Tuna akiba ya pesa dollar bilion 5.3

Ngoja tuone mwisho wake

Sioni hatua stahiki zikichukuliwa, labda tuendelee kupaza sauti, lakini sioni hatua stahiki kulingana na hali halisi. Sikatai kwamba kuna hatua lakini haziridhishi. Kuna kamati nadhani tatu kukabiliana na hili janga, lakini nguvu ya hizo kamati ni ndogo kwakweli. Unapoona waziri wa afya anasema sasa wameamua kusema ukweli, hapo ujue kuna tatizo la dhahiri la kiutendaji.
 
Sema kuwa hatoi pesa kwenye mahitaji ya watu, ila ingekuwa ni kwenye vitu angefanya hivyo. Hapa sio suala la mihemko, rais badala ya kutoa pesa vinunuliwe vifaa tiba kwa ajili ya ugonjwa unaoshika kasi, yeye anataka watu wasali ili ugonjwa uishe! Una akiba ya $5.3b kama 12t tshs, kisha una kipimo kimoja cha ugonjwa nchi nzima, unaokula maisha ya wananchi wako kisha useme hafanyi maamuzi ya mihemko! Huu sio utetezi bali ni wendawazimu.
Huna uelewa kumzidi Jiwe. Ungelikuwa na uwezo huo, ungelikuwa umeishaishauri Chadema ikajenga Ofisi ya Makao Makuu.
 
Rekebisha kauli yako. Kuna maabara moja tu ambayo ni maabara ya taifa sio kipimo.Ukisharekebisha rudi.

Chagu huwa sitolewi kwenye hoja za msingi kwa mbinu dhaifu hivyo. Kuna vipimo vingi hilo sikatai lakini ni vya kupima magonjwa kadhaa kama una dalili, ila udhibitisho kabisa wa Covid-19 huwa unapatikana kwa sample kuletwa kwenye maabara ya taifa hapa Dar. Nina uwezo wa kujua kuwa napiga ngumi nzito kiasi gani, hivyo mindgames hazinitoi mchezoni kirahisi. Ninachokisema hapa najua kinaingia kwa kiasi gani kwenye target.
 
Ok, vipimo gani ulikuwa una maanisha tindo .
 
Hiyo Akiba ndio muda wake huu kutumika, au hujui kuwa hiyo akiba ni ya kutumika kwa mazingira haya? Je kama hazitatumika sasa, hizo fedha ni akiba kwa ajili ya hali gani?
Wewe unashauri tutumie hiyo Akiba kama nani? Tindo mwenye jina la bandia khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Yaani nchi ya watu milioni 55 tuna $5B pekee hii ni aibu sana.

Aibu kwako ambaye hufahamu haya mambo huwa yanafanyika vipi, miezi 6 sio nchezo haijawahi kutokea tangu tupate tupate uhuru (nafikiri kama ilitokea ni wakati wa mwl Nyerere tena kabla ya Azimio la Arusha au baadaye kidogo). Nenda kaangalie statistics uweke hapa.
 
Ok, vipimo gani ulikuwa una maanisha tindo .

Vipimo vya Covid-19, sio lazima viwe kila mkoa, lakini wangalau vinaweza kuwa kila kanda ili kusogeza huduma karibu. Mbali ya hicho kipimo cha Covid, Ventilators Ni muhimu hasa kwenye hospitali zinazopokea wagonjwa, ni vyema sehemu zenye wagonjwa wengi zikipata upendeleo wa ziada.
 
Hili ni gonjwa jipya kabisa. Halijawahi kutokea hapa duniani. Mpaka sasa kila nchi inajipanga namna ya kukabiliana nalo. Kwa mda huu mfupi unataka kila kanda iwe na maabara? Kwa muda mfupi huu wa siku nne unataka ventilators 3000? Ukiona nchi kama Usa gonjwa linawasumbua weka siasa kando.
 
Huna uelewa kumzidi Jiwe. Ungelikuwa na uwezo huo, ungelikuwa umeishaishauri Chadema ikajenga Ofisi ya Makao Makuu.

Ni kweli sina uelewa kumzidi yeye na wala sihitaji kuanao, ila hilo halimaanishi kuwa sina uwezo wa kutambua mambo.

Mimi sio mwanachama wa cdm, bali shabiki wa kutupwa wa cdm. Ninachoweza kutoa ni ushauri wa huku huku jukwaani, na hata hivyo ushauri sio sheria, wanaweza kufuata au kuupotezea. Cdm kukosa ofisi yenye hadhi yake ni udhaifu wa wazi, na sio mara moja nimewaambia kuwa hilo linawapotezea credit, na pia nimewahi kushauri zaidi ya mara moja namna ya wao kujenga ofisi yenye hadhi yao. Hata hivyo mada hapa sio ujenzi wa ofisi vya cdm.
 
Hili ni gonjwa jipya kabisa. Halijawahi kutokea hapa duniani. Mpaka sasa kila nchi inajipanga namna ya kukabiliana nalo. Kwa mda huu mfupi unataka kila kanda iwe na maabara? Kwa muda mfupi huu wa siku nne unataka ventilators 3000? Ukiona nchi kama Usa gonjwa linawasumbua weka siasa kando.

Ukitaka kujua mtu kaishiwa hoja utaona anachomeka maneno ya weka siasa kando. Hakuna siasa kwenye hoja zangu,na hata kama zipo still niko kwenye jukwaa sahihi la mambo ya siasa. Huenda unazitazama hoja zangu kwa jicho la kisiasa, ndio maana unafikia hitimisho la kisiasa. Huu ugonjwa hauna siku 4 hapa nchini, huenda ulitaka kumaanisha kitu kingine, lakini ukakosa neno sahihi.

Sio lazima kila kanda kuwe na maabara, lakini sitaki kuamini kuwa na kipimo cha huo ugonjwa ni lazima uwe na maabara maalum. Tayari hospitali zote za kanda zina maabara, labda unidhibitishie kipimo hicho cha Covid kinahitaji maabara maalum. Jitahi unapojenga hoja zako usilazimishe kupata ushindi maana utapoteza nguvu ya hoja zako.

Chagu, angalia kichwa cha habari kinasema tuna akiba ya $5.3b, hiyo ni kama 12t tshs. Hata tukitoa tu $500m tunaweza kufanya jambo serious la kupambana na huu ugonjwa na sio kuwa na sala kwa siku tatu, au kuwa na kamati tatu zisizo na nguvu stahiki ya hili tatizo. Ninachokiona hiyo akiba aliyokuwa akisema rais kuwa na tunayo hatuna, bali alisema vile kwa ajili ya kusaka kiki ya siasa nyepesi. Ndio maana nyie watetezi wa hii serikali hamna jipya kwenye hii mada, zaidi ya kuchomekea lugha za ubabaishaji, mara sijui weka siasa kando, mara sijui mleta mada ana chuki na rais.
 
Aibu kwako ambaye hufahamu haya mambo huwa yanafanyika vipi, miezi 6 sio nchezo haijawahi kutokea tangu tupate tupate uhuru (nafikiri kama ilitokea ni wakati wa mwl Nyerere tena kabla ya Azimio la Arusha au baadaye kidogo). Nenda kaangalie statistics uweke hapa.

Haibadilishi ukweli kwamba ni pesa ndogo sana. Tumekuwa watu wa kuringia umasikini siku hizi. Yaani na rasilimali zote za Tanzania Gas, mbuga, mashamba na watu milioni 55 unataka kusifia $5B inawezekana wewe hujui hii pesa ilivyo ndogo. Corona yenyewe inaweza kuchukuwa hata mwaka. Kuna mambo mengi hayajawahi kutokea Tanzania kwasababu ya viongozi wabaya lakini hii bado ni ndogo sana
 
Mkuu hebu nitajie nchi 10 tu, katika Afrika ambazo zinaweza kuwa na akiba ya miezi sita? Then tulinganishe. (NB: Ondoa nchi ambazo zinauza mafuta). BTW niliomba statistics mbona hujaleta au ndio ule ubishi wa kakakuona?
 
Tunapoteza muda kubishania umasikini. Kama nchi yetu inatumia $10B kwa mwaka mzima ni maaikini sana Mungu atusaidie 🙏
 
Kweli aisee. Kuna post nyingine ukisoma aibu unaona wewe msomaji. Hiyo akiba kwetu huwekwa katika dollars na huwa na lengo la kuukimu uchumi kuagiza bidhaa nje ambazo ni lazima kulipa kwa pesa hizo za kigeni.

Hivyo hao ndugu watoa maoni kuwa hazina itumike wakati huu ambapo hatujui hata mwelekeo halisi wa tatizo hili, ndio wale ambao huendaga shule kusomea ujinga.

Wanaposikia Marekani inatoa $tr. 2 kuutibu uchumi wao wanadhani na sisi pia tuna uwezo huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ususahau kua sisi ni donor country, nchi tajiri, uwezo huo tunao. Tutoe pesa kuokoa uchumi. Pesa ipo ya kuendesha nchi mkezi 6 ya dharula.
 
Back
Top Bottom