NSSF: Kwa miaka 2 ya Rais Samia, Mali za Shirika zimefikia Trilioni 8 kutoka Trilioni 5.2 Machi 2021

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,112
49,826
Katika kile kinachoonekana kama mapinduzi ya mafanikio ya nssf, Mkurugenzi Mkuu Ametoa salute Kwa Uongozi wa Rais Samia Kwa kuwawesesha kurekodi Ukuaji wa Asilimia 55% ndani ya miaka 2 ya Rais Samia huku uwekezaji wa mfuko ukiongezeka kutoka Sh.Triolion 5.2 machi 2021 Hadi Trilioni 8 June ,2023 ,sawa na Ongezeko la sh Trilion 2.8.
---
Ni funga kazi pengine unaweza kusema hivyo! Baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba kubainisha mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Mfuko katika kipindi cha Machi 2021 hadi kufikia tarehe 30 Juni 2023.

Mshomba amesema hayo tarehe 25 Septemba, 2023 jijini Dar es Salaam, wakati akitoa wasilisho la utekelezaji wa majukumu ya NSSF kati ya Machi 2021 hadi Juni 2023 kwenye kikao kazi baina ya Mfuko, wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR).

Amesema NSSF imefanikiwa kuandikisha wanachama wapya 547,882, kati ya tarehe 1 Machi 2021 na 30 Juni 2023 na kwamba idadi ya wanachama wachangiaji iliongezeka kwa asilimia 36 kutoka 874,082 tarehe 1 Machi 2021 hadi kufikia wanachama 1,189,222 tarehe 30 Juni 2023.

“Siri ya mafanikio hayo kuwa ni pamoja na mkakati wa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sera nzuri za kuvutia wawekezaji, pamoja na utekelezaji wa mpango wa Mfuko katika uandikishaji wanachama na matumizi ya TEHAMA,” amesema.

Kuhusu makusanyo ya michango amesema katika mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2023, kwa mwezi yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 97.67 iliyofikiwa tarehe 1 Machi 2021 hadi kufikia TZS bilioni 143.05 kwa mwezi katika mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2023.

Hata hivyo, amesema makusanyo ya michango kwa mwaka yameongezeka kwa asilimia 43 hadi kufikia shilingi bilioni 1,718.28 katika mwaka ulioishia tarehe 30 Juni 2023 ukilinganisha na shilingi bilioni 1,201.05 zilizokusanywa katika mwaka ulioishia tarehe 30 Juni 2021.

Amesema uwekezaji wa Mfuko pia uliongezeka kwa asilimia 111 kutoka shilingi bilioni 3,395.46 tarehe 1 Machi 2021 hadi kufikia shilingi bilioni 7,153.23 tarehe 30 Juni 2023. Kati ya mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2021 na mwaka ulioishia tarehe 30 Juni 2023, thamani ya vitega uchumi vya Mfuko imekua kwa asilimia 55 hadi kufikia shilingi bilioni 7,153.23 tarehe 30 Juni 2023 kutoka shilingi bilioni zilizokuwa tarehe 30 Juni 2021.

Chanzo: Wasafi

My Take
Nssf na pssf zilitaka kufa baada ya Wazalendo uchwara wa awamu ya 5 kupora pesa za Shirika na Kupeleka walilojua wao huku wakiacha Wastaafu wanataabika.

Hongera sana Rais Samia,mara zote nakuita wewe ndio Mama wa Uchumi wa Tanzania na mama wa Taifa.

View: https://twitter.com/dailynewstz/status/1706545428936712316?t=nu6q3ZBY4NBkPIcDqxqArg&s=19
 
Screenshot_20230926-125823.jpg
 
Angeeleza Kwa nini wanataka kuajiri watu kinyemela angeeleweka vema.

Mkurugenzi kaamua kujitokeza kuweka mambo sawa ili justification ya kuajiri hao contract uwe na mashiko na hii ndio itumike kama hoja kwamba wamesaidia mfuko kupata faida

Hili likemewe Kwa nguvu zote, Kwa Nini watoe hizo taarifa Sasa?
 
Aaah. Mimi mkurugenzi wa NSSF alinilipa mafao yangu ndani ya siku mbili (yalikuwa kiduchu lakini yalikuwa na umuhimu mkubwa sana kwangu kwa kuwa yalikuja wakati wa uhitaji). Abarikiwe sana. Sina ugomvi naye!
Namuombea adumu kwenye hicho kiti mpaka kustaafu.

NB: Ila mkurugenzi. Kuna ka balance kalisalia kwenye akaunti yangu branchi ya Kinondoni (Ubungo plaza). Waelekeze vijana wako wanilipe fasta maana walikatalia faili langu tangu Dec 2022!
Waambie wasisahau kuongeza sifuri moja nyuma 😀😀😀

Wako mkulima, Bemendazole
20210725_220956-1-1.jpg
 
Toa ujinga hapa,kwanza Ajira za mashirika Kwa Sasa hazihitaji kibali Cha Utumishi wamerejeshewa wao waajiri kama zamani.

Pili watu wa Ajira za mkataba wako maeneo yote ya Serikali sawa na wanaojitolea hivyo Ajira zikitoa lazima wapewe kipaombele.

Ni Aisha uamue kujitolea au upate Ajira ya mkataba ya malipo kiduchu na stahiki finyu Ili nafasi zikitoka upate kipaombele.
 
View attachment 2763139
Ingekuwa wakati wa Jiwe ungesubiria miaka 2
 
Toa ujinga hapa,kwanza Ajira za mashirika Kwa Sasa hazihitaji kibali Cha Utumishi wamerejeshewa wao waajiri kama zamani.

Pili watu wa Ajira za mkataba wako maeneo yote ya Serikali sawa na wanaojitolea hivyo Ajira zikitoa lazima wapewe kipaombele.

Ni Aisha uamue kujitolea au upate Ajira ya mkataba ya malipo kiduchu na stahiki finyu Ili nafasi zikitoka upate kipaombele.
Umejibu kama tutusa bila kushirikisha ubongo, jaribu siku nyingine ushirikishe ubongo au ukae kimya ukiona unayotakiwa kujibu yamekuzidi uwezo
 
My Take
Nssf na pssf zilitaka kufa baada ya Wazalendo uchwara wa awamu ya 5 kupora pesa za Shirika na Kupeleka walilojua wao huku wakiacha Wastaafu wanataabika.

Hongera sana Rais Samia,mara zote nakuita wewe ndio Mama wa Uchumi wa Tanzania na mama wa Taifa.

View: https://twitter.com/dailynewstz/status/1706545428936712316?t=nu6q3ZBY4NBkPIcDqxqArg&s=19

Unawaza kwa kutumia Nini mkuu?

Mifuko ilitaka kufa awamu ya nne.

Awamu ya tano ikaweka mipango mathubuti na baadhi ya Mifuko ikaunganishwa na ndio hayo NSSF wanajisifu Leo.

Bila kuunganishwa NSSF ingekuwa wapi sijui!

Awamu ya Nne ajina January walikopa mabilion ya Hela ambayo hadi Leo hawajarudisha. (Unaweza ukagugu hizi habari) .

Awamu ya Sita imekopa hapo NSSF kuliko awamu nyingine zote kwa ujumla.
 
Toa upumbavu wako hapa,aliyepora pesa za mifuko ni Mwendazake au Jakaya? Aliyevuruga investments za mifuko ni Jakaya au Magufuli?

Kama huna akili usijadili na mimi
 
Back
Top Bottom