Tunahitaji chama kipya?

Kuanzisha chama kipya si jawabu kwani tuna utitiri wa vyama na hakuna mabadiliko.

Well!

Watanzania wanatakiwa kuingia mitaani kila siku na mabango ya kudai changes na haki bila kuogopa kupigwa na Polisi. Kwa kufanya hivi mabadiliko na haki vitapatikana katika kipindi cha wiki moja tu

Where is the starting point? Nani anatakiwa astimulate that awareness kny mioyo ya Watanzania?
 
Nadhani mengi yalishasemwa na mwenye heri Nyerere. Tusubiri tu mpasuko toka chama tawala na ndio mwanzo wa vuguvugu halisi na harakati za kupembua chuya na mchele. Zaidi ya hapo, hakuna cha chama kipya kwa staili nyingine
 
Uongozi wa chama hicho utatoka wapi? Ndani ya wapiganaji wa kambi ya upinzani (Slaa, Zitto) watakaojitoa huko? Au ndani ya wanaoitwa wapinga ufisadi ndani ya chama tawala (Mwakyembe, Kilango) watakaorudisha kadi? Je, kitakuwa na wapiganaji wa nje ambao majina yao halisi hatuyajui (Mwanakijiji, Rev Kishoka)?

Tupange safu ya uongozi wa chama hicho ambacho nadhani inabidi kiitwe Chama Cha Uhuru (CHACHU):

Mwenyekiti: Dk. Wilbroad Slaa
Katibu Mwenezi: Mzee Mwanakijiji
Mweka Hazina: Comrade Companero
 
He!he!he!he!he!ee ...unajimegea pande mzee?.....sikulaumu hivyo ndivyo inavyotokea ktk uhalisia wa siasa zetu hapa bongo......!
 
Ndugu yangu nafikiri unafikiria kuwa na "fikra mbadala" katika uendeshaji wa shughuli za umma. Labd pia unazungumzia uwezakano wa kuwa na serikali bila siasa. Mm, hiyo ni shughly nzito. Mimi nafikiria kuwa na 'Jerry Rawlings'. asafishe nchi, ajenge uchumi na kuweka near water tight system ambayo itazuia usisadi kurudi. Oh yes change is just arroud the corner and you and I are part of it.
 
Yeah! I think CHACHU is the solution. Well let's just say I like the word, lakini kwa sababu maneno huumba, may it can work!
 
Chama ninachokifiria hakitafanana na chama chochote ambacho kipo sasa hivi; kimuundo, kiitikadi, kimwelekeo na kimfumo. Kitakuwa ni chama ambacho kinarudisha nguvu ya kutawala kwa wananchi wenyewe. Chama ambacho kitakuwa radical in its ideology, liberal in its pursuit of economic prosperity, and conservative in its application of the rule of law and justice. It will be an attempt to bring immediate and recognizable change in our society.

It will stand on certain principles that were the foundations of the building of our Republic. It will not be a mere creation of an idealist but a true manifestation of the reality of our ambition we have as a people. Believe me... change is coming.
 
Mzee Mwanakijiji,

Tatizo sio vyama bali ni watu, tatizo ni Watanzania ambao wengi ni wababaishaji, wezi, mafisadi.

Tunayoyasema hapa JF hatuyaamini kabisa.

Kama kuna watu wanataka kuleta mabadiliko, tayari tuna vyama vingi, ingieni kwenye hivyo vyama na anzeni mapambano kuanzia chini.

Kama neno la injili lisemavyo " Huwezi kuweka divai mpya katika viriba vikuu kuu. Vitapasuka". Katika hali hii tunaitaji mapinduzi (sio ya kijeshi) ya kifikra. Tunaitaji wanamapinduzi watakaokuwa na platform mpya sio hizi zilizochoka na zilizojaa mizengwe tele. Hatuna muda wa kuzawazisha internal bickering za kina Chadema. NCCR Mageuzi kwanza ndio tuanze kazi ya mapinduzi ya kweli. Tunaitaji divai mpya katika viriba vipya. We need a frewsh start.
 
Hatuna muda wa kuzawazisha internal bickering za kina Chadema. NCCR Mageuzi kwanza ndio tuanze kazi ya mapinduzi ya kweli. Tunaitaji divai mpya katika viriba vipya. We need a frewsh start.

point nzito; kama tunaweza kutengeneza mtumbwi ukatuvusha ng'ambo kwanini tuokoe meli inayozama!?
 
Chama ninachokifiria hakitafanana na chama chochote ambacho kipo sasa hivi; kimuundo, kiitikadi, kimwelekeo na kimfumo. Kitakuwa ni chama ambacho kinarudisha nguvu ya kutawala kwa wananchi wenyewe. Chama ambacho kitakuwa radical in its ideology, liberal in its pursuit of economic prosperity, and conservative in its application of the rule of law and justice. It will be an attempt to bring immediate and recognizable change in our society.

It will stand on certain principles that were the foundations of the building of our Republic. It will not be a mere creation of an idealist but a true manifestation of the reality of our ambition we have as a people. Believe me... change is coming.

MM;

Katika Zama hizi za mkanganyiko wa Kisiasa na Vyama, ni vigumu sana watanzania kutofautisha Pumba ni Zipi na Mchele ni upi. Watanzania bado hawajaamka kisiasa kabisa.

Takwimu za uandikishaji wapiga kura na hata wanaojitokeza kupiga kura zinadhihirisha hilo. Jambo la kimsingi basi liwe ni kubadili hali hii.

Bado napenda kufikiri kuwa katika zama hizi mbinu aliyotumia Mwalimu Nyerere kuanzisha chama cha kisiasa inaweza ikafanya kazi zaidi leo kuliko wakati mwingine wowote. Mwalimu na wenzake walibadili chama cha TAA kikawa TANU.

Sasa hivi kuna baadhi ya NGO ni moto wa kuotea mbali kuliko hata vyama vya siasa. Vikipenda, vinaweza vikajiua na kujibadilisha viwe vyama vya siasa.

Alternatively; Mchungaji akipewa Support ya kutosha na kulipolish wazo lake na document zote muhimu. Watu wakawa-recruited hapa na hata kwingineko na kuanzisha Fund ya kukiwezesha chama kwa ajili ya take-off, basi kuna uwezekano wa kufanya kitu bora.

Watu wengi makini na wenye uwezo wa kisiasa ni wanataaluma makini ambao wameajiriwa au wanafanya shughuli zao, hawajaona bado seriousness katika siasa. Hao ndio inatakiwa kuwa-target kwa kuanzia.

Ninao uzoefu na hawa wenye uwezo wengi, bahati mbaya sana kwa sababu ya mafanikio yao katika maisha, wanaona kama siasa si sehemu yao. Wanaweza wakashawishika kujiunga wakiona umakini katika chama, just like TAA and then TANU.
 
The Tanzanian, and ofcourse one of African political guru, Julius Kambarage wa Nyerere alipata kusema, upinzani wa kweli utatoka CCM

Investment ambayo imefanyika kwenye hiki chama si ya wanaCCM na Mafisadi pekee, ni kila mtanzania. Tusiiache ipotee

Kilicho muhimu ni kuingia hukohuko CCM, kuwaacha mafisadi na CCM maslahi or CCM-Mtandao yao, nasi tuondeke na CCM ile ya kina kawawa, sokoine na Nyerere

Nina imani hicho chama bado kipo, na kinaweza kuwa kizuri tuu kuliko kipya katika mfumo wa sasa
 
Nadhani ni wakati wa kuchukua ile kadi sasa...

MKUU KWA HALI ILIVYO SASA CHAMA SIO MUHIMU SANA, CHA MUHIMU KUWA NA WATU WENYE UCHUNGU NA NCHI YAO, HATA KAMA UKIPENDI CCM, LAKINI UNAONA KABISA KUNA MTU MZURI NDANI YA CCM BAC NI HERI KUMPIGIA HUYO KULIKO KUMPIGIA WA CHAMA CHAKO AMBAYE ATAENDA KUWA WA NDIO NDIO BUNGENI, mifano hipo mingi tu kama Chadema kuna mbunge kijana ambaye nadhani hata wa CCM walimpa kula na alikuwa kwa maslahi ya Watanzania, lakini sasa keshakengeuka, kwa hiyo Hatuwezi kumchagua kwa sababu Ya U-Chadema, bora hata tupigie chama chochote chenye "MTU",
 
Mkuu Mwanakijiji Tatizo siyo Idadi ya Vyama. Mbona Viko Vingi tuu
 
Hapa ndipo tulipoanzia.. jibu linakaribia kuwa la kweli kabisa.. mabadiliko huja kwa kuletwa siyo kwa kuombewa na kungojewa..
 
Uongozi wa chama hicho utatoka wapi? Ndani ya wapiganaji wa kambi ya upinzani (Slaa, Zitto) watakaojitoa huko? Au ndani ya wanaoitwa wapinga ufisadi ndani ya chama tawala (Mwakyembe, Kilango) watakaorudisha kadi? Je, kitakuwa na wapiganaji wa nje ambao majina yao halisi hatuyajui (Mwanakijiji, Rev Kishoka)?

Tupange safu ya uongozi wa chama hicho ambacho nadhani inabidi kiitwe Chama Cha Uhuru (CHACHU):

Mwenyekiti: Dk. Wilbroad Slaa
Katibu Mwenezi: Mzee Mwanakijiji
Mweka Hazina: Comrade Companero

Kama slaa ana mawazo mazuri kama hayo ya chama kipya "nafasi anayo huko chadema" atekeleze period!
Mzee Mwanakijiji kama hana chama aende kumuunga mkono slaa
Companero nenda jimboni kwanza usikike
 
Najiuliza kama kuna watu wameanza kuwa kama mimi; vyama vyote vya kisiasa vilivyopo nchini haviwezi kutupatia kile tunachohitaji kama taifa. Siyo CCM, CHADEMA, CUF au TLP ambacho kilivyo sasa kinaweza kuwa tumaini la Watanzania. Je kuanzisha chama kingine ambacho kitatoka kwa wananchi na chenye ajenda ya mabadiliko ya kweli na kikiongozwa na watu wenye mwelekeo wa mabadiliko na wasiogopa political confrontation na ambacho hakitasita kufanya what is necessary to restore law and order and a constitutional rule kitaweza kuwa na nafasi.

Chama ambacho mrengo wake itakuwa ni kuhakikisha kuwa hakuna kuremberiana macho na mafisadi tena wala kuufafanua ufisadi bali kuushughulikia moja kwa moja.

Chama ambacho kitalenga kuleta mabadiliko ya kimfumo na kimuundo wa serikali yetu ndani ya miaka mitano ya kuingia madarakani kikibeba ajenda ya mabadiliko ya kweli (kikatiba, kisiasa, na kiutendaji) huku kikiwashughulikia kama simba mkali wale wote ambao wamelifikisha taifa letu hapa ikiwemo kutaifisha mali zao, kuwasweka jela na wale ambao ni vigogo wa ufisadi "kunyongwa" kama wanavyofanya huko China!

Chama ambacho hakitawabembeleza wawekezaji kama wakwe zetu!

Au ndiyo tubanane mumu kwa mumu huku tukiulizana "kajamba nani'!

Lets hope hakitaanzishwa na kuhodhiwa na wanaopenda umimi, wenye kupenda kusifiwa kila wanachokifanya, wasiokimbilia ajenda kwa ajili ya umaarufu, wasiopenda kujishabihisha na MWalimu kwa nia ya kupata uhalali na wanafiki wengine wenye kupiga kelele wakiwa nje lakini wakifunguliwa mlango tu kushiba harufu za ulaji wanabadilika hata lugha...na rangi pia

omarilyas
 
Lets hope hakitaanzishwa na kuhodhiwa na wanaopenda umimi, wenye kupenda kusifiwa kila wanachokifanya, wasiokimbilia ajenda kwa ajili ya umaarufu, wasiopenda kujishabihisha na MWalimu kwa nia ya kupata uhalali na wanafiki wengine wenye kupiga kelele wakiwa njelakini wakifunguliwa mlango tu kushiba harufu za ulaji wanabadilika hata lugha...na rangi pia

omarilyas

inaonekana una matatizo na watu wengi sana ambao ungependa wawe utakavyo... ukiangalia hivyo unavyovisema unaweza kukuta wapo wengi tu wenye sifa hizo kwenye vyama karibu vyote vilivyopo sasa. Ndio maana tumehitaji chama kipya.
 
kwa mtaji huu tutafikisha mivyama 100 kwani hakuna mwanadamu asiyekuwa na mapugufu.hata CCJ iliyoanzishwa hivi karibuni itakumbana nadhahama hii hii,let wait and see.Kosa halikimbiwi bali hutatuliwa,hata tukianzisha vyama lukuki hatutakosa makosa kwani binadamu ni wale wale.ufumbuzi sio kuanzisha chama kipya ufumbuzi ni kuboresha vyama vilivyopo.
 
Back
Top Bottom