We ndo hata hujitambui, uwezo wako wa kufikiri ni wa kikenyakenya, hilo uliloliandika lina manufaa yapi kwa taifa, mdomo hujenga na hubomoa pia, utumie hata kwa kunywa mbege tu kama huna akili wala hekima kichwani, wachaga ndo kabila lililosambaa zaidi nchini, hali ilivyo kwa sasa inawanufaisha, ikibadilika waathirika wakuu mtakuwa ni ninyi pia. Then, kama hujui hili, ukabila unakufa Tanzania, kunajengeka kabila moja lenye lugha moja na tamaduni moja, kitchen party iko uchagani, usukumani, unyakyusani, uzalamoni na kotekote, wote tunakula viepe na ugali, wote tunavaa suruali na mashati, wapo ktk makabila yote wasiojua lugha tu za asili za makabila yao achilia mbali kutopitia mila zao nyingine, hao wanaokwenda kaskazini kwa sasa ni watanzania tu wa huko wala si wachaga. Lidumu taifa Tukufu la Tanzania. Mungu ibariki Africa.