Tuliyoyasema: Mabilioni ya NSSF et al ya "uwekezaji" hayalipiki!! - Ripoti ya CAG yafichua

Leo nimegundua kwa nini NSSF wako bega wa bega na CCM, wanajua ili waendelee kufaidi huu mfumo fisadi ni lazima waibebe ccm inayolinda na kuhamasisha ufisadi. Kuna kipindi nchi ilizongwa na mgogoro wa umeme wakaandamana na Ngeleja kudai watafunga mtambo wa kuzalisha umeme wa dharura kumbe ni ghilba kwa watanzania wasizidi kuichukia ccm. Kiama chao chaja 2015
 
Nilishawahi kuzungumzia hii kitu inatisha sana, serikali ikifulia tu inakimbilia kwenye Pensheni.

1. Kuinasua TBC serikali ishasema inazungumza na mifuko ya pensheni ipate billioni 14, wakati TBC yenyewe haina vyanzo vyovyote vya mapato kuweza kulipa deni.

2. HESLB (Bodi ya mikopo) Serikali imechukua pesa nyingi za pensheni na vijana hawarudishi hadi sasa hali tete, juzi juzi tu PSPF wamechomoa kuiongezea pesa HESLB. Tatizo unakuta katibu mkuu wa Hazina yupo kwenye kwenye hizi bodi sasa hapo kuna mgongano yaani serikali ikikopa kama inajikopesha yenyewe maana sisi wadau tunaochangia uwakilishi wetu kwenye bodi za mifuko mdogo sana kama haupo labda board member 1 tu.

3.Mabibo Hostel na NSSF hatujui kama deni limelipwa au la

4. UDOM ndio mama yangu yaani balaa tupu...

5. PSPF imelipa watumishi wa umma ambao hawajawahi hata kuchangia kwenye mfuko na serikali inadaiwa deni kubwa. Zitto kapiga kelele wee naona amechoka

Yaani hii mifuko sijui kama huwa ina wataalam wa "acturial" wa kupiga mahesabu au inaendeshwa tu kwa matakwa ya wanasiasa? Mimi nadhani matatizo ya pensheni yaliyotokea North America kwa impact ya "babyboomers" kustaafu na sisi yatatukuta maana now tupo wengi sana wa 30's and 20's tulio kwenye ajira na wote tutastaafu kipindi kimoja. Unless mabadiliko makubwa yafanywe vinginevyo ni balaa kubwa kwa sisi wastaafu wa baadae. Nawashauri kama wameshindwa kabisa hawa mifuko bora wawekeze kwenye dhamana za serikali tu.
 
QUOTE=MKeshaji;3711599

Mimi hata sielewi kwenye hii mifuko wafanyakazi wanawakilishwa na nani. Ninachoona ni kwamba hawa jamaa huwa wanafanya maamuzi "kwa niaba" ya wenye pesa zao (wafanyakazi), japo maamuzi yao mengi hayapendwi na wahusika wanaodunduliza pesa zao za kila mwezi.

Mkuu wafanyakazi ndiyo wanapashwa kuwa share holders wa NSSF, Management haipashwi kuwa na autonomy kubwa kupita kiasi, pawepo check and balance - watu wachache hawapashwi kuamua ni jinsi gani funds za walala hoi zitumiwe bila ya kupata kibali kutoka kwa members (au wawakilishi wao) wa mfuko huo hii ni hatari sana.

Nimewahi kusema mara kadhaa kuwa kunahitajika kufanyika utaratibu abao utamnufaisha mfanyakazi wakati anaendelea kutoa michango yake. Sifurahishwi na mfumo uliopo sasa ambao naona umekaa kidhurmati. Ati ukiwa umechangia michango 180 na una umri wa kustaafu miaka 55-60 basi huna budi kusubiri pensheni, ambayo kiukweli utalipwa muda mfupi sana kabla ya kufa. Sehemu kubwa ya michango inabaki kuwa "faida" kwa mfuko wa jamii.

Mimi nafikili mbinu hii ndiyo inaiwezesha kutumia funds bila kuwa na umakini wowote maanake wanajua at the end of the day - floating funds ni nyingi muno kiasi kwamba zinaweza kuziba hasara, kama wenge kuwa wamajipanga vizuri kuwasaidia wafaya kazi kwa nia nzuri wangeweka mfuko maharuma wa kuwasaidia wafanyakazi kujenga au kununua nyumba wakati wanafanya kazi na kuwawekea bima incase kunatokea matatizo kama vile: Vifo, kuacha kazi kwa gafla au kuhugua ilil mhusika/mrithi hasinyanganywe nyumba yake, misaada isihishie kwenye ku-fund matibabu tu which's peanut.

Wakati huo huo sielewi ni kwa nini mifuko hii inaona risk kumkopesha mwanachama wakati huo huo inapoteza pesa nyingi sana kuwakopesha wafanyabiashara wakubwa ambao si wanachama. Vile vile kuwekeza katika miradi ambayo haimnufaishi moja kwa moja mwanachama.

Si hilo tu, wakati mwingine hizo hela huwa azilejeshwi kabisa - mimi nashindwa kuelewa mantiki ya kumkopesha mafanya biashara ambaye siyo mwana chama, ndiyo maana nasema uendeshaji wa mashirika haya una walakini mkubwa sana ambao unapashwa kuwa-addressed the soonest, for the benefit ya wafanyakazi.Mfuko huu uonekane una nia thabiti ya kuwakomboa members wake kiuchumi siyo kunufaisha watu wengine.


Nadhani sasa ni muda muafaka kwa wanachama wa mifuko kudai haki zao ambazo zitawafanya wanufaike na michango yao sasa badala ya kusubiri "mafao ya uzeeni"

Well said mkuu, nafikili Agency iliyo anzishwa kuangalia mwenendo ya mashirika haya ita-play a +ve role kuondoa kasoro hizi za msingi.
 
Tanzania bwana mpaka tunachekesha. Hakuna tunaloweza kufanya bila kujidhuru wenyewe? Ukiona watu na tasibihi zao ndefu utadhani ibada iko kweli moyoni. Inakuwaje tunaruhusu hii dhuluma juu ya wachangiaji wa NSSF?
 
Hivi hazina na wizara ya fedha wanajua vizuri athari za kufanya mifuko hii ndo sehemu ya kupatia fedha kwa urahisi?

Kipindi mimi na wewe tunapanga foleni ya kudai pensheni tunapigwa mabomu ya machozi wao watakuwa kaburini na watoto wao wameshawaachia mazingira mazuri wanakula bata tu.
 
Kama kweli CAG Tz amesema hayo katika ripoti yake pasi na kubainisha nini kifanyike kuokoa fedha hizo atakuwa hamna kitu na amechoka kazi.

Mimi nilifikiri alitakiwa kwenda mbali zaidi kwa kuonyesha udhaifu upo wapi? katika mikataba au namna ya kuchambua michanganuo hiyo kabla kuingiza fedha au kuna ujanja gani unaotumika?.

Kama atabainisha hayo atakuwa ameliokoa NSSF.
 
Kama kweli CAG Tz amesema hayo katika ripoti yake pasi na kubainisha nini kifanyike kuokoa fedha hizo atakuwa hamna kitu na amechoka kazi.

Mimi nilifikiri alitakiwa kwenda mbali zaidi kwa kuonyesha udhaifu upo wapi? katika mikataba au namna ya kuchambua michanganuo hiyo kabla kuingiza fedha au kuna ujanja gani unaotumika?.

Kama atabainisha hayo atakuwa ameliokoa NSSF.
Mkuu karibu tena jamvini.
 
mimi ni mwanachama wa mfuko huu japo michango yangu sio kiasi kukubwa sana lakini nina uchungu nayo tena sana.

Ukweli ukiangalia mradi kama wa Kigamboni (kwa mfano) pamoja na hiyo mingine mwisho wake utakuja kuwa kama 'Machinga Complex', ni ufisadi tu japo watanzania tulio wengi huwa hatuko proactive lakini ukweli unabaki pale pale kuwa 'the end will justify the means'


nimefuatilia majadialiano bungeni wakati wa mjadala wa SSRA kila suala lililotiliwa mashaka na wabunge (ambao kweli nafikiri wasiwasi wao ni valid) ulikuwa brushed aside kuwa SSRA iko pale kuhakikisha itakwenda vizuri( wanataka tuamini SSRA ndiyo muarobaini mimi naona hiki ni kichaka kingine cha kubariki kuibiwa kwa watanzania masikini waliowekeza kwenye hii mifuko)
 
Ndio maana NSSF hawataki kuwa transparent katika kuonyesha matumizi na makusanyo yao. Mark Bomani alilalamika wiki chache zilizopita kuwa NSSF pamoja na makampuni mengine ya nje hawatoi ushirikiano katika kuonyesha mapato na matumizi ya hela wanazokusanya.
Pale ni wizi mtupu...project nyingi zinakuwa inflated kuliko gharama zake halisi zilivyo. Tusipoangalia nao watafilisika muda sio mrefu. Maana watanzania kazi yetu si kuifilisi nchi mpaka waje wawekezaji.

Mkuu NSSF Hawawezi kuwa transparent kwa sababu serikali kwa kutumia udhaifu uliopo inatumia fedha za NSSF kwa kushirikiana na Maofosa wa NSSF Kwa matumizi binafsi ,pia mabilioni ya akiba ya wafanyakazi yanatumika sivyo wakati mtumishi yaani mteja wa NSSF anahangaika kupanga foleni kudai malipo yake anajibiwa utumbo na mtumishi wa NSSF ambae ni mtoto wa kigogo,mtoto huyo huyo anauwezo wa kukopeshwa mpaka milioni mia fedha za akiba kwa liba nafuu.
Hata ajira za NSSF ni kwa watoto wa wastaafu wa NSSF tu.
 
Mifuko ya hifadhi ya jamii si mali ya wanachama. Tafadhali fuatilia sheria inayounda mifuko husika. unapoisoma utagundua kuwa mifuko hiyo ni mali ya serikali. Mifuko yote imeundwa ili kuiepusha serikali na wajibu wake wa kuihudumia jamii!. ndiyo sababu serikali ina 100% control of those funds. Kinachosemwa majukwaani kuwa mifuko ni mali ya wanachama ni gilba tu za hao wezi!!
 
nimefuatilia majadialiano bungeni wakati wa mjadala wa SSRA kila suala lililotiliwa mashaka na wabunge (ambao kweli nafikiri wasiwasi wao ni valid) ulikuwa brushed aside kuwa SSRA iko pale kuhakikisha itakwenda vizuri( wanataka tuamini SSRA ndiyo muarobaini mimi naona hiki ni kichaka kingine cha kubariki kuibiwa kwa watanzania masikini waliowekeza kwenye hii mifuko)
. SSRA hongereni. Wadau tuwape muda tusiwahukumu ni mapema sana kufika hapo tu ni MUUJIZA na tunamshukuru Mungu!.
 
Kuna baadhi yetu tumekuwa na wasiwasi sana na huu uwekezaji wa fedha za wanachama wa mifumo ya hifadhi ya jamii mkubwa kati yao ukiwa ni wa NSSF. NSSF siyo mfuko pekee lakini ndio mfuko ambao unatumiwa sana kuwekeza kwenye miradi mingi na mkataba mkubwa ambao wengi watakuwa wanaufahamu ni wa ujenzi wa daraja la KIgamboni. CAG katika ripoti yake anadokeza vitu vichache ambavyo vinapaswa kuangiliwa na wanachama na watu wote wanaofuatilia mambo haya:



My Take:
Je wanachama wa NSSF na mifuko mingine ya jamii wanapaswa kujali jinsi mifuko hii inavyowekeza?

Mwanakijiji nilipitia hii report sikuliona hili jambo,
ila ulipoliweka nikabidi nirudi kutafuta, naona kama presha imepanda maana nimechangia NSSF kwa miaka mingi!
 
Kwa mliowahi kufikia na kutembelea UDOM ni kweli value for money inaonekana; kwamba UDOM imegharimu/inagharimu karibu bilioni 400!? hasa baada ya taarifa kuwa baadhi ya majengo tayari yalishaanza kuvuja na kuwa na nyufa?
 
Kwa mliowahi kufikia na kutembelea UDOM ni kweli value for money inaonekana; kwamba UDOM imegharimu/inagharimu karibu bilioni 400!? hasa baada ya taarifa kuwa baadhi ya majengo tayari yalishaanza kuvuja na kuwa na nyufa?
Je wanachama wa mifuko ya pensheni wamejiangaisha kujua kuhusu gawio kutoka Azania Bank?
inavyoonekana sio kuwa Watanzania tumelala na kuhitaji kuamshwa bali 'tumekufa' na kilichopo ni uhitaji wa 'kufufuliwa'!

Nasema hivi kwa sababu kama ingelikuwa usingizi muda wa kusinzia umeshaisha ikiwa ni pamoja na kelele nyingi zilizopigwa zingeliweza kutuamsha.

Siamini kama binadamu aliye 'hai' anaweza kuchangia pesa kutoka kwenye mshahara/kipato chake halali halafu akashindwa kufuatilia pesa yake inaenda wapi ikiwa ni pamoja na kuhoji! Usishangae kusikia watu walioliona hili ndio wanabakia kusema kuwa hii nchi ni Mungu tu wa kuinusuru ...kwa vile wanajua ndiye ana uwezo wa 'kufufua'


 
Back
Top Bottom