Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,502
- 16,712
Mnamo Mei 9 mwaka huu 2010 mwenyekiti wa CHADEMA bwana Freeman Mbowe alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Wasso huko Ngorongoro alimtaka raisi Jakaya Mrisho Kikwete ajiuzulu na kuondoka Ikulu mara moja. Kisa kushindwa kuwalipa wafanyakazi kiwango cha chini cha sh.315,000!
Kila siku za uchaguzi zinavyokaribia yaonesha watanzania wanazidi kukosa heshima kwa raisi wao. Kumfukuza rais aliyechaguliwa namna hii pia ni kuwakosea heshima mamilioni ya watanzania waliomchagua.
Sababu za kushindwa kuwalipa wafanyakazi kima cha chini Kikwete alizieleza na nyinyi mwawajua wanaofilisi uchumi wa nchi, mbona makucha yenu hamjayakunjua kiasi hicho kwao.
Rais wetu akicheka mwanuna na akinuna kwenu ni nongwa. Nyinyii!