Tume ya Warioba kutafuna bil. 40/-

Ni pesa ya kawaida sana jumla watalipwa billion4.8 tu yaani kila mtu M162 kwa kipindi chote hicho cha miezi 18. (300,000*30*18=162,000,000) (162,000,000*30=4,860,000,000). Yataka uzalendo wa kweli mtu kuacha kazi zako zoooote kwa miezi18 ili ukaingize MILIONI162
Halafu hazikatwi kodi! Tuendelee tu kugharamia SIASA kama mazuzu huku shule zetu zikiwa hoi, zahanati hazina hata panado, mahakama za mwanzo zikiwa mbavu za mbwa na WATANZANIA wakinunua kilo ya unga kwa zaidi sh 1000 sasa.
 
Si mnataka katiba mpya sasa mnalalamika nini? Kombani aliwaambia hatuwezi kuandika katiba mpya sababu ni ghalama kubwa, mkamuona mpumbavu..

Na wewe sasa unaongea nini?ni bora ungekaa kimya.
 
Ni pesa ya kawaida sana jumla watalipwa billion4.8 tu yaani kila mtu M162 kwa kipindi chote hicho cha miezi 18. (300,000*30*18=162,000,000) (162,000,000*30=4,860,000,000). Yataka uzalendo wa kweli mtu kuacha kazi zako zoooote kwa miezi18 ili ukaingize MILIONI162

Huu ni ufisadi wa wazi wazi kabisa kama ni kweli wanalipwa laki 3 kwa siku,hawa viongozi huwa hawafikirii?
 
Source muandaaji wa malipo.

Jamani watu wanapopewa madaraka katika serikali yetu huwa kuna kamsemo "KAULA" sasa ndo nazidi kupata picha ya kauli hiyo.

Je ni watanzania wangapi wanaweza kuamini kuwa wajumbe wa kamati ya katiba wanalipwa sh. 300,000/= kwa siku katika shughuri zao toka waapishwe?

Najua sio rahisi kuamini lakini ndo ukweli wa mambo.

Na mtoa taarifa kadai kwanza tume hii haikuwa kwenye bajeti na imechangia kukwamisha baadhi ya miradi na huduma kwa jamii kwa sababu lazima walipwe na watimiziwe wanayotaka.

My concern;
Sasa kama wanafunzi wanakosa mikopo na wafanyakazi wanakosa mishahara kwa wakati kwa manufaa ya wachache tunaenda wapi????
Ni kweli kiasi hiki ni kikubwa mno. Lakini, ifikie mahali tukubali kuwa gharama ni lazima kwa mambo fulani fulani. Kwa mtu ambaye ametoka nje ya Dar na hana mshahara wowote na kwa upande mwingine anafamilia, kiasi hiki ni kikubwa lakini sio kikubwa sana. Lazima tukubali kuwa usifike wakati mjumbe mmoja akajiuzulu kwa sababu tu, nachokipata katika tume hii hakilingani na mapato yake nje ya tume. Watu walioteuliwa ni watu ambao ni waadalifu kwa kiwango kikubwa, ni weledi waliotukuka na wana hadhi inayowafanya wasiwe omba omba. Nawashauri watanzania wenzagu tukuikubali gharama hii kwa kazi muhimu.
 
Only in Tanzania ambako mtu anaweza kubisha kitu asichokijuwa!!.....interesting.
hahahahahaaa..........
Unabisha usichokijua..........yani unakuwa kama NAPE.........anasema asiyoyajua, na anakomaa nayo, kumbe kaambiwa aseme.....hajui hata yana maana gani na kwa nini yasmwe hivyo
 
Mpaka wanaingia katika ofisi zao walikuwa wameshatumia Bilioni 5!

SOSI; Mathias Chikawe!
 
kama watafanya kaziyao kwauhakika na ukweri poa nigharakuwanakatiba mpya kuliko kuwa na iliyopo na kumbukanigharama maradufu kubakinailiyopo sasa
 
Dosama hii taarifa yako iongezee nyama kidogo ili iaminike!
Kwasasa sitatoa comment yeyote.
 
Kama hivyo mbona ni kidogo sana? hata dollar 200 kwa siku haifiki. Mie kama malipo ni hayo ningejitowa kwenye kamati, kazi zangu zinaniingizia zaidi ya hizo kwa saa 1.
 
Ni kweli kiasi hiki ni kikubwa mno. Lakini, ifikie mahali tukubali kuwa gharama ni lazima kwa mambo fulani fulani. Kwa mtu ambaye ametoka nje ya Dar na hana mshahara wowote na kwa upande mwingine anafamilia, kiasi hiki ni kikubwa lakini sio kikubwa sana. Lazima tukubali kuwa usifike wakati mjumbe mmoja akajiuzulu kwa sababu tu, nachokipata katika tume hii hakilingani na mapato yake nje ya tume. Watu walioteuliwa ni watu ambao ni waadalifu kwa kiwango kikubwa, ni weledi waliotukuka na wana hadhi inayowafanya wasiwe omba omba. Nawashauri watanzania wenzagu tukuikubali gharama hii kwa kazi muhimu.
Kama kweli wana sifa hizi na mapenzi makubwa kwa nchi yao na WATANZANIA masikini wangekataa kiwango hiki cha posho. Shida kubwa tuliyonayo WATANZANIA ni kila mtu nafsi yake kwanza. Kweli kuratibu maoni ya katiba mpya kunatugharimu kiasi hiki? Tuchukue tu ile katiba ya jirani zetu Kenya tu-copy na ku-paste na ku-replace neno Kenya na Tanzania. Katiba ile ni nzuri sana kwa kiwango kikubwa.
 
Kama hivyo mbona ni kidogo sana? hata dollar 200 kwa siku haifiki. Mie kama malipo ni hayo ningejitowa kwenye kamati, kazi zangu zinaniingizia zaidi ya hizo kwa saa 1.
Wakati Ulaya na Marekani kuna akina Lionel Messi, Kristiano Ronaldo, Bill Gates, Yaya Toure, Kobe Bryant, Beyonce,...., wanalipwa kwa vipaji na ubunifu wao, hapa kwetu WANASIASA na SIASA wanajilipa sana kodi zetu. Yana mwisho haya. JMK ameamua kutuchafulia wale ambao tulidhani ni WAZALENDO, WAFIA NCHI.
 
Pesa ndogo sana kwa wajumbe, ingawa itaonekana nyingi kwa wenye njaa. Kuna wajumbe wana uwezo wa kuzalisha kiasi hicho kwa masaa matatu tu! Kumbuka hawaendi na sufuria kama "Wabunge wa Pemba".
 
source muandaaji wa malipo.

Jamani watu wanapopewa madaraka katika serikali yetu huwa kuna kamsemo "kaula" sasa ndo nazidi kupata picha ya kauli hiyo.

Je ni watanzania wangapi wanaweza kuamini kuwa wajumbe wa kamati ya katiba wanalipwa sh. 300,000/= kwa siku katika shughuri zao toka waapishwe?

Najua sio rahisi kuamini lakini ndo ukweli wa mambo.

Na mtoa taarifa kadai kwanza tume hii haikuwa kwenye bajeti na imechangia kukwamisha baadhi ya miradi na huduma kwa jamii kwa sababu lazima walipwe na watimiziwe wanayotaka.

My concern;
sasa kama wanafunzi wanakosa mikopo na wafanyakazi wanakosa mishahara kwa wakati kwa manufaa ya wachache tunaenda wapi????

katiba is priceless.....hakuna gharama halisi ambayo utasema inatosha kwa katiba......katiba ni maisha yetu ....nadhani hata maisha hayana bei...!!!
Juhudi yeyote ya kutaka kufanya shilingi 300,000 [dola 140] wanayolipwa hawa wajumbe kwa siku ionekane suala la kuongelea ...naiona kama wivu wa kawaida kabisa .......what is 300,000 ...???? Tuacheni wivu ...waacheni wafanye kazi............au ulizeni majirani zetu kenya walitumia shilingi ngapi kuunda katiba ....?? Katiba ina gharama???
 
The end justifies the means. Kwa jinsi tunavyohitaji katiba ya watu kwa ajili ya watu, nitakubali hata walipwe 500,000 kwa siku. Ili mradi tu wafanye kazi kwa niaba ya walipa kodi.
 
ww mtoa mada acha kuwadanganya watu wenye akili zao,apo kwenye 300,000 mi sjui lakini Wamenunuliwa magari 60 sio kweli,we sema una yako ya kunyimwa boom, jipange upya apo tunekushtukia.
wametofautina mtu mwisho ambae ni dereva anapewa laki moja per day....wengine mpk 450000.....acha ubishi kama hujui kaa kimya
 
Makubwa ila sishangai kwa tz maana nchi hii tukoutumwani mwa ccm kujinasua nikuituma kuzimu na ukoloni wake hata fulana, kofia khanga, ubwabwa ndio chanzo cha haya yote.
 
Tusipokuwa makini JF itakuwa kijiwe cha porojo wewe usipende kuokota maneno mitaani unaleta JF, unasema wanalipwa 300,000 kwa siku ni posho tu hiyo bado mshahara wanalipwa kiasi gan?
Wewe kama huamini hiyo,
basi tutajie wewe wanalipwa ngapi!!
 
Kama hivyo mbona ni kidogo sana? hata dollar 200 kwa siku haifiki. Mie kama malipo ni hayo ningejitowa kwenye kamati, kazi zangu zinaniingizia zaidi ya hizo kwa saa 1.

Kazi gani hizo mkuu? Zile za uongozi wa wilayani? Maana huko watu wanatafuna bwana
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom