Tuliyoyasema: Mabilioni ya NSSF et al ya "uwekezaji" hayalipiki!! - Ripoti ya CAG yafichua

Leo nimegundua kwa nini NSSF wako bega wa bega na CCM, wanajua ili waendelee kufaidi huu mfumo fisadi ni lazima waibebe ccm inayolinda na kuhamasisha ufisadi. Kuna kipindi nchi ilizongwa na mgogoro wa umeme wakaandamana na Ngeleja kudai watafunga mtambo wa kuzalisha umeme wa dharura kumbe ni ghilba kwa watanzania wasizidi kuichukia ccm. Kiama chao chaja 2015
unganisha na hizi dots mkuu alafu ujue ukubwa wa tatizo.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/252547-tanzania-inaonekana-kituko-katika-eac-community.html
Tanzania's case is slightly different. Because Chama Cha Mapinduzi (CCM or the Party of Revolution) has been in power so long, in its socialist era the parastatal and state sectors became deeply entrenched in business.

The Tanzanian parastatal sector is the most pervasive in East Africa, and its bureaucrats are closely linked to or are part of the CCM apparatus.
 
Kwa mliowahi kufikia na kutembelea UDOM ni kweli value for money inaonekana; kwamba UDOM imegharimu/inagharimu karibu bilioni 400!? hasa baada ya taarifa kuwa baadhi ya majengo tayari yalishaanza kuvuja na kuwa na nyufa?

MKJJ, UDOM ni mbaya kupita maelezo!! Ujenzi wa pale ni kama walichukua mafundi mitaani! Si unajua ujenzi wa TZ, mafundi wapi mitaani tu, wale ambao wanajua kupanga matofali na kuchapia mchanganyiko wa cement na mchanga!

Honestly, no value for money...
 
mwanakijiji mbona haya mambo tulishajadili humu tokea 2010 na 2009

hii kitu ni very serious

Hiyo UDOM ni govt bond ambayo NSSF imewekeza kwa serikali. hii inatisha NSSF kuinvest 48% kwenye govt bonds.

Haya mashirika yako katiaka hali mbaya sana kifedha yaani yana pension deficit kubwa sana sijui itakuwaje uko mbeleni. watu wanasumbuliwa sana kupata pension zao.

Haya mashirika yanatakiwa ya binafsishwe ili yaendeshwe kwa ufanisi zaidi. Hizo hela zilizopotea ingekuwa private company watu wangekuwa wananyea debe siku nyingi. Siku haya mashirika yatakapokuwa mahututi ndio tutatafuta wawekezaji



link https://www.jamiiforums.com/tanzania-2010-2015/27111-mtei-amwonya-kikwete-5.html#post1077736


jibu: hii sio investment nzuri kwa member wake
NSSF investment facts
48% govt bonds (hapa ndio utaona majengo kama udom, polisi, PCCB na miradi mingineyo ya serikali)
18% properties( hapa utakutana na vitu kama ubungo plaza, quality ambayo ukusanyaji wake wa rent ni tata na majengo mengi)

govt bonds zinajulikana duniani kote kama ni safe kwa hiyo interest yake ni ndogo sana..... na kama interest ni ndogo pia returns zake ni ndogo pia, na kwa ajili return ni ndogo kwa hiyo pengo la pension linajengeka ndani ya nssf (kwa lugha ya kigeni "pension black hole"), na mjenzi wa hili pengo si mwingine bali ni dr dau...

kama dr dau ame invest nusu ya nssf kwenye govt bonds hii ni dhairi kwamba nssf haiko diversified, serikali ya TZ ikikumbwa na misukosuko na ku default on payments kampuni ya kwanza ku bust itakuwa NSSF

wataalamu wanasema america lives on china credit card, china wameivest savings zao nyingi kwenye american bonds, lakini american bonds ni safest bonds in the world, pamoja na mtikisiko wa uchumi america haja default bonds zao, ukae ukijua TZ sio marekani wao wata default tuuu......

kwa kifupi juu ya NSSF, bonds na serikali (udom, polisi na mengineyo ni mikakati ya serikali, NSSF ni credit provider na watu wanaolipia interest ya hiyo credit ni walipa kodi wa TZ)
mambo yakifanywa na america kwa kupitia mauzo ya bonds zao kwa china huwezi kusema china ndio wamefanya unasema marekani
na mambo yakifanya na TZ kwa kupitia mauzo ya bonds zao kwa NSSF, crdb, nmb huwezi kusema NSSF ndio wamefanya unasema serikali ndio imefanya.....

wakati umefika NSSF kukopesha wanachama wake ambao wanahela zao pale na hizo hela zitumike kama security


link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/33532-hongereni-nssf-kwa-kufanya-hivi-4.html#post518357
 
tutaishia kuja kuuana ndugu zangu. yani watukamue 10% ya mshahara kila mwezi halafu tuje kurushana mafao yetu. tunakoelekea ni kubaya hii serikali inaugua kansa ya ufujaji kwa kweli. khaaa
 
Dau yupo pale NSSF kuiba tu nagia yake ya kujilinda kuwa ni mtu safi ni kujidai mswalihina anasali ofisini!! Hana lolote yupo pale kuwanufaisha mabwana zake na sio wanahisa wachangiaji wa huo mfuko!
 
Kana kwamba hayo madudu hayatoshi, NSSF inajitayarisha kuingia ubia na makampuni hewa ili kufua umeme. Wanachama wake hawana habari wala hawahusishwi katika matumizi ya michango yao.
 
Na wakifa na fedha zetu tutawalazimisha kufufuka, mfanyakazi anakatwa say kwa miaka 30 hala mafao yake hayana riba pamoja na wao kufanya ufisadi kwa miradi yenye gharama kubwa, mbaya zaidi ni pale wafanyakazi wanapozungushwa kupata mafao yao yasiyokuwa na riba.
 
Kuna wakati suala haili liliandikwa na gazeti moja la kiswahi..na bwana Ramadhani Dau Mkurugenzi mkuu wa nssf akalijibu..ila hakujibu hoja ya msingi kwamba miradi yote inayowekeza nssf ni ya shinikizo la kisiasa na pia mfuko mzima unatumiwa kisiasa, kujaribu kuwekeza kwa vile serikali imeshindwa kuwekeza,
lakini hakujibu suali la msingi...WANACHAMA WANAFAIDIKA NA NINI NA INVESTEMNTS HIZI?

Ukweli wanachama wawafaidiki chochote kwani kwanza benefits zao ni ndogo sana unapoweka akiba yako sana sana utapata michango yako ulio wekeza na faida kiduchu sana ...
leo kuna watu wanapata mishahara mpaka 3,000,000 kwa mwezi hii ina maana anaweka 600,000 kwa mwezi kwa mwaka ni sawa na 7,200,000.00 ..sasa kama mwanachama atafanya kazi miaka 20 basi atakuwa amewekeza zaidi shs 144,000,000 !
interest bank ya saving ni zaidi ya 10% kwa mwaka hivyo unapowekeza matarajio upate zaidi kwa compaound interest...
katika soko la invesmets kwenye mashirika ya nje unapochangia kiasi kama hichi unakuwa covered kwa best medical insurance available..unapata life cove ambapo kama utafariki kabla ya compulsory retirement
age basi your bread winner watalipwa the sama pension kama umefikia umri wa kustaafu!..NSSF UKIFA KABLA YA MUDA NDIO MTIHANI KUPATA HIZO PESA KWANZA NA ITS ONLY MICHANGO YAKO!!!

PIA MIFUKO KAMA HII NJE NI KUWA KAMA UTASTAAFU KWA SABABU ZA KIAFYA BASI PIA UNATAKIWA KULIPWA 75% YA MALIPO AMBAYO UNASTAHILI KAMA UMEFIKIA KUSTAAFU, NA UTAPOFIKA UMRI WA KUSTAAFU UNALIPWA ASILIMIA 100 YA MAFAO YAKO...HIZI NDIO SCHEME ZENYE FAIDA KWA WANACHAMA
DAWA NI KURUHUSU MIFUKO YA BINAFSI KUSHINDANA NA MIFUKO HII YA SERIKALI, LAKINI NINAPO CHANGIA MILLION KUMI KWA MWAKA BILA YA LIFE COVER, BILA YA BEST MEDICAL INSURANCE BILA YA EARLY RETIREMENT BENEFITS , NI MIFUKO YA KITAPELI.
 
Kuna baadhi yetu tumekuwa na wasiwasi sana na huu uwekezaji wa fedha za wanachama wa mifumo ya hifadhi ya jamii mkubwa kati yao ukiwa ni wa NSSF. NSSF siyo mfuko pekee lakini ndio mfuko ambao unatumiwa sana kuwekeza kwenye miradi mingi na mkataba mkubwa ambao wengi watakuwa wanaufahamu ni wa ujenzi wa daraja la KIgamboni. CAG katika ripoti yake anadokeza vitu vichache ambavyo vinapaswa kuangiliwa na wanachama na watu wote wanaofuatilia mambo haya:

My Take:
Je wanachama wa NSSF na mifuko mingine ya jamii wanapaswa kujali jinsi mifuko hii inavyowekeza?
NSSF pia wamewekeza the jubilee insurance tanzania ltd..lakini kampuni hii kwa miaka 9 ilishindwa kugawa mgao wa dividends na mpaka sasa hakuna faida yoyote ambayo wamepata nssf.... wenye jubilee wanajua wanachokifanya...
sasa kuna hilo la daraja la kigamboni sijui mie kama mwanachama nitapata faida yoyote kwetu....mfuko hautumiki kama pensehni kwetu
 
[h=1]CAG: NSSF hatarini kufilisika [/h]
6db9d786bc77dd73357197bb3040a188.jpg

Na Reginald Miruko - Imechapwa 18 April 2012
Mwanahalisi



MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) uko hatarini kufilisika na kupoteza fedha za wanachama wake.

Hii inatokana na serikali kushindwa kurejesha katika mfuko huu, mabilioni ya shilingi iliyokopa au kudhamini katika miradi mbalimbali.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya 2010/2011, fedha za wanachama, hata katika mifuko mingine ya jamii, ziko hatarini kupotea.

Mbali na NSSF, mifuko mingine inayotajwa kuwa katika hatari hiyo ni Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF); Mfuko wa Wafanyakazi wa Serikali Kuu (PSPF), Mfuko wa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF) na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF).

Kulingana na taarifa ya CAG, sehemu kubwa ya fedha za wanachama ambazo hazijarejeshwa, zilikopeshwa kwa serikali kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Katika chuo hiki, NSSF peke yake iliingiza Sh. 234.1 bilioni. Mifuko iliyosalia ilitoa jumla ya Sh. 181.3 bilioni.

Katika ujenzi wa UDOM, PPF ilitoa Sh. 39.99 bilioni, PSPF (Sh. 105.9 bilioni), LAPF (Sh. 22 bilioni) na NHIF (Sh. 13.4 bilioni). Fedha hizo na riba yake hazijarejeshwa.
Ripoti ya CAG, Ludovick Utouh, inasema kutorejeshwa kwa mikopo hiyo, iliyochukuliwa au kudhaminiwa na serikali, ni kinyume cha sheria ya udhamini ya mwaka 1974.

“Kutolipika kwa mikopo hii iliyodhaminiwa na serikali kunaiweka mifuko hii ya hifadhi katika hatari ya kupoteza fedha za wanachama na kuhatarisha uwezo wa mifuko kufanya uwekezaji zaidi,” anasema na kuongeza:

“Kushindwa kulipa madeni taasisi hizi ambazo baadhi yake zilipata udhamini wa serikali, kunatia shaka iwapo upembuzi wa kina wa wakopaji ulifanywa na mifuko ya kijamii kabla ya kutoa mikopo hiyo.”
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau hakupatikana kwa maelezo kuwa alikuwa kwenye mkutano mkoani Mbeya.

Lakini Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume amesema mikopo kwa serikali imetolewa kwa uangalifu na inalipwa bila matatizo na kwa misingi ya kibiashara.

“Mikataba ya kisheria imesainiwa kukidhi mazingira mbalimbali ikiwa ni pamoja na iwapo itacheleweshwa…. Hakuna hatari yoyote ya fedha kutolipwa wala kupoteza fedha za wateja,” amesema Chiume.
Lakini CAG katika taarifa yake ya kurasa 183, anasema, “Ukubwa wa kibiashara kati ya serikali na mifuko unatia shaka kutokana na kusuasua kwa serikali katika ulipaji madeni yake. Hii inahatarisha uendelevu wa mifuko hii.”

Katika ukaguzi wake, CAG amebaini kuwa NSSF ilitoa Sh. 234.1 bilioni kwa mradi wa UDOM, lakini mkataba uliosainiwa ni wa Sh. 35.2 bilioni tu. Hii ni hatari kwa fedha za wafanyakazi na wastaafu.

Akifafanua suala la fedha kwenye mkataba kutofautiana na fedha zilizotolewa, Chiume alisema mkataba ulitakiwa kuwa mmoja ambao ulisainiwa wakati wa awamu ya kwanza.

Chiume alisema kwa awamu ya pili, kilichotakiwa ni kusaini addendum (makubaliano ya nyongeza), ambayo “yako mbioni kukamilika.”
Utouh anaripoti, “Majengo kwa ajili ya awamu ya kwanza yalikamilika na kuwekwa katika matumizi mwezi Septemba 2008. Mpaka wakati wa ukaguzi 2010/2011, mfuko ulikuwa haujafanikiwa kukusanya malipo ya pango kutoka serikalini.

Kwa msingi huo, hadi sasa limbikizo la riba limefika thamani ya Sh. 14 bilioni,” anasema Utouh.
Mkopo huo ulitolewa kwa utaratibu wa kubuni, kujenga, kumiliki na kuhamisha ambapo mfuko ungepokea kodi iliyokokotolewa kwa riba ya asilimia 15 kwa kipindi cha miaka kumi.

Vilevile CAG amebaini kuwa majengo yaliyojengwa kwa mkopo huo, hayako kwenye vitabu vya UDOM wala katika vitabu vya NSSF, kutokana na uelewa tofauti uliopo kati ya pande mbili zinazohusika.

Kuna mikanganyiko katika uelewa kwa serikali na mifuko ya hifadhi, ameeleza CAG. Wakati mifuko inasema fedha zilizotumika kujenga majengo hayo zilikuwa mikopo kwa serikali, yenyewe serikali inadai fedha hizo ni uwekezaji wa kawaida wa mifuko hiyo.

Mbali na UDOM, serikali pia haijalipa jumla ya Sh. 19.77 bilioni zilizotumika katika ujenzi wa ukumbi wa bunge, ambazo hazilipwi kulingana na makubaliano. Hadi wakati wa ukaguzi, NSSF ilikuwa inadai Sh. 8.96 bilioni, PPF (Sh. 7.9 na LAPF Sh. 2.91.

Pia upo mkopo mwingine wa NSSF wa Sh. 5.33 bilioni na riba ya asilimia 15 kwa miaka kumi, uliotolewa kwa ajili ya ujenzi wa “taasisi ya serikali ya kiusalama” mwaka 2007.
Mfuko mwingine uliowekeza katika mradi huo ni PSPF uliotoa Sh. 6.4 bilioni.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, NSSF kwa udhamini wa serikali ilikopesha taasisi kwa shughuli mbalimbali.
Kwa mfano, ujenzi wa nyumba za polisi kwa Sh. 20 bilioni na Sh. 12. 9 bilioni kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mwaka 2007 kwa ajili ya ujenzi wa Machinga Complex, Ilala.

“Hadi sasa hakuna malipo ya riba wala sehemu ya mkopo hiyo yaliyofanywa. Hii ni kinyume cha mkataba,” inasema sehemu ya ripoti ya CAG.
Kwa upande wa Machinga Complex, hadi tarehe 30 Juni 2011, mkopo na riba yake ulikuwa umefikia Sh. 15.3 bilioni.

Ripoti ya CAG imeainisha pia mikopo mingine ambayo hailipwi kulingana na mikataba ya mifuko hiyo, bila ya kutaja viwango vyake.
Mikopo hiyo ni iliyotolewa kwa Continental Venture (T) Limited, Meditech Industrial Co. Ltd, General Tyre (GT), Kiwanda cha Sukari Kagera, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) na mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio amesema hajaona ripoti ya CAG na yuko safarini Tanga.
Hata hivyo amedokeza kuwa hivi karibuni walikaa na CAG kujadili suala hilo na kubaini makosa ya kifundi katika uhasibu baina ya mifuko na serikali katika ujenzi wa UDOM; hivyo CAG kuahidi kuyashughulikia kwa upande wa serikali.

Alipoulizwa ni makosa yapi hayo, Erio alimtaka mwandishi awasiliane na kaimu wake, Stephen Alfred ambaye ilielezwa kuwa yuko kwenye mkutano. Hadi tunakwenda mitamboni, Alfred hakupatikana.
 
Hii easy, waliokopeshwa elimu ya juu hasa waliosoma UDOM kwa mfuko was serikali baada ya kumaliza na kuajiriwa km vile waalimu nk si waanze kukatwa hiyo fedha? pia wapo wasomi wengi walisoma kwa mikopo huu ndio wakati wa wao kuanza kurudisha hilo deni.

Wasomi rudisheni pesa mlizolipiwa ada na serikali, hamoni mnachangia kuifilisi nchi?
 
Mwanakijiji nilipitia hii report sikuliona hili jambo,
ila ulipoliweka nikabidi nirudi kutafuta, naona kama presha imepanda maana nimechangia NSSF kwa miaka mingi!
 
Ukweli mchungu kuhusu namna fedha za wafanyakazi zinavyotafunwa kwa maslahi ya CCM na washirika wake wachache. Hii ni sehemu tu ya hotuba Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Wizara ya Kazi na Ajira, Cecilia Paresso.

Watu waliolazimika kusafiri kwenda Dodoma kwenda kutisha na ku-lobby watu ili habari hizi zisiwafikie wafanyakazi kupitia vyombo vya habari, wajibu hoja badala ya kufukia uvundo chini ya zulia.

..........

MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika kipindi chote cha miaka mitano tumeshauri mambo yafuatayo kuhusiana na mifuko ya hifadhi ya jamii hapa nchini;

1.Kuunganisha mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii na kubaki chini ya usimamizi wa Wizara ya Kazi na Ajira lengo likiwa ni kuirahisishia Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi za Jamii katika kutekeleza Sheria moja nakuunda vifungu sawa vya kisheria vitakavyosimamia utekelezaji na uendeshaji wa mifuko hii. Tulipendekeza PPF na NSSF iunganishwe na kuwa mfuko mmoja kwa ajili ya Sekta Binafsi vilevile LAPF, PSPF na GEPF iunganishwe na kuwa mfuko mmoja kwa ajili ya Sekta ya Umma.

2. Tumeitaka serikali kuwa na jitihada za haraka kunusuru uhai wa Mifuko ya Hifadhi ya jamii kwa kulipa fedha walizochota kwa ajili ya uwekezaji katika miradi mikubwa kama ambavyo imeonyeshwa katika Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2012/2013, 2013/2014 lakini ripoti ya CAG ambayo imetolewa hivi karibuni ya 2014/2015.

Mheshimiwa Spika,Ni kweli kuwa sikio la kufa halisikii dawa. Madeni sugu ya serikali yanatishia uhai wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini huku Mamlaka ya Usimamizi ya Mifuko hiyo (SSRA) ikitoa angalizo kwa serikali kuhusiana na hali hiyo kufuatia kuidai Sh. trilioni 8.43 kuwa hali hiyo inaweza kukwamisha mifuko hiyo kuwalipa mafao wanachama wake, kujiendesha yenyewe na kuwekeza katika miradi mbali mbali.

Mkurugenzi wa SSRA, Irene Isaka alitoa tahadhari hiyo Oktoba mwaka jana mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa kuwakutanisha wakurugenzi wa mifuko ya hifadhi ya jamii, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Mkuu wa Hesabu za Serikali, SSRA na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo alieleza kuwa iwapo serikali itaendelea kukopa na kutopeleka michango ya wanachama wake, mifuko hiyo itaathirika kiasi cha kushindwa kulipa mafao kwa wanachama wake.


?Tuliyonayo, mifuko yetu ni ya pensheni, hasara ni ya mifuko. Mwanachama hatamsamehe mwenye mfuko kwa kushindwa kumlipia, kadri deni linavyoongezeka ndivyo Mfuko unaumia na baadaye kushindwa kulipa mafao yanayotakiwa.?

Mheshimiwa Spika, Kauli hii ni ya msimamizi mkuu wa mifuko ya hifadhi ya jamii ambaye ndiye mwenye dhamana ya uhai wa mifuko hii. Mara kadhaa Kambi ya upinzani imeelezea na kuonya jinsi ambavyo madeni haya ambayo ni pamoja na PPF (bilioni 192), NHIF ( bilioni 107), NSSF ( bilioni 467), PSPF ( bilioni 4.29), LAPF ( bilioni 170) na GEPF (bilioni 6.86) yanavyohatarisha uhai wa mifuko hii.

Si Raisi Kikwete wala viongozi waandamizi wa CCM wenye kuelewa kuwa, hili ni bomu litakapolipuka muda wowote. Ieleweke kuwa hakuna mpinzani yeyote anayepinga miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM). Tunachokipinga ni kitendo cha Serikali kutumia fedha za wachangiaji wa mifuko kwa miradi yake ambayo ingeweza kutekeleza ipasavyo kwa kutumia fedha nyingine na kama ingefuta misamaha ya kodi, ingepigana ipasavyo kuzuia ufisadi na ubadhirifu kama wa ESCROW, EPA, RICHMOND- DOWANS na/ au kama ingeweza kupunguza matumizi makubwa ya serikali.

Mheshimiwa Spika,
Huwezi kuukataa ukweli kuwa utawala wa awamu ya nne umeshindwa kuipa wizara ya fedha uwezo wa kitaasisi wa kukusanya kodi matokeo yake, serikali inakuwa inakodolea macho fedha za mifuko ya hifadhi ya jamii na hii ni dhambi ambayo haitafutika machoni pa watanzania.

Na sasa tunaelewa ni kwa nini serikali ilikuwa inaishinikiza wachangiaji wa mifuko wasichukue pensheni zao mpaka wafikishe umri wa kustaafu ambao ni miaka 60, kwa kuwa wanajua umri wa maisha ya wa watanzania ni miaka 52. Hatuwezi kuwa na serikali ambayo ina trade-off na ustawi wa maisha ya watu wake, hii ni aibu kubwa!


MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA JAMII (NSSF)

Mheshimiwa Spika, mfuko wa hifadhi ya jamii, NSSF, ni mojawapo ya mifuko ambayo mbali ya kutoa mafao ya kustaafu na huduma zingine kwa kadri dira na dhima yake lakini bado inajishughulisha katika uwekezaji kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika,
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo ni kwamba mbali ya kuwekeza kwenye ujenzi wa majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma na Daraja la Kigamboni, pia NSSF ina miradi ifuatayo ya ujenzi wa nyumba;

i. Nyumba 300 za Mtoni Kijichi (PHASE I &II) ?Nyumba hizo zilikwisha uzwa tayari

ii. Nyumba 800-Flats 500 na Villas 300 (PHASE III) ambao umegharimu shilingi bilioni 137.

iii. Mradi wa AZIMIO SATELITE -Kigamboni wenye Nyumba 7160 (Flats &Villas) ?Utagharimu shilingi bilioni 871

iv. Mradi wa Dungu Farm-Kigamboni (Flats 568) Utagharimu shilingi bilioni 140

v. Mradi wa MZIZIMA TOWER nyumba ya Ghorofa 32 unaotarajiwa kumalizika Juni 2017, ambao utagharimu shilingi bilioni 233. Lakini hadi sasa bado mradi haujaanza.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi sio kama inapinga uwekezaji unaofanywa na NSSF, je uwekezaji huo unafanywa kwa kuangalia kipindi ambacho miradi hiyo itarejesha faida za uwekezaji (return on investment)?

Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 3.12 cha mwongozo wa Msimamizi wa Mifuko ya Hifadhi(SSRA) wa mwaka 2003, pamoja na kanuni zake kuhusu uwekezaji salama wa mifuko na marejeo yake ya mwaka 2012 ni kwamba, mifuko inatakiwa kuwekeza asilimia 70 ya mali zake kwenye dhamana (T-Bills) na hati fungani ( T-Bonds), asilimia 25 ya mali zake kwenye Miundombinu, asilimia 30 ya mali zake kwenye mali isiyohamishika (Real Estates).

Je, ni kwa kiasi gani NSSF imefuata Sheria na kanuni kuhusu uwekezaji wake mpaka sasa kwa kufuatia mgawanyo uliotajwa?

Mheshimiwa Spika, NSSF walinunua majengo ya Manji (EPZ-Project) kwa jumla ya shilingi bilioni 47.5 mwaka 2006, kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, ni kuwa majengo hayo hayakuwa na thamani hiyo wakati NSSF inayanunua. Pamoja na hayo, mradi huu unasemekana mpaka sasa kutorudisha thamani ya uwekezaji kwa muda. Kambi ya Upinzani Bungeni inahusisha upandishaji huo wa thamani isiyo halisi kuwa ni mojawapo ya mianya ya watendaji wa NSSF kujipatia 10% kwa miradi isiyo na tija.

Aidha, kodi ya mwaka ya Jengo hilo inayotokana na upangaji, haijaweza kuakisi marejesho ya faida ya uwekezaji huo kwa kuwa mradi huo mpaka sasa umeshindwa kurudisha hata nusu ya fedha zilizowekezwa na hivyo kuhatarisha uwezo wa mfuko kutoa marejesho kwa wanachama wake.


Kwa mujibu wa sheria ya SSRA, Benki Kuu ndio mamlaka ya kuhakikisha mifuko inafanya uwekezaji makini, je kwa uwekezaji huu ambao taarifa ya CAG ilisema kuwa unauweka mfuko katika hali ya kuweza kufilisika na hivyo wanachama kukosa mafao, Wizara ya Fedha inatoa majibu gani?

Mheshimiwa Spika, kuonesha kuwa uwekezaji wa NSSF umekuwa ukiongozwa na matakwa ya watu binafsi, kuna jengo la ghorofa 4 lililojengwa Kigoma kwa gharama ya shilingi Bilioni 7 na limekamilika sasa ni miaka 2, lakini hadi muda huu halijapata mpangaji. Kambi ya Upinzani inahitaji kupata majibu ya uhakika kuhusu uwekezaji huu usio na tija ni nini hatma ikiwemo uwajibikaji wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi kwa kushindwa kuusimamia mfuko ipasavyo?

Mheshimiwa Spika, NSSF imenunua ardhi mikoa kadhaa kwa bei ambayo ni zaidi ya ile ya soko (Inflated price) na mwishowe viwanja hivyo vinakosa wanunuzi. Kambi Rasmi ya Upinzani inaona kuwa NSSF kukataa kuwekeza kwenye dhamana za Serikali na kuwekeza kwenye majengo ni wa kutia shaka na ni mwanya wa watendaji wake kupokea rushwa au makampuni yanayopewa kandarasi za ujenzi ni makampuni yao na hivyo uwekezaji huo kuwanufaisha wao binafsi na si wanachama wa mfuko.

Kambi ya Upinzani Bungeni, inataka majibu ya kina kutoka kwa Wizara juu ya uwekezaji mzima unaofanywa na NSSF bila kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo kwa kuwa ni dhahiri kuwa uwekezaji mkubwa usio na tija unaofanywa na NSSF unahatarisha kwa kiwango kikubwa uhai wa mfuko huu.

 
Back
Top Bottom