Dr Matola PhD
Platinum Member
- Oct 18, 2010
- 61,430
- 108,589
Nakubaliana na wewe sana tu labda pengine sisi tujiulize kama tume hii ni huru ama laa, uwezo wa kila mmoja wao kiutendaji. Maana wajumbe wa tume hii asilimia 90 ni wana CCM na katiba tunayoitaka sii ya kukilinda chama kimoja, siasa ya Ujamaa na kujitegemea au utawala wake tena, bali kulinda muungano ktk Utaifa wetu.
Pili, swala la wajumbe wa Zanzibar na bara pengine lingezungumziwa uwezo wa watu hawa 17 toka bara kuweza kuifanya kazi kwa ufanisi sawa na Zanzibar ikiwa wajumbe wa Zanzibar wana asimilia ndogo ya kukusanya mawazo yao tofauti na bara ambako wananchi ni wengi sana kupita kiasi. Hivyo kinachotazamwa ni kuwawezesha hawa wajumbe waifanye kazi yao kwa ufanisi maana namba za population hazifanani.. Hayo tu ndio hoja yangu kubwa kuhusiana na tume hii..
Mkuu kwenye hoja yako ya kwanza sina wasi wasi sana na idadi ya wana CCM maana baadhi yao na hasa Mwnyekiti Warioba ni majeruhi wa siasa za Makundi na hasa mtandao wa JK uliomuundia zengwe Salim asiwe Rais wetu nadhani nao wamepata rungu la kumalizia hasira zao siyo kwa kufanya upendeleo bali kwa kutenda haki, sina wasi wasi sana na hili.
Hoja yako ya pili nadhani Kamati ya Chadema inayofanya uchambuzi wake ndiyo itakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuliongelea hili nina uhakika wanalifahamu vyema na hata Tundu Lisu alishawahi kuliongea hili Bungeni akaonekana kama adui wa Wanzanzibar.