Tume ya Warioba kutafuna bil. 40/-

Tume ya Warioba kutafuna bil. 40/-

Data zako ni sahihi kabisa.Hawa jamaa wamenunuliwa na Freemasons ili waingize ujinga wao kama ushoga kwenye katiba.Nawashanga akina Mvungi, Warioba ,Butiku na Baregu kukubaliana na ufisadi unaofanywa na tume,huku wao ndio waliokuwa wanajifanya Makomandoo dhidi ya vita ya ufisadi.Ndugu zetu poleni sana,kumbe ilikuwa njaa tu. tayari.
Source muandaaji wa malipo.

Jamani watu wanapopewa madaraka katika serikali yetu huwa kuna kamsemo "KAULA" sasa ndo nazidi kupata picha ya kauli hiyo.

Je ni watanzania wangapi wanaweza kuamini kuwa wajumbe wa kamati ya katiba wanalipwa sh. 300,000/= kwa siku katika shughuri zao toka waapishwe?

Najua sio rahisi kuamini lakini ndo ukweli wa mambo.

Na mtoa taarifa kadai kwanza tume hii haikuwa kwenye bajeti na imechangia kukwamisha baadhi ya miradi na huduma kwa jamii kwa sababu lazima walipwe na watimiziwe wanayotaka.

My concern;
Sasa kama wanafunzi wanakosa mikopo na wafanyakazi wanakosa mishahara kwa wakati kwa manufaa ya wachache tunaenda wapi????
 
Manake kwa miezi 18 kila mtu atalamba 162,000,000tshs
Maana yake kama wako 20 jumla ni 3.2mil
Kweli Tz sio maskini kabisa na wahisani komaeni ela za misaada ziende moja kwa moja kwenye miradi
 
Possibly CCM hawana imani na hii tume na sasa wanaanza kuipunguzia umaarufu kabla haijaanza kazi kwa ama kuvujisha siri za malipo na matumizi ya rasilimali ama kuzusha mambo.

Binafsi sioni sababu za kulaumu kama malipo hayo ni kwa siku watakazokuwa site (Vijijini na mijini kwenye mazingira tofauti na risks tofauti) wakifanya kazi, yaani chakula na malazi ila wanapokuwa ofisini wanalipwa mshahara wao tu. Tofauti na wabunge ambao wao wanajulikana makazi yao maalum ni dodoma hivyo mtu anaweza kupanga nyumba kwa mwaka mzima na kuwa anafikia wakati wa vikao

Ila pia sioni tatizo kama malipo haya hayatawafanya wajione wanatakiwa kulipa fadhila kwa chama fulani ambacho serikali yake ndiyo imeidhinisha malipo haya.
 
Kwa kweli Mungu wa Majeshi aingilie kati juu ya suala hili, kwani hata wale niliwaona kuwa ni waaminifu kumbe walikuwa hawajapata nafasi tu ya kuitafuna Hazina yetu ambayo hivi sasa ni nyeupeeeeeeee!!!!!! Najiuliza hivi zile barabara zinazojengwa kwa kutumia fedha za ndani kwa asilimia 100 zitakamilika kweli ama hata kujengwa? Au ndio zimeishia hapo hapo. Tuwe wakweli na sio wanafiki kupiga kelele na huku tukipewa ulaji tunatulia kimyaaaaaaaaaaa!! Ama kweli.

Mtumishi wa Mungu wa Eliya
 
What is the big deal, they deserve the payment. Mbona hamhoji malipo ya vikao bungeni?.
 
Tume sio kazi, hao jamaa wana majukumu mbali mbali ambayo wanayaacha kwenda kwenye hivyo vikao. Na pia mkumbuke kwamba hiyo tume sio ajira , hao jamaa hawakutani kila siku! Pengine mara 4 kwa mwezi.
 
Nafikiri hata hivyo wanapunjwa. Inategemeana wanalipwa kama nini. Kama ni allowance basi ni ya kawaida, lakini kama wanaichukulia kazi yao kama consultancy, basi hiyo hela haitoshi kwa siku. Na sidhani kama wanalipwa laki tatu wakati wowote. Lazima itakuwa ni laki tatu wanapokuwa kwenye shughuli fulani particularly nje ya ofisi. Kisheria kama ni consultancy basi wanatakiwa walipwe dola 350 kwa siku. Piga hesabu wangepaswa kulipwa bei gani kwa hela ya madafu! Nadhani its just fair.
 
unashangaa nini lazima ujue kuwa hiyo ni specific assignment associated with high risk.hii kazi ndugu ni ya hatari na ndiyo maana wamewekewa hadi walinzi.leo ukiajiriwa na un ukapelekwa darful dau lake si mchezo sababu ni mazingira hatarishi.
Labda nikukumbushe tume ya chacha wangwe ya kukusanya maoni ya kujiunga ea kwa tanaznia walilipwa tzs.600,000.

Acha porojo subiri watutengenezee katiba ya kuja kumshitakia kikwete fastaaaaa


kwa nini hii tume nayo isiwe ni kazi ya wito kama madaktari na walimu? Yana mwisho
 
Tusipokuwa makini JF itakuwa kijiwe cha porojo wewe usipende kuokota maneno mitaani unaleta JF, unasema wanalipwa 300,000 kwa siku ni posho tu hiyo bado mshahara wanalipwa kiasi gan?

Usipende tu kulaumu na kulalama kama hupendi hapa jf pawe mahali pa porojo basi njoo na takwimu zako kuonyesha wanalipwa kiasi gani kama posho, mishahara n.k ili kuzipinga takwimu zilizotolewa zaidi ya hapo na wewe ni mpiga porojo tu mwingine!
 
Tume sio kazi, hao jamaa wana majukumu mbali mbali ambayo wanayaacha kwenda kwenye hivyo vikao. Na pia mkumbuke kwamba hiyo tume sio ajira , hao jamaa hawakutani kila siku! Pengine mara 4 kwa mwezi.

wewe unajua unachoongea au unashabikia tu! kama tume itakutana mara 4 kwa mwezi itatumia miaka mingapi kuzunguka Tanzania nzima yenye takriban kilometa za mraba milion moja na idadi ya watu karibu milioni 42? think before you write anything here!
 
Mkuu ulikiwa hujui kwamba kuingia kwenye Tume ama Kamati yoyote ni deal? Laki tatu kwa siku kwa miezi 18, nyumba ya serikali na gari lenye dereva na mafuta; deal or no deal?

Wabunge nao naona sasa watapata nguvu ya kudai nyongeza ya posho zao.

kwani umeambiwa posho yao haikuongezwa?
 
Tuache maskhara,je nafasi za kazi zimeisha?mimi nataka hata kufagia pale.mwenye kujua amwage hapa tuone cv zetu kama zinaweza kutusaidia kuuaga umasikini.
 
Heshima mbele mkuu,
nakubaliana na weye 100%

Hujaelewa ni kwa nini mpaka leo Ezekiel Maige analalama kwamba ameonewa? je Mwakyembe hukuona alivyotoka India haraka haraka kabla hata hajamaliza matibabu ili asitemwe Uwaziri na akawashushuwa viherehere wote waliokuwa wanashabikia kwamba kawekewa sumu?
 
UFAFANUZI WANGU KWA JAMBO ILI.
Malipo ya posho kwenye tume maalum kama hizi kiwango chake kiko wazi kabisa kwa mujibu wa WARAKA WA UTUMISHI WA UMMA .Mwenyekiti na Katibu wanalipwa kiwango sawa na wajumbe wanalipwa pungufu kidogo na Sekretariati wanalipwa pungufu kidogo pia.Kwa mfano Kamati za Zabuni Mwenyekiti na Katibu wake wanalipwa kati ya 150,000-450,000 per sitting kulingana na hadhi ya Taasisi.Pia Tume maalum kama hii ya Katiba Mwenyekiti , Katibu na wajumbe wake wanalipwa posho na siyo mishahara ,hivyo uwezekano wa kulipwa fedha hizo kiasi cha 300,000/- au zaidi ni mkubwa na wala hakuna ubishi wowote.
Tukubali wajumbe watafanya kazi kwa maslahi ya watanzania, na gharama katika demokrasia haiepukiki.Tatizo lililopo ni kuwa tulianza vibaya kwa muundo kutekwa na chama cha mafisadi na pengine tungekuwa na wajumbe wachache na sekretariati ndogo yenye kutumia gharama kidogo.
 
Mie nilishangaa kumuona Mwenyekiti, Jaji Warioba akikubrief siku moja kuwa wameajiri watumishi 71 lakini hata sikumoja sijawahi kuona tangazo la kazi ya ajira ya tume ya katiba katika vyombo vya Habari.Je wameajiri kwa kutumia utaratibu gani kupata watumishi hao?.Wasjie wakawa wameajiri watumishi kutoka wahite house dodoma au Lumumba ofisi ndogo ya chama
 
Ni katika kasma namba 8 ambapo kila mjumbe atalipwa posho ya Tshs 450,000/= kwa siku au tshs mil. 294 hadi julai 2013.

Mwenyekiti na makamu wake wana pia fungu la takrima. Watanunuliwa magari 56 kwa bil. 10/=, na wafanyakazi wasio wajumbe wametengewa bil. 4.3/= kama posho ya kujikimu.

Chanzo: Nipashe
 
Sijaelewa Mkuu,Hebu fafanua japo kidogo maana wengi Habari kama hivi zinatumipa tukiwa tumefumba Macho.
 
Back
Top Bottom