Tume ya Warioba kutafuna bil. 40/-

Tume ya Warioba kutafuna bil. 40/-

Nilisema hapa siku moja baadhi ya wachangiaji wakasema ni umbea

Kweli mkuu ulishawahi kuleta huu uzi mie pia nilikupinga lakini leo nimeona kwenye vyombo vya habari nimeudhunika sana...big up mkuu.
 
Hivi tume imejaa, au bado inahitaji watu? Nataka kuomba kujiunga nayo!
 
Wizi Mtupu. Hiyo pesa si ingetupa ajira na Mishaara vijana tuliomaliza Vyuo..katiba mpya itakuwa na Utumbo ule ule.
 
JAMANIII TUENDELEE KUKAA KIMYA NI UPEPO TUUUUUUUUUUU UTAPITAAAAAAAAAAAAAA:eyebrows:
 
wakati mwingine ni masikitiko makubwa kuwa mtanzania!!!
hivi kweli 450 per day inasaidia nini katika kuongeza ubora wa katiba??
sikatai wao kulipwa vizuri lakini sop kwa kiwango hicho.nigeelewa kama pesa nyingi zingetumika kuhakikisha watu wengi wanafikiwa ili watoe maoni hayo.
kwa mtazamo wangu,hii ni kujipendekeza kwa nyinyiemu ili tume ifanye kazi kwa mwongozo wao ili waedelee kutuibia.kwa malipo hayo na posho nyingine,wanatume watalewa tu,najua mawazo ya magamba yalivyo na strategy za kijinga.
ila kiukweli inasikitisha sana maana tunafanya mabo kama sio nchi vile,na ndiyo maana ukiongelea tanzani ni kama taifa moja lenye vitaifa vidogo ndani yake,matajiri na maskini.ukuangalia shule zetu zipo za aina mbili,huduma za afya,yaani sijui ni nini kinachotuunganisha kati yetu.
MUNGU ATUOKOE MIKONONI MWA WANYANG'ANYI HAWA.
 
Tume nyingi za Rais wanalipana posho hiyo nakumbuka hata ile ya EPA walikamata 450,000 kwa siku!
 
Source muandaaji wa malipo.

Jamani watu wanapopewa madaraka katika serikali yetu huwa kuna kamsemo "KAULA" sasa ndo nazidi kupata picha ya kauli hiyo.

Je ni watanzania wangapi wanaweza kuamini kuwa wajumbe wa kamati ya katiba wanalipwa sh. 300,000/= kwa siku katika shughuri zao toka waapishwe?

Najua sio rahisi kuamini lakini ndo ukweli wa mambo.

Na mtoa taarifa kadai kwanza tume hii haikuwa kwenye bajeti na imechangia kukwamisha baadhi ya miradi na huduma kwa jamii kwa sababu lazima walipwe na watimiziwe wanayotaka.

My concern;
Sasa kama wanafunzi wanakosa mikopo na wafanyakazi wanakosa mishahara kwa wakati kwa manufaa ya wachache tunaenda wapi????

Ongezea pia wamepangishiwa zile apartment karibu na ikulu kwa mwezi$2500x30x36 na imelipwa cash!
 
Ndiyo maana madokta wameamka kutaka usawa lakin majority ya watanzania hawajielewi! .all the best DOCTORS STRIKE
 
Ebu soma gazeti la nipashe ya leo usikie mamboooooo

ww mtoa mada acha kuwadanganya watu wenye akili zao,apo kwenye 300,000 mi sjui lakini Wamenunuliwa magari 60 sio kweli,we sema una yako ya kunyimwa boom, jipange upya apo tunekushtukia.
 
kwani wabunge wanalipwa kiasi gani si 200000/= kwa siku kama walivyokuwa wakidai. wapi wanakazi ngumu kwa sasa wabunge au wajumbe wa katiba. by the way hao ni presidential appointment na kama tulivyokariri et pred app lazima walipwe pesa nyingi, kweli maskini anajua namna ya kujiongezea umaskini
 
Vizuri gharama bwana. Tunahitaji katiba kwa gharama yoyote. Nahisi hivi ni vijisenti pia.
 
Hizi tetesi zinatokana na mfumo wetu wa serikali kutokuwa na uwazi. Mi nadhani malipo na marupurupu ya hii tume yangewekwa wazi.
Nakataa kuiminisha nafsi yangu kama kweli wanalipwa TZS 300,000 kwa siku. Haingii akilini hata kidogo. Kwanza hizo hela za kila siku wanalipwa kwa majukumu gani? Ina maana hawana mshahara wa mwezi?

1. Magari wamekusanya toka mifuko ya hifadhi ya jamii na madereva wake. Wachangiaji PPF, PSPF nk ndio wanaolipia gharama hizi za usafiri.

2. Tshs 300, 000 ni pale wakiwa nje ya Dar.
 
fikiria SALIM A. SALIM hana makazi DAR, na anatakiwa afanye kazi ya umma akiwa Dar, wakati huo huo atatakiwa asifanye kazi nyingine yoyote kwa ajili yake na familia yake zaidi ya ile ya tume. pendekeza alipwe kiasi gani? kwa kazi (msalaba) wanayotakiwa kuifanya, hiyo posho ya sh. 300000/= wala si chochote kwa vigezo vyote. pamoja na kwamba mgawanyo wa raslimali zetu haufanywi kwa haki kwa raia wake lakini si kweli vilevile kwamba inatakiwa igawiwe sawasawa (lazima itegemee na uzito wake). kazi inayofanywa na akina warioba si kila mtu anaweza kuifanya. kazi maalumu kwa watu maalumu kwa malipo maalumu. kama katika tume hiyo kuna na watu wa hovyo hovyo basi hiyo ni juu ya aliyewateua. ndiyo maana watu kama kofi anan yuko kila pahala duniani kushughulika na kutatua migogoro. kwani akina ali hassan mwinyi hawapo? mbona hawaendi huko? Ni kazi maalumu kwa watu maalum, na malipo yake lazima yawe maalumu. ni kazi inayoinvolve brain na risk zote. tuwaacheni wachape kazi.
 
Back
Top Bottom