Tume ya Warioba kutafuna bil. 40/-

Tume ya Warioba kutafuna bil. 40/-

Mimi nadhani ni sawa tu hasa ukichukulia kazi yao ni nzito sana na itakuwa ya kihistoria
Wakati wazee wetu wanapigania uhuru walilipwa sh ngapi kwa siku? Tuendelee tu kuigharamia SIASA halafu kila mtu anajidai kushangaa kwa nini bajeti ya maendeleo ni ndogo!
 
Wakati wazee wetu wanapigania uhuru walilipwa sh ngapi kwa siku? Tuendelee tu kuigharamia SIASA halafu kila mtu anajidai kushangaa kwa nini bajeti ya maendeleo ni ndogo!

Wakati wazee wanapigania Uhuru walikuwa hawana resources za kuwawezesha, hivyo wangelipana kutoka wapi? Ni kweli wali-deserve kulipwa vizuri dailly hata Dola1000 ishu ni kwamba kulikuwa hakuna pesa, tukitaka kila kitu tukifanye kwa kuangalia wazee wetu walifanya nini tutaanza kuvaa ngozi za ng'ombe ili tusitofautiane nao sana
 
Kwa nini kukusanya maoni tena kutoka kwa wasiojua KATIBA ni nini itugharimu namna hii? Kwamba wanaounda tume hii wana akili sana? Tunaogopa watahongwa? Na nani? 450,000/= kwa siku kwa MTANZANIA wa kawaida kama Mzee wetu Waryoba ni nini hasa! Katiba yenyewe itaandikwa basi?
 
Unajua kuwa wajumbe wa kamati ya katiba wanalipwa sh. 450,000= kwa siku na wamenunuliwa magari 60?
Kwa mwaka kila mjumbe kuvuna zaidi ya milioni 300/-

Wasio wajumbe yaani watumishi kutumia bilioni 4.3/-

Hapa lazima kuna siri iliyofichwa kwenye mabano. Lazima kuna kitu kinapikwa na hawa jamaa si bure.

Kuna Mbunge alihoji Bungeni kwamba SERIKALI INA SIRI GANI KUTENGA MABILIONI YOTE HAYO kwa kamati hii ya Marekebisho ya Katiba?Je, ni hongo,rushwa,bakshishi au takrima????

Hili swali ni la msingi sana. Inavyoonekana ni kwamba SERIKALI INATAKA HII KAMATI ICHAKACHUE MUUNDO WA KATIBA MPYA. KWAMBA KAMATI HII ITAKUWA IMEPEWA MAELEKEZO MAALUMU TOKA CHAMA TWAWALA NA LAZIMA IYAINGIZE KWENYE KATIBA HIYO MPYA KWA KISINGIZIO CHA KUWA WANANCHI NDIWO WALIOTAKA!!

Hapa utakuwa ni ushwetani mtupu!

Jamani hata kama tunaihitaji katiba mpya malipo hayo ni makubwa sana. Tena ni allowance kwa siku. Jamani tunaipeleka wapi nchi hii? Busara gani ilitumika kupanga kiasi hicho kikubwa yaani 450,000 kwa siku moja kwa mtu mmoja? Kwa kweli tumerogwa na aliyeturoga kafa!
Unajua kuwa wajumbe wa kamati ya katiba wanalipwa sh. 450,000= kwa siku na wamenunuliwa magari 60?
Kwa mwaka kila mjumbe kuvuna zaidi ya milioni 300/-

Wasio wajumbe yaani watumishi kutumia bilioni 4.3/-
 
si nyingi tena kusema kweli ni kidogo, ni dola 300 tu kwa siku. Kazi yenyewe ni ngumu sana halafu magari strong ni lazima. Kwa watu walowahi kuzungukia nchi hii wanaelewa maana ya kupewa magari.

Kwa kweli mchakato huu ungefanywa kwa njia tofauti mbadala, gharama zingepungua. Lakini hakuna aliyetoa mawazo mchakato huu ufwanyweje hivyo hamna sababu ya kulalamika au siyo Pasco?
 
sina tatizo na malipo hayo kwani hata mchanganuo wake siujui. maswali ninayojiuliza ni kama timu hii iliyopewa kazi adhimu ya kukusanya maoni ya uundwaji wa katiba mpya inaendelea kula mishahara ya utumishi katika maeneo yao ya kazi hasa ukizingatia kuwa wengi ni waajiriwa wa umma.
 
Back
Top Bottom