Tuna akiba ya pesa dollar bilion 5.3

1587260934556.png
 
Kwa hiyo sababu ya chuki na mkuu wa nchi ndio ukaamua kuunganisha ujumbe wako na kichwa cha habari! Alafu mpaka sasa kuna mapungufu yoyote katika kuhudumia hawa waliougua kwa bahati mbaya mpaka anyofoe toka akiba iliyopo?
Kama akiba haiwezi kutumika kununulia barakoa ili wananchi wajikinge na kuwakinga wenzao dhidi ya coviidii, hiyo akiba itakua na maana au faida gani?
 
TUACHE SIASA.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Hiyo Akiba ndio muda wake huu kutumika, au hujui kuwa hiyo akiba ni ya kutumika kwa mazingira haya? Je kama hazitatumika sasa, hizo fedha ni akiba kwa ajili ya hali gani?
Tusiwaamini wanasiasa wa nchi hii.leo wanaongea hili na kesho wanabadilika.subiri kesho utasikia hawana fedha za kulipa mishahara.Tuombe Mungu gonjwa hili liishie mbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo unataka hela yote ya hazina itumike kutibu korona?
fedha zikiisha na korona akazidi kupamba moto kipi kitafuata?
Tujaribu kutumia akili na sio mihemko ya kisiasa hasa kwenye mambo ya Kitaifa.
Nani kasema yote wakati wa majanga kama Kuna akiba unapunguza kidogo kukabiliana na majanga ya Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo hayo ya kuandika bila kuwaza kwa mapana.

Kumbuka hata Corona wapinga serikali walitoka mapovu bila kuzingatia kuwa maamuzi ya kiongozi wa nchi yanakuwa yanatazama jambo kwa mapana na yanazingatia taarifa nyingi za siri. Na wanajifanya vipofu wa kutoona dhamira ya serikali ya kusongesha nchi mbele kuliko awamu nyingi zilizopita.

Kwenye mambo ya msingi ya taifa letu vizuri kuweka ushabiki mbali.
 
Za kuweza kuendesha serikali kwa miezi 6 bila kukusanya kodi hata nchi ikiwa na janga au vita

Mkuu alinukuliwa zaidi ya mala 5 akisisitiza.

Yeye yupo anachangiwa na wakina Rostam,*
Anachangiwa na wachina, anachangiwa na walahoi wa bongo, anaomba mkopo IMF wa 190+US dollar million.

Kumbe Mungu uwa achelewi kuumbua mtu muongo

Tunazidiwa na nchi kama Rwanda, Kenya, South, Misri, Ghana na nigeria wote wametoa pesa hazina kiasi kuokoa uchumi.

Je serikali haina taarifa kwamba kuna kiwango cha mitaji kimeshaanguka? Je bado hawana taarifa kuna watu washapoteza ajira? Wamefanya nini kuokoa sector ya utali Tanzania?

Je wanafanya nini kwa watu waliokuwa wamekopa uku wakiwa wanatoa ajira kibao kuweza kuwaondolea malejesho angalau kwa miezi 3 ili kulinda ajira za walalahoi?
Jamaa Yuko kwenye mkakati mkali kuhakikisha anapata kura zote, Hadi za nchi jirani zinazotuzunguka
 
Hii ni sehemu ya hotuba ya Waziri wa fedha wakati wa bunge la mwisho...

38. Mhe. Spika, benki za maendeleo zinajumuisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania -TADB na Benki ya Maendeleo TIB. Kati ya mwezi Julai 2019 na Machi 2020, benki za maendeleo zimetoa mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 54.44 sawa na asilimia 32.9 ya kutoa mikopo ya shilingi bilioni 164.84. Kati ya kiasi hicho, Benki ya Kilimo Tanzania ilitoa mikopo yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 35.86 sawa na ufanisi wa asilimia 176.3 ya lengo la kukopesha shilingi bilioni 20.34 na benki ya TIB shilingi bilioni 18.58 sawa na asilimia 12.86 ya lengo la kukopesha shilingi bilioni 144.5.

Nataka kuamini akiba ya fedha za kigeni kuwepo kwenye chungu BoT kama ambavyo kwa uchache tumeona kuna uhakika wa uwepo wa zaidi bil 125 ambayo ni zaidi ya asilimia 88 zilibaki Benki ya uwekezaji.

Hii fedha bila shaka ingeweza kutumika kama investment financing kwenye strategic project.
Mathalani BoT inaweza kutoa dhamana ya Mtanzania kuwekeza kwenye kiwanda cha sukari ili kukidhi deficit ya sukari ambayo kila mwaka tuna-import.
Au BoT ingeweza kutoa dhamana kuanzisha kiwanda cha madawa ya binadamu na madawa na mifugo ambapo by more than 90% tuna-import.

Uwekezaji kama huu ambao unapunguza imports, kwa kuzalisha ndani na kuongeza ajira na kungeza tax base, kuongeza mzunguko wa fedha ndani iko haja BoT na Hazina wakamsaidia Mkulu kwa kubuni strategic investment zenye quick return on investment kwa kuzingatia available market ya Tanzania na SADC.

Mkulu yuko vizuri, ila wasaidizi wake lazima waje na strategi solution namna gani uwepo wa dollar namna gani unaweza kutumika kama dhamana na ya mid term and long term investment projects za kuongeza uzalishaji na thamani ya mazao kimkakati kutoka pamba kwenda nyuzi au kitambaa
kutoka kahawa ghafi mpaka instant coffee

Mambo haya kutegemea SIDO na VETA pekee kama solution, sio sawa. Tunaweza kutafuta brains humu humu ili kuona namna gani ya kujenga laverage ili walau say 20% ya akiba ya BOT ikitumika kama dhamana kwa kukuza au kuchochea uwekezaji, TANZANIA ya viwanda yenye kulenga kukuza uchumi wa kati wa kutoka low mid economy ya USD kwenda juu zaidi ya hapo.
 
Akiba hutumika pale njia zote zipofunga. Ndio unatumia tena kwa akili. Hata ukiwa na kibubu huwezi kukivunja kwa shida ambayo unaweza itatua bila kuvunja kibubu. Kuvunja kibubu ndio inakuwa option ya mwisho kabisa.
We hufai kuwa hata kiranja wa chekechea kwa akili kama hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
,,🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kumbe tulikuwa na hela ya kuendesha nchi kwa miezi 6!Sasa hii story ya Samia ya akiba ya miezi 3,mbona unaonekana ni ushindi mkubwa wakati tulishafika mpaka miezi 6?
 
Back
Top Bottom