Wanunuzi wa vyakula kutoka nje ya nchi watumie dola kununua vyakula kutoka katika maghala ya serikali

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,109
22,561
Kila mara wananchi tulipohoji kuruhusiwa Kwa wafanyabiashara Kutoka nje ya nchi kuingia nchini kununua mazao ya vyakula mashambani kwa pesa za kitanzania, tulijibiwa kuwa " Tusimpangie MKULIMA wapi auze mazao yake".

Pesa za Umma zimetumika kuagiza mbolea na pembejeo za KILIMO nje ya nchi Kwa Dollars, iweje wafanyabiashara Kutoka nje ya nchi waruhusiwe kununua nafaka mashambani kwa pesa za madafu?

Pesa ya wananchi imetumika kuweka RUZUKU kwenye Bei ya mbolea Ili MKULIMA anunue Kwa Bei himilivu, iweje wafanyabiashara Kutoka nje waruhusiwe kwenda mashambani kununua mazao Badala ya kununua masokoni?

Tukilea mtindo huo kuzoeleka, KARIAKOO itakosa wanunuzi Kutoka nje ya nchi maana watakimbilia mashambani kumpiga MKULIMA.

Makampuni Kutoka nje yataingia mashambani kununua maembe, machungwa, parachichi nk nk, masoko yetu yatafanya KAZI Gani kama mnyororo huo utafupishwa kiasi hicho?

Kwanini Serikali itumie tena hazina ya pesa za kigeni kuagiza Mchele na vyakula nje ya nchi wakati ingeweza kuyanunua mazao hayo muda huu na yakatunzwa katika maghala yaliyoko katika mikoa mbalimbali nchini?

Jukumu mojawapo muhimu la wizara unayosimamia ni kuhakikisha MKULIMA ananufaika na JASHO lake, lakini pia wizara inawajibika kuhakikisha inadhibiti mfumuko wa Bei holela.

USHAURI.

1. Wanunuzi wa mazao ya vyakula Kutoka nje waelekezwe kununua mazao kwenye maghala ya Serikali au kwenye masoko makubwa ya mikoa na wilaya na waje na Dollars, maana hivi sasa Nchi yetu Ina uhaba wa pesa za kigeni.

2. Vikundi vya wakulima viwezeshwe mikopo Ili vifanye package ya bidhaa zao Ili wauze nje ya nchi Kwa pesa za kigeni.

3. Maghala ya Serikali yafunguliwe katika miezi ya September Hadi February Ili kusaidia wakulima na wananchi kununua vyakula Kwa Bei nafuu kipindi ambacho wanasubiri kukomaa Kwa mazao Yao.

Kwa kufanya hivyo, Serikali itaweza kudhibiti mfumuko wa Bei maana itajua Kwa HAKIKA demand ya soko la ndani ni kiasi Gani hivyo kuuza ziada nje bila kuathiri Bei katika masoko ndani ya nchi.

ANGALIZO;Lipo TISHIO la njaa litakaloikabiri Dunia miaka michache ijayo hivyo, Nchi inatakiwa kuhakikisha inaweka akiba ya CHAKULA itakayodumu angalau Kwa miaka mitatu Ili kuhakikisha utulivu unakuwapo nchini endapo tutapitia kipindi hicho kigumu.

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen.
 
Wewe mtupu Sana kwenye uchumi na fedha...unataka biashara ya ndani ifanyike kwa pesa ya nje!!?
 
  • Je hao wafanyabiashara wanakuja na Tsh toka watokako?
  • Kama hujui mambo uliza jombaa
Najua hawatoki watokako na shilingi, nataka mfumo wa ununuzi wao udhibitiwe Ili Tupate pesa za kigeni ktk mfumo ulio wazi Si huu wa gizani.
 
Wewe mtupu Sana kwenye uchumi na fedha...unataka biashara ya ndani ifanyike kwa pesa ya nje!!?
Namaanisha uwepo mfumo thabiti Si holela kama ilivyo sasa,

Bidhaa za KILIMO zinunuliwe na wafanyabiashara wageni masokoni Si shambani.

Nani ajuaye wananunua Mahindi
na mchele pekee? vp ikiwa wanasafirisha bidhaa zingine kwa kificho?
 
Namaanisha uwepo mfumo thabiti Si holela kama ilivyo sasa,

Bidhaa za KILIMO zinunuliwe na wafanyabiashara wageni masokoni Si shambani.

Nani ajuaye wananunua Mahindi
na mchele pekee? vp ikiwa wanasafirisha bidhaa zingine kwa kificho?
Mbona unahangaika!?..mwanzo umezungumzia mazao yanunuliwe kwa Dola kwa kuwa tuna upungufu wa Dola,Sasa hivi hoja nyingine..tuliza subwoofer!!
 
Ngoja mataahira yake yakwambie una nongwa na wakulima
Sidhani kama watakuwa wanakuzidi wewe na mleta mada kwa utahiri.

Maana mwenye akili hata kidogo kabisa angewe,a kutambua wanunuzi wa nje hawawezi kuingia nchini na shilingi ya Tanzania. Au mliambiwa kuwa shilingi ya Tanzania ndiyo sarafu ya Afrika nzima?
 
Najua hawatoki watokako na shilingi, nataka mfumo wa ununuzi wao udhibitiwe Ili Tupate pesa za kigeni ktk mfumo ulio wazi Si huu wa gizani.
Aliyekuambia kuwa ununuzi unafanyika kwa kificho ni nani?
 
Namaanisha uwepo mfumo thabiti Si holela kama ilivyo sasa,

Bidhaa za KILIMO zinunuliwe na wafanyabiashara wageni masokoni Si shambani.

Nani ajuaye wananunua Mahindi
na mchele pekee? vp ikiwa wanasafirisha bidhaa zingine kwa kificho?
Hizo bidhaa nyingine za kificho watakuwa wanaweka ndani ya matumbo yao? Au hujui kanuni za gari kuvuka mpaka wa nchi moja kuingia nyingine?
 
Aliyekuambia kuwa ununuzi unafanyika kwa kificho ni nani?
Kama yanayofanyika hayana ridhaa ya wananchi wengi, hiyo ni biashara ya kificho, gizani.

Unadhani wananchi tunafurahi mfumuko wa Bei za vyakula masokoni?

Ingepigwa kura ya wazi kukubali au kukataa maamuzi ya Sirikali chini ya Bashe kufanya ayafanyayo, uwe na HAKIKA wananchi tungemfuta KAZI maramoja siku hiyo hiyo.
 
Sidhani kama watakuwa wanakuzidi wewe na mleta mada kwa utahiri.

Maana mwenye akili hata kidogo kabisa angewe,a kutambua wanunuzi wa nje hawawezi kuingia nchini na shilingi ya Tanzania. Au mliambiwa kuwa shilingi ya Tanzania ndiyo sarafu ya Afrika nzima?
Umenikumbusha kauli za yule mwanasheria mkuu aliyemwita mbunge mmoja TUMBILI, lakini baada ya KASHFA Ile kuwa wazi na waziri mkubwa kujiuzulu, TUMBILI halisi alijulukana ni nani.

Ikiwa viongozi wetu Kwa mlango wa nyuma ndio wanaomiliki Kampuni hizo na kusafirisha vyakula nje ya nchi, tutazijua na kudhibiti vipi biashara hizo ikiwa wanakwenda kuficha ukwasi wao nje ya nchi?

Mara zote mtu wa kipato Cha chini Huwa Hana mtetezi.

Tusubiri.
 
Hatimaye Wizara ya KILIMO imepiga MARUFUKU WANUNUZI Kutoka nje kwenda moja Kwa moja Kwa wakulima kununua mazao ya vyakula.

Wameelekezwa kwenda kununua katika MAGHALA yaliyosajiliwa na wizara Ili kudhibiti mfumuko wa Bei,kudhibiti ulaghai na KUTUNISHA mfuko wa pesa za kigeni nchini.

Tusichoke kutenda mema,maana tutalipwa Kwa wakati wake tusipozimia Roho.

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen.
 
Waziri BASHE ungejiuzulu Ili kumpisha mwingine aje na Utaratibu mzuri wa kusimamia WANUNUZI Kutoka nje maana mwanzo uliruhusu waingie Hadi mashambani kuvuruga demand and supply chain.
 
Ni jambo jema Serikali kusikia ushauri tuliotoa.

BASHE ajitafakari ikiwa anatosha ktk nafasi hiyo.

Pia turudi ktk mjadala wa uuzwaji bandari yetu bila UKOMO, mjadala huu Bado haujaisha.

Haikubaliki kuuza bandari zote za bara, MKULIMA akitaka kuexport akapate KIBALI DP world!!!!

Haikubaliki.
 
Back
Top Bottom