Hiyo ni kweli tupu. Na kwa bahati mbaya,ukiwa DIT kwa mfano,matumizi ya hesabu hizo unakutana nayo hapo hapo. Kwa mfano,kwenye masomo ya Strength of Materials,kwenye First and Second Moment of Inertia nk,bila kujua hizo dx or dy ili kupata xtreme fibre points kama zile Modulus,Y and X Bar(Centroid and centroidal axis perpendicular distances) perpendicular to X or Y Axis,ndugu yangu lazima ubebeshwe virago kwa Supplementary na discontinuation.
Kwa mfano,unaambiwa locate centre of mass au Centroid ya maumbo yafuatayo
1. Triangle
2. Rectangle& Square
3. Cycle
4. Composite figure
Na maumbo hayo unapewa vipimo vyake ni kwa mfano Upana 'w' na urefu 'l', pembetatu unapewa kitako 'b' na kimo 'h', hakuna namba wala nini. Hapo anakuambia locate hiyo Centroid about X- Axis na Y- Axis. Hakika kama hujui Intergral,lazima utoe macho.
Kwa mfano majibu kwa pembe tatu ni h/3, 2h/3 na b/3 na 2b/3 kutegemea swali limetaka nini. Lakini kwanza lazima ukate umbo lako katoka infinite small portion dx au dy ikiwa na limit 0-h au limit 0-b. Nimeanza kusahau,kwa sababu ni muda mrefu.