Tunaanza na Tume Huru Kwanza

Tume ya Jaji Nyalali ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi iliweka bayana kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, ni lazima kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya.
Tume ya Nyalali ilisema '' ni lazima kwanza kuwe na Tume huru ya uchaguzi na kuandikwa katiba mpya''. ACT wanakubali mambo hayo yanaenda sambamba!
Jeshi la Polisi linaingiaje kwenye mambo ya siasa? Kazi ya jeshi ni kusimamia sheria za nchi.
''Kuambiana ukweli na kuwa na utayari wa kubadilika''. Kule Zanzibar kumefanyika miafaka mingapi na hali ipoje leo hii. Kuna utayari gani kwa CCM waliopora chaguzi! utayari wanaozungumzia ACT ni upi huo
ACT wanaamini kukiwa na Tume huru basi Wabunge watachaguliwa kwa uhuru.
Hapa ndipo ninapoona ACT wana tatizo la kufikiri. Hivi si waliwahi kuwa na Tume huru Zanzibar?
Kwa mamlaka gani Jecha aliharibu uchaguzi alioshinda Maalim?
ACT hawakumbuki Jecha aliondolewaje, alipelekwa wapi na aliamriwa aseme nini?

Tume huru haina uhusiano na uhuni unaofanywa. Mtu akiporwa Form si tatizo la tume ni uvunjaji wa sheria na wahusika ni Polisi. Hujuma za mawakala si tatizo la tume ni uratibu wa CCM, Polisi na vyombo vya usalama.
Tunarudi pale pale kwamba wao wanaamini uchaguzi unahujumiwa na Tume. Hawana habari kuwa uratibu wa hujuma za uchaguzi ni wa mfumo mzima.
4. Iwapo kwa sababu zozote zile, Mchakato wa Katiba Mpya hautakamilika hadi wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, Tume Huru itakayoundwa itaweza kusimamia chaguzi hizo kwa uhuru na haki.
Kule kule wanaamini Tume huru itamaliza tatizo la uhuni. Hawakumbuki Jecha alifanya nini kwa msaada wa nani na kwanini hakukuwepo na hatua dhidi yake. Si Jecha alikuwa na Tume huruiliyowashirikisha CUF ambao ni ACT
Katiba pendekezwa iliandikwa na CCM, kusema kwamba maoni ya Tume ya Warioba yachanganywe na uhuni wa CCM ni ku adulterate maoni ya Wananchi.
ACT Katiba pendekezwa ni mali ya CCM. Wananchi wanataka kurudi ktk Tume ya Warioba
Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi Wapatikanaje?

1. Sheria mpya ya Uchaguzi (National Elections Act 2022) iweke utaratibu kuwa Watanzania wanaotaka kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi waombe kazi kufuatia tangazo la wazi kwa umma.
Kumbe tayari kuna sheria imeandaliwa!!
3. Kamati ya Uteuzi ifanye usaili (interview) kwa uwazi kwa waombaji wote na kuchuja majina ambayo yatapelekwa kwa Rais kwa ajili ya uteuzi.
Kwanini Rais awe na mkono wa uteuzi? Rais anatakiwa aidhinishe jina. Rejea tume ya uchaguzi ya Ghana. Rais hana mamlaka yoyote ya kuteua majina au kupewa lundo la ma
Changamoto pekee ni kuwa Katiba Pendekezwa haikutokana na maoni ya pande zote kwa sababu Wabunge wengi wa Upinzani walisusia upigaji kura.
Forget about katiba pendekezwa. Turudi kwa Rasimu ya Warioba.
ACT hii katiba pendekezwa iliandikwa na CCM
ACT katiba pendekezwa iliandikwa na CCM na haihitaji maboresho yoyote. Hii ilifuta maoni ya Tume ya Warioba ambayo ni maoni ya wananchi. Katiba pendekezwa si maoni ya Watanzani, ni Bunge la CCM.
Ninatilia shaka uelewa wa ACT Wazalendo! kuna tatizo kubwa wanajitahidi kulisukuma mbele
Huwezi kuwa na Tume huru ya uchaguzi katika mfumo wa dhulma ACT!

Kuna tatizo kubwa sana na nadhani kuna kitu kipo nyuma! mtakuja baini ikiwa ni too late

ACT na CCM wanaserikali ya pamoja kule Zanzibar, huku bara hatuna GNU na ACT wasijaribu kututumbukiza katika matatizo hayo. Kuna motive behind , ipo siku watu wataelewa tunamaanisha nini. Kuna kitu!
 
Wasi wasi wa ACT ni kuwa kuna uchaguzi wa serikali za mitaa 2024. ACT wanaamini watashinda chaguzi hizo. Hivi wakipata viti 5000 dhidi ya 40,000 kuna maana gani?
ACT wanaamini kuna uchaguzi 2025 na Tume huruikiwepo watashinda. Hivi wakishinda viti 50 vya ubunge dhidi ya 200 vya CCM wataleta mabadiliko gani? Hapo si ndipo watapiga mhuri kwa CCM kufanya mauza uza yao.

Kosa la ACT ni lile walilofanya Chadema mwaka 2010. JK alitangaza kuanzishwa mchakato wa katiba mpya. CDM wakasema Rais amefanya jambo jema na Wamefarijika. Tuliwaambi kuwa hiyo si njia sahihi, mchakato ulitakiwa uanzie Bungeni ili waweze kuuratibu

Matokeo yake mchakato ukawa mali ya 'Rais' na matokeo yake tunayajua
Hilo ndilo kosa la ACT kutaka Tume huru na Wajumbe wake wapatikane kwa mazingira ya sasa

Haraka ni ya nini ACT?
 
Nimesoma Hoja za ACT ni nzuri na zinaeleweka shida ya Chadema ni wanataka Katiba mpya kama wimbo ila hawajaleta hoja za ushawishi kwanini Katiba mpya

ACT wamesema Tume huru kwanza na wametoa sababu

Chadema njooni na sababu kwanini Katiba mpya kwanza

Hapa itaturahisishia kupima kipi kianze, hoja zitoke kwenye Uongozi wa Chama sio kwa watukanaji mitandaoni
 
Wafuasi wa kilichokuwa chama kikuu cha upinzani wanavyoushambulia uzi wa ACT wazalendo ni dhahiri wanatambua 2025 hali ni mbaya kwao.
Mtake msitake 2025 ACT wazalendo wanakwenda kupata wabunge wengi
Labda Pemba
 
mzee kama CCM hawataki hiyo katiba mpya itapatikana vipi? Please explain kwa mfano tu tume hii iliyopo ndio isimamiye kura ya maoni ya katiba mpya itakuwaje please lete fikra zako
 
Traitors at work
 
t
then what the way forwad kama CCM hawataki Please
 
nani asiye wajua ninyi kuwa ni mapandikizi ya mbogamboga? Ukweli ni kwamba chama chenu hakina ushawishi wowote ule bara ukiondoa zanzibar ambapo wana Cuf waliwajoin kumfata Maalim.Hamna mvuto wa kisiasa kabisa. Udini umewajaa na hamna jipya!
 
Katiba ya chama gani inaruhusu vipindi viwili? Tuwekee hapa kifungu kilichosiginwa. Halafu unaonekana mweupe kichwani. Tukishasema rais rais akifanya ujinga anaenda jela anaenda kweli. Muulize baba yako Zuma Nini kikimkuta. Au muulize baba yako wa kambo Kenyatta Nini kikimkuta kwenye BBI.

Rais anajifanyia anayotaka kwa sababu sisi(katiba)Ndio tumempa mamlaka. Kwa katiba hii hata Malaika itamlevya kwa madaraka. Ila tukimwonesha njia yakupita naye atafuta humohumo. Funguka wewe.
 
Si mnatuambia yesu kajizaa , Hivi akili inakubali hii kitu ??
Nakutahadharisha dogo

Kama Huna Ilimu ya deen/Imani piga ukimya!

Nifahamishe hili! Kuna Jambo gani Mwenyezi Mungu Hawezi??
 
Yaani hata wewe unainhia kwenye mitego ya Hawa waramba viaty wa kiongozi mkuu wa chama,
Kati ya Mzazi na mtoto yupi alianza kuzaliwa?
 
Hawezi kuolewa wala kunya
Duuh! Umeandika as if ni mc wake



بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ

[ AL - BAQARA - 117 ]
Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi pasina ruwaza; na anapo taka jambo basi huliambia tu: Kuwa! Nalo huwa.

Kambishie mungu wako kuwa ww ni muongo kuna hili....huwezi??
 
Huyo ni Nani anayesema hapo ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…