Tume ya Warioba kutafuna bil. 40/-

Is it the fact au ni maneno ya kusikia sikia tu? Kuna tofauti kati ya haya mambo mawili.
 
Asante mkuu watu ohh tunamwombea mpambanaji apone arudi haraka kwenye mapambano yako wapi sasa hawa watu hawana tofauti
Hujaelewa ni kwa nini mpaka leo Ezekiel Maige analalama kwamba ameonewa? je Mwakyembe hukuona alivyotoka India haraka haraka kabla hata hajamaliza matibabu ili asitemwe Uwaziri na akawashushuwa viherehere wote waliokuwa wanashabikia kwamba kawekewa sumu?
 
si kwa nini wanalipwa 300,000...................Kujua kwa nini wanalipwa 300,000 ndio jambo la msingi

Tukipata gharama zilisababisha kufikia kiwango hicho itasaidia mjadala.

kama chanzo chako ni mtu anayewalipa anaweza kukusaidia kueleza mchanganuo wa malipo hayo hadi kufikia 300,000.
 
Mimi nadhani malipo haya ni halali kabisa, na hata malipo ya wafanyakazi yalipaswa kuzingatia vigezo walivyotumia kuilipa tume.Kumbukeni kwamba hawa watu wamekubali kuacha kwa muda majukumu yao binafsi ya kila siku, kwa mamana nyingine shughukli zao au makampuni yao yatapungukiwa na ufanisi kwa wao kutokuwepo ktk usimamizi.
Kwa hiyo lazima wewe uliyewateua bila wao kuomba u-compansate loss that they going to encounter a loss of their business income due to their absence.
 
Si mnataka katiba mpya sasa mnalalamika nini? Kombani aliwaambia hatuwezi kuandika katiba mpya sababu ni ghalama kubwa, mkamuona mpumbavu..
 
Mimi nadhani malipo haya ni halali kabisa, na hata malipo ya wafanyakazi yalipaswa kuzingatia vigezo walivyotumia kuilipa tume.Kumbukeni kwamba hawa watu wamekubali kuacha kwa muda majukumu yao binafsi ya kila siku, kwa mamana nyingine shughukli zao au makampuni yao yatapungukiwa na ufanisi kwa wao kutokuwepo ktk usimamizi.
Kwa hiyo lazima wewe uliyewateua bila wao kuomba u-compansate loss that they going to encounter a loss of their business income due to their absence.
Si kweli!
Wengi wao ni waajiriwa wa taasisi za serikali ukiacha wastaafu wachache!...na kawaida ukiwa kwenye ofisi ya serikali, ni dhamana tu, na si kwamba wewe usipokuwepo kuna kazi zitasimama kabisa, haitakiwi kuwa hivyo!
Labda nitakuelewa kwa habari ya familia, kuwa zitawakosa.
 
Hayo ni matumizi mabaya sana ya pesa. Yaani mtu alipwe 300,000/= per day kwa kazi gani???

Huu ni uonevu sana, kuna watu wangapi wanapata shida huku mtaaani jamani. Loo nimekoma kuwa Mtanzania na ninayefahamu haki zangu. Kila kukicha kuna vituko vinaibuka hapa bongo unashindwa hata kuamini ukweli wa hayo mambo. Nfikiri mshahara huo ni hongo ya kuleta Katiba mbaya....(without prejudice).
 
Mzee wetu Butiko kulalama kutapungua sasa. Mwenyekiti Warioba yeye ni laki nne mbali na pensheni yake nzito ya 80% ya mshahara wa Makamu wa Rais kila mwezi. Hofu yangu mimi ni kama unalipwa namna hii kama vile UNAHONGWA unabaki HURU kweli? Sio kwamba anayekulipa ndie anachagua wimbo? Mzee Warioba na wenzako mna uchungu na hali ilivyo kwa WATANZANIA walio wengi? Cabinet mpya Ufaransa juzi wameamua kupunguza mishahara yao kwa 1/3.
 
Mkitaka kujuwa pesa ni sabuni ya roho zile kelele za kina Butiku sasa zimeshapata tiba ya kudumu hutowasikia tena na zile kelele zao kama mnavyomuona Mwakyembe naye alivyoridhika na maisha bila kujali anakufa taratibu.

Kwa siyejuwa vizuri hapa namaanisha nini muangaliaeni kwa makini sasa hivi Maalim Seif Sharif Hamad hata ile sigida yake imefutika haionekani tena. inshort amenawiri.
 
ww mtoa mada acha kuwadanganya watu wenye akili zao,apo kwenye 300,000 mi sjui lakini Wamenunuliwa magari 60 sio kweli,we sema una yako ya kunyimwa boom, jipange upya apo tunekushtukia.

hilo la magari mpya nililiskia ila nimesahau takwimu,lakini watanunuliwa magari mapya mdau,tena ilitangazwa kwenye media like ITV
 
Mzee wetu Butiko kulalama kutapungua sasa. Mwenyekiti Warioba yeye ni laki nne mbali na pensheni yake nzito ya 80% ya mshahara wa Makamu wa Rais kila mwezi. Hofu yangu mimi ni kama unalipwa namna hii kama vile UNAHONGWA unabaki HURU kweli? Sio kwamba anayekulipa ndie anachagua wimbo? Mzee Warioba na wenzako mna uchungu na hali ilivyo kwa WATANZANIA walio wengi? Cabinet mpya Ufaransa juzi wameamua kupunguza mishahara yao kwa 1/3.
Hii ni kashfa nyingine. Warioba, Salim na Augustino Said wanalipwa pensheni ya viongozi wakuu wastaafu. Ifuatiliwe tujue kama nao wanapokea posho hizi ili tuwaanike majukwaani jinsi wanavyotuibia. Si haki kuwatendea wananchi hivi hata kama sheria inaruhusu wakati vyouni wanachuo wanaambiwa serikali haina pesa ya mkopo. Nimemsoma juzi Maige alivyoandika kuwa kajiwekea hazina Mbinguni nikashangaa ni Mbingu gani anayoiongelea.
 
ww mtoa mada acha kuwadanganya watu wenye akili zao,apo kwenye 300,000 mi sjui lakini Wamenunuliwa magari 60 sio kweli,we sema una yako ya kunyimwa boom, jipange upya apo tunekushtukia.

Kama ni uongo ukweli ni upi?,mwenzio anajenga wewe unabomoa!!!
 
Source muandaaji wa malipo.

Jamani watu wanapopewa madaraka katika serikali yetu huwa kuna kamsemo "KAULA" sasa ndo nazidi kupata picha ya kauli hiyo.

Je ni watanzania wangapi wanaweza kuamini kuwa wajumbe wa kamati ya katiba wanalipwa sh. 300,000/= kwa siku katika shughuri zao toka waapishwe?

Najua sio rahisi kuamini lakini ndo ukweli wa mambo.

Na mtoa taarifa kadai kwanza tume hii haikuwa kwenye bajeti na imechangia kukwamisha baadhi ya miradi na huduma kwa jamii kwa sababu lazima walipwe na watimiziwe wanayotaka.

My concern;
Sasa kama wanafunzi wanakosa mikopo na wafanyakazi wanakosa mishahara kwa wakati kwa manufaa ya wachache tunaenda wapi????

Halafu tunajiuliza kwa nini Tanzania ni masikini!!!?
 
mtu mwenye busara na mwenye kupenda ukweli na kuchukia uongo na majungu, angetuwekea source ama exhibit/ ushahidi wa kuthibitisha taarifa hizi. Mtu yeyote anaweza kukurupuka na kusema anachofikiria. Kama tukifanya tu kienyeji haina maana, na Great Thinkers maana yake ni nini????
 
Ni pesa ya kawaida sana jumla watalipwa billion4.8 tu yaani kila mtu M162 kwa kipindi chote hicho cha miezi 18. (300,000*30*18=162,000,000) (162,000,000*30=4,860,000,000). Yataka uzalendo wa kweli mtu kuacha kazi zako zoooote kwa miezi18 ili ukaingize MILIONI162
 
Hii ni kashfa nyingine. Warioba, Salim na Augustino Said wanalipwa pensheni ya viongozi wakuu wastaafu. Ifuatiliwe tujue kama nao wanapokea posho hizi ili tuwaanike majukwaani jinsi wanavyotuibia. Si haki kuwatendea wananchi hivi hata kama sheria inaruhusu wakati vyouni wanachuo wanaambiwa serikali haina pesa ya mkopo. Nimemsoma juzi Maige alivyoandika kuwa kajiwekea hazina Mbinguni nikashangaa ni Mbingu gani anayoiongelea.
Ukiwafuatilia watakwambia hii ni posho sio mshahara! JMK alikuwa anakerwa mno na kelele za wazee hawa. Amewanyamazisha permanently. Amewapa kazi ambayo kwa umri wao haikupaswa kuwa yao. Katiba mpya itamsaidia nini Warioba, SAS, Butiko na Agustino Ramadhani ambao wameshavuka 70?
 
Back
Top Bottom