Tunahitaji chama kipya?

Tunahitaji chama kipya?

kwa mtaji huu tutafikisha mivyama 100 kwani hakuna mwanadamu asiyekuwa na mapugufu.hata CCJ iliyoanzishwa hivi karibuni itakumbana nadhahama hii hii,let wait and see.Kosa halikimbiwi bali hutatuliwa,hata tukianzisha vyama lukuki hatutakosa makosa kwani binadamu ni wale wale.ufumbuzi sio kuanzisha chama kipya ufumbuzi ni kuboresha vyama vilivyopo.

vyama vilivyopo sasa hivi haviwezi kusahihisha makosa yake; they are too rigid. Hata ikibidi tufikie vyama 200 as long as hatimaye tutapata chama ambacho kinaweza kweli kukidhi matamanio na haja za watanzania.. I'm fine with that. Kwa sababu kikipatikana vingine vitakufa vifo vya asili tu..
 
Hatutafika mwisho na wala hatutakipata chama unachokitaka wewe.
 
ndio maana ni bora kuanzisha kile ninachokitaka mimi au kushiriki katika kubadilisha kimojawaop kilichopo kiwe ninavyotamania.. si unajua change is not something we wait for.. it is something we bring.
 
Kazi ipo kwa atitude hii. ...is it about teritorry....
 
of course.. usichojua unachotaka utakubali unachopewa; na usiposhiriki kuleta unachotaka utashirikishwa kupokea wanachotaka.. I know where I stand. Do you?
 
True,ndio maana watu ambao hawapigi kura huwa naona ni wajinga kabisa,kwasababu taka wasitake viongozi watachaguliwa,so kutokupiga kura na kuomba Mungu peke yake ndio ujinga wenyewe kwasababu vipi kama watakaopiga kura watatuwekea "Mashetani?"sad enough wengi wa watanzania hawapigi kura.....Ni muhimu juhudi za chama kipya pia kikatoa msisitizo kwenye kuwapata wananchi ambao si wapiga kura kabisa na hawajihushi na mambo ya vyama,wale waliokata tamaa na mambo ya siasa na huku wakiwa hawajui kuwa wana uwezo wa kuzibadilisha siasa hizo kwa kupiga kura na mambo kufanyika kwa maslahi ya Taifa.

Sina figures kwa uhakika kuwa ni wananchi asilimia ngapi hupiga kura,pengine percentage hiyo inaweza kuwashtua watu wengi kwasababu wenye kuwachagua viongozi wa nchi ni asilimia ndoho sana ya watanzania wote.

Hadi pale wananchi watakapoona ni kweli kuna uwezekano wa kuwa na something other than ccm,umuhimu wa kuiweka ccm benchi na kuwahabarisha wananchi kwamba wao ndiyo wenye nchi na kwamba uongozi ni dhamana tuliyowapa waliochaguliwa.....Pia viongozi walioko madarakani ni kama mkataba na kama si executed(kwamba sasa wamfanya yale waliyo ya ahidi wakati wa kampeni na hivyo kupewa kura) basi tuna uwezo wa ku rescind contract hiyo.....

wananchi wapewe shule at the same time God willing hii ccj iwe the real thing....We'll c,Mungu hawatupi waja wake!If its a true deal,then we will prevail eventually and God willing.......to certainly be victorious!
 
of course.. usichojua unachotaka utakubali unachopewa; na usiposhiriki kuleta unachotaka utashirikishwa kupokea wanachotaka.. I know where I stand. Do you?

Siko self centered kama wewe; and besides in your teritorry mr 'me, I and my self', never.
 
Mimi nafikiri muda wa kufanya mabadiliko upo na hali na moyo wa Watanzania kwa sasa kisiasa umeongezeka sana, kila jambo na wakati wake, wakati wakupanda na kuvuna wa CCM umekwisha, sasa ni wakati wa kujenga na kuimarisha nchi yetu, hakika hapa ndani ya javi kuna vichwa vya kutosha sioni haja kutaja majina

Swali la msingi kwanini havijitokezi kungombea uongozi ndani ya nchi yetu? Nini wanaogopa? na kwa nini?

Watanzania tumekuwa watu wa kuandika katika forum na magazetini lakini unapofika wakati wa chaguzi wale wale wala rushwa, Mafisadi etc ndiyo wanachukua na kurudisha form, hakuna hata mmoja wetu anayetaka kujaribu, sasa tutaendelea na mentality hii mpaka lini, ni wakati wa kubadilika ni wakati wa mabadiliko.

Jamani twendeni tukawaondoe hawa jamaa kuanzia vijiji mpaka mjini, Mabadiliko yanawezekana.
 
ndio maana ni bora kuanzisha kile ninachokitaka mimi au kushiriki katika kubadilisha kimojawaop kilichopo kiwe ninavyotamania.. si unajua change is not something we wait for.. it is something we bring.

Hapa ndio penyewe...hatuwezi kuwa tuanzisha mivyama kila kukicha kwa kisingizio vilivyopo havifai..
 
tatizo tumekuwa tukiandika kny forum miaka nenda rudi...

since watu wana mwamko sana hapa ndani kwa nini tusianzishe chama?..

mie ningependa kuona..haya tunayodiscuss humu hayaishii hapa kwenye kundi moja dogo la watu wachache wenye mwamko,bali yanawafikia majority ya watu nje ya jamiiiforums ambao hasa ndio wapigaji kura..!

ila kutoka forum mpk chama ni step moja kubwa sana,lol
 
Mimi binafsi nimechoka sana na tabia ya vyama hivi Tanzania and vyote vinafanya kazi ya kupiga kelele na pia kujifanya kama vile wao sio wanahusika, Nimechoka na vyama kama CCM. Tunahitaji watu wapya kabisa na sio hawa hawa
 
Tatizo la watawala wetu hatukuwaomba watuongoze lakini wanapotokea wapinzani wa kweli wanaanza kulialia kuwa "hawa waacheni kwani wana uroho wa madaraka"
Chama cha siasa ni sulihisho kwa hali halisi ya nyakati hizi. Tusubiri uamuzi wa mahakama kuhusu mgombea binafsi
 
Mwanakijiji,

Nafurahishwa sana na michango yako. Sijawahi hata siku moja kukuandikia au kukujibu makala yako yoyote. Mimi ni mmoja wa watu tunaovutiwa sana na michango yako. Na huwa nasoma michango yako yote.

Leo naandika kwa kuwa umenistua.......nimehisi kama unataka kuweka mpira kwapani na kutundika njumu. Nafahamu kuwa kuna wakati unafikia hatua ya kukata tamaa kwa kuona kuwa pamoja na mawazo yako mazuri pengine nguvu na ushawishi wako una kikomo. Nikukumbushe tu kuwa 'mwale mdogo wa mshumaa hufukuza giza'. Hivyo, usikate tamaa kwa kuwa kila siku bila kujua unatengeneza shujaa mmoja ama unagusa sikio na moyo mmoja wa mtu mpya.

Nikirudi kwenye hoja yako ya hitaji la chama kipya. maoni yangu ni hatuhitaji chama kipya. Kwa maoni yangu, Sera za CCM ni sera za kitaifa. Ni za kitaifa si kwa sababu ya umahiri wa viongozi wa sasa, ila ni kwa sababu ni Chama kilichoundwa kwa mtazamo wa kuwa Chama cha Umma, chenye agenda ya Umma (Mass Party). Isitoshe, CCM imekuwa madarakani kwa miaka 49 ya uhuru wetu ( Nikijumlisha na TANU) na hivyo kuwa sehemu ya utamaduni wetu. Kama kuanguka kwa CCM ndio kungezaa vyama vingi mwaka 1992, basi hoja yako ingekuwa na mantiki, tungehitaji chama Kipya. Lakini kwa kuwa CCM imeendelea kuwepo katika mfumo wa vyama vingi, utakuta kuwa vinavyoitwa vyama vya upinzani si kitu zaidi ya kuwa mchepuo wa CCM kisera au kivuli cha Chama fulani kutoka nje.

Vyama vyetu vya upinzani ni 'reactionary'. Vimezaliwa kutokana na kuwepo CCM si kutokana na vuguvugu la mabadiliko ya mfumo lililotokana na umbwe wa falsafa, itikadi au sera. Ndiyo maana utakuta kwa kiasi kikubwa vimekuwa vikiishi kwa kuibomoa na kuikandia CCM tu. Nafasi ya mawazo mbadala ni finyu. Tatizo lao kubwa ni kutoridhika tu kwa namna ambavyo sera na itikadi ya asili ya CCM isivyoshughulikiwa ipasavyo. Sio kosa la wapinzani ama mapungufu yao, ila ndio mazingira yanavyowalazimu.

Hivyo, leo hii, hata ungeanzisha Chama kipya, sitarajii kuwa kitakuja na itikadi ama sera tofauti na zilizopo. Na kwa kiasi kikubwa, ili Watanzania wakuelewe, lazima utagusa yale maeneo ambayo watanzania wanayathamini. Utaongelea amani, mshikamano, usawa wa binadamu, utu na kujitegemea. Hii ndio misingi ya utamauni wa siasa (political culture) ya Tanzania. Na hii iko katika CCM. Narudia tena, si kwa kuwa CCM ni werevu sana, isipokuwa tu, historia imeipa CCM tunu na dhima hiyo. Ahadi za Mwana Tanu na baadae mwana CCM zimeendelea kuhodhiwa na CCM, baadhi ya misingi na falsafa za kiuongozi zilizokuwapo kwenye Azimio la Arusha zimeendelea kuhodhiwa na CCM. Hivyo, Tanzania kwa kiasi kikubwa ni CCM. Ndio maana Baba wa Taifa aliwahi kusema kuwa " Bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba". Ni imani yangu kuwa, masuala haya ya Ahadi za mwana TANU, Azimio la Arusha na hususan maadili ya uongozi vingekuwa kwenye Katiba ili viwe mali ya wote na si CCM pekee. Tanzania ni muhimu zaidi kuliko CCM. CCM yaweza kuondoka siku moja....lakini taifa linapaswa kuendelea kuwepo.

Kwa mantiki hiyo, niungane na waliotangulia kusema kuwa tatizo tulilokuwa nalo katika uwanja wa siasa leo hii ni ukosefu ama udhaifu wa uongozi ambao unazaa wanasiasa hovyo. Tukipata viongozi wazuri, vyama vilivyopo na sera zilizopo zatosha. Hata ukiangalia CCJ na ujio wake, ukisoma kile wanachokisimamia utagundua kuwa si kipya bali ni kile ambacho CCM wameacha kukisimamia na kukisemea ilihali kipo katika sera na miongozo yake. Katika nchi maskini kama zetu, siasa ni maji, chakula, elimu, afya na miundombinu. Hizo ni agenda za kitaifa. Wananchi wetu wanahitaji matumaini ya maisha yao na vizazi vyao. Hakuna Chama kitakachokuja na agenda mbali na hizi na kikubalike.

Changamoto iliyo mbele yetu ni kupata uongozi huo. Nadiriki kusema kuwa tatizo tulilokuwa nalo leo katika vyama tulivyokuwapo ni kuwa vyama vya upinzani vingali vikiongozwa na viongozi wa kizazi cha kwanza cha mageuzi (1st generation of opposition leaders). Viongozi wa Kizazi cha Kwanza cha mageuzi ( Mrema, Lipumba, Seif, Mtikila, Mbatia na Cheyo) ambao kuwa kwao upinzani kulikuwa ni aidha kuchukizwa au kuenguliwa katika mfumo wa CCM wangali ni viongozi hadi leo. Nakiri kuwa walifanya kazi nzuri sana lakini utume wao umefika kikomo. Wafuate nyayo za Mtei, Makani , Chipaka, Marando na wengine waliostaafu.

Kizazi cha Pili cha Mageuzi (Mbowe, Slaa, Ruhuza, Lwakatare, Lissu) ni kizazi cha pili cha mageuzi. Nacho kinakaribia kukamilisha utume wake ambao ulikuwa ni kuchepuka kutoka kwenye siasa za kupandikiza chuki na kuamia kwenye siasa za kujenga hoja, kutoa fikra mbadala, kuhubiri utaifa na kuongelea agenda za kitaifa (mfano rasilimali za nchi) na hasa kupata busara ya kutumia BUNGE kama chombo cha mabadiliko kuliko majukwaa ya kutupiana lawama na kupaka matope CCM. Kizazo hiki kimeleta mapinduzi katika upinzani ya kifikra na kiutendaji.Sasa tunapata mawazo mbadala juu ya mfumo wa kuendesha nchi mfano "Sera ya Majimbo". Kizazi hiki bado kina jukumu kubwa la kuandaa kizazi cha tatu cha makada na wapinzani wa kitaifa (humu wako wakina Mdee, Mnyika, Zitto na wengineo).

Hakika tunakwenda vizuri kama taifa. Yafaa tuvute subira. Suluhisho si kuing'oa CCM madarakani. Tena ni kosa kubwa kutaka kuing'oa CCM ghafla. CCM ni zaidi ya chama katika Tanzania. Ni taasisi kubwa, ni imani, ni historia, ni utamaduni na zindiko la nchi hii. Imeishi nasi kwa miaka 49 (including ya TANU) na haiwezekani ikaondolewa ghafla na nchi hii ikabaki salama. Ni heri ife taratibu na kansa yake yenyewe wakati upinzani ukikomaa na kupata mbadala wake. Tuongozwe zaidi ya dira ya Tanzania kwanza. Tuisaidie CCM kwa kuiboresha, tuipe upinzani wa kuisaidia kama inavyofanyika katika BUNGE hili la 2005-2010. Vyama vilivyoleta Uhuru vina mapungufu yake lakini si sumu......Botswana inaongozwa na Chama kikombozi na tawala na uchumi wake unakwenda vizuri na nchi inatawalika na imetulia.

Nimalizie tu kwa kusema kuwa, sishawishiki kuwa tunahitaji Chama chochote kipya kwa sasa.

Tanzania itajengwa na wenye moyo! Tanzania, Tanzania..... nakupenda kwa moyo wote!
 
Sheba thanks for the useful post
Nimependa ulivyo analyse vizazi vya mageuzi ni kweli ukiangalia kizazi cha kwanza cha mageuzi cha kina Cheyo,Mrema,Seif, Kambona, Babu nk utagundua ni wanamageuzi waliotokana na aidha kuenguliwa kwenye chama au serikalini kwa hiyo mapambano yao yalijawa zaidi na muhe muhe wa kulipiza kisasi, kwa hiyo tunahitaji wanamageuzi chipukizi wasio wa silika kama hizo wanamapinduzi/mageuzi halisi, vile vile kama ulivyosema hata mimi sikatai kama wanamageuzi wa kwanza hawakuwa na mchango lakini kila kitu kina mwanzo na mwisho wake wataheshimika sana kama sasa watapumzika na kukiachia kizazi kipya cha wanamageuzi kinachochipukia cha kina Zitto na wengine.
 
Swadakta..
tatizo ni mimi na wewe.nilikuwa kijijini hivi karibuni hayo tunayoongea hayapo kabisa,ukiwa fisadi kijijini kwako wewe ni KING/QUEEN.wao neno fisadi kwao halipo kabisa. ukienda huko na msururu wa magari ya kifisadi na mwingine aende na pikipiki ya kukodi wilayani mtapokelewa tofauti kabisa.!!

Kwa hiyo hatuhitaji chama chochote sisi wapenda mabadiliko tuingie humohumo tuwaondoe hao waliopo tuwa-replace na wenye uzalendo. hii mijadala tunayoifanya hapa watu wanaiona.

Nilipokuwa hapo Dar niliusikia mjadala wa nani anamiliki JF mi nilikaa pembeni nawasikia na ni watu wa kawaida sana ,Dada mmoja akipendezwa sana na Mzee Mwanakijiji. Tukaze buti Msg zinafika....mzee mwanakijiji ungekuwa wa kwetu sasa una wake kumi kwa jinsi akina dada wanavyokuulizia.......

Haya ndio mawazo ya watu wa mjini,hawajui kijijini wanajua nini.jaribu kwenda kijijini utaona mengi.
 
Back
Top Bottom