Tume ya Warioba kutafuna bil. 40/-

Tume ya Warioba kutafuna bil. 40/-

hao wajumbe wanaandaliwa kifikra ili kui-favor magamba, hakuna uwiano wa malipo na uhalisia wa maisha ya mtanzania na kazi wanayokwenda kuifanya..
 
Labda kama wengi wa tunaotumia jf tu watu wa daraja ya chini sana. Lakini vinginevyo haiwezi kuingia akilini kufikiria kwamba eti warioba (ex-pm), salim (ex- oau), jaji augustino (ex-chief justice), prof. Baregu, butiku (ex-chief secr) etc wanaweza kuandika kwa kuchakachua katiba eti tu kwa sababu ya posho ya hata kama ni sh. 500,000/ ( si dola ni za tz). Tuache uchovu wa kufikiri na tusifikiri hayo maisha ya hovyo hovyo tuliyomo ndiyo kila mtu anatakiwa ayaishimo. Hawo wazee wataichakachua katiba labda kwa matakwa yao mengine, ama ya ki-ccm au kwa fikira zao zitakavyowatuma. Kumbukeni tume hiyo ndiyo itakayoandika katiba. Mawazo mengine yote toka kwa wananchi au kwa yeyote awaye yatafanyiwa interpretation na tume na itayaweka inavyoona tume.
 
kwani pesa hizo zinatofauti na zile za msafara wa father house,wapewe tu bila kujali watatulete nini
 
Ole wao watukusanyie maoni yasiyo na mashiko na hatimaye tupate Katiba mbovu: hizo bilion 40 watazirudisha watake wasitake.
 
Big up wachumi daraja la kwanza - 'ceteris paribus' the more the marupurupu the better the katiba.
 
Japo demokrasia ni gharama...... Ila gharama hii ya kuelekea demokrasia haikai kichwani kabisa!
 
afu mnasema hii nchi haina hela....ndo maana madaktari wanagoma wala siwalaumu, infact ningeshauri nchi nzima tugome
 
Eti sh 300,000/= kwa siku ni pesa ya kawaida; ila kima cha chini cha sh315,000/= kwa MWEZI ni pesa nyingi.

Hadi inachefua yaani!
Na output yenyewe itakavyokuwa imechakachuliwa!
 
Hapa sasa nimeelewe maana ya kauli hii ya waziri wa zamani wa sheria "Serikali haina hela ya kuandaa katiba mpya"! Kipindi kile sikuelewa alimaanisha nini.
 
fikiria SALIM A. SALIM hana makazi DAR, na anatakiwa afanye kazi ya umma akiwa Dar, wakati huo huo atatakiwa asifanye kazi nyingine yoyote kwa ajili yake na familia yake zaidi ya ile ya tume. pendekeza alipwe kiasi gani? kwa kazi (msalaba) wanayotakiwa kuifanya, hiyo posho ya sh. 300000/= wala si chochote kwa vigezo vyote. pamoja na kwamba mgawanyo wa raslimali zetu haufanywi kwa haki kwa raia wake lakini si kweli vilevile kwamba inatakiwa igawiwe sawasawa (lazima itegemee na uzito wake). kazi inayofanywa na akina warioba si kila mtu anaweza kuifanya. kazi maalumu kwa watu maalumu kwa malipo maalumu. kama katika tume hiyo kuna na watu wa hovyo hovyo basi hiyo ni juu ya aliyewateua. ndiyo maana watu kama kofi anan yuko kila pahala duniani kushughulika na kutatua migogoro. kwani akina ali hassan mwinyi hawapo? mbona hawaendi huko? Ni kazi maalumu kwa watu maalum, na malipo yake lazima yawe maalumu. ni kazi inayoinvolve brain na risk zote. tuwaacheni wachape kazi.

Nadhani ndugu yangu umejisahau kuwa tunawaongelea watanzania wenzetu. Katiba itawahusu hata wao. Hiyo pesa wanayolipwa c sahihi kwa uchumi wetu. We unafikiri wanaofanya kazi ngumu ni wao peke yao!?
Ualimu, udaktari, na nyingine nyingi, zote ni kazi maalum. So, usihalalishe malipo hayo kwa kuita kazi yao ni maalumu. Hakuna kazi isiyohusisha brain and risk.
 
Unajua kuwa wajumbe wa kamati ya katiba wanalipwa sh. 450,000= kwa siku na wamenunuliwa magari 60?
Kwa mwaka kila mjumbe kuvuna zaidi ya milioni 300/-

Wasio wajumbe yaani watumishi kutumia bilioni 4.3/-[JFMP3][/JFMP3]
 
Madaktari na walimu waendeleo kusota tu!haivumiliki hata kidogo hii
 
Mimi nadhani ni sawa tu hasa ukichukulia kazi yao ni nzito sana na itakuwa ya kihistoria
 
Si mchezo, mpaka huu mchakato ukiisha, wakina Kagwair ni mabilionea, kweli aliyekuwa nacho anaongezewa.:A S confused:
 
Back
Top Bottom