Asante lakini hapo kwenye Sakramenti si muumini analipia mfano wakati wa kuandikisha mafundisho si huwa kuna malipo muumini analipia kabla ya kuanza mbona unasema ni bure?Kwenye Kanisa Katoliki kuna taasisi za aina 3
1. Religious, hizi ni huduma za kidini, kiroho na kiimani, kama ibada ya misa, sacrament, maombezi, na huduma zote za kiimani, ubatizo, komunio, kitubio, kipaimara, ndoa, mpako wa mwisho, upadirisho, mazishishi, huduma hizi ni bure.
2. Charity, hizi ni huduma za kusaidia jamii kwa Kanisa kujitolea sehemu na jamii kuchangia sehemu ya gharama!, huduma hizi ni kama afya kwenye mahospitali ya mission na elimu kwenye mashule na vyuo vya kanisa ambazo gharama hizo ni not for profit, sio kuzalisha faida.
3. Uzalishaji mali na kufanya biashara, kanisa Katoliki pia lina huduma za uzalishaji mali na kufanya biashara, hizi ni business as usual kama Cathedra Bookshops, kukodisha maeneo, kama Msimbazi centre au pale Magomeni, mahoteli, hostels, viwanda, etc, ni biashara kama biashara nyingine.
Tumaini Media, does both, inatoa huduma za uinjilishaji bure, huduma hizi zinagharimiwa na michango ya waumini, kama Marafiki wa Tumaini Media, hivyo vipindi vyote vya dini ni bure, news pia ni bure. Ila pia Tumaini Media inafanya biashara kwa kupokea vipindi vya nje vinavyolipiwa, kampuni yangu ya PPR inapeleka vipindi na tunalipa vinarushwa kibiashara, japo bei zap ni bei poa.
P