Tuliyoyasema: Mabilioni ya NSSF et al ya "uwekezaji" hayalipiki!! - Ripoti ya CAG yafichua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuliyoyasema: Mabilioni ya NSSF et al ya "uwekezaji" hayalipiki!! - Ripoti ya CAG yafichua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 17, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna baadhi yetu tumekuwa na wasiwasi sana na huu uwekezaji wa fedha za wanachama wa mifumo ya hifadhi ya jamii mkubwa kati yao ukiwa ni wa NSSF. NSSF siyo mfuko pekee lakini ndio mfuko ambao unatumiwa sana kuwekeza kwenye miradi mingi na mkataba mkubwa ambao wengi watakuwa wanaufahamu ni wa ujenzi wa daraja la KIgamboni. CAG katika ripoti yake anadokeza vitu vichache ambavyo vinapaswa kuangiliwa na wanachama na watu wote wanaofuatilia mambo haya:

  My Take:
  Je wanachama wa NSSF na mifuko mingine ya jamii wanapaswa kujali jinsi mifuko hii inavyowekeza?
   
 2. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Sijui watanzania tutaacha lini kuboronga boronga mambo
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2012
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ni pale awamu ya pili ya ujenzi inapotumia pesa nyingi kuliko awamu ya kwanza, tena bila idhini...
  Yale yale aliyoyahoji Mh. Cheyo kuhusu matumizi ya serikali yasiyoidhinishwa....

  Halafu shirika lina wasomi wengi hilo, kuliko Bunge letu!!!
   
 4. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  inaelekea usomi sio chanjo ya kuboronga!!

   
 5. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi hata sielewi kwenye hii mifuko wafanyakazi wanawakilishwa na nani. Ninachoona ni kwamba hawa jamaa huwa wanafanya maamuzi "kwa niaba" ya wenye pesa zao (wafanyakazi), japo maamuzi yao mengi hayapendwi na wahusika wanaodunduliza pesa zao za kila mwezi.

  Nimewahi kusema mara kadhaa kuwa kunahitajika kufanyika utaratibu abao utamnufaisha mfanyakazi wakati anaendelea kutoa michango yake. Sifurahishwi na mfumo uliopo sasa ambao naona umekaa kidhurmati. Ati ukiwa umechangia michango 180 na una umri wa kustaafu miaka 55-60 basi huna budi kusubiri pensheni, ambayo kiukweli utalipwa muda mfupi sana kabla ya kufa. Sehemu kubwa ya michango inabaki kuwa "faida" kwa mfuko wa jamii.

  Wakati huo huo sielewi ni kwa nini mifuko hii inaona risk kumkopesha mwanachama wakati huo huo inapoteza pesa nyingi sana kuwakopesha wafanyabiashara wakubwa ambao si wanachama. Vile vile kuwekeza katika miradi ambayo haimnufaishi moja kwa moja mwanachama.

  Nadhani sasa ni muda muafaka kwa wanachama wa mifuko kudai haki zao ambazo zitawafanya wanufaike na michango yao sasa badala ya kusubiri "mafao ya uzeeni"
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Ndio maana NSSF hawataki kuwa transparent katika kuonyesha matumizi na makusanyo yao. Mark Bomani alilalamika wiki chache zilizopita kuwa NSSF pamoja na makampuni mengine ya nje hawatoi ushirikiano katika kuonyesha mapato na matumizi ya hela wanazokusanya.
  Pale ni wizi mtupu...project nyingi zinakuwa inflated kuliko gharama zake halisi zilivyo. Tusipoangalia nao watafilisika muda sio mrefu. Maana watanzania kazi yetu si kuifilisi nchi mpaka waje wawekezaji.
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Wasomi wa Tanzania badala ya kuwa inovative, wanafikiria kuiba tu. NSSF ina madudud mengi sana kwenye hizi project zake za uwekezaji. Ipo siku tunagundua yanayoendelea nyuma ya pazia.
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Mimi nikiwa kama Mwanachama wa NSSF sijawahi kupata gawiwo lolote au riba kutoka kwenye hiyo miradi wanayowekeza kwa kutumia pesa zetu halafu wanatudanganya kwamba tunawakilishwa kwenye bodi ya NSSF kupitia wawakilishi wetu!!

  Am sick & tired na huu usanii tunaofanyiwa na NSSF, na kinachonishangaza ni kwamba Mwanachama hata kama una matatizo huwezi kukopa kwenye mfuko huo, ila wahindi kama Manji wanakopeshwa mabillion ya pesa na hata ukitaka kusitisha uanachama wako basi hiyo adhabu utakayopata then utajuta ni kwa nini ulijiunga kuwa Mwanachama.
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sasa nimeanza kuelewa kwa nini nilikuwa nachukia pension. Dhuluma tupu. Hivi MD aliyestaafu 80s analipwa 30,000 per month, hii ndio stahiki yake? inflation? devaluation. Wiziiiiiiii. Je hao wafagizi?
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Hizi investment zinawanufaisha baadhi ya watu wachache ndani ya mfuko huo maana wanachezea sana hela kwa kupandisha gharama za miradi. Sisi tunaochangia hatujawahi kuona wala kugawiwa faida yoyote inayotokana na uwekezaji huo. Huo si wizi mtupu! Halafu wanawekeza hela hizo hata bila ya kupata ridhaa ya wachangiaji. Mhh!!
   
 11. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  NSSF janga la kitaifa nasubiri nione improvment ndani ya hii miezi mi3 nisipoona najitoa kabisa naenda mfuko mwingine kwani sioni faida yake.
   
 12. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Wafanyakazi wa Tanzania tuna hasara! Huku NSSF huku NHIF huku TRA huku EWURA wote hawa wanataka mgao kwene kamshahara ketu na faida hatuioni. tutapona kweli jamani?
   
 13. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwanakijiji,
  Kwanza naona hiyo link uliyoitoa haifunguki….may be u can do something ili tuweze kuipitia na kuchangia kwa makini zaidi.

  Now, let me come back to the topic. Endapo ningepewa option ya kuvumilia miradi kadhaa ya NSSF iliyopo, huenda ningeuvumilia mradi wa UDOM lakini kama kuna mradi ambao siwezi kuutetea kwa namna yoyote basi ni mradi wa Daraja la Kigamboni....!! Utetezi wa kuwapo Kigamboni New City sizani kama una mashiko yoyote hasa nikizingatia kwamba sioni uwezekano wa uwepo wa Kigamboni New City kwavile tu kuna Daraja la Kigamboni ingawaje ni rahisi kuwapo kwa kitu kinachofanana na Daraja la Kigamboni toka hata kwa private invvestors endapo tu patakuwa na Kigamboni New City! Hii, ni simulizi ya kuku na yai----Daraja la Kigamboni linaweza kuwepo lakini pasiwepo na Kigamboni New City na hivyo kufanya mradi mzima kuwa ni much more white elephant project kuliko ilivyokuwa projected!
   
 14. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Wapi kuna nafuu?
   
 15. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #15
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mkuu Ndahani,
  hii ni nchi ambayo kila mtu kutoka kila idara katika kila mradi wanafikiria kupiga tu.
  Nchi ya WAPIGAJI kama tunavyosema huku mtaani.....
  Inasikitisha sana, kwamba sababu zilizoua mashirika ya umma miaka ilee bado inaendelea kutafuna hivi vishirika vichache hadi leo!
  Sisi sijui ni mijitu ya namna gani?
  Nakubaliana na mtu wangu fulani alisema "Watanzania ni watu pekee wanaoishi katika nchi yao kama wageni, kwamba kuna siku watarejea kwenye nchi yao nyingine"
   
 16. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sijui namna gani mifuko ya jamii sehemu zingine duniani inavyosimamiwa lakini kwa hapa naona kuna mapungufu mengi na ya msingi:
  • Wanachama hawana mamlaka na namna michango yao inavyosimamiwa,
  • Mifuko ya pension huamua kwa "hisani" mafao gani wanachama wapatiwe
  • Uteuzi wa wakurugenzi wa mifuko hii hufanywa kama zawadi na waziri anayesimamia mamlaka hizo badala ya "wanahisa" ambao ni wafanyakazi wanaochanga michango hiyo
  • Wafanyakazi hawana namna yoyote ya kuwawajibisha watendaji na wakurugenzi wa mifuko hii pale wanapotenda kinyume na matarajio yao

  Kwa maneno mengine wafanyakazi wamewekwa kitega uchumi cha kuwanufaisha wanasiasa na wapambe wao kupitia mifuko hii ya jamii
   
 17. d

  dotto JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tunalazimishwa kuchangia but hatushirikishwi kuhoji matumizi yake. Hii ni aina ya wizi wa mchana.
   
 18. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #18
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Hii mifuko ya Jamii imekaa kiusanii sana ,hawa wametengeneza njia za kutafuna fedha za walalahoi kwa style mpaya .NSSF imekuwa ni kama Investment Bank ambapo inamilikiwa na wanahisa wasiozidi kumi,ni hatari sana kwa mustakabali wa nchi yetu.Katiba mpya inapaswa mambo kama haya tuyaweke bayana .Wanalipana mishahara mikubwa pasipo sababu yoyote.
   
 19. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #19
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Tulishasema haya siku nyingi sana! Hii miradi mwisho wake ni kuua NSSF, huu mfuko umekuwa unatumiwa sana kutekeleza miradi kisiasa. JK alikurupuka kupokonya wazo la UDOM toka kwa CDM; akafanya moja ya malengo yake; kama kawaida yake hufanya mambo mengi tu bila mipango. UDOM was supposed to be developed in stages/phases! Yeye na mkurupukaji mwenzake manywele wakaja na sera yao ya "piga yote mara moja" madhara tunayaona... Walifanya the same Mkwawa, kule nako, tutayaona tu, time will tell.

  Wa-TZ ni watu tulozoea kujifunza on a hard way; we are proud of this! Report ya CAG, ilipaswa kumuasha JK, nilitegemea ange kaa magogoni kujipanga, yeye huyoooo Brazil, ziara zake huwa hazina tija zaidi ya aibu tu!! Aibu tutapata atakapo adress OGP forum...as ususal!!

  Their gang sucks...
   
 20. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mimi ni mwanachama wa mfuko huu japo michango yangu sio kiasi kukubwa sana lakini nina uchungu nayo tena sana.

  Ukweli ukiangalia mradi kama wa Kigamboni (kwa mfano) pamoja na hiyo mingine mwisho wake utakuja kuwa kama 'Machinga Complex', ni ufisadi tu japo watanzania tulio wengi huwa hatuko proactive lakini ukweli unabaki pale pale kuwa 'the end will justify the means'

   
Loading...