Ni kweli kiasi hiki ni kikubwa mno. Lakini, ifikie mahali tukubali kuwa gharama ni lazima kwa mambo fulani fulani. Kwa mtu ambaye ametoka nje ya Dar na hana mshahara wowote na kwa upande mwingine anafamilia, kiasi hiki ni kikubwa lakini sio kikubwa sana. Lazima tukubali kuwa usifike wakati mjumbe mmoja akajiuzulu kwa sababu tu, nachokipata katika tume hii hakilingani na mapato yake nje ya tume. Watu walioteuliwa ni watu ambao ni waadalifu kwa kiwango kikubwa, ni weledi waliotukuka na wana hadhi inayowafanya wasiwe omba omba. Nawashauri watanzania wenzagu tukuikubali gharama hii kwa kazi muhimu.