Tumeumia, lakini chonde chonde tusiandamane...

Kama unatoka kwenda kwenye maandamano ya amani unajidanganya. Ukweli ni unaenda vitani, umejiandaa? Wenzako wamejiandaa na silaa zote za kivita.
 
Siku Lisu alipotua nchini kulikuwa na tishio la Serikali kuwa ole wao watakaoandamana. Maelfu walijitokeza, waliandamana. Hakuna cha taarifa wala kibali cha Polisi. Serikali/polisi waliwafanya nini?

Pamoja na ukatili wa serikali hii, hawana ubavu wa kuzuia maandamano kwa sababu jamii ya kimataifa ipo na wananchi. Na wanajua ninj kitatokea kama wakiwaua au kuwajeruhi wananchi.

Tuache woga, tuandamane kwa maelfu. Na tayari wamekwishaonywa ole wao wapige mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Una familia ako inakutegemea ,acha ujinga
 
Lolote unalofanya hapa duniani lina pande mbili positive na Negative,Ukitaka kuandamana andamana tu wala usijiulize, sana, ila jikumbushe swala moja tu je kwani wao wataishi miaka 200? Mkapa kawaua wapemba wengi 2001 Leo hii yuko wapi?2/11/2020 na kuendelea

Kuandamana ni haki ya raia. Hii ni haki yetu wala hatudanganyiki. Twendeni, wakitaka watukamate wote. Twendeni, wakitaka wakatuuwe wote waone kama wao watabakia salama.

Nyomi+ ina suluhu ya ubazazi huu.

Tusipangiane wala kulazimishana. Tusizuiane wala kushurutishana kwenye haki zetu.

Vitisho vyao vime boomer!

Tunaotaka kuandamana hiyo ni haki yetu. Maandamano yatabaki kuwa ya amani na hatutakubali kuzuiwa.

Nitakuwapo Tahrir square inshallah.

Cc: Athumani Mambosasa.
 
Hhahahahaha maafisa vipenyo wako makini sana kuyavuruga maan doggedamano

Eti wanajifanya nao wamechukizwa mno na wizi wa uchaguzi. Hahaaa haa.

"They should tell that to the birds!"

Hatudanganyiki!
 
Yaani uandamane kwaajili ya watu wachache waliokatizwa mrija wa ruzuku??

Kwa taarifa yenu zipo ripoti zinazodai mwenyekiti wa chama kimoja cha upinzani anayetakatisha fedha za ruzuku kwa matumizi yake binafsi.
 
Kuandamana ni haki ya raia. Hii ni haki yetu wala hatudanganyiki. Twendeni wakati shule wote. Twendeni wakatuuwe wote waone kama wao watabakia salama.

Nyomi+ ina suluhu ya ubazazi huu.

Tusipangiane wala kulazimishana. Tusizuiane wala kushurutishana kwenye haki zetu.

Vitisho vyao vime boomer!

Tunaotaka kuandamana hiyo ni haki yetu. Maandamano yatabaki kuwa ya amani na hatutakubali kuzuiwa.

Nitakuwapo Tahrir square inshallah.

Cc: Athumani Mambosasa.

 
nawaza ..........
hapa yani fundi ujenzi ameacha kazi zake site yuko barabarani na kono bao lake na kobiro anataka uchaguzi urudiwe uchaguzi urudiwe...

Wauza maduka wamefunga maduka wako barabarani wameandamana uchaguzi urudiwe.....

mama. ntilie wameacha kupika na kuuza chakula walishe na familia zao wapo barabarani kuandamana uchaguzi urudiwe uchaguzi urudiwe....

wanavyuo hawaendi kuhudhuria lecture class wapo kwenye maandamano
Ati uchaguzi urudiwe uchaguzi urudiwe haki haki....

me niache kufanya kazi zangu kujishughulisha kupambana kwa ajili ya familia yangu kisa mboeee,,lishuu, mude sijui,,Act , chedema kisa hawajashinda uchaguzi haaa haaa weee hiyo haipo wakapambane wenyewe huko. kwani ikija lizuku tunagawanaga sote

Mwanasiasa sikiliza mimi siyo mtaji wako. pambana na hustle zako never kutuhusisha na mambo zenu huko mnapokulaga zile M12, M200 mnakumbukaga kurudishaga fadhila kwa wananchi walio waweka madarakani .?

nikadhurike wakati wewe unapambana kutimiza ndoto zako za saa 72 kuwa waziri mkuu wakati unajua na mimi na ndoto zangu za saa 24 kuwa baba Bora kwa familia yangu.

kesho Jumatatu ni siku ya kazi wananchi tutaenda kufanya kazi na nyie muingie barabarani kufanya kazi kwa ajili ya kulisaka tonge mlilopoteza .





Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Zitto kama ana vidhibiti vya kuchezewa rafu anaweza kwenda mahakamani.

Kabla hujaandamana jiulize;

1. Je, lengo lako ni kupindua serikali iliyoko madarakani? Kama ndio, je uko tayari kupambana na vyombo vilivyowekwa kisheria kuilinda serikali isipinduliwe? Je, uko tayari kukabiliana na kesi ya uhaini?

2. Nini unategemea kitatokea baada ya hayo maandamano? Kama ni uchaguzi mpya, je nani ataitisha huo uchaguzi na kwa mujibu wa sheria ipi? Kama ni tume mpya, je nani ataiunda na kwa kutumia sheria gani?

3. Je, una uhakika watu wote wanaokuja kuandamana wana lengo lilelile unalofikiria wewe kichwani? Hakuna mtu anayetaka kutumia maandamano hayo kufanya uhalifu? Iwapo watakuwepo wahalifu, je uko tayari kuwa sehemu ya watakaochukuliwa hatua ya uhalifu?
Hiyo namba 3 mkuu si umeona washenzi wengi tu humu Jf wanajinadi kwamba watabeba vidumu vya petrol na viberiti, hapo unategemea wenye dhamana ya kulinda nchi na wananchi wake watawaacha hao majuha
 
Watanzania wanaoishi Ughaibuni wameshaanza maandamano yasiyo na ukomo
 
Maandamano yasiyo na ukomo uwezo huo watanzania hawana, kwanza watakula wapi, nani atawaletea chakula? Vinginevyo itawezekana kama kuna mtu anagharamia maandamano hayo
 
Hatimaye uchaguzi mkuu wa 2020 umekamilika na kutuletea matokeo ya kushangaza. Sio siri kuwa uchaguzi haukuwa huru, haukuwa wa haki wala haukuwa wa wazi. Ushahidi wa uhalifu uliofanywa dhidi ya demokrasia ulikuwa mwingi na kila mahali. Hakika, watu wengi wameumizwa kwa yaliyofanyika.

Baada ya kutangazwa matokeo, viongozi wa vyama vya upinzani, hususan Chadema na ACT, walijitokeza hadharani kutangaza kutoyatambua matokeo. Hili ni jambo sahihi kwani hamna namna unaweza kuukubali uchafuzi ule uliobatizwa jina la uchaguzi.

Shida ipo katika hatua zilizotangazwa za kupambana na udhalimu na ujambazi uliofanyika dhidi ya demokrasia.

Vyama vya upinzani vimetangaza maandamano yaisyo na ukomo yatakayoanza kesho Jumatatu Novemba 2.

Tujiulize maswali mawili: Kwanza: je maandamano ni muhimu? Pili: Je maandamano yanawezekana na yataleta tija inayotegemewa katika muktadha wa Tanzania?

Nikianza na swali la kwanza, hakika maandamano ni muhimu, tena ni muhimu sana. Maandamao ni moja ya njia muhimu za kujieleza katika siasa za kidemokrasia, haki ambayo inatajwa hata kwenye katiba ya nchi (rejea uhuru wa kujieleza na kutoa maoni).

Kwa hiyo, katika hali ya kawaida, ilikuwa ni muhimu kuandamana kuelezea kutoridhishwa na uchafuzi wa uchaguzi uliofanyika.

Hata hivyo, kuhusu swali la pili, kwamba, je maandamano yanawezekana na je yataleta tija? Jibu, bila shaka, ni hapana. Nina hoja tatu za msingi za kuamini maandamano hayataleta tija.

Hoja ya kwanza ni ukatili wa vyombo vya dola utakaopelekea watu wengi kuumizwa, iwapo watajitokeza. Uzoefu wa Zanzibar na maandamano yaliyowahi kuitishwa huko nyuma dhidi ya utawala wa awamu ya tano, yakiwemo yale ya UKUTA na yale ya Mange Kimambi, unaonesha kuwa hii ni serikali ya kikatili isiyojali kabisa utu na haki za binadamu.

Katika utawala wa serikali ya awamu hii, uhai wa binadamu hauna thamani hata kidogo. Watakuua na hawatajali. Kwa nini viongozi wa upinzani muwapeleke watu kwenye kifo hali mnaelewa kiwango cha ukatili wa serikali hii?

Tuseme, watu wameandamana na baadhi kadhaa wamekamatwa na kuwekwa ndani. Je, vyama hivi vilivyoitisha maandamano vina uwezo wa kwenda kuwatoa ndani kwa kuwawekea dhamana au itakuwa kila mtu na lwake? Naelewa kiuhakika kabisa kuwa wengi kati ya watakaojitokeza (kama kweli watajitokeza) ni vijana wadogo, maskini ambao huenda familia zao hazina mbele wala nyuma na zinawategemea katika kutafuta riziki. Je mmewafikiria hao wategemezi?

Ukweli ni kuwa, kuna idadi kubwa ya Watanzania wasioridhishwa na ukandamizaji wa demokrasia., lakini changamoto za kimaisha wanazokabiliana nazo ni kubwa mno kuwafanya wajali. Hivyo, ni wazi kuwa, watakaojitokeza kwa maandamano ni watu wachache sana, jambo ambalo litarahisha kazi ya vyombo vya dola ya kuwashughulikia.

Na baada ya kushughulikiwa kikatili, naamini vijana hao hawatarudia tena kuandamana. Jambo hili likitokea litaipa serikali dhalimu ya CCM ushindi wa kisaikolojia. Watasema na kutangaza duniani kote, ‘Aagh ni wakorofi wachache tu waliokuwa wakileta ukorofi.’

Ndugu viongozi wa upinzani kutoka vyama vya ACT na Chadema, jaribuni kuwalelewa watu mnaowaongoza, na tafadhalini msiwapitishe katika njia wasiyoimudu kwani wafuasi huenda wakaamua kuacha hata kuunga mkono mapambano ya kidemokrasia. Kuwafanya watu waandamane hivi sasa ni sawa na kukamua jipu lisiloiva.

Nini kifanyike? Mambo mawili ni muhimu sana. Kwanza, vyama viendelee kupaza sauti za kupinga uchafuzi wa demokrasia uliofanyika kwa kutumia vyombo mbalimbali ili kunyanyua uelewa miongoni mwa wananchi na hivyo kupata uungwaji mkono. Hoja isiwe chama kipi ni mahiri zaidi katika kuleta maendeleo bali ulinzi wa demokrasia yetu.

Pili, viongozi wa upinzani na wanaharakati wengine wajaribu kushawishi jamii ya kimataifa kwanza kutotambua uchaguzi na matokeo yake na kisha kuibana serikali ya Magufuli irudie uchaguzi baada ya kufanya mabadiliko ya kisheria yanayokandamiza demokrasia.

Kwa kumalizia, ni vyema kwa vyama vya upinzani kujitathmini. Baada ya kufanyiwa dhulma walizofanyiwa, Je nini wanaweza kufanya ili vyama hivi viendelee kuheshimika na kukubalika mbele za wananchi?
 
Maandamano yasiyo na ukomo uwezo huo watanzania hawana, kwanza watakula wapi, nani atawaletea chakula? Vinginevyo itawezekana kama kuna mtu anagharamia maandamano hayo
 
Hahaha kwani maandamano yanaanzia wapi na kuishia wapi, na nini theme ya maandamano?!
 
Back
Top Bottom