Tuna Kisa Gani na Comoro Tena?.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuna Kisa Gani na Comoro Tena?....

Discussion in 'International Forum' started by PakaJimmy, Apr 13, 2010.

 1. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwa waliotazama habari jana TBC1, waziri wetu wa mambo ya nje, Berbard Membe anatuhumiwa na vyama pinzani vya nchi hiyo kwamba alifanya ziara nchini Komoro ambayo ilionyesha wazi upendeleo kwa Chama tawala cha nchi hiyo kinachoongozwa na Rais Osambi.

  Inadaiwa hakutoa nafasi kwa Kambi ya upinzani ya huko kukutana naye, kitendo ambacho kimewaudhi sana wananchi hao, hasa ukizingatia nchi hiyo iko katika mgogoro wa kiuongozi, ambapo inaonyesha Osambi anataka kung'ang'ania kuendelea kutawala kwa kutumia ushawishi wa Bunge.
  Ikumbukwe pia Tanzania ilishalaumiwa na kambi ya upinzani ya Malawi enzi za Ben MkaaHapa juu ya shida ya namna hii!

  Sasa swali ninalijiuliza mimi, Tanzania sisi tuna nini na Komoro ya watu jamani?..Mbona tunaonyesha kuimezea mate sana nchi hii na kuitiatia vidole?...Ziara za wakuu wa nchi hizi mbili kutembeleana zimekuwa za mara kwa mara sana..!

  Embu wana jamvi tuitazame hii maneno kwa undani!
   
 2. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2010
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  PJ, nilibaki kinywa wazi nikimsikiliza Membe! Utafikiri anaongelea mkoa mmojawapo wa Tanzania. Hata ingekuwa ni Umoja wa mataifa wanongelea hili jambo tungeona diplomasia katika matamshi yao. Hivi hawa watu wetu huko chuo cha diplomasia huwa wanasoma nini? Ni kulewa madaraka au ni ubabe wa kweli, au tunataka kuwavuta kama Zanzibar? Who are we to speak with that tone? I though I went to a wrong theater that is why I was watching a wrong movie!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  ..Nadhani kitendo cha kupeleka majeshi kule kimetufanya kuwa na hisa za utawala huko!
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  So Comoro imekuwa kama ni koloni la Tanzania!!
  Very Funy.
  Viongozi wetu wameshaivuruga Tanzania yetu, sasa wanahamia kuivuruga Comoro.
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Ila hili la Comoro litakuja watokea puani hili, Huyu membe na wenzie sijui wana hisa gani huko Comoro. Mbona kule Zimbabwe hawakwenda?
   
 6. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huenda Comoro ni koloni letu..sijui tulilitwaa lini ama tulipoenda kumg'oa Kanali Bakar. Mie nilivyomuangalia alivyokuwa akiongea kwa jazba sikumuelewa kabisa....tuiache Comoro ijiamulie mambo yake sie si kiranja wa nchi hiyo.
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kiukweli Tanzania ni kilanja wa kisiri siri Afrika mashariki na ya kati, viongozi hawataki tu kusema... Ukiangalia kiundani karibu nchi zote za Afrika Mashariki na ya kati kama vile Burundi, Rwanda DRC, Comoro, Uganda kote serikali ya Tanzania imetia mkono wake kusaidia kuwaweka madarakani viongozi waliopo.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Sa ni nani alietupa madaraka haya ambayo ni mzigo wa lawama?
  Tunaonekana nchi ya mazuzu kwa kuingilia mambo ya watu kila kukicha!...huh!
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,450
  Likes Received: 5,838
  Trophy Points: 280
  ...na kuacha yetu kwa mbachao
   
 10. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ni ajabu mzee, comoro wenyewe wana interest na Ufaransa, wabongo masikini wanainyemelea, labda na sisi tunataka kuwa na kakoloni ati, zanzibar tu inatuyumbisha, comoro kusiko kuwa na lolote kuna nini? au kwasababu kuna wangazija wengi, na baadhi ya viongozi wa nchi yetu ni wangazija? sijui......kaazi kwelikweli. pata potea.
   
 11. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Idadi kubwa ya waliosoma Chuo cha Diplomasia wako barabarani?
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mkuu, ni taarifa au swali?...sijakusoma vizuri!
   
 13. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Inaelekea watawala wetu ni mafundi wa kutatua matatizo yaliyo nje ya mipaka yetu lakini yetu ya humu humu ndani yanawashinda!! Kila leo watu wanachinjana huko Tarime na maalbino bado wanakatwa mikono lakini watawala wanaona afadhali kupeleka askari Darful / Comoro kuliko kuimalisha usalama wa wadanganyika!! Kwa staili hii ya kufoka foka Bernard Membe Urais anaoutafuta atausikia kwenye bomba tu!!
   
 14. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #14
  Apr 13, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mimi naona kama kuna maslahi ya nchi kuwekeza huko ni bora tuende tu ila tuwe carefully.Tupige hatua kwa fursa zote positive.Membe nae sometimes anashindwa kuwa mjanja,inabidi awe mpole sehemu ambayo anaona anahisiwa vibaya huku akipiga mahesabu makali ya jinsi ya ku-maximize our interests huko
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Mende kayakoroga tena, nimesikia yule rais wao amekataa kutoka madarakani labda ndo ushauri alopewa!
   
 16. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #16
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kuachia ukiranja kuna ugumu wake.
   
 17. bona

  bona JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  unajua unaweza kusoma ukafaulu lakini elimu yako isikukomboe ambayo ndio shabaha kubwa ya elimu, kwani wangapi wanamaliza chuo lakini uwezo wa utendaji ni mdogo, huyu chinga ( membe ) ame graduate ktk vyuo bora kabisa duniani kama udsm first degree na the famous john hopkins kule usa kwa master degree, lakini hajapata ule ukombozi kusudiwa kutoka kwenye elimu ambao huo unakuja kutoka kwenye ku practise kile ulichokisoma uyu amefaulu masomo na kupata masters yake apo na akaishia apoapo! ili ndio tatizo tulilonalo dhidi ya wasomi wetu uchwara, wanavyeti wamefaulu lakini ukombozi hawajaupata kutoka kwenye iyo elimu yao. tulipata shida bure ya kupeleka majeshi kumsaidia mtu kwa sababu ya urafiki, imagine
   
Loading...