Baba Paroko
Member
- May 9, 2007
- 22
- 4
Mkuu Kasana umenikumbusha mbali sana maana ishu ya tebo ilikuwa soo hasa pale wale walimu wanoko waliokuwa wanavuka hataile tebo ya 12 na kwenda mpaka ya ishirini, maana tebo ya saba, tisa ni noma sasa huko kwenye 13, 17, 19 je?. Oyaa mnakumbuka sayansi kimu, ile ya kutengeneza maakuli skuli halafu mnapata maksi. Pia kun ishu moja huwa inaniboa nikikumbuka mpaka leo; NAMBA Yaani mtu unawahi shule kinoma ili uwe namba moja. Mnakumbuka tobo bao, usiombe hiyo ichezwe darasani wakati nje mvua inanyesha! Mnakumbuka mtihani wa mwisho wa darasa la saba, pale ambapo mnaanza say na hisabati baada ya hapo mnaenda kucheza mpaka mnajisahau mnakuja kuitwa mtihaniiiiiiiiii!!! mnaenda tena mkimaliza the same. HALAFU MWISHO KABISA MNAVUNJA PENI, KALAMU N.K
(jina langu nalihifadhi kwa sababu za kisiasa)""Kwako dada mpendwa, salamu nyingi sana zikufikie hapo ulipo. Utakapo kujua hali yangu, mimi ni mzima wa afya, hofu ni kwako uliye mbali na upeo wa macho yangu (wakati tupo darasa moja, yeye alikuwa anakaa mbele yangu).
Dhumuni la barua hii ni kukuambia kuwa nakupenda sana, yaani huwa silali kwa kukuwaza wewe. Napenda uwe mpenzi wangu.
Wako mpenzi.......Idimi
ha ha ha ,mzee yaani imenibidi nicheke kweli kweli, duh mzee!.chekeni kwanza kabla sijamalizia
Nikiwa darasa la tano, nilimuandikia barua hii dada Agness, alikuwa mrembo si utani (sijui alipo kwa sasa).
(jina langu nalihifadhi kwa sababu za kisiasa)"
Sasa Agnes kumbe ile barua ikawa imemkera sana (nadhani alikuwa bado mtoto kuweza kutambua mambo haya). Si akaifikisha kwa mwalimu Chale (alikuwa mwalimu wa zamu) bila mimi kujua. Ikagongwa kengele,wote tukatoka madarasani. Nilikuwa sijashitukia dili muda huo. Nikaitwa mbele ya hadhara, barua ikasomwa pamoja na sahihi yangu ya majigambo pale chini.
Mnihurumie kwa yaliyonipata, chekeni kwanza kabla sijamalizia!
Nikiwa darasa la tano, nilimuandikia barua hii dada Agness, alikuwa mrembo si utani (sijui alipo kwa sasa).
(jina langu nalihifadhi kwa sababu za kisiasa)"
Sasa Agnes kumbe ile barua ikawa imemkera sana (nadhani alikuwa bado mtoto kuweza kutambua mambo haya). Si akaifikisha kwa mwalimu Chale (alikuwa mwalimu wa zamu) bila mimi kujua. Ikagongwa kengele,wote tukatoka madarasani. Nilikuwa sijashitukia dili muda huo. Nikaitwa mbele ya hadhara, barua ikasomwa pamoja na sahihi yangu ya majigambo pale chini.
Mnihurumie kwa yaliyonipata, chekeni kwanza kabla sijamalizia!
Umenikumbusha mbaaaaaaaaali na barua za mapenzi
Tatizo langu lilikuwa kwamba nikiandika barua ya mapenzi sipati mtu wa kumpa (middlegirl/broker), na yule binti niliyekuwa namtaka kusoma ilikuwa shida kidogo. Basi nikawa namfukuza wakati wa mwagano hadi namshika na kumsomea barua niliyomwandikia...kaaazi kweli kweli......mana kabla sijakubaliwa yule binti akawa ame improve kusoma, technically I became a tutor!!!
Ha ha ha hii issue ya kutakana shuleni ilikuwa kiboko. Nakumbuka nilivyokuwa darasa 7, kuna siku mmoja nilimwazima (nilimpatia) binti mmoja, tuliyekuwa tunasoma nae, mkanda wa video wa Home Alone (part 1). Basi yule binti aliporudisha ule mkanda, akapachika, ndani ya kasha, kipande cha karatasi kilichoaandikwa "Nakupenda. Mbona unaninyanyasa mtoto wa watu." Dah ebwanee nasemaje....hiyo line inanikuna mpaka leo hii. Huwaga nasisimuka kila nikiikumbuka yaani.
Washikaji, hiyo yote tisa, Mnakumbuka tulikuwa tunaenda shule peku peku, halafu baridi la Asubuhi si mchezo. wakati mwingine njiani kulikuwa na nyasi kibao kabla mazingira yetu hayajaharibiwa, basi ukitembea inabidi upige mahesabu maana umande ulikuwa wa baridi ukizingatia hata viatu hujavaa.
Halafu ingine ni ile nyumbani hakuna pasi, au kwa sababu ya michezo mingi unachelewa kunyoosha nguo, sasa kulikuwa na technolojia ya asili. unakunja vizuri uniform zako unazitandika chini ya shuka halafu unazilalia juu, Asubuhi ukiamka si mchezo panga zimesimama kiroho mbaya.
Hivi mnakumbuka kwamba wanafunzi wengi ilikuwa wanaenda shule pekupeku?? na wakti wa mapumziko kwenye mpira jamaa watakataa usicheze mpaka uvue "mdundo" viatu vyako........enzi hizo safari buti na viatu flani hivi vya bora vyeusi kwa mbele vipana tulikuwa tunaviita "vita," na raba flani hivi za canvas watoto wanafua na kupaka chaki ili viendelee kuwa vyeupe ndio vilikuwa vinatamba. Kenya wenzetu bado wana safari buti sisi mmmmmmmmmh, tena sidhani hata Bora shoe company ime survive wimbi hili la "ukimwi" wa maendeleo!!!.
YNIM
Du aisee hizi safari buti zilikuwa safi sana. Nakumbuka zilikuwa haziishagi. Pamoja na kuzipigia madochi sana kwenye soccer. basi unakuta enzi zile mzazi anakuchunia kukununulia viatu vingine mpaka ulivyokuwa navyo viishe au mguu ukue. Sasa kwa wale wakina andunje kama mimi, tulijikuta tunavaa safari buti mmoja kuanzia darasa la 5 mpaka la 7. Nakumbuka za kwangu ilibidi nizichanje wembe, vinginevyo ningeingia level ya unjuka nimevitinga. Mguu uligoma kukua kabisa!
wazee mbona hamjagusia enzi hizo ukitaka kuanza darasa la kwanza lazima uuvushe mkono kwenye kichwa ushike sikio la upande wa pili, ukishindwa tu,ujue wewe unarudia vidudu. hahaha!
Hii kiboko!
Ndg Sahara, hii mbinu imeniacha hoi sana. Nadhani hii ilikuwa kabla ya asi za mkaa ama sio?
Duh mzee kumbe umewahi kuwa mnene, mimi nilikuwa Monita, tena monita mwenyewe monita wa Msitari,darasa letu lilikuwa na Mistari minne kila msitari na monita wake, sasa mimi msitari wangu ulikuwa na wasichana wazuri kweli(kwa mujibu wetu wakati huo). sasa kuna kabinti kamoja nilikuwa nakazimia kichizi, kenyewe kalikuwa kanakaa siti ya mbele karibu na ubao,mimi nilikuwa nakaa nyuma kabisaNani alikuwa Kaka Mkuu kama mimi hapa JF? Naoma tubadilishane uzoefu. Mimi nilikuwa kaka mkuu nikiwa darasa la sita.