwapata "vihiyo" kibao/ Yule aliyeingia kwenye kashfa na kina diamond motors na mapajero ya MaDC aliwekwa pale ujenzi chini ya katibu mkuu kama engineer alikuja kujulikana alikuwa "boiler technician". Hivyo diaspora siyo lazima kuwa na watu unaotegemea; wachimba makaburi, watunza elderly homes" wengi wameshaharibika na wala hawana mpango na siasa za TZ wanaganga njaa huko!!
 
Tanzanians in diaspora community comprise of people who ran from the challenges in the country. Majority escaped the system including National Service for those who matured at the time. Unlike Kenyans most Tanzanians are hardly surviving abroad. Most are turning back as failures in the system they thought could make them live their "Dreams". Because of wisdom in political system in India where Diaspora are bared from participating in politics particularly leadership I advice Tanzanians to reject the army of "wabangaizaji" who were misled by rogue politicians like KINANA that they can land into land of honey and milk through CCM(political leadership).

Hii ni kweli kabisa Tumewaona wengi hata huu mkutano wa CCm juzi wamealikwa wengi wao wanawaza ubunge tuu hakuna ni ya dhati ya kuisongesha mbele nchi hii.
 
Kwa nini?


Naona Matola kakujibu. Kwa kuongezea serikali inatumia kodi kwa shughuli zingine kama kulipa mishahara na kutoa huduma za jamii. Ujenzi wa mabarabara ni gharama kubwa. Hivyo serikali ikitumia kodi kwa mara moja kujenga mabarabara, itakosa pesa za kulipa mishahara na kutoa huduma zingine za jamii.

Kwa kutumia mikopo au bonds, serikali italipa ujenzi wa barabara mara moja huku ikitumia kodi kwa shughuli nyingine za maendeleo. Baada ya ujenzi ukiisha au ukiwa bado unaendelea, serikali itatumia sehemu ndogo ya kodi kulipa mikopo au bonds kwa muda mrefu.

Kama ujenzi wa barabara utaongeza mzunguko wa pesa, kutakuwa na ongezeko la ukusanyaji wa kodi ambao utawezesha serikali kulipa madeni yake huku ikiendelea kutoa huduma zingine za kijamii.

Serikali ambayo hipo makini katika ulipaji wa mikopo na bonds zake, siku zote inapata mikopo yenye riba ndogo kwa sababu wawekezaji hata wale wenye pesa ndogo wana uhakika wa kulipwa pesa zao. Hivyo kuna watanzania wengi hususa ambao wapo kwenye diaspora ambayo wananunua bonds za serikali ya Marekani.

Watanzania hawahawa wangeweza kununua bonds za serikali ya Tanzania, iwapo serikali yetu ingekuwa mlipaji mzuri. Hivyo kuna michango mingi diaspora wanayoweza kuifanya kwa kutumia paundi mia moja au mia mbili.

Kitu kinachoshindikana ni kuwa serikali ya Tanzania ikitoa bonds kwa watu wake na baadaye kushindwa kulipa, tutabadilisha serikali mara moja au kuwachinja viongozi. Hivyo viongozi walichohamua ni kutumia misaada, mikopo yenye riba kubwa, na matumizi ya rasimali asilia kwa sababu matumizi mabaya ya vyanzo hivyo vya pesa havifanyi watu kuwa na hasira za kutaka mabadiliko.
 
Wana jf,

Kuna baadhi ya maswali najiuliza kuhusu matawi na washirika wa vyama hivi nje ya nchi:

1) Kikatiba hawawezi kupiga kura (kuna utaratibu wa katba mpya au marekebisho ya taratibu za uchaguzi za kuwawezesha washirika hao kupiga kura?)

2) Kihistoria nini mchango wa washirika hawa ktk siasa za Tanzania?

3) Kama 1 na 2 hapo juu hazina uzito ya nini viongozi wetu kuruka majuu kwa ajiri yao?

4) Kuna michango hasi au chanya upatikana ktk mikutano hiyo? ni hipi? Kwa uelewa wangu mdogo, ndo maana nauliza maswali mengi hapo juu ilinielimishwe, walioko diaspora hasa nchi nyingi za Afrika magharibi wamekuwa hawazitendei nchi zao vyema kwani mara nyingi utoa misaada ktk uasi.

5) Swali la kichokozi; huyu kwenye ID ya Tuntemeke ni nani? Ni msemaji wa cdm diasipora? Ni mshirika asi wa cdm ktk mikutano ya Dr. Slaa diaspora ( samahani ningeuliza swali ili ktk uzi wake lakini yeyote aweza nisadia hapa)
 
Honestly,hata mimi sioni umuhimu wao au mchango wao,hizi safari za viongozi wa vyama kwenda huko na kufanya mikutano nao kwa maoni yangu ni ufujaji wa fedha za vyama,kwanza wako wangapi ?Pili hata kura hawapigi,tatu nimewahi kufuatilia harambee zao mabalimbali za kuchangia maendeleo na vyama,sana sana wakijitahidi wanachanga millioni 15 za Tanzania,sasa faida yao ni nini?Wengi hasa hasa wanaoshabikia magamba ni watoto wa viongozi waliopewa favour ya kwenda huko kwa fedha za walala hoi,hawajui reality za maisha ya watanzania wa vijijini,upande wa pili na wale walioenda kwa struglle zao na kwa akili zao ,awa wengi wao ni watoto wa wakulima na wa uswahilini na wanaelewa machungu ya watanzania.
Kwa maoni yangu awa the so called diaspora hawana umuhimu wowote kwenye politics za nchi hii,hiyo michango yao wanayochangaga hailingani na gharama za viongozi wanaopokwenda kuwaona,hizo millioni 15 hata ukifanya harambee ya kawaida tu ya wanachama walala hoi itapatikana.Ni mawazo yangu kuwa viongozi wa vyama wanaenda kutalii na shopping na wake zao in the name of the Diaspora. I stand to be corrected.
 
Back
Top Bottom