Tunahitaji chama kipya?

Siyo CCM, CHADEMA, CUF au TLP ambacho kilivyo sasa kinaweza kuwa tumaini la Watanzania.

Mkuu MMJJ,
Pole sana maana naona umechelewa kuyaona haya hasa baada ya kutumika sana.

Kwa mtazamo wangu, hivi vyama vyote bado vinafaa sana bali vinahitaji ukarabati wa hali ya juu. Ushauri wangu kwa kifupi;
  1. CHADEMA: Mbowe aondolewe uenyekiti na nguvu ya baraza la wazee ipunguzwe. Nepotism ndani ya chama nayo ipigwe vita na ipewe adhabu kali.
  2. CUF: Lipumba na Maalim Seif waachie ngazi. Uundwe mkakati ndani ya CUF kupiga vita udini na kutoa adhabu kali kwa watakaoendekeza udini katika chama.
  3. TLP na vyama vingine: Wajiunge na wapinzani wenzao.
  4. CCM: MwanaCCM mmoja ajitolee mhanga na kumpiga risasi Kikwete ili tuondokane na hili balaa analolipalilia la ufisadi na kutowajibika. Wengine watakaofuata watanyooka.
 
hili naweza kukubaliana nalo,na walau linamake sense!tuwachukue ''wapiganaji'' halafu tuwagawanye kwa TETRANOMIAL DISTRIBUTION wakapande mbegu zao njema kwenye hici vyama
 
naona tunaleta 1-800-GET-INDICTED hotline news.

Wanaotaka kumpiga risasi rais hawasemi humu, wanaosema humu hawako serious.

Msitake kuwapa sababu wakuda.Juzi naambiwa Bob Matiku alikuwa anashauri JF ipigwe kibomu.
 
Tumieni utaalamu wenu hapa hapa JF. Mtengeneze Sera na Katiba.

Mkishamaliza hilo, tafuteni wanachama na viongozi

Mkishaona mkot tayari kwenda mtaani kupata wengine zaidi endeleeni.

Kisha mtasajili chama kipya ambacho kitakuwa kimesikiliza kila kitu ambacho Tanzania inatakiwa kuwa nacho.
 
Hongera kwa wazo MM.Mwanakijiji.
Nakubaliana na hoja kwamba vyama hivi tulivyonavyo vimeshindwa kukidhi matarajio ya watz....suluhisho kubwa ninaloliona mimi sio kuanzisha chama kipya....suluhisho ni wajitokeze watu kama 10 tu wenye dhamira ya kweli ya kulibadili taifa hili. Condition kubwa lazima wawe na rasilimali fedha sio kugawia watz, bali kuendesha mkakati wao wa kuelekea Ikulu....ndani ya miaka5 wanaweza....Nasema haya kwasababu hata kambi ilomfikisha JK Ikulu haikuwa kubwa, ni watu wachache tu, walikuwa na uwezo kifedha na kimikakati, wakafanikiwa kupenya...kama wangekuwa na ndoto njema kwa taifa lao, leo tungekuwa tunakunywa juice ya utawala wa wanamtandao...lakini kwakuwa walikuwa na dhamira ya kufika ikulu bila kujua cha kufanya wakiwa ikulu ndio sababu taifa linazidi kwenda shimoni...hayo ndio maoni yangu. tatizo hapa ni wanasiasa wenye nguvu ya fedha kutekeleza mikakati ya kuhamasisha na kuwapanga watanzania kwa mabadiliko..watz wako tayari, tatizo ni vyama vingi haviko tayari...hata CCM sio mbaya, ubaya wake unatokana na udhaifu wa upinzani....inaboronga ktk maneo mengi kwasababu haini tishio la kupoteza madaraka....lakini wakiona tishio, ccm itafanya vizuri automatically....mana itajua kwamba ikiboronga inaweza kupigwa chini kwenye uchaguzi....Kwaiyo ushauri wangu tujikusanye watu kama 10, tuwe na uhakika wa nguvu ya fedha kutekeleza mkakati.....tukitekeleza, ni mawili; ama tunachukua dola na kuiendesha vizuri kwakuwa tunadhamira njema, au tutakuwa tishio na hivyo ccm itatishika na kubadilika, hivyo kuwatumikia watz na kusababisha neema kwa watz...lengo ni neema kwa wazt, au sio MM.mwanakijiji?
 
naona tunaleta 1-800-GET-INDICTED hotline news.

Wanaotaka kumpiga risasi rais hawasemi humu, wanaosema humu hawako serious.

Msitake kuwapa sababu wakuda.Juzi naambiwa Bob Matiku alikuwa anashauri JF ipigwe kibomu.

BR fahamu kuwa mawazo haya siyo ya juu juu tu, ni wazi ukiangalia sana utaamini jinsi walivyojipanga kubaki madarakani na jinsi wanavyolindana, ili mtu aingie pale kushika usukani itabidi awe amekula kiapo cha kuendeleza kulindana. Mfano mzuri wa jinsi ambavyo Afrika viongozi wanaweza kuwa wagumu kukubali makosa yao mpaka nchi inaingia shimoni ni ule wa Zimbabwe. Hapa kwetu hakuna tofauti maana wanapokezana vijiti tu kama utani. Wote wanafanana lakini wakiingia waningia kwa gia mpya tu halafu hakuna kinachobadilika. Tulianza na Mr Clean tukatoka na uozo, tukafuatia na kasi mpya na ari mpya sasa wala haileweki ni direction ipi na tumesimama kabisaaa!
Kitendawili hiki kitateguliwa je?? Kwa kweli wadanganyika tunaogopa sana tunapotishiwa na kumwaga damu lakini hapo ndipo woga wetu unapokuwa shamba la wenzetu. Ninahakika haitawezekana mpaka apigwe mtu au watu risasi ni dhahiri tutapoteza na roho zisizo na hatia lakini hapo ndipo mtego wa uwezekano wa mabadiliko makubwa ya nchi yetu ulipotegwa. Wenyewe wanafahamu kabisa. Tunaposema hivi hatuna maana kuwa tunaomba hayo yatokee au tunayapanga ila inaonyesha jinsi ambavyo jamii imechoshwa na ubabe wa CCM.
 
Kwa mtazamo wangu, hivi vyama vyote bado vinafaa sana bali vinahitaji ukarabati wa hali ya juu. Ushauri wangu kwa kifupi;
  1. CHADEMA: Mbowe aondolewe uenyekiti na nguvu ya baraza la wazee ipunguzwe. Nepotism ndani ya chama nayo ipigwe vita na ipewe adhabu kali.
  2. CUF: Lipumba na Maalim Seif waachie ngazi. Uundwe mkakati ndani ya CUF kupiga vita udini na kutoa adhabu kali kwa watakaoendekeza udini katika chama.
  3. TLP na vyama vingine: Wajiunge na wapinzani wenzao.
  4. CCM: MwanaCCM mmoja ajitolee mhanga na kumpiga risasi Kikwete ili tuondokane na hili balaa analolipalilia la ufisadi na kutowajibika. Wengine watakaofuata watanyooka.
Mkuu, hebu tufahamishe hiyo unayooita Nepotism ndani ya chadema ndo ipi...usinambie habari za Mbowe na Mzee Mtei wala Ndesamburo na Owenya...utakuwa huishii hapo,utafika mpaka kwa kina Walker Bush na George Bush...Indira Gandhi na Rajiv Gandhi...Desiree Kabila na Joseph mwanawe...list ndefu, katika mambo ya siasa,hasa siku hizi, ni mamno ya kawaida iwapo yatakwenda katika mkondo sawa.
Halafu unambie huo udini wa CUF ndo upi...hizi habari nimeanza kuzikia Zanzibar, na walokuwa wakizieneza katika balozi za kimataifa ni usalam wa taifa zanzibar...wakitekeleza mkakati wa CCM...wa "ukitaka kumuuwa mbwa mpe jina baya" pengine wewe ni mmoja wao au unashabikia jambo usilolijuwa kwa kufuata fitna na maneno ya uadui na chuki tu.
Halafu hata kama hatuipendi CCM au JK kwanini ulete habari za mauwaji...halafu ndo iweje, ndo ufisadi utakwisha siku ya pili tu tukishamzika JK...come on...this is seriou business kama huna la kusema kaakimya usituletee habari za kihalifu hapa...it sounds treasonous lakini nashangaa Mods, wapo kimya tu
hili naweza kukubaliana nalo,na walau linamake sense!tuwachukue ''wapiganaji'' halafu tuwagawanye kwa TETRANOMIAL DISTRIBUTION wakapande mbegu zao njema kwenye hici vyama
Halafu na wewe mtu mzima unaunga mkono pumba...unanichefua 'asa!
 
Ndugu zangu,
Hata lini mtadumu katika kubalizi kwa kauli tu juu ya suluhu ya masaibu ya taifa letu?
Yako wapi MATENDO yenu?
Wajitokeze basi watu hapa wenye nia njema tupeane kazi za kufanya.
 
Nadhani hakuna haja ya kuanzisha chama kingine bali kuna haja ya kufuta vyama vyote vya siasa.......haya mambo ya vyama ni kuiga tamaduni zisizo na tija. Tunaweza kufuta vyama na kuwa na serikali makini walau kwa muda ili utaalamu ufanye kazi badala ya siasa kuwa kila kitu. Tukishafikia mahali watu wamebadilika kifikra na kutambua uzalendo na umuhimu wao katika kujenga taifa ndio tunaweza kuamua ni mfumo upi unafaa kuongoza taifa letu.

Mmmmmh. . .. .
 
Kwani kile chama cha COPA cha Afrika Kusini kilianzishwa lini na kilifanya vipi katika uchaguzi wao?
 
Endeleeni na porojo baada ya kula chips na kuku wa KFC. madamu NEC au tume ya uchaguzi ni CCM hata watanzania wote waipigie kura Chadema basi mshindi ni CCM. Na huyo Mrema munaemsifu hawa CCM wenyewe bado walikuwa wamelala 95 ndio maana wakawaruhusu kupata kura nyingi lakini walipo amka sasa hakuna mpizani atakaye ruhusiwa kupata kura asilimiya hat 20% na CUF hawataachiwa kushinda hata kiti kimoja cha ubunge bara kwa makusudi maalum.
 
Kwani kile chama cha COPA cha Afrika Kusini kilianzishwa lini na kilifanya vipi katika uchaguzi wao?

COPE ilianzishwa Disemba 2008 na kushiriki uchaguzi Mei 2009 na kupata 8% ambayo ni wabunge 34 katika Bunge la Afrika kusini. Ni mafanikio makubwa sana.

MDM Msumbiji imeanzishwa mwezi Machi 2009 na kushiriki uchaguzi mwezi Oktoba na wamepata juzi 11% sawa na wabunge 27 katika Bunge la Msumbiji.

Hata hivyo Mwanakijiji, tunahitaji chama kipya? Mavyama yote yaliyopo hapa nchini hayawezi kuboreshwa? Kuanzisha chama kipya ni kurudi nyuma. Tuangalie matatizo tuliyonayo sasa kama yapo na kutatua.

Napenda tukumbuke kuwa Mrema alitoka CCM kwenda NCCR mwezi March 2005, Oktoba akapata 28% ya kura za Urais na 31% ya kura za wabunge a jumla opposition ilikuwa na 40% ya kura za wabunge ingawa ilikuwa na kiasi cha asilimia 22% ya wabunge. Hii ni kutokana na mfumo wa uchaguzi tulio nao ambao hautoi fursa ya vyama vidogo kukua.

Hivyo basi mfano wa COPE na MDM sio mfano sahihi kwa Tanzania.
 
.......... Mavyama yote yaliyopo hapa nchini hayawezi kuboreshwa? Kuanzisha chama kipya ni kurudi nyuma. Tuangalie matatizo tuliyonayo sasa kama yapo na kutatua..........

Nani wakuviboresha vyama hivyo?new members wawe encouraged kujiunga na walete mabadiliko huko ndani?Kama ni hivyo wanapewa nafasi hiyo?

Je kama ni hao hao viongozi walio kny vyama hivyo ndio wakuleta mabadiliko kipya gani tutugemea kutoka kwao, wameshindwa kufanya tangible changes kwa miaka zaidi ya kumi, tutarajie nini kutoka kwao? Kwangu mimi sitarajii maboresho yeyote kutoka kwa viongozi waliopo sasa kwani most of them ni kama ''wamefulia kisiasa'' wameshindwa kabisa kukuza mitaji yao midogo ya Kisiasa, kinachotokea sasa waliowengi wao wanafilisika, mitaji yao imekwisha!

Mimi sipo kny chama chochote, lakini kama mtazamaji nikiwa nje ya uwanja wa mpambano naona vyama vilivyopo vina matatizo lukuki ikiwa ni pamoja na yafuatayo;
  • Viongozi waliomadarakani ni wabinafsi kupita kiasi, taasisi wanazoongoza ni kama ''wamezibinafsisha'', zinaendeshwa kama vile maduka yao ya binafsi kutumika zaidi ''kujikimu'' na si kuendeleza mipambano ya kisiasa country wide and internationally.
  • Vyama vilivyovingi vimekosa focus kabisa.....mmojawapo ya malengo ya kuanzisha chama, ni kuongoza dola.......vyama vyetu vimekosa kabisa kufocus kny hili kiasi kwamba huwezi kuona kwamba hata mwaka 2020 au 2030 chama fulani kinaweza kushika dola....hakuna hizo dalili kabisa.
  • Kukosa mikakati ya kisiasa....(lack of political strategies) .....sina uhakika kama vyama vyetu vyote vina mikakati mizito ya kisiasa inayotekelezeka, zaidi ya kulumbana tu! Kwa mfano ile operation Sangara ya Chadema, ingekuwa improved na isiishie kufanya mikutano tu, bali kuimarisha vyama vyao kuanzia ngazi za vijiji vyote vya Tz na kuhakikisha wanakamata serikali nyingi za mitaa kwa kuhamasisha wananchi wengi kwenda kupiga kura.....ni less than 5% ya watz wote ndio wanaweza kuwa wamepiga kura juzi kny serikali za mitaa......wapinzani wanafanya nini? Katika kipengele hiki kwa mfano, vyama vyetu havijaweza kuwafikia watanzania wengi zaidi na kuuza sera zao ili kuweza kuongeza idadi ya wanachama wao mijini na vijijini.....!mi binafsi kwa mfano nimekuwa ni kijaribu kuvisoma vyama mbalimbali, ili nipate kimoja cha kujiunga nacho, lkn mpk sasa sijaona,labda pengine nimekosa mwongozo au sijadedicate muda mwingi for this.....lkn ukweli vyama vyetu havina mikakati ya kisiasa, km ipo si achievable!
  • Vyama vingi vina ukata wa hali ya juu......! havina mikakati mizuri ya kuongeza mapato yao pia pindi wapatapo udhibiti wake ni mbovu sana!
  • Uroho /uchoyo wa madaraka......
  • Vinakosa ''fair playing ground'' baina yao na chama tawala, na vimeshidwa kabisa kupush for ''fair playing'' grounds ktk miaka yote zaidi ya kumi!
Ndo maana kutokana na mambo kama haya wakati mwingine hufikiri kwamba labda tunahitaji chama kingine mbadala wa vilivyopo sasa!
 
Tatizo sio vyama vya siasa.Hata kama tukiwa na vyama 10000000. Sio jibu la matatizo.Tatizo kubwa ni watanzania waliobweteka wakizani viongozi wa vyama watafanya kila kitu

Ni jukumu la watanzania kichangi halia na maliakwenye vyama na sio kuaachi kiongozi fulamnia kutoa fedha zake kuchangia chama halafu kusubiri awakilishe na kupigania haki za wanachama lazima ataweka maslahi yake kwanza then ya wanachama

Tutabakia hivi hivi kama watanzania hatuta shirika moja kwa moja katika ulingo wa siasa
 
Mimi naamini tunaweza kuanzisha chama cha siasa kitakachotoka kwa wananchi wenyewe (kama alivyoshauri MM). Tunaweza kupeana mawazo humu kuhusu namna ya kuasisi chama hicho ambacho naamini kitapata nguvu haraka sana kutokana na msimamo utakaojiwekea wa kuleta mabadiliko ya kweli. Vyama vya upinzani tulivyo navyo sasa ni kama vya watu fulani na wafuasi wao wachache. Angalia Chadema ya akina Mbowe, NCCR Mageuzi ya Mbatia na CUF ya akina Seif na Lipumba. Tusikate tamaa, ni lazima tuangalie namna ya kulikomboa taifa hili kutoka mikononi mwa mafisadi na wapambe wao waliopo serikalini.
 
kwa jinsi watu wamepiga kura tena kuichagua CCM daliili ya uwepo wa watu hao katika nchi yetu is almost zero! Watanzania wamefikia mahali pa kuridhika na maisha wanayoishi na siasa zilivyo zinaendeleza mawazo hayo hayo.

WAliotuangusha katika haya ni vyama vikubwa viwili cha CHADEMA na CUF. Vyama hivi ningekuwa na uwezo ningefuta katika historia yetu na viongozi wao kuwatupa katika kisiwa cha usahaulifu tuanze upya kwani vinasimama leo hii kama kikwazo thabiti na dhahiri cha mabadiliko tuyatakayo!
what happen wamefanya nini? wamevunja katiba na sheria ya nchi? wamevunja sheria za chama chao au nini?
Pili issue ya Prof. safari kushindwa uchaguzi mkuu wa CUF mimi nafikiri Prof. Safari hajui siasa yeye mwenyewe ni tatizo...zitto na mbowe..nafikiri wazee wa chadema ni tatizo..if that is the case..then..kwa CUF inabidi ndani ya chama atokee mtu ambaye anaweza kupambana kukwelikweli na lipumba na kuhusu wazee wa chadema nafikiri ni kuondoa hako ka-mandate ya wazee kwenye system ya demokrasi bado nina "Imani na CUF na Chadema" tunatakiwa kuwabana kwelikweli mpaka waelewe.
 
Unafahamu hawajavunja sheria wala katiba ya nchi. Lakini wamefuata na hadi leo ni kama wameikubali Katiba isiyokuwa sahihi kwa mfumo wa leo. Katiba isiyokidhi mahitaji ya taifa hili la leo huku wakijua wazi kuwa hawatakaa washinde katika harakati za kutaka kumkomboa mtanzania kutoka katika umasikini, maradhi na ujinga. Wameshindwa hata kukaa pamoja wapange makakati wa pamoja. Wamekubali kugawanywa kijanja janja/kijinga jinga na CCM. Wanajiona kila siku wakidhoofika lakini hata hawajaonekana kujifunza kutokana na makosa yao. Wangekuwa wamejifunza mpaka leo hii tungekuwa tumeona angalau wamekuwa wamoja wakaunganisha nguvu zao kwenye majimbo machache na kuondoa tofauti zao tukajua kweli ni vyama komavu na vyenye nia nzuri. Badala yake vinazidi kuonekana ni vya kimakundi zaidi. Havijaelewa nini Tanzania leo!
 
Naona Dawa yake ni kususia uchaguzi na bora watu kusiwe na uchaguzi maana ndio chanzo kikuu
 
Kuanzisha chama kipya si jawabu kwani tuna utitiri wa vyama na hakuna mabadiliko.

Watanzania wanatakiwa kuingia mitaani kila siku na mabango ya kudai changes na haki bila kuogopa kupigwa na Polisi. Kwa kufanya hivi mabadiliko na haki vitapatikana katika kipindi cha wiki moja tu.
 
lazima kuwepo na leaders behind the scene(ambao wanaheshimika duniani na Tanzania) wanaowaingiza watu mitaani otherwise..wakipigwa bomu moja la machozi na kuzingiziwa kwamba ni magaidi na wametumwa na Osama..hutawaona tena usoni..wengine wazee wetu wamekuwa victim of dicteta nyerere ..kuongea tunaweza kwenda barabarani..lol naona bado.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom