Tunajua Mengi tunanyamaza, Lissu kudharau Mamlaka ya Ikulu kumefanya kufifisha juhudi zilizopangwa na Rais Samia kuleta maridhiano

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Ilikuwa Tarehe 13/4/2021 Lissu alikutana na Joseph na kuomba Connection ya Kuongea na Katibu mkuu apate kuwasiliana na Rais kwakuwa kulikuwa na nia ya Samia kuongea na Vyama vya Upinzani, na bado niwe wazi Leo ntafunguka bila kuegemea upande, Samia naye aliona si vema kukutana na vyama vya Upinzani vya Akina Cheyo bali aliilenga Chadema kwakuwa alitambua kabisa uchaguzi wa mwaka 2020 kulifanyika maigizo ya hali ya hatari sana kuyatangaza matokeo,

Pamoja na kwamba Chadema walikuwa wamesha surrender kwa Magufuli ambaye katangulia mbele ya haki sasa , ndani ya Serikali na CCM Kuna watu bado wana mawazo chanya waliona itakuwa si vema kuongoza nchi bila maridhiano,

Mzee Warioba, akiwa na wenzake wanne walikutana na wazee wa CCM na kuomba kwamba hawafurahii kuona watanzania wenzao wako nje ya nchi Kama wakimbizi hivyo Kesi zote zifutwe za uhaini na uchochezi warejee nchini mara moja! Maana orodha inaonesha wanaopaswa kufungwa ni 22 na waliwekewa mitego Mpakani na viwanja vyote vya ndege!!

Samia alisikiliza ushauri wa wazee na kukubali juu ya Suala la kukutana na Upinzani, bwana LISSU alivyo jua hayo kutoka Kwa Rwehumbiza Acting reprentative akawa ame omba sasa kuongea na Samia Kwanza yeye Kama yeye, Samia akakubali kabisa, kilichofuata Lissu akatumiwa mwakilishi kukutana naye akamkwepa (Rutabanzibwa) .

Akapigiwa Simu na Rais mwenyewe akasema anipigie Kwa kufuata Utaratibu Mungeniandaa Mapema juu ya kuongea naye sikurupuki kuongea naye! Wakamuuliza lini akasema, akapigiwa tena hakupokea Simu.

Huku akiendelea na Mazungumzo na wenzake kuwa Samia Hana Uwezo wa Kuongoza nchi, She is not in capacity of being a President of Tz na Wanaojadiliana naye wanavujisha Siri na Sauti Pia,

Ndipo Sasa hawa Kina SIRRO, na Mchengerwa wakamwambia Samia kuwa hawa wanakuchezea kwakuwa wewe ni mwanamke! Kwa Magufuli wasingefanya haya!! Hivyo basi acha kesi ziendelee kawaida kama ambavyo zimeshakuwa drafted awali, waende wenyewe Kujitetea wakikutwa na hatia wawajibike, wakikutwa hawana hatia basi waendelee na shughuli zao!!

Ndo yakaendelea ya Mbowe kuwekwa ndani,

Kwanza Samia angeongea nao ingeleta picha Tofauti sana!!

Wito wangu , Tunatakiwa Kupata Taasisi zilizo imara ambazo hazitegemei Rais anaamua nini bali sheria na KATIBA inasema nini, Kwakuwa scenario nzima inaonesha kuwa Kesi zimekuwa drafted kwa tamko la Magufuli Kwa sababu kadhaa bila ushahidi, alafu wanaotaka zifutwe bado wanaweka matumaini zifutwe na Samia bila kufuata Sheria inasema nini!!!!

KATIBA MPYA NDO DAWA!!

Britanicca
 
..huu ni UONGO.

..unataka kusema ni rahisi kwa mamlaka kubambika watu kesi na kuwaumiza kuliko kufanya maridhiano?

..kama Chadema ndio tatizo nini kilichomzuia Rais SSH kukutana na vyama vingine huku Chadema wakiwekwa kando ili kila mtu ajue ni wakorofi?

..Rais SSH alikuwa na uamuzi wa kuridhiana au kuendeleza ukatili na unyama wa awamu ya 5. So far muelekeo aliochukua unajulikana.
 
Ilikuwa Tarehe 13/4/2021 Lissu alikutana na Joseph na kuomba Connection ya Kuongea na Katibu mkuu apate kuwasiliana na Rais kwakuwa kulikuwa na nia ya Samia kuongea na Vyama vya Upinzani, na bado niwe wazi Leo ntafunguka bila kuegemea upande, Samia naye aliona si vema kukutana na vyama vya Upinzani vya Akina Cheyo bali aliilenga Chadema kwakuwa alitambua kabisa uchaguzi wa mwaka 2020 kulifanyika maigizo ya hali ya hatari sana kuyatangaza matokeo,

Pamoja na kwamba Chadema walikuwa wamesha surrender kwa Magufuli ambaye katangulia mbele ya haki sasa , ndani ya Serikali na CCM Kuna watu bado wana mawazo chanya waliona itakuwa si vema kuongoza nchi bila maridhiano,

Mzee Warioba, akiwa na wenzake wanne walikutana na wazee wa CCM na kuomba kwamba hawafurahii kuona watanzania wenzao wako nje ya nchi Kama wakimbizi hivyo Kesi zote zifutwe za uhaini na uchochezi warejee nchini mara moja! Maana orodha inaonesha wanaopaswa kufungwa ni 22 na waliwekewa mitego Mpakani na viwanja vyote vya ndege!!

Samia alisikiliza ushauri wa wazee na kukubali juu ya Suala la kukutana na Upinzani, bwana LISSU alivyo jua hayo kutoka Kwa Rwehumbiza Acting reprentative akawa ame omba sasa kuongea na Samia Kwanza yeye Kama yeye, Samia akakubali kabisa, kilichofuata Lissu akatumiwa mwakilishi kukutana naye akamkwepa (Rutabanzibwa) .

Akapigiwa Simu na Rais mwenyewe akasema anipigie Kwa kufuata Utaratibu Mungeniandaa Mapema juu ya kuongea naye sikurupuki kuongea naye! Wakamuuliza lini akasema, akapigiwa tena hakupokea Simu.

Huku akiendelea na Mazungumzo na wenzake kuwa Samia Hana Uwezo wa Kuongoza nchi, She is not in capacity of being a President of Tz na Wanaojadiliana naye wanavujisha Siri na Sauti Pia,

Ndipo Sasa hawa Kina SIRRO, na Mchengerwa wakamwambia Samia kuwa hawa wanakuchezea kwakuwa wewe ni mwanamke! Kwa Magufuli wasingefanya haya!! Hivyo basi acha kesi ziendelee kawaida kama ambavyo zimeshakuwa drafted awali, waende wenyewe Kujitetea wakikutwa na hatia wawajibike, wakikutwa hawana hatia basi waendelee na shughuli zao!!

Ndo yakaendelea ya Mbowe kuwekwa ndani,

Kwanza Samia angeongea nao ingeleta picha Tofauti sana!!

Wito wangu , Tunatakiwa Kupata Taasisi zilizo imara ambazo hazitegemei Rais anaamua nini bali sheria na KATIBA inasema nini, Kwakuwa scenario nzima inaonesha kuwa Kesi zimekuwa drafted kwa tamko la Magufuli Kwa sababu kadhaa bila ushahidi, alafu wanaotaka zifutwe bado wanaweka matumaini zifutwe na Samia bila kufuata Sheria inasema nini!!!!

KATIBA MPYA NDO DAWA!!

Britanicca
Ndugu Tundu Lissu ni "bwakubwaku".....

"Too much know" asiye na ulimi wa nidhamu wala heshima.....

Si kila MTANZANIA anaihitaji katiba mpya.....
 
Akapigiwa Simu na Rais mwenyewe akasema anipigie Kwa kufuata Utaratibu Mungeniandaa Mapema juu ya kuongea naye sikurupuki kuongea naye! Wakamuuliza lini akasema, akapigiwa tena hakupokea Simu!!!
Huku akiendelea na Mazungumzo na wenzake kuwa Samia Hana Uwezo wa Kuongoza nchi, She is not in capacity of being a President of Tz na Wanaojadiliana naye wanavujisha Siri na Sauti Pia,
Kwahiyo Samia amezungukwa na watu wapenda vurugu. Kulikuwa na sababu gani kuvunjisha sauti za mazungumzo?

Acha twende hivi hivi, kama mbwai na iwe mbwai.

Lkn pia mleta mada tutakuamini vipi kwamba ulichoandika si uzushi na uvumi bila ushahidi?
 
Nakubali hata hotuba ya Mbowe siku akisema anaongea ataongea kwa busara,fact na sauti ya heshima
Mbowe huwa anajifanya anaongea kwa busara kwasababu za kibiashara na maslahi. Ndio maana baada ya kuona dalili za kupoteza mwaka 2020 aliwakusanya kundi lake lote kwenda Mwanza kwenye sherehe za Uhuru kumbembeleza Magu wapate maridhiano ila hawakufanikiwa.

Baada ya Magu kufa, ilibidi Mbowe atafute kwa nguvu kile alichokipoteza na mwisho wa siku ndio yuko mahabusu.

Lissu yeye huwa ni mihemko tu. Kwanza alishatangaza kwamba kiongozi yeyote wa CDM akikamatwa wamekubaliana hakuna kumwekea mawakili wala dhamana na kama ni polisi wakae nae tu.

Lakini sasa hivi wako busy na mawakili na kuchangisha michango ya pesa za wajinga.
 
Mama Samia Raisi wetu mpendwa mm nakuomba Uvae tu VIATU vya Marehemu hata kama vitakupwaya hawa watu ni PUNDA hawendi mpaka kwa bakora ,waswahili chakula cha simba tu ,huna wema wowote utaofanya wasikuseme kwa ubaya watie adabu sana ili wanyoeke.
Keshanyooka mwenyewe. Sasa hivi ameamua kuegemea uzanzibari wake ili angalau apate faraja toka kwa nduguze.
 
Mama Samia anawahitaji wapinzani hasa CDM kuliko tunavyodhani, huwezi kutawala kwa raha huku makundi mengine yanasonokena, inakuuma mno mno kama Mkuu wa nchi. Hivi unafikiri maza anafurahia kuwaona wana CDM wanakimbizwa kila kukicha na mapolice na wengine magelezani kwa kesi za kisiasa? Naye ana roho na ana imani yake.

Yeye afanye tu utaratibu wa kisheria akutane nao awasikilize - yanawezakana yatatuliwe mengine wawekeane timeframe. Haya madaraka na haya maisha huwa yanapita tu ndugu zangu, kwani yeye Maza alidhani atakuwa Rais wa Tanzania miezi 7 iliyopita? mmeona eee - haya tupendane kwani sisi wote ni waja wake yeye mmoja tu aliye juu - yaani Mola wetu.

CCM hebu wekeni wepesi bac maana nasikia nyie ndiyo wasilibaji wakuu ili Maza asiongee na wapinzani...ndiyo !!
 
Back
Top Bottom