Liwagu
JF-Expert Member
- Jan 25, 2017
- 5,289
- 6,339
Mwenye masikio naasikie.Zitto kama ana vidhibiti vya kuchezewa rafu anaweza kwenda mahakamani.
Kabla hujaandamana jiulize;
1. Je, lengo lako ni kupindua serikali iliyoko madarakani? Kama ndio, je uko tayari kupambana na vyombo vilivyowekwa kisheria kuilinda serikali isipinduliwe? Je, uko tayari kukabiliana na kesi ya uhaini?
2. Nini unategemea kitatokea baada ya hayo maandamano? Kama ni uchaguzi mpya, je nani ataitisha huo uchaguzi na kwa mujibu wa sheria ipi? Kama ni tume mpya, je nani ataiunda na kwa kutumia sheria gani?
3. Je, una uhakika watu wote wanaokuja kuandamana wana lengo lilelile unalofikiria wewe kichwani? Hakuna mtu anayetaka kutumia maandamano hayo kufanya uhalifu? Iwapo watakuwepo wahalifu, je uko tayari kuwa sehemu ya watakaochukuliwa hatua ya uhalifu?