Tume ya mabadiliko ya katiba

Katuletee tahmin zaid tujue wakatoliki wangapi?,waanglikana wangapi?,Ansaar wangapi na Bakwata wangapi ili tuchambue zaidi maana naona huna muda wa kujadili elimu ya wajumbe,uzalendo wao,uzoefu wao ukimaliza pitia kujua wachaga,wahaya,wahehe,waha wapo? Ukimaliza ulizia chadema,CUF na CCM wapo? Sie tutaendelea kujadili hadidu za rejea,integrity yao,sifa zao n.k!

Sengoro mbona unamjibu VIBAYA MUASISI wetu? hayo ni maoni yake jamani na tunashukuru ametoa kilicho moyoni mwake.
 
Kama aliyoanzisha thread hii ni Edwin Mtei aliekuwa gavana wa BoT na Mwanzilishi wa CHADEMA, basi we have a serious problem.
 
Mzee Mtei, siamini kama ni wewe ndio umeandika hii thread au mjukuu wako anatumia ID yako..

Zanzibar ni nchi kamili sio sehemu ya Tanganyika halafu umenisikitisha kuonyesha udini wako kwenye hiyo orodha.

Ebu toa maoni yako ulikuwa unataka hiyo tume iwe na muundo gani kuliko kukosoa tu.
Udogo wa Zanzibar haiwakoseshi haki ya kuwa nchi kamili.

Zanzibar ni sehemu ndogo sana ya Tanzania.
 
Udini lazima uonekane sasa..kwa sababu umeletwa. Mtu kichwa nazi hana hoja kaishia kuleta udini. Sasa waukemee, mbona wapo kimia? Udini sasa upo na watu wanahoji, msiwabane sana kwa sababu wanaongea kitu kilichopo na kilicholetwa nchini kwetu.

Udini ni hatari, lakini sasa hivi ni mbinu ya wakubwa kupata kuchaguliwa. Hivyo hautokuja ondoka udini hadi hapo utakapotekeleza madhara yake..

Sisi tunaolalamika kwenye keyboards hatuwezi kuondowa udini. Tukitaka udini utoweke sharti huyo aliyeuleta afanye yafuatayo..
(1) aukemee kwa nguvu zote
(2) matendo yake yafanane na maneno yake..
(3) Sisi tukimwangalia usoni tuone ile seriousness ya maneno yake

bila kufanya hivyo, udini upo na hautoki. Waacheni watu waangalie majina ya dini, wahesabu composition za kamati, walalamike hadi jambo litokee..

safi sana. tusingetaka udini tusingezipokea hizo dini in the first place.
aneyedai tusizungumzie dini ni mnafiki.
dini zipo na zina wafuasi wengi kuliko vyama vya siasa mnataka ziwe elephants in the room?
 
Babu Mtei Kateleza aisee.......mbaya zaidi yeye ni mmoja wa CDM Founders.......it leaves a lot to be desired........duuhh
 
Mzee amechemka, hata kama wangekuwa wameteuliwa watu wa kundi moja wote,iwe kidini,kisiasa, kikabila n.k.
Kazi ya tume siyo kuunda katiba mpya bali ni kuratibu ukusanyaji wa maoni. Bunge la katiba ndiyo muhimu zaidi.
 
"yeyote anaeangalia tume ya katiba kwa misingi ya dini za wajumbe amefilisika kimawazo,ni kirusi dhidi ya utanzania wetu azomewe" ZITTO KABWE(2012). Safi sana zitto waelimishe hao wadini hasa huyo Mzee mtei.
 
Siamini kama mtei alikuwa Governor wa BOT inawezekana hata katika kutoa vyeo alizingatia dini na kabila ndio maana na Mbowe akafanya kazi BOT wakati elimu yake mashaka makubwa!!!!

Mzee Mtei ilikuwaje ukamtia mbowe BOT na ulimpa kazi gani karani?
 
huyu mzee ni mdini sana,na hiki chama alichokiasisi kimelalamikiwa sana kukumbatia udini.Mungu sasa anatudhihirishia waliokuwa wanayaficha na kuyapinga mbele ya watanzania
 
Mzee Mtei,

Heshima Kwako. Kwanza kabisa mimi nakuunga mkono asilimia zote na kiukweli Tume hii imebeba Wazanzibari wengi kuliko watanzania bara ile hali katiba inayobadilishwa ni ya Tanzania Bara... Sidhani kama zanzibar wana matatizo zaidi ya tunayopata sisi.

Nilchokiona hapa ni dhamira ya kuwa Katiba mpya haipo kwa hawa CCM lasivyo kuna malengo ya Mtu fulani au upande fula yanataka kutimizwa kupitia tume hii...

Hivi ina maana watu wote tanzania Bara wakihiji jambo fulani liwepo kwenye katiba mpya maana yake ni hadi ridhaa ya watu 1.5mil siyo..

Hii haikubaliki na hata kama ni kwa gharama ya kuvunjika kwa muungano.

Mimi ni Raia wa Kawaida na sioni nachofaidika na muungano zaidi ya wanasiasa.. Watanzania Bara tusiogope na tuwe na Moyo. Kwa sasa nachokiona kwa CCM nikuhakikisha wanatimiza kila kinachotakiwa kwenye ule muungano
'
MIMI NINGESHAURI KAMA INAWEZEKANA WATUMIE ILE RATIO YA WABUNGE WA BARA NA ZANZIBAR KWENYE BUNGE LA MUUNGANO KATIKA TUME HII, NA KATIKA MAAMUZI KUHUSU MAMBO YA BARA WAAMUE WANAOTOKA BARA NA ISSUE ZA Z'BAR WAAMUE WA KULE.

Hii tume utafikiri tuna idadi sawa ya eneo na watu. Zaidi mimi naona itafika mahali tutakuwa na 50% kwa kila kitu bila kujali nini.

WANASIASA WOTE WAKONGWE WALIOTUMIKIA NCHI WAKATI WA utawala wa NYERERE NA AWAMU YAKE YA KWANZA HAWAFAI KABISAA KUWEMO KTK TUME HII. hawa watu kama kina waroba, Dk salimu, butiku na jaji ramadhani wote hawatatupatia haki katika kumnya,ng'anya nguvu za utawala raisi wa nchi. kulifanya bunge, mahakama kuu na executive branch ziwe na nguvu sawa hawa wanasiasa wakongwe hawawezi kabisaa kupinda nguvu za raisi.

Ikifikia muungano, hapao ndipo hawataweza kabisaa kufanya lolote la maana kama kuwa na raisi mmoja, waziri mkuu mmoja na mwanasheria mkuu mmoja. hawa wote wamelowea kumuabudu nyerere na kuona kila alilolitenda ni zuri kupita kiasi.

sasa tume ya uchaguzi kweli itakuwa huru? nchi badi inatembea ktk njia ya ujamaa na kujitegemea? haya hayatabadilika kama hawa wansiasa wakongwe wakiwemo ktk tume hii ya katiba.

we are investing in fever the desease will be the profit in 2015 general election!!!
 
In the interest of fairness I think all the major stakeholders of this review should have been consulted on the composition of the panel. To dispel any doubts of bias and build confidence throughout this process.

Chadema being the initiators of this process should have been consulted to create a level playing field for all
 
Muasis wa CHADEMA mzee MTEI,amesema kuwa tume ya katiba iliyoundwa hivi karibu na JK imejaa waislam wengi!

SOSI: JAMBOLEO
 
haituzuii kupata katiba mpya. ninachoona wazenji ni wengi wakati wanawakilisha watu wachache. anyway, tunajua kama haitakuwa nzuri, CDM tutatengeneza nyingine ndani ya mda mfupi itakayokuwa ya watanzania wengi
 
Back
Top Bottom